JACADUOGO2.
JF-Expert Member
- Dec 13, 2010
- 930
- 217
CHADEMA sasa inabidi tuamke na tuache kulewa sifa mijini wakati maeneo mengi ya vijiji hatujafanya chochote na tunasubiria mpaka uchaguzi mkuu au uchaguzi mdogo. Haipendezi hata kidogo.
Kumekuwa na tabia ya viongozi wa CHADEMA ngazi ya taifa kuongeza na kuzidisha nguvu pale ambapo tayari wananchi wameshapata mwanga kuliko maeneo mengine ambayo bado hayajaamka. Kwa mfano nguvu nyingi za Chama zinaelekezwa Arusha, Mwanza na Mbeya ambapo tayari kuna mwamko.
Maeneo ya vijijini yamesahauliwa sana. Kwa mfano wilaya nyingi zilizopo vijijini ni tabu tupu.
Naomba tujibu hoja badala ya kumshambulia mtoa hoja. Mimi ukiniuliza kuwa nimefanya nini, jibu ni kuwa nimewahi kugombea udiwani kwenye kata ya Nyahongo jimbo la Rorya kwa tiketi ya CHADEMA kwenye uchaguzi mdogo October 2011 na nilishindwa kwa tofauti ya kura 64 na CCM na tayari nimefungua matawi matatu ndani ya kata yangu na tuna ofisi ya kata safi sana na tumesimika viongozi wote ngazi msingi hadi kata na kila baada ya muda fulani narudi kuongeza nguvu ndani ya kata na jimbo!
Kwa sasa niko Sikonge Tabora katika kutafuta maisha na kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa madiwani hapa Sikonge (Ipole na Kiloleli) mchango wangu wa kihali na mali umeonekana na ninajivunia kuchangia ushindi katika kata ya Ipole. Kitu ambacho ni historia kwani tangu enzi na enzi CHADEMA haijaambulia kata yoyote ndani ya wilaya ya Sikonge.
Tuchangie namna ya kuongeza nguvu ya CHADEMA maeneo ya vijijini, tusisubiri 2015! Ahsanteni wadau.