Chadema na Mwenendo Wa Wapiga Kura Tanzania

Mchambuzi

JF-Expert Member
Aug 24, 2007
4,850
9,405
Kilichonipa hamasa kuja na mjadala huu ni kauli ya hivi karibuni ya Katibu Mkuu wa Chadema Dr. W.P. Slaa aliyoitoa kama sehemu ya majibu yake kwa Mzee Samuel Sitta aliyetoa kauli kwamba ‘Chadema haipo tayari kuongoza nchi kwa sababu bado hakina hazina ya kutosha ya viongozi'. Katika majibu yake kwa Mzee Sitta, Dr. Slaa alitamka yafuatavyo (nanukuu):

["Leo nalazimika kumzungumzia MTU, Watanzania wanajua mara chache sana CHADEMA huwa tunalazimika kuzungumzia WATU badala ya MASUALA…"].

Dr. W.P Slaa, August 2012

Nia yangu leo SIO kujadili suala la Dr. Slaa na Mzee Sitta; nimenukuu tu sehemu ya maneno ya Dr. Slaa in order to set this discussion in its context. Kwa ujumla wake, mjadala wangu utalenga zaidi kwenye kujadili mwenendo wa kisiasa, hasa chaguzi katika nchi yetu kutokana na ukweli kwamba ushindani wa kisiasa pamoja na mikakati inayotumiwa na vyama vingi nchini wakati wa kampeni za uchaguzi ipo centred zaidi on PERSONALITIES rather than ISSUES; Nadhani sote tunaelewa madhara ya mwenendo huu katika demokrasia ni yepi, hivyo ni muhimu kumpa Dr. Slaa pongezi kwa kuchukua hatua za kuondokana na hilo, kama kiongozi wa kitaifa wa chamakikuu cha upinzani Tanzania. Moja ya mambo makubwa yanayo dhoofisha demokrasia nchini Tanzania ni pamoja na uwepo wa ‘OMBWE LA ITIKADI' miongoni mwa vyama vyote vyasiasa (pamoja na chama tawala - CCM), jambo ambalo linapelekea wananchi wengi kuchagua viongozi kwa vigezo vilivyo nje kabisa ya MASUALA yanayozunguka maisha yao (hasa kiuchumi na kijamii), na badala wanatumia vigezo vya UTASHI/HAIBA YA WAGOMBEA, Mazoea,Ukabila, Udini, Ubaguzi wa Jinsia n.k.

Specifically,nitajadili Siasa za ‘MASUALA' vis-à-vis Siasa 'WATU' kwa kutumia ‘reference' yamambo yaliyojiri' katika Uchaguzi Mkuu wa Rais na Wabunge (2010). Katika tazamatazama zangu, nimegundua uwepo wa ‘DISCREPANCIES' kubwa sana kwenye matokeo huko majimboni baina ya washindi ngazi ya Urais [kwenye kura za Rais majimboni] dhidi ya washindi katika ngazi za Ubunge kwenye majimbo mbalimbali. Nitalifafanua hili baadae kidogo. Ni matarajio yangu kwamba mwisho wa siku, sote tutaoshiriki katika mjadala huu tutafanikiwa kujifunza mambo mengi baada ya kubadilishana mawazo, experience, lakini kwa nia ya kujenga na sio kubomoa, kwani hivyo ndivyo tutaweza kuimarisha demokrasia nchini Tanzania.

Let me declare at the outset kwamba mimi ni Mwanachama wa CCM ninayeamini katika demokrasia ya kweli, lakini muhimu zaidi, ninayeamini kwamba: BILA CHADEMA MADHUBUTI, CCM MAKINI HAIWEZEKANI.

Katika mjadala wangu, nitafanya ‘reference'kwa kwenye majimbo kumi na tano ambayo Chadema ilishinda viti vya ubunge kwenye uchaguzi uliopita (2010):

  • Ilemela;
  • Ubungo;
  • Singida Mashariki;
  • Nyamagana;
  • Arusha Mjini;
  • Ukerewe;
  • Moshi Mjini;
  • Kawe;
  • Hai;
  • Mbeya Mjini;
  • Karatu;
  • Rombo;
  • Mbozi Magharibi;
  • Iringi Mjini;
  • Kigoma Kaskazini;

Katika mjadala wangu, nitajaribu kuchambua matokeo mbalimbali katika majimbo haya kwangazi ya Urais na Ubunge baina ya CCM na Chadema; Ni matumaini yangu kwamba hii itatusaidia sote kwa pamoja kubaini MAPUNGUFU na CHANGAMOTO zinazotukabili kama nchi yenye Demokrasia changa, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea 2015.

