CHADEMA na tishio la Tendwa kukifuta Chama kisa Maandamano/M4C

Wakumbuke wakikifuta chama wananchi watakataa. Hivyo inabidi wayatatue kwanza yanayolalamikiwa na Chadema watanzania wapate nafuu ya maisha alafu wawategee wananchi wakiwa wamesahau uchungu wa haya maisha ndiyo wakifute Chama lakini kwasasa watanzania wengi hawana cha kupoteza kwenda barabarani
 
Itategemeana sana na sababu zitolewazo na pande zote mbili, juu ya kuingia barabarani ama kuafiki chama mojawapo kifutwe.
 
We acha hizo nao wanaakili hawatadhubutu kwani Jay wa K anajua hatukumchagua na waTZ wameamka hawatakifuta na wakijaribu utaona waTZ wa 2010 - 2015 wakoje. Wee juzi January sukari 1kg Tsh.1400/= sasa Tsh.2000/= Sembe 1kg. Tsh.400 sasa Tsh.600 halafu wale wanaosema ukweli wafutwe Mtanzania gani atakubali na kukaa kimyaa??? Labda matajiri wa CCM nao ni wachache mnoooooooo!
nauli ya daladal nayo imeshapanda
 
Huwezi kufuta harakati,

Huwezi kufuta mwamko,

Huwezi kufuta mienendo na misukumo mbalimbali kwenye jamii inayopelekea mabadiliko..

Huwezi kumzuia mtoto asibalehe... na kufikia utu uzima

Huwezi kuizuia Tanzania ibalehe...

CCM wanashindana na yote haya...are they right in th mind?

Katika hayo unachofuta ni nini ....Jina au Magwanda...???

CCM waache mambo ya kitoto, wajikosoe, watumie busara wajiunge na chadema na kuipitisha nchi kwenye mageuzi ambayo ni muhimu na yalazima kijamii!!!

CCM show your maturity ...and save the Nation!!!
 
Ni ngumu mkuu wala cdm hakifutwi kwani hakijafanya kosa lolote kikatiba. Achana wa wale mburura sisiemu wahahe tu!
 
wanangu chama cha siasa sio kipande cha karatasi cha a4 ambacho tendwa ameweka saini.
Aidha chama ni cha watu wenye mlingano sawia waliosukumwa na itikadi ya chama hicho ima mbaya au nzuri.
Hivyo basi itikadi huwezi kuifuta kwa ufutio bali hufutwa kwa itikadi mbadala. mf; CDM inaweza ikajifuta yenyewe ikibadili itikadi na kuwa chama cha kutetea ufisadi.
Chama cha siasa chochote kazi yake ni uchochezi, Kuchochea fikra mpya/mbadala vichwani mwa watu, ili waiangushe serikali iliyo madarakani. na sio kukipamba chama tawala.
Mamlaka ya kufuta Itikadi tendwa huna.
 
HBakifutwi ni vitisho tu , nani anaweza kuufuta umma? CDM ndio huo umma wajaribu tu waone moto pple wate go street mimi nikiwa mmoja wapo. CCM ni mburura tu na hao vibaraka wao Tendwa, Mrema, Cheyo na wewe uliyekuwa na Tendwa
 
Wakifute tu kwani wale wa-egypt au watunisia waliwatoa madarakani madikteta wa nchi zao kwa kuunganishwa na chama? Azma yetu iko pale pale hata wakiifuta cdm lazima tuwang'oe manyang'au ccm!
 
Very true,
Binafsi asbh ya leo nimekutana na kuongea ANA KWA ANA na mh. Tendwa, na amenieleza hivi (very briefly)
  • Ya kwamba chadema walishapewa ONYO toka kwa msajili juu ya nyendo za kufanya siasa.
  • Ya kwamba kusiwepo na cheche zenye muamsho wa kuvunja amani.
  • Kwamba...hatosita kukifuta chama hicho.
  • Ameshawaita na kuwaeleza jinsi ya kufanya siasa, mwendo wao utaangukia mrama
  • Anatambua kuwa inapata misaada toka Germany na mwezi uliopita wajerumani walikuwepo nchini.
  • Anatambua wanapata msaada toka chama cha Republican cha USA.
  • Anajijua kuwa kwa kipindi hiki anawindwa sana.
  • Ameshawahi kuvifuta vyama vya siasa na hashindwi kukifuta chama hicho.
  • Kuna mambo mengi akiainisha 'criminal offense' juu ya chama hicho, ila ameshawaandikia ONYO kali.
Kwa ufupi ni maongezi yangu binafsi nae mheshimiwa juu ya suala hilihili na ni ya ana kwa ana, source ni MIMI MWENYEWE MPEVU. Jana pia walikuwa TBC1 kuweka sawa mambo hayahaya.

em toeni propaganda hapa. kama vipi kamsaisieni chiligati kazi kabisa tujue1. kama chadema kikifutw si wafuasi tunabaki na itikadi zake!! kwani itikadi nazo zinafutwa?? hivi mu watu gan msokua na uchungu na hii nchi.??
 
