Tanzania hakichaguliwi chama anachaguliwa kiongozi. Mifano ni mingi tu, haina haja ya kuirudia.
Chadema haitoweza kushinda uchaguzi wa Urais nchi hii ikimsimamisha Slaa au Mbowe
Au umchukuwe Slaa akagombee ubunge Uzini si itakuwa kiroja
Nadhani maana yako ni kwamba hakichaguliwi chama bali MGOMBEA, kwani ni wanasiasa wachache sana ndani ya CCM kwa mfano wenye sifa za kuitwa viongozi, ndio maana hata vijiweni tunaitana 'vipi kiongozi', kwani dhana ya uongozi ndani ya CCM baada ya kuondoka Mwalimu and to an extent Mkapa ni vituko kuliko mantiki. Vile vile hoja yako hii inatoa ishara kwamba nguvu ya CCM sio itikadi au sera bali viongozi waliopo na jinsi gani wanatumia mamlaka ya uongozi na taasisi zake kukifanya CCM kiwe na nguvu;
Kauli hii kidogo ina utata kwani haujaifafanua kama una maanisha ushindi wa kwenye sanduku la kura au ushindi wa mezani, au iwapo Slaa na Mbowe hawana mvuto kwa wananchi au iwapo Chama tawala hakipo tayari kuona hawa wawili wakishika madaraka ya nchi; yote haya yanajadilika, ila ukiwa wazi zaidi;
Hii hoja sijaelewa maintiki yake ni nini hasa, je inahusiana na mjadala wetu kuhusu LOCALISM? Vinginevyo hata Lowassa, Pinda, Membe, Mwandosya, Migiro, wote hawa hawezi kushinda ubunge jimbo la Uzini;
Hoja zako ni nzuri sana Mchambuzi. Kama ulivyoainisha kuwa iwe mahali pa CDM kujipanga wakati wa kuelekea 2015, ni vyema pia tukatafakari kwa kina yaliyotokea kwenye uchaguzi uliopita.
Hivi leo tukijiuliza, ilikuwa je, Maalim Seif S Hamadi ashindwe kura za Urais Visiwani, na wakati huo huo Prof Lipumba amshinde JK kwenye kura za Urais za Visiwani?
Kila ninapo tafakari hili, linaniondolea uwanja tambarare wa kusema kweli hizi margins za ushindi wa JK dhidi ya Slaa zilikuwa sahihi. Je, Kweli Lipumba alikuwa Maarufu kuliko JK visiwani na wakati huo huo Shein akawa Maarufu kuliko Hamadi visiwani?
Lkn kama ulivyosema, kwa kuwa hakuna data inakuwa vigumu kuyafanyia kazi. Hii inanikumbusha pale Mzee wa Mapesa alipokosa hata kura za familia yake ya karibu sana (mkewe na wanawe) katika kituo chao cha nyumbani!
Kutukuka synonym yake ni tukufu; sio sahihi kusema Kikwete ni mtukufu, kwanini unaenda mbali hivyo, au kwa sababu ni rais wa sasa? na atakaekuja 2015 akiwa wa CCM atakuwa mtukufu pia au sio? Na Kikwete ataendelea kuwa mtukufu au utukufu wake utaisha na urais wake? nielewavyo mimi utukufu hauna kikomo, kwahiyo ni vyema ukatafuta namna nyingine ya kumuelezea Rais kikwete, kwani nina uhakika hata yeye neno mtukufu asingelipenda;Tanzania hachaguliwi mgombea kwa kuwa ni mgombea tu, watu huchakuwa kiongozi wao. Kama unachaguliwa mgombea kama unavyotaka iwe, kwanini asichaguliwe Slaa kuwa Rais? si na yeye alikuwa Mgombea? au kwanini asichaguliwe Mbowe uchaguzi wa 2005? nae si alikuwa mgombea? Naam, Watanzania wengi hawakusita kumchaguwa kingozi wao waliyejuwa atawaletea mabadiliko ya ukweli nae anafanya kweli. Jakaya Mrisho Kikwete, kiongozi wa kutukuka.
Ushindi wa Kwenye sanduku la kura na ushindi wa mezani ndio nini? Mimi naelewa watu wanapiga kura zinahesabiwa anatangazwa mshindi. Sanduku la plastic linatumika kubebea kura, meza zinatumika kura zinapohesabiwa.