Baada ya kusema haya, sasa niingine kwenye uchambuzi wa majimbo kumi na tano niliyoyataja awali.

  • JIMBO LA KIGOMA KASKAZINI
Nimeanza na jimbo hili kwa sababu kuu mbili: Kwanza, mbunge wa jimbo hili, ZITTO, tayari ameshaonyesha nia ya kugombea Urais 2015 kupitia Chadema; na pili, Zitto amekuwa Kiongozi wa Chadema Taifa kwa muda mrefu. Kigoma Kaskazini ni moja ya majimbo ambayo mshindi wa ubunge kwa tiketi ya Chadema (kwa karibia 10% dhidi ya CCM), hakufanikisha Ushindi(kura za jimboni ngazi ya Urais) kwa mgombea Urais kupitia Chadema Dr. Slaa. I find this to be ironic. Katika jimbola Zitto, Kikwete alimshinda Dr. Slaa kwa margin kubwa sana (32%), na hii ilikuwani ‘defeat' kubwa kwa Dr. Slaa kuliko majimbo mengine yote ambayo Chademailishinda viti vya ubunge. Ni muhimu tukumbuke kwamba katika uchaguzi wa 2010, Zitto alikuwa anatetea kiti chake (HAKUWA MGOMBEA MPYA); pia Zitto aliingia katika uchaguzi huu akiwa ni mmoja wa wabunge wenye mvuto mkubwa sana katika MASUALAYA KITAIFA, lakini ajabu ni kwamba hakuweza kumsaidia Dr. Slaa kushinda katika nafasi ya Urais ambayo ni ya ngazi ya Taifa. Matokeo ya uchaguzi Urais (2010) Kigoma Kaskazini yanazaa maswali yafuatayo:

a)
Je, kushinda kwa Zitto Ubunge lakini kushindwa kwa Dr. Slaa Urais Kigoma Kaskazini ni ishara kwamba watanzania wengi huchagua wabungekwa vigezo vya LOCALISM na RAIS kwa vigezo vya NATIONALISM?

b)
Kigomani moja ya mikoa ambayo ipo nyuma sana kimaendeleo katika nyanja nyingi; Je mwenendo huu wa wapiga kura unatupa taswira gani kuhusu wapiga kura wa mikoa kama Kigoma na mingineyo iliyopo nyuma kimaendeleo?

c)
Kwa vile sasa ni wazi kwamba Zitto ana mikakati ya kugombea Urais 2015 kupitiaChadema; Je, kama hakuwa na uwezo wa kushawishi wapiga kura wake wamchague Dr.Slaa kiti cha urais, kama walivyomchagua yeye kiti cha ubunge, what's the justification and rationale juu ya uwezo wake kushinda Urais (ngazi ya taifa)2015? Inawezekana justification and rationale ipo, lakini tukija jadili hili, nimuhimu tuanze na dhana ya "CHARITY BEGINS AT HOME".

  • JIMBO LA HAI
Jimbola HAI ni muhimu pia kulitazama in the context of our discussion kwa sababu hili ni jimbo analotoka Mwenyekiti wa Chadema Taifa – Freeman Mbowe. Kwa mujibuwa takwimu za matokeo ya uchaguzi HAI, yaliyojiri katika jimbo hili hayana tofauti kubwa na yale ya Kigoma Kaskazini kwa Zitto. Kwa mfano, Mbowe alimshinda mpinzani wake wa CCM kwa karibia 10% (sawa na Zitto Kigoma Kaskazini); vile vile Dr. Slaa alishindwa na Kikwete kwa 31% (karibia sawa na ushindi wa Kikwete dhidi ya Dr. Slaa Kigoma Kaskazini); I also find this to be ironic. Matokeoya jimbo la HAI pia yanazaa maswali yale yale (rejea hapo juu) tuliyojadili kuhusiana na matokeo ya Kigoma Kaskazini.

