CHADEMA na tishio la Tendwa kukifuta Chama kisa Maandamano/M4C

Tendwa mwenyewe wakati wa kuanza kampeni 2010 alipelekewa malalamiko kuwa CCM na JK mwenye anakiuka maadili na sheria ya uchaguzi, kuzidisha muda, kutumia sms kuchochea na kukashifu, alifanya nini? si alihalalisha maovu hayo ya CCM maana ndio walomteua?
na sasa matisho yake kwa CDM nani hajui kuwa anatetea kulinda CCM iliyomteua?
umma unamtambua fika kwa porojo zake. akithubutu kuigusa CDM ataikimbia mwenyewe, hasira ya umma
 
Si rahisi kukifuta kama wanavyosema ingawa uwezo huo wanao. Kwanza litatokea vurumai kubwa la ndani na pia watapata political pressure nje kwa kufuta chama halali kinachokubalika na watu wengi (wanalijua hili). Pili, ningewasifu kama wangeweza kukifuta kwa kutimiza ahadi za CCM na CDM kwa pamoja, hii itadhoofisha ajenda za CDM. Lakini huwezo huu hawana sababu ya umbumbumbu na ulafi wa mali za umma. Imedhibitika kwamba, ukiwa mtu makini na kuwa na uchungu na nchi hii, CCM hawakupendi kabisa. Wapo wazuri ndani ya CCM ila wanabaki kwa roho ngumu tu, na sijawasikia wakipingana na CDM. Na ndiyo maana, watu makini hawaendi tena CCM, waliopo huko wanaondoka na mliobaki wachache muondoke. Labda cha kuwashauri hawa wenzetu, watoe boriti kwenye macho yao ndipo waweze kuona kibanzi kwenye macho ya wenzao Kumbe kelele za mlango zinaweza kukosesha usingizi, warekebishe mlango basi na siyo wavunje nyumba.
 
hana ubavu wa kufuta chama chenye nguvu kama cdm. Hamna mtz mwenye ubavu wa kufuta cdm. Huyo tendwa hata jimbo lake analokaa kawe linashikiliwa na cdm na kwao rombo mbunge ni wa cdm, atakimbilia wapi
 
wewe na huyo tendwa wako wote ni mambumbumbu! Wajarb waone kuwa watz ha2jalala km wanavyodhan. Kwnza 2na uchngu na maisha magum so ha2ogopi m2.
 
Never ever,,,haiwezekani hawa jamaa wanajaribu kutisha wananchi ili kutukatisha watu jamaa,,haya ni mawazo mufilisi na kamwe hawatadhubutu,,siku wakifanya hivyo ndio itakuwa mwisho wao,
 