Maana ya neno kiroja ni kitu kinachozaa hisia za mshangao; sasa cha kushangaza Slaa akishinda huko ni nini, kwamba yeye ni mkristo? Mbara? hoja yako hii inaelekea kwenye mjadala usiokuwa na tija;Hapana, siongolei "localism" naongelea kiongozi ambae wataona anafaa wapiga kura wa Uzini hususan kwa maadili. Ndiyo maana nikasema ukimpeleka Slaa kugombea "Uzini" kitakuwa ni "kiroja". Kitongoji cha "Uzini" nimekichaguwa kwa maana yake na ndio maana sikusema Micheweni au Kwa Mtipura, na hakihusiani na hayo majina mengine yote uliyoyaweka.
Kutukuka synonym yake ni tukufu; sio sahihi kusema Kikwete ni mtukufu, kwanini unaenda mbali hivyo, au kwa sababu ni rais wa sasa? na atakaekuja 2015 akiwa wa CCM atakuwa mtukufu pia au sio? Na Kikwete ataendelea kuwa mtukufu au utukufu wake utaisha na urais wake? nielewavyo mimi utukufu hauna kikomo, kwahiyo ni vyema ukatafuta namna nyingine ya kumuelezea Rais kikwete, kwani nina uhakika hata yeye neno mtukufu asingelipenda;
Kuhusu Kikwete kuwa kiongozi wa kweli kwa mtazamo wa wananchi, hilo kwa kweli sifahamu; nachofahamu ni kwamba nikiwa kama mwana CCM 2005 tuliweza kupata 80% ya kura, lakini five years later tukapata about 61% ya kura; kama tuna nia ya dhati ya kujenga chama chetu cha CCM ni muhimu tuache ushabiki wa kutukuka na kufanyia kazi takwimu hizi ili tujue tulikosea wapi, na turekebishe maeneo gani katika kipindi hiki kilichosalia cha miaka mitatu;
I raised hizi issues kutokana na hoja yako kuwa ya kuchanganya kidogo i.e. kuhusu Dr. Slaa na Mbowe hawawezi kushinda; haikuwa na ufafanuzi na bado haina ufafanuzi; vinginevyo kushiriki katika GAME kwa attitude kwamba fulani hawezi kushinda ni strategy mbaya sana; the right strategy ni kuchukulia kwamba hapa ushindi ni 50/50, hii itakusaidia kujipanga badala ya kuhamaki na pengine kuleta madhara pale utakaposhindwa.
Maana ya neno kiroja ni kitu kinachozaa hisia za mshangao; sasa cha kushangaza Slaa akishinda huko ni nini, kwamba yeye ni mkristo? Mbara? hoja yako hii inaelekea kwenye mjadala usiokuwa na tija;
Kikwete ni kiongozi aliyetukuka, ukipenda meza hukupenda tema. Jee, kuna tatizo Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ni Mtukufu? Huujuwi Utukufu wa kuwa Rais ndiyo maana unapata shida na hilo neno.
Slaa na Mbowe wameshabwagwa vibaya sana na Kikwete, kila mmoja kwa wakati wake, na hao si "Chaguo la Mungu".
Slaa na Uzini ni kiroja, la hasha si kwa dini zao, hukusoma neno "maadili" katika post ile? usitake niseme kuwa una macho lakini hayaoni.
Kabla sijaendelea na mchango wangu mdogo kuhusu hii mada, nimekutana na hii na nimeona bora niiseme kwa mujibu wa ufahamu wangu au nielezwe kaam sivyo ilivyo.Kuhusu swali lako la kwanza, uchaguzi huru ukija leo, bado CCM itashinda kwa sababu, again and again huwa nasisitiza umuhimu wa Chadema kulitazama upya suala la kanuni ya uchaguzi kwamba mshindi ni mshindi; kwani kwa jinsi hali ilivyo leo, CCM (Kikwete) akishinda tena leo kwa 50.9% na Chadema (Dr. Slaa) kwa 49.1%, kwa kanuni ya mshindi ni mshindi, CCM itaibuka kidedea tena; ushindi wa Chadema sana sana utakuwa uundwaji wa serikali ya pamoja kwama ile ya CUF na CCM Zanzibar; ;
Ushindi wa Kwenye sanduku la kura na ushindi wa mezani ndio nini? Mimi naelewa watu wanapiga kura zinahesabiwa anatangazwa mshindi. Sanduku la plastic linatumika kubebea kura, meza zinatumika kura zinapohesabiwa.