  • JIMBO LA SINGIDA MASHARIKI
Mwaka2010, Singida Mashariki ilipata mbunge mpya na mgeni katika ulingo wa siasa/bungeniTundu Lissu alimshinda mpinzani wake wa CCM kwa karibia 6%; Lakini kwenye jimbohili, Dr. Slaa alishindwa na Kikwete (CCM) kwa 32% ambayo ni sawa na kwa Zitto (Kikwete beat Dr. Slaa by 32%) na karibia sawa na kwa Mbowe (Kikwete beat Dr. Slaa by 31%);Lakini hapa kuna kitu kimoja worth mentioning: Licha ya ugeni wa Lissu kwenye Siasa,ushindi wa Lissu jimboni haukuwa na utofauti mkubwa na ule wa Zitto na Mbowe (interms of percentage of votes won); Vile vile, licha ya ugeni wake, Lissu hakutofautiana na wakubwa wake wa kazi (Zitto & Mbowe) in terms of delivery of votes kwa Dr. Slaa dhidi ya Kikwete, pamoja na kwamba Zitto na Mbowe tayari walikuwa tayari na uzoefu wa ubunge lakini pia wanajulikana kitaifa zaidi yaLissu, hivyo walitegemewa to perform better katika kura za Dr. Slaa;

Pia niseme kwamba – kuna dalili kubwa kwamba mwaka 2015, Lissu ataongeza margin ya ushindi wake jimboni kwake, lakini vile vile kuna uwezekano mkubwa ‘to deliver'kura kwa mgombea Urais Chadema 2015 pamoja na kwamba Singida kihistoria ningome kubwa sana ya CCM tofauti na Kigoma (kwa Zitto) au Kilimanjaro (kwaMbowe); Ni kwa maaana hii, Lissu anabakia kuwa hazina kubwa sana ya Chadema hata ngazi ya Urais kwa siku za usoni (hata 2015). Lissu ataipa CCM wakati mgumu sana kama atasimamishwa na Chadema 2015 pengine kuliko mgombea mwingine yoyote nje ya Dr. Slaa. Lakini huu ni mjadala tofauti na nisingependa kwenda huko kwa sasa.

So far, tumesha jadili majimbo matatu ambayo Dr. Slaa alianguka kwa margin kubwadhidi ya Kikwete. Kabla sijaendelea na majimbo yaliyobakia, ningependa kuorodhesha ‘TOP FIVE' ya majimbo ambayo wabunge wake hawakuweza kumsaidia Slaa kupata kura dhidi ya Jakaya Kikwete 2010:

a) Kigoma Kaskazini – Zitto: Dr. Slaa lost by 32% to Kikwete; [note – Zitto hakuwa mbunge mgeni na pia tayari alikuwa ni kiongozi wa Chadema Taifa, hivyo kuwa na nafasi ya kuvuta wapiga kura wengi zaidi kuliko wabuge wapya];

b) Singida Mashariki – Lissu: Dr. Slaa lost by 32% to Kikwete;[note – Lissu ni mbunge mpya na hakuwa na nafasi ya uongozi ya kisiasa ndani ta Chadema Taifa; Vile vile traditionally, Singida ni moja ya ngome nzito sana za CCM kama ilivyokuwa kwa Tanga ambapo wagombea wa CCM hata wakiwa wa ovyo hupita tu;

c) Hai– Mbowe – Dr. Slaa lost by 31% to Kikwete; [note – Mbowe alishawahi kuwa mbunge miaka ya nyuma, na pia amekuwa kiongozi wa kisiasa wa Chadema ngazi ya taifakwa muda mrefu];

d) Mbozi Magharibi – Silinde – Dr. Slaa lost by 27% to Kikwete; [note – Silinde ni mbunge mpya lakini aliweza kuwapiku Zitto na Mbowe kwenye delivery ya votes kwa Dr. Slaa dhidi ya Kikwete majimboni mwao];

e) Iringa Mjini – Rev. Msigwa – Dr. Slaa lost by about 10% to Kikwete; [note – Msigwa kama ilivyokuwa kwa Lissu na Silinde ni mbunge mgeni/mpya lakini bado na yeye delivered more votes kwa Dr. Slaa kuliko Mbowe na Zitto];

