CHADEMA tufanye kweli

Joblube

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
369
151
Wana JF

Niwakati ambao CHADEMA inapatamashambulizi kutoka kila kona na vyama vyote vinajaribu kila njia kibomoa CHADEMA, hii imedhihirisha muungano wa vyama vya upinzani kwa Tanzania hautafanya kazi. Natoa ushauri kuwa kwa kuwa wanaongeza mashambulizi sisi ambao sio viongozi ndani ya CHAMA tuwachie viongozi wajibu baadhi ya propaganda zao, sisi wengine tupeleke hasira zetu katika kuhakisha kila mtu aliyekaribu na sisi maofisini,majumbani, marafiki wa mtu mmoja mmoja na hata unayekutana naye njiani anaeleweshwa ubaya wa CCM na faida ya kutoa CCM madarakani, tufanye kazi kwa vitendo zaidi ili kuliokoa taifa hili ninauhakika mia kwa mia kila mmoja wetu akidhamiria kuafanya kweli tutashinda. Inchi hii ya Tanzania haitaenda popote bila kuifanya CCM kuwa chama cha upinzani. Angalia jinsi wanavyowaanda vijana wao wa UVCCM kuja kututawala na sio kutuongoza, tazama jeuri zao kwa sababu ya viburi vya baba zoa. Mwisho tuhakikishe yeyote anayekuja CHADEMA kutafuta maslahi binafsi kwa njia haramu alaaniwe kwa gharama yeyote ile.

Pamoja wenye uchungu na nchi yetu tunaweza.
 
FALSAFA NZURI YA CHAMA CHA SIASA NI SHARTI IAKISI JAMII HUSIKA NA
UHALISIA WA MATUMAINI / NDOTO ZAO, MAZINGIRA WANAMOISHI,
URAHISI KUKUMBUKIKA / KUELEWEKA KWA FALSAFA YENYEWE NA YENYE KUENDANA VILIVYO NA KIPINDI KATIKA MAISHA WANAMOISHI

Nitangulie kuwapa hongera sana sana tena sana CHADEMA kwa kuweza kuibuka na falsafa ambayo kiujumla ni sura halisi ya matakwa ya Wa-Tanzania na safari yetu ndefu kama jamii moja katika maisha haya. CHADEMA na falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" yatoooosha!!

Hakika kwa ufahamu wangu falsafa ya CDM imekidhi misingi yote muhimu kiasi cha kutosha kututambulishia kwamba CHADEMA ni watu gani katika jamii yetu, wanaamini katika lipi na siku zote tuwafanyie tathmini katika uendeshaji wa shughuli za kila siku katika taifa hili huku wananchi tukizingatia misingi gani hasa zinazotambulika rasmi.

Ndio, Falsafa ya Chama Cha Siasa si sawa na mtu kufanya ziara binafsi kwenye mbuga za wanyama kokote duniani. Wala Jambo hili halipigiwi KOFULI MLANGONI kwamba haukua nalo jana leo hii ukitangaza kuwa nalo basi ni kosa la jinai - laa hasha!! Hivyo mtu kusema kwamba labda kwa kuwa Mwenyekiti Mstaafu, Mhe Edwin Mtei, katika mahojiano yake na vyombo vya habari pengine miaka 5 iliyopita hakulitaja falsafa ya Chama; hiyo peke yake hakizuii chama kuweza kupiga hatua zaidi kwa KUJIPA SURA HALISIA kisiasa nchini.

Kiukweli, kupokezana kule kete la majukumu ndani ya Chama na hiyo ndio maana tunasema CHADEMA ni cha Wa-Tanzania wote na wala si mali ya mtu binafsi kama vilivyo vyama vingine vya mifukoni hapa nchini hivyo kama Mzee Mtei aliweza kutekeleza hatua fulani muhimu kwa uhai wa chama hiki basi nasisi Vijana Wa-Tanzania wenye mali yao tunaendelea kukamilisha mengine na mengi zaidi mazuri bado yako njiani yanakuja - kaeni mkao wa ushindi kote nchini!!

Nielewavyo mimi, falsafa ya Chama Cha Siasa kwa maelezo miepesi ni UJUMLA WA MAWAZO NA FIKRA yanayotafuta kumtambulisha mtu na au Chama na kile anachokiamini, kupenda kuliona likitendeka kwa jamii yake na kwamba yuko tayari kuwekeza muda na rasilmali nyinginezo muhimu kuendeleza fikra na mawazo hayo kwa faida na maendeleo ya jamii katika ujumla wake.

le majibu ya maswali ya msingi kama vile; (1) nyinyi kama Chama cha siasa wananchi tuwatambueni kuwa muu akina nani hasa?? (2) mnaamini katika mambo yepi hasa ambayo lasimamia ambayo ndiyo itakayokua ni chimbuko na muongozo wa shughuli zenu zote kiutendaji kama chama.

Na kwa mantiki hii ndipo nako tunapotangaza kwamba ni mwisho wa SIASA ZA MKUMBO huku tukifungua ukurasa mpya wa siasa za kisasa zenye kuegemea misingi ya wazi na iliotukuka mioyoni mwa Wa-Tanzania tuliowengi.

Hadi hapo nawashauri vijana wenzangu kote nchini na wananchi kwa ujumla kwamba maadam sote tumeshajionea madhara makubwa yalioletwa na falsafa mpya ya Chama fulani nchini; falsafa ya 'Kasi Mpya, Nguvu Mpya na Ari Mpya' pasipo kuelewa hasa dira zima ya wapi tunakopelekwa kama taifa, na hatimaye kutokea ajali ya mwaka kisiasa ambapo chama hicho hivi sasa kimeparaganyika vipande 200 kidogo, ni muda muafaka sote tukajiunga CHADEMA leo hii na wala si kesho.

Hakika CHADEMA pekee ndiyo nyumba salama kisiasa kwa watu wa rika zote, dini zote, rangi zote, jinsia zote na daraja zote za uelewa sawa na vile ambayo hata Marehemu Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere aliiona na kutuambia kwa kinywa kipana sote nchini.
 
Back
Top Bottom