Hu mfumo unaendeshwa na katiba na sasa hivi kuna mchakato wa kubadili katiba. Usijidanganye kuwa kubadili chama ndio mwisho wa matatizo. Vyama vipya na hususan chama chenye mfumo kama wa chadema havifai kabisa, unaona wazi kabisa kuwa viongozi wa chadema hata maadili hawana, halafu unategemea lipi jema kutoka kwao?
Unaona kabisa jinsi wanavyoongea, wanavyosambaza chuki mpaka wanafikia kusema wazi kabisa kuwa hii nchi "haitatawalika" halafu bado unafikiri kuwa wao watakuwa bora? huo ni ufinyu wa mawazo. Nyota njema huonekana alfajiri. Chadema hawana madaraka ya nchi tunaona damu zikimwagika kila wanapopita wakishika madaraka jee?
Kwanza wasahau kupewa madaraka kwa kura, za nani? msidanganyike.
Mchambuzi,
Mkuu wangu samahani kidogo sikupata kukuelewa vizuri... Ulipotoa mifano ya jimbo la Zitto, Mbowe na Dr.Slaa (as the big three) Kisha kuonyesha ushindi wa wabunge hao lakini sio Dr. Slaa ktk kiti Urais inanipa taabu kidogo zinapokutana.. Je, una maana kwamba Chadema hawana mtu zaidi ya Dr.Slaa (kama madai ya Sitta) aliyeshindwa na JK ,au Dr.Slaa hakufaa angekuwa mtu mwingine pengine Chadema wangeshinda ktk majimbo hayo kutokana na kwamba wabunge wake walishinda au JK ni zaidi ya Dr.Slaa...
Mimi binafsi napata shida sana kuamini Popular vote vinavyotumika hasa pale wananchi walipoichagua Chadema kutokana na msukumo wao ktk mageuzi ilihali wakijua kwamba kwa kuichagua Chadema serikali ya CCM itakwaza maendeleo yao kama walivyokuwa wakijitangaza ktk ilani zao za Uchaguzi.. CCM walisema wazi mkiwachagua Chadema mtakosa maendeleo na bado watu hawa wakamchagua mbunge mgombea wa Chadema, sasa nashindwa kabisa kuunganisha wala kuelewa mtu alomchagua Mbunge wa Chadema lakini akamchagua rais kutoka CCM akijua hatapata maendeleo au labda walidhani JK na CCM ni vitu viwili tofauti?...hii kidogo inanipa shida kuelewa japokuwa sipo vichwani mwa hawa wananchi ambao ndio tunataka kuwalaumu na sio chombo kinachohusika na uchaguzi..
Nafikiri yaliyotokea mwaka 2010 hayawezi kuwa na majibu sahihi hasa baada ya kulazimishwa kukubali matokeo. Kama tulivyolazimishwa kuamini mkataba wa Richmond na Dowans haukuwa na matatizo au swala la rada..Na binafsi yangu nisingependa hata kuwazia kilitokea nini maana NDIVYO TULIVYO...
Nakumbuka tuliwahi kufanya hivyo baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 na nilipigwa vita wala sii mchezo lakini mwisho wa siku Chadema ilimsimamisha Dr.Slaa kama nilivyokuwa nikisema japokuwa nilichukiwa sana mwanzoni na wapambe halafu Mbowe mwenyewe ndiye aliyependekeza kwanza kumsimamisha Dr.Slaa..Mkuu Mkandara,
Asante kwa mchango wako. Kuhusu suala la wabunge wa Chadema kushinda kura za ubunge majimboni kwao lakini kushindwa kumsaidia mgombea wao wa urais humo humo jimboni kwao kwa kweli hata mimi limeshindwa kuingia akilini, na ni moja ya sababu moja kubwa kwanini nimekuja na mada hii; nashukuru umeliona hili suala kwamba halijakaa vizuri tofauti na wengine ambao mtazamo wao ni tofauti sana, hasa wakijaribu kulitolea ufananuzi kuliko kujikita katika kuangalia kama mapungufu yapo ili kulitafutia ufumbuzi wa kwa siku za huko mbeleni;