Yafuatayo ni majimbo mengine ambayo pamoja na kwamba Kikwete alishinda, lakini kwa margin ndogo sana ya percentage of votes:

  • JIMBO LA UBUNGO
Mnyika ni mbunge mpya ambae alimshinda mgombea wa CCM kwa karibia 12%; katika ngazi ya Urais Kikwete alimshinda Dr. Slaa kwa asilimia ndogo sana (about 5%); Hivyo Mnyika delivered more votes kwa Dr. Slaa kuliko Mwenyekiti wake (Mbowe - Hai),na Naibu Katibu Mkuu wake (Zitto – Kigoma Kaskazini);

  • JIMBO LA ROMBO
Selasinini mbunge mpya ambae alimshinda mpinzani wake wa CCM kwa kama 3%; Ngazi ya Urais, Kikwete alimshinda Dr. Slaa kwa kama 12%; Ingawa Kikwete alishinda kura za Rombo, lakini bado Selasini nae, kama ilivyokuwa kwa Mnyika na wengine ambao tutawaona, delivered more votes kwa Dr. Slaa kuliko walivyofanya Mbowe naZitto majimboni kwao;

  • JIMBO LA KAWE
Mbunge wangu mahiri ‘Halima Mdee' alimshinda mgombea wa CCM kwa karibia 9%; Kwenye ngazi ya Urais kwa kawe, Kikwete alimshinda Dr. Slaa kwa margin ndogo sana, only 3%;

Mwisho nimalizie na majimbo ambayo wabunge wa Chadema walifanikiwa kuwashawishi wapiga kura wao kumchagua Dr.Slaa dhidi ya Kikwete.

  • JIMBO LA ILEMELA
Kiwia ni mbunge mpya na alishinda kwa kama 7% dhidi ya CCM; Kwa ngazi ya Urais ilemela, Dr. Slaa alimshinda Kikwete kwa karibia 2%; [note: Kiwia ni mbunge mpya na hakuwa na nafasi ya uongozi Chadema Taifa lakini bado Dr. Slaa alishinda jimbo la ilemela, tofauti na majimbo ya Zitton a Mbowe];

  • JIMBO LA UKEREWE
Machemli alimbwaga Mama Mongella kwa karibia 16%; kwa ngazi ya Urais Ukerewe, Dr. Slaa alimshinda Kikwete kwa karibia 2%; [note:- Machemli ae ni mbunge mpya na hakuwa na nafasi yoyote ya uongozi Chadema Taifa, lakini bado alimsaidia Dr. Slaa kushinda ukerewe, tofauti na majimbo ya Zitto na Mbowe];

  • JIMBO LA ARUSHA MJINI
Kamanda Lema alimbwaga mpinzani wake kwa karibia 20% na kufanya jimbo hili kuwa ni moja ya majimbo ambayo Chadema ilishinda kwa margin kubwa sana ngazi ya ubunge; Kwan gazi ya Urais Arusha mjini, Dr. Slaa alimshinda Kikwete kwa karibia 16%; [note– Lema nae ni mbunge mpya na hakuwa na nafasi yoyote ya uongozi Chadema Taifa, lakini bado alimsaidia Dr. Slaa kushinda Arusha Mjini, tofauti na majimbo ya Ztto na Mbowe];

  • JIMBO LA KARATU
Natse alimshinda mpinzani wake kwa karibia 20%, na kufanya karatu pia kuwa moja ya majimbo ambayo Chadema ilishinda urais kwa margin kubwa; Kwenye ngazi ya Urais, Dr.Slaa alimbwaga Kikwete kwa karibia 27%; lakini hili ni jimbo tofauti kidogo kwani hapa kulikuwa na ‘Slaa Factor' in play; ingekuwa ajabu kama Dr. Slaa asingepata kura zaidi ya Kikwete Karatu; Lakini kwa jinsi tulivyo ona mwenendo wa wapiga kura, kwa majimbo ya Hai na Kigoma Kaskazini, haitakuwa ajabu sana kwa Mbowe au Zitto iwapo watagombea Urais, kushindwa na mgombea wa CCM 2015 kwenye kura za majimboni kwao ngazi ya Urais;