Kauli za Ttendwa, msajili wa vyama vya siasa nchini wakati anahojiana na shirika la utangazaji tanzania,TBC ni za kuchochea kuvunjika kwa usalama na kuanzisha vurugu kwa makusudi ili kutimiza malengo ya kisiasa ya chama cha mapinduzi,CCM,kisha baadae kuhalalisha lawama zao dhidi ya chama cha ukombozi tanzania,CHADEMA.
Ttendwa aliyepewa dhamana ya kusajili vyama vya siasa kwa kuzingatia sheria zilizopo ndani ya katiba,sasa ameanza kutishia kubomoa ustawi wa vyama vya siasa ambavyo alivisajili kwa malengo kukidhi matakwa ya chama tawala.
Maneno na kauli za bwana,kama vitatekelezwa kwa vitendo vinaweza kuvunja amani na kuchochea vurugu zisizo na mwisho.
Jana Ttendwa akidhani kwamba anawafurahisha CCM,alienda mbali na kutamka kuwa anaweza kuchukua hatua za kukifuta CHADEMA kwa kile alichokiita UCHOCHEZI kwenye maandamano na mikutano ya hadhara.
Kama kauli kauli hii ilitokana na utashi wa Ttendwa mwenyewe bila ushawishi wa CCM,Ttendwa halitakii mema TAIFA letu,kama pia kama alishinikizwa kutishia kukifuta CHADEMA halitakii mema Taifa letu
Ni kitu ambacho hakiwezekani kukifuta chama cha siasa chenye ufuasi mkubwa wa mamilioni ya watu bila kusabisha vurugu nchini.Kukifuta chama cha siasa kikubwa ni mwanzo wa kuvunja usalama.
Uzoefu unaonyesha mahala popote dola ilipopiga maarufuku vyama vya siasa vilivyokuwa na ufuasi mkubwa mazingira ya amani yalitoweka katika nchi hizo.
Kufuta vyama vya siasa kama Ttendwa alivyoropoka jana,kunaweza kuwafanya watu wamiminike mitaani kufanya maandamano au kwenda msituni kupigania haki zao.Kwasababu Ttendwa ana amejikita katika kambi ya chama tawala,hili hawezi kulifikiria
Kauli za watu kama akina Ttendwa hazitakiwi kuvumiliwa wala kuachwa kana kwamba zina tija kwa Taifa.Tayari Ttendwa ameshaamusha hisia za chuki kwa wafuasi na wapenzi wa chama cha ukombozi,CHADEMA.
Kwa kuwa ni kweli kwamba kwa Ttendwa kutishia kukifuta CHADEMA,hali ya usalama inaweza kuwa mashakani,basi TTENDWA akamatwe kwa kauli za" uchochezi"
 
Kauli za Ttendwa, msajili wa vyama vya siasa nchini wakati anahojiana na shirika la utangazaji tanzania,TBC ni za kuchochea kuvunjika kwa usalama na kuanzisha vurugu kwa makusudi ili kutimiza malengo ya kisiasa ya chama cha mapinduzi,CCM,kisha baadae kuhalalisha lawama zao dhidi ya chama cha ukombozi tanzania,CHADEMA.
Ttendwa aliyepewa dhamana ya kusajili vyama vya siasa kwa kuzingatia sheria zilizopo ndani ya katiba,sasa ameanza kutishia kubomoa ustawi wa vyama vya siasa ambavyo alivisajili kwa malengo ya kukidhi matakwa ya chama tawala.
Maneno na kauli za bwana,kama vitatekelezwa kwa vitendo vinaweza kuvunja amani na kuchochea vurugu zisizo na mwisho.
Jana Ttendwa akidhani kwamba anawafurahisha CCM,alienda mbali na kutamka kuwa anaweza kuchukua hatua za kukifuta CHADEMA kwa kile alichokiita UCHOCHEZI kwenye maandamano na mikutano ya hadhara.
Kama kauli kauli hii ilitokana na utashi wa Ttendwa mwenyewe bila ushawishi wa CCM,Ttendwa halitakii mema TAIFA letu,kama pia kama alishinikizwa kutishia kukifuta CHADEMA halitakii mema Taifa letu
Ni kitu ambacho hakiwezekani kukifuta chama cha siasa chenye ufuasi mkubwa wa mamilioni ya watu bila kusabisha vurugu nchini.Kukifuta chama cha siasa kikubwa ni mwanzo wa kuvunja usalama.
Uzoefu unaonyesha mahala popote dola ilipopiga maarufuku vyama vya siasa vilivyokuwa na ufuasi mkubwa mazingira ya amani yalitoweka katika nchi hizo.
Kufuta vyama vya siasa kama Ttendwa alivyoropoka jana,kunaweza kuwafanya watu wamiminike mitaani kufanya maandamano au kwenda msituni kupigania haki zao.Kwasababu Ttendwa ana amejikita katika kambi ya chama tawala,hili hawezi kulifikiria
Kauli za watu kama akina Ttendwa hazitakiwi kuvumiliwa wala kuachwa kana kwamba zina tija kwa Taifa.Tayari Ttendwa ameshaamusha hisia za chuki kwa wafuasi na wapenzi wa chama cha ukombozi,CHADEMA.
Kwa kuwa ni kweli kwamba kwa Ttendwa kutishia kukifuta CHADEMA,hali ya usalama inaweza kuwa mashakani,basi TTENDWA akamatwe kwa kauli za" uchochezi"
 
Ndo hayo tanayoyasema mapungufu ya Katiba iliyopo. Unadhani mtu kama Tendwa asingekuwa ameteuliwa na serikali ya ccm angezungumza vitu alivyosema jana??