Hiyo ni ndoto ya mchana, kufuta CDM ni ngumu kama ilivyo vigumu kwa ngamia kupenya katika tundu la sindano!

Unajua hawa sisiemu sasa WANAHAHA wanajua fika kuwa mwisho wao 2015 umewadia.

kwanza hawana mgombea yeyote anayekubalika 2015 na wamepoteza mwelekeo kabisa sasa homa imeshapanda na presha iko juu saaana.

Wamekwisha sasa wanataka kutumia ubabe kuzima nguvu ya uma hapo wameteleza.

CDM itadumu daima
 
TENDWA report ya matumizi ya vyama ktk kampeni 2010 Umesha itoa kwa wananchi?miezi mingapi sasa inaisha?badala ya kufanya kazi uliyoajiriwa nayo wewe unatumiwa kama tiara!natumai kwenye katiba mpya ofisi yako tutaiondolea mbali
 
nani atakayethubutu kukifuta Chadema???
wadanganyeni serikali yako yote ikose misaada wanayoikimbilia.
Kama serikali ingekuwa safi na kuthibiti matumizi mabaya ya pesa basi wasingekuwa wanategemea pesa za wahaisani na hapo wanagekuwa radhi hata kufuta kila chama watakacho,lakn bila hivyo hilo sio rahisi kabisa.
 
hao ni mamluki tu hivyo wapotezee
em toeni propaganda hapa. kama vipi kamsaisieni chiligati kazi kabisa tujue1. kama chadema kikifutw si wafuasi tunabaki na itikadi zake!! kwani itikadi nazo zinafutwa?? hivi mu watu gan msokua na uchungu na hii nchi.??
 
Tukumbuke......mwili unaweza kufa bali roho huishi milele.

Chadema (mwili) kinaweza kufutwa lakini azma ya umma (roho) ya kutaka ukombozi itaishi milele.

Infact, azma hii itahuishwa zaidi pale Chadema kitakapofutwa - kosa ambalo watawala wataja kulijutia milele!!
Ukisema Chadema=Uma unakosea,maana Uma ni Watz wote sasa ckukubalii kwamba Watz wote ni Chadema,nyie wanachadema ndio mtajiju na hao wajerumani na wamarekani wenu kama alivyoeleza Mh hapo juu
 
Hata wakifuta cdm, mbegu walizopanda za mwamko wa kisasa miongoni mwa watanzania, na hasa vijana zitaendelea kumea
 
Kwa hali iliyopo ni dhahiri chadema kinaweza kufutwa na viongozi wake kuwekwa ndani kama wahaini. Ccm wametoa tamko, msajili katoa tamko. Hivyo ni dhahiri chadema haina muda duniani. Nachouliza sie wapenzi wa CDM Tuhamie chama gani baada ya hapo.

Atakayeifuta CHADEMA ndiye anayetakiwa kutafuta nchi pa kukimbilia. hilo halina siri na wala halihitaji mjadala.
aanze kwa kuifuta CCM kwa kuangamiza maelfu ya wanawake na watoto kwa magonjwa, umaskini, ufisadi na kuchochea udini.... wathubutu!
 
Very true,
Binafsi asbh ya leo nimekutana na kuongea ANA KWA ANA na mh. Tendwa, na amenieleza hivi (very briefly)
  • Ya kwamba chadema walishapewa ONYO toka kwa msajili juu ya nyendo za kufanya siasa.
  • Ya kwamba kusiwepo na cheche zenye muamsho wa kuvunja amani.
  • Kwamba...hatosita kukifuta chama hicho.
  • Ameshawaita na kuwaeleza jinsi ya kufanya siasa, mwendo wao utaangukia mrama
  • Anatambua kuwa inapata misaada toka Germany na mwezi uliopita wajerumani walikuwepo nchini.
  • Anatambua wanapata msaada toka chama cha Republican cha USA.
  • Anajijua kuwa kwa kipindi hiki anawindwa sana.
  • Ameshawahi kuvifuta vyama vya siasa na hashindwi kukifuta chama hicho.
  • Kuna mambo mengi akiainisha 'criminal offense' juu ya chama hicho, ila ameshawaandikia ONYO kali.
Kwa ufupi ni maongezi yangu binafsi nae mheshimiwa juu ya suala hilihili na ni ya ana kwa ana, source ni MIMI MWENYEWE MPEVU. Jana pia walikuwa TBC1 kuweka sawa mambo hayahaya.

Wewe na Tendwa ni ZERO
 
Back
Top Bottom