  • JIMBO LA MOSHI MJINI
Mzee Ndesamburo alishinda kiti cha ubunge kwa karibia 28%, pia moja ya majimbo ambayo Chadema ilipata ushindi mkubwa sana ngazi ya ubunge; kwa ngazi ya Urais,Dr. Slaa alimshinda Kikwete kwa karibia 12%; Kwa mtazamo wangu, ilitakiwa ZITTO na MBOWE nao pia wachangie ushindi kwa Dr. Slaa kwa mtindo wa Mzee Ndesamburo (kura za Urais Moshi Mjini),Dr. Slaa (kura za urais Karatu) na wengineo;

  • JIMBO LA MBEYA MJINI
Hili ni jimbo ambalo Chadema ilishinda margin kubwa kuliko yote Tanzania kwa ngaziya ubunge - Sugu a.k.a Mr. II, alimshinda mpinzani wake kwa 30%; Kwa ngazi yaUrais, Dr. Slaa alimshinda Kikwete kwa karibia 13%; [note: Sugu alikuwa mbunge mpya na hakuwa na nafasi yoyote ya uongozi kitaifa ndani ya Chadema lakini bado alimsaidia Dr. Slaa kumshinda Kikwete Mbeya mjini, tofauti na matokeo ya majimbo ya Zitto na Mbowe];

Ningependa kuhitimisha na maswali na nadharia tete kwa nia ya kuongezea mjadala huu uhai zaidi:

MASWALI YA KUJADILI NI MANNE

1. Je,wakati wa kupiga kura, Watanzania hutarajia mambo gani kutoka kwa yule wanae mchagua kuwa Mbunge wao?

2.
Je,wapiga kura hutarajia mambo gani kutoka kwa yule wanaemchagua kuwa Rais wa nchi?

3. Je, PERSONALITY (MTU) & ISSUES (MASUALA) hutumiwa vipi na wanasiasa na pia je, hutumikaje na wananchi katika kuchagua viongozi wao (wabunge na rais)?

4. Je, Watanzania huchagua wabunge kwa vigezo vya LOCALISM? NATIONALISM? AU VYOTE VIWILI?

Katika hili la Localism na Nationalism, napendekeza NADHARIA TETE (Hypotheses) mbili. Naomba ieleweke kwamba nia yangu kuja na hizi nadharia tete ni kutengeneza mazingira bora ya mjadala huu na sio vinginevyo. Naomba haya yasichukuliwe kwamba ndio UKWELI ULIOSADIDIKA.

NADHARIA TETE ZA KUJADILI NI HIZI ZIFUATAZO:

  • NADHARIA TETE YA KWANZA:
Wananchi huchagua wabunge kwa matarajio kwamba kiongozi huyo atajuhusisha zaidi na local issues and grievances; wananchi hawategemei mtu watakayemchagua kuwa mbunge wao ajihusishe sana na masuala ya kitaifa, isipokuwa kama masuala hayo yana uhusiano wa MOJA KWA MOJA na majimbo yao.

  • NADHARIA TETE YA PILI:
Wananchi wa Tanzania huchagua Rais kutokana na mapenzi fulani waliyonayo juu ya nchi yao ya Tanzania ambapo wapo tayari kujitolea kwa hali na mali katika kuilindana kuitetea nchi yao ya Tanzania. Mapenzi haya kwa Tanzania yanahusishwa moja kwa moja na CCM kwasababu CCM ndio imeizaa TANZANIA, tofauti na TANU ambayo iliikomboa nchi ya TANGANYIKA, taifa ambalo lilipotea pamoja na TANU. Mapenzi na Uzalendo wa wapiga kura kwa TANZANIA unaenda sambamba na kuichagua CCM kwani ni kwa sababu ya CCM, wao wanajihisi ndio watanzania, na wanajivunia kuwa WATANZANIA, hasa kutokana na ujenzi wa Taifa uliofanywa na CCM katika maeneo kama vile amani, umoja, udugu na mshikamano.