Mambo yote haya yaende sambamba na katiba MPYA. Ndiyo kiboko ya watu kama kina Tendwa itapatikana
 
Barua ya onyo iliyoandikwa na Tendwa kwa CDM ni ya kiuonevu na inavunja misingi ya utawala bora.

Nasema hivyo kwasababu katika sakata hilo Tendwa ndiye mlalamikaji na wakati huo huo hakimu.

Ili haki itendeke Tendwa anapashwa aachie ngazi kwa muda, apatikane mtu hasiyekuwa na upande, na Tendwa awasilishe tuhuma zake kwake na vielelezo vya ushahidi alivyonavyo. Halafu na CDM kwa upande wake ipewe fursa ya kujitetea ndipo uamuzi utolewe.
 
Wana jf napenda tu kutoa ushauri wangu kwa Mzee wetu Tendwajinsi alivyoongea jana ni vizuri Kama msajili wa vyama asiegemee upande wa chama chochote kwa kauli ya jana watu wengi walimwona ameegemea upande wa ccm anatakiwa kusikiliza kwanza kabla hajatoa tamko lolote kwa tamko lake kweli kila mtu kutoa wanaccm wanasema kufutwa kwa chadema ndo kutatokea maafa au kutoweka kwa amani Tanzania nasema hivo sababu watu wengi sana mitaani kila mahali Tanzania wanaongelea hicho.
Hilo ni ombi langu.
 
Kwa nini aswaite hao viongozi wa Chadema wajadili hizo kauli za uchochezi? Sababu kukifuta chama ni hatua ya mwisho.
Siasa zinaonekana kuwa ni ngumu sana nchi hii, sababu kama chadema wanapita kwa wananchi kuwaeleza sababu za maisha yao kuwa magumu, na wananchi kila mtu kwa nafasi yake anaona huo ugumu wa maisha chadema watafanya nini zaidi ya kutumia hiyo point kuishutumu serikali ya ccm ambayo ipo madarakani karibu miaka 50? Hilo si ndio lengo la vyama vya upinzani?

CCM wanatakiwa wakae chini wajibu hoja, warudishe imani ya wananchi kwao kwa kuonyesha mikakati ya kupunguza ukali wa maisha wameipangaje na wanatekelezaje, wakifanya hivyo chadema hawatakuwa na point katika hilo
 
Hivi ni nani wa kumfukuza kazi John Tendwa? Hafai kuwa msajili wa vyama vya siasa. Aende kujiunga na Mafisadi CCM.
 
CDM kupitia kwa Kimesera wamesema wameijibu barua hiyo na wanamtaka athibitishe tuhuma zake dhidi ya CDM,mi namsubiri kwa hamu aje na huo uthibitisho!
 
Tendwa ametoka kupiga kinywaji nafikiri akili yake imejaa ulevi subutu uone kama hatutaingia msitumi we mwehu nini
 
Wana jf napenda tu kutoa ushauri wangu kwa Mzee wetu Tendwajinsi alivyoongea jana ni vizuri Kama msajili wa vyama asiegemee upande wa chama chochote kwa kauli ya jana watu wengi walimwona ameegemea upande wa ccm anatakiwa kusikiliza kwanza kabla hajatoa tamko lolote kwa tamko lake kweli kila mtu kutoa wanaccm wanasema kufutwa kwa chadema ndo kutatokea maafa au kutoweka kwa amani Tanzania nasema hivo sababu watu wengi sana mitaani kila mahali Tanzania wanaongelea hicho.
Hilo ni ombi langu.

usiwe na wsiwasi sidhani kama alikuwa nakili timamu ni pombe sana huyu
 
Back
Top Bottom