Nilipendekeza nadharia tete mbili katika original post yangu (rejea post hiyo sehemu za mwishoni) kama njia ya kuchokoza mjadala ili pengine tuweze kubaini mwenendo wa wapiga kura tanzania katika hili upo vipi; Vinginevyo nia yangu nyingine ya kuja na mada hii ni kujaribu kutafuta majibu juu ya hoja hizi hizi za wengi wetu humu kwamba matokeo ya 2010 hayakuwa halali kwahiyo uchambuzi wake nao ni batili; kwa mtazamo wangu, tukifany akazi backwards katika takwimu hizi, tutaweza kugundua mapungufu mengi sana ambayo yatasaidia kubaini pengine ni wapi ndio kura zilichakachuliwa; bila ya kuchambua mwenendo wa wapiga kura na matokeo katika majimbo mbalimbali, hatutaweza kufanikisha lengo hili, vinginevyo ni imani yangu kubwa kwamba ni dhahiri hatutapata majibu ya mia kwa mia lakini angalau tutapata mwanga juu ya suala husika;
Ukipata muda naomba uangalie nadharia tete zangu mbili ambazo sana sana ni za uchokozi lakini nina imani zitatusaidia kuchambua na kubaini mengi;
Mchambuzi sijui kwanini mimi napata shida sana kuwalewa watuw anaosema "itikadi bora na sio bora itikadi? Kwani ni dhahiri kwamba kwa Sasa Chadema hawana itikadi bora, bali bora itikadi; ". Hii dhana imesambaa sana humu ndani.Ila naamini ukitoka na kumuuliza mwanaCCM wa kweli kuhusu CDM halfu umwambie hicho hapo juu atakuambia ukweli...Wengi wao wanajaribu kwepesha ukweli kwa kusema "...ni wazuri sana ila Vurugu..." au kingine kinachofanana na hicho amabye yeye ndio kamezeshwa.Mkuu Kobello,
Nashukuru kwa mchango wako; unaposema kwamba wapiga kura tanzania hutazama personalities kwa sababu vyama havina itikadi zinazoeleweka wazi, lakini hasa zinazouzika kwa wananchi walio wengi, nakubaliana na wewe kwa hili mia kwa mia; lakini pale Dr. Slaa anaposema kwamba kwa kawaida Chadema inajadili masuala na sio watu, kwa mtazamo wako, Chadema ifanye nini kuboresha kile anacholenga kukijenga Dr. Slaa, hasa katika mazingira ya itikadi bora na sio bora itikadi? Kwani ni dhahiri kwamba kwa Sasa Chadema hawana itikadi bora, bali bora itikadi; same applies to CCM;
Nimependa pia hoja yako kuhusu mwamko wa wapiga kura uchaguzi wa 2005, kwani unazidi kushindilia hoja yako kwamba mwenendo wa wapiga kura wengi Tanzania ni kuchagua WATU, na sio chama wala masuala yanayosimamiwa na Chama; Kuna ukweli katika hili, lakini je, nini mtazamo wako kuhusu upigaji kura kwa wabunge kwa vigezo nilivyojadili vya LOCALISM vis-a-vis vigezo vya NATIONALISM kwa nafasi ya Urais?
Mimi hapa nitazungumzia dhana tu lakini kwa mujibu wa uzoefu wangu.
Katika hali ya kawaida ya kibinadamu na kisaikolojia, pia kwa kuzingatia unazi wa Watanzania kwa vyama vyao; na ingawa mwananchi ana uhuru wa kuchagua kile anachokipenda, si rahisi kwa mtu wa jimbo hilo hilo, akapewa karatasi za wagombea wa uraisi, ubunge na udiwani, akatia kura kwa mgombea wa chama tafauti katika kila karatasi.
Ninachotaka kusema hapa, na hii narudia tena kuwa ni dhana yangu tu kwa sababu niliyoeleza hapo juu, hatuoni kama kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Dr. Slaa kushinda kwenye majimbo ya Kigoma Mjini, Hai na Singida, lakini Kikwete akaibuliwa mshindi kwa uchachakuaji wa matokeo?
Just thinking aloud.
Nitarejea baadaye kwa mchango wa kina ambao hautakuwa umeathiriwa na wasiwasi wangu wa hapo juu.