Naomba nisisitize tena kwamba hizi ni nadharia tete tu ambazo zinaweza kuwa TRUE au FALSE, hivyo mjadala wetu ukielekea huko, kutakuwa na tija zaidi. Vinginevyo, huu sio UKWELI ULIOSADIKIKA.

Nawasilisha.
 
Mimi hapa nitazungumzia dhana tu lakini kwa mujibu wa uzoefu wangu.

Katika hali ya kawaida ya kibinadamu na kisaikolojia, pia kwa kuzingatia unazi wa Watanzania kwa vyama vyao; na ingawa mwananchi ana uhuru wa kuchagua kile anachokipenda, si rahisi kwa mtu wa jimbo hilo hilo, akapewa karatasi za wagombea wa uraisi, ubunge na udiwani, akatia kura kwa mgombea wa chama tafauti katika kila karatasi.

Ninachotaka kusema hapa, na hii narudia tena kuwa ni dhana yangu tu kwa sababu niliyoeleza hapo juu, hatuoni kama kulikuwa na uwezekano mkubwa wa Dr. Slaa kushinda kwenye majimbo ya Kigoma Mjini, Hai na Singida, lakini Kikwete akaibuliwa mshindi kwa uchachakuaji wa matokeo?

Just thinking aloud.

Nitarejea baadaye kwa mchango wa kina ambao hautakuwa umeathiriwa na wasiwasi wangu wa hapo juu.
 
Kuhusu suala la uchaguzi kuchakachuliwa, nililifikiria sana kabla ya kuja na mada hii lakini nikaona kwamba kwa ujumla wake, Chadema will play it safer kwa kuyafanyia kazi matokeo haya kuliko kuyadharau kwamba hayana uhalali kutokana na taarifa zilizosambaa kwamba matokeo yalichakachuliwa, hasa kwa vile haijulikani ni wapi matokeo yalichakachuliwa; either way, still Chadema needs numbers za kufanyia kazi as they prepare for 2015, na takwimu za matokeo ya uchaguzi wa 2010 ni moja ya number muhimu sana kuzifanyia kazi katika miaka hii mitatu iliyobakia; huu ndio mtazamo wangu;
 
Halafu utasikia wapuuzi fulani wakieneza propaganda za kishenzi eti chama fulani ni chama cha wachaga na wakristo! Huko Hai na Rombo ambako Kikwete alishinda kwa kishindo wanaishi manyani? Na huko Mbeya alikoshindwa ni familia ya mchaga?

Au utasikia wakieneza uzushi eti ni chama cha wakristo kana kwamba kwenye chama chao hakuna hao wachaga na wakristo. Kama mnawatukana na kuwadhihaki hao wachaga na wakristo maana yake mnataka chama chenu kiwe na akina nani?

CCM acheni upuuzi wenu, mnakolipeleka taifa siko! Kawaeleimishe kwanza hao "ndugu" zako kuhusu hili ndipo uje na hiyo analysis yako hapa kwa ajili ya discussion.
 
Kusingekuwa na uchakachuaji ambao ulikuwa wazi kabisa ktk uchaguzi ningeweza kuamini analysis yako na conclusions zako. Lakini kwa kuwa uchakachuaji wa matokeo ulikuwa mkubwa mno huwezi kujenga hoja yako ktk msingi mbovu au usiokuwepo kabisa na kutoa conclusions. Hii topic ingekuwa na maana sana kama matokeo yasingechachuliwa kwa sababu tafakari na reasoning yetu ingejikita katika msingi wa ukweli. Na hivyo conclusion zetu zingekuwa na ukweli pia. Ni maoni yangu tu mkuu.
 