Mna nafasi nzuri huko CCM za kuleta mabadiliko ili na sisi tuwe na ushindani thabiti dhidi ya upinzani lakini mnadhania mnayoyafanya ni mnakijenga chama kumbe mnakibomoa. Mkija shtuka, hasa uhalisia wa mambo utakapo kick in, tayari itakuwa ni too too late; Sisi vijiweni huku tunaendelea kukipigania chama kwa mwendo mdogo mdogo na tunafanikiwa kujijengea heshima, huku pia tukikilinda chama katika vicinity zetu, na for some reasons, hao hao mnaowatukana wanatuheshimu, wapo tayari kujenga taifa kwenye maeneo yaliyo over and above siasa za vyama kwa kushirikiana na sisi ingawa tupo vyama tofauti kwani wanatutofautisha sana na wengi ya waliopo jikoni;
Ingekuwa busara sana kama mngeweka sura zenu na majina yenu mjulikane kuliko kujificha na majina na picha za uongo; vinginevyo kila la kheri huko jikoni mkuu;
Mchambuzi sijui kwanini mimi napata shida sana kuwalewa watuw anaosema "itikadi bora na sio bora itikadi? Kwani ni dhahiri kwamba kwa Sasa Chadema hawana itikadi bora, bali bora itikadi; ". Hii dhana imesambaa sana humu ndani.Ila naamini ukitoka na kumuuliza mwanaCCM wa kweli kuhusu CDM halfu umwambie hicho hapo juu atakuambia ukweli...Wengi wao wanajaribu kwepesha ukweli kwa kusema "...ni wazuri sana ila Vurugu..." au kingine kinachofanana na hicho amabye yeye ndio kamezeshwa.
Si kweli watu wanavyoamini kuwa Tanzania watu wanachagua Mtu na si chama .Ukweli ni kwamba CDM iliplay role kama brand by itself na hivyo kuwabeba wabunge wake wengi sana.Tofauti na JK kama JK kipindi cha kwanza aliwabeba sana wabunge wa CCM kwa ule upepo wa umaarufu alioanza nao.
Mchambuzi huwezi amini hizo sababu nilizokupa mapema kabisa ni very real zaidi ya unavyoweza dhani.Hizo factors ukiziweka kama equalizer ,halafu kila parameter ipande na kushuka kama ilivyochangia kuongeza kura kwa mshindi kwa kila jimbo ,utashngaa sana.Kwani ni sehemu chache sana zitakuwa na additional parameters.Ni vitu niliobserve mikoa karibu nane niliykuwepo kabla ,kipindi cha kura na baadaye.Niliongea na watu wengi sana kila nilipokuwepo.Si habari ya kufikirika.
Pia nimesikia watu wakilalamikia CDM kuchelewa mtangaza mgeombea,kwa CDM ilikuwa ni strategy ya kuwasurprise CCM, na ilifanya Kazi vizuri sana.Waliwashangaza kuwa alikuja mtu mpya na hawakuwa na options nzuri sana kwani wamefanya nae kazi kwa karibu na kumkubali.Na after shocks bado zinawatafuna sana CCM.CCM walikuwa wameandaa rundo la scandles za kuzusha wakidhani atakuwa Mbowe kwa vile walikuwa na taswira ya CUF,TLP,NCCR.Mbowe kawa Free kutanya kazi nyingine muhimu kwa chama.
Mchambuzi,
..JK tayari alikuwa Raisi, kwa hiyo ni vigumu mgombea kama Slaa, out of nowhere, kuweza kumpiku.
..kitu kingine kilichomsaidia JK ni MTANDAO mkubwa wa CCM uliopo vijijini, rasilimali watu[watumishi wa serikali, polisi, wasanii, jumuiya za chama, waandishi wa habari] pamoja na FEDHA nyingi zilizotumika wakati wa kampeni.
..pia sina uhakika kama timu ya kampeni ya CDM ilikuwa inaielewa vizuri saikolojia ya wapiga kura. kwa mtizamo wangu, wapiga kura wa Tanzania, kutokana na umasikini wao, wana-respond vizuri zaidi kwa mgombea mwenye kutoa ahadi lukuki aliyokuwa akifanya JK. naamini kulikuwa na kiasi fulani cha mapungufu ktk campaign message ya CDM as it relates to uelewa na matamanio ya wa-Tanzania.
..mwisho, naomba nieleze kwamba CDM had a better candidate compared to CCM. Hata CUF walikuwa na mgombe mweledi zaidi kulinganisha na yule wa CCM. Hicho ndicho kilichopelekea CCM kukwepa kushiriki kwenye mdahalo wa wagombea Uraisi. In the future, CDM waangalie their campaign message, pia wahakikishe wana mtandao mkubwa, na zaidi wawe na fedha na vitendea kazi kwa ajili ya kampeni.