Kama nilivyomjibu mchangiaji mwingine kuhusu suala la uchaguzi kuchakachuliwa, nililifikiria sana kabla ya kuja na mada hii lakini nikaona kwamba kwa ujumla wake, Chadema will play it safer kwa kuyafanyia kazi matokeo haya kuliko kuyadharau kwamba hayana uhalali kutokana na taarifa zilizosambaa kwamba matokeo yalichakachuliwa, hasa kwa vile haijulikani ni wapi matokeo yalichakachuliwa; either way, still Chadema needs numbers za kufanyia kazi as they prepare for 2015, na takwimu za matokeo ya uchaguzi wa 2010 ni moja ya number muhimu sana kuzifanyia kazi katika miaka hii mitatu iliyobakia; huo ndio mtazamo wangu mkuu;
 
Kuhusu suala la uchaguzi kuchakachuliwa, nililifikiria sana kabla ya kuja na mada hii lakini nikaona kwamba kwa ujumla wake, Chadema will play it safer kwa kuyafanyia kazi matokeo haya kuliko kuyadharau kwamba hayana uhalali kutokana na taarifa zilizosambaa kwamba matokeo yalichakachuliwa, hasa kwa vile haijulikani ni wapi matokeo yalichakachuliwa; either way, still Chadema needs numbers za kufanyia kazi as they prepare for 2015, na takwimu za matokeo ya uchaguzi wa 2010 ni moja ya number muhimu sana kuzifanyia kazi katika miaka hii mitatu iliyobakia; huu ndio mtazamo wangu;
Napenda saana uchambuzi wako. Mara nyingi uko objective!.. Hivi Zombe, rejeao, ze marcopolo na ritz hawajapita?.. Utasikia DINI na KANDA!
 
Napenda saana uchambuzi wako. Mara nyingi uko objective!.. Hivi Zombe, rejeao, ze marcopolo na ritz hawajapita?.. Utasikia DINI na KANDA!

Sijawaona hao humu mkuu,lakini sio kawaida yao kushiriki katika thread zangu; nashukuru kwamba kwa mtazamo wako, mada yangu ina nia ya KUJENGA, na sio KUBOMOA, kwani nimeanza kushambuliwa kwamba kwa uzi huu, nina agenda ya siri ingawa mtoa hoja hiyo hajatoa ufafanuzi kujenga hoja yake iwe na mashiko;
 
Kwanza nikupongeze kwa data bila kujua usahihi wake ila ni directive.
Kuna Mengi.Ila mimi naweza sema elimu,dini, hofu, na mabaki ya umaarufu wa Kikwete, mazoea, smear compaign za ccm-b, ahadi binafsi za rais.

-Kuna maeneo watu hawakuwa tayari mpigia Dr. Slaa kwa vile alishaambiwa kuwa Padri.Na hii ni very serious hata kwa Wakristu wenyewe.Hata madhehemu yanayoogopa catholics,achilia mbali waislam ambao bado wanalia na vatican/mfumo Kristo.Bora zimwi likujualo/ulijualo Kikwete kuliko Slaa wasiye mjua na wengine wakisema bora wetu kwa vile tumedhulumiwa sana.

-Kuna maeneo watu hawakuwa wanajua kusoma na kuandika na hivyo walitegemea mawakala waliweza vipi pata nafasi ya kuwasaidia kwa stail elekezi.Au hata mpiga kura kuwajua wagombea ubunge wao na Kikwete ambaye vijijini nguo na vipeperushi vimejaa Picture zake ila kutomjua Dr. Slaa sana.

-Kipindi cha pili kikwete hakuwa amepoteza umaarufu ulimuingiza madarakani kipindi cha kwanza kwa kishindo huku akifunika kabisa madhaifu ya CCM.Bado kuna watu walikuwa hawajafikia mahalai pa kujiuliza maswali juu ya uwezo wake.

-Kikwete alitoa ahadi binafsi kila kukicha alikuwa disperate aliahidi mbingu na nchi.Tena kwa kujiamini na kwa vile watanzania hupenda viungo vya kudanganywa kidogo basi hapakuwa na time ya kumuuliza maswali.hata hivyo rais hakuweka nafasi ya maswali magumu ya pao kwa papo.

-wengine ni hofu ya kuitoa CCM.CCM wamefikisha ujumbe wa hofu kuwa wakiingia wapinzani amani itapotea.ubunge hawakuogopa kwa vile walishwahi ona mifano mingi.

-wapinzani dhaifu tayari walishaingia line kwa ccm na hivyo pale walipohisi kuwa CCM haina nguvu na wao hawawezi shinda walisema wazi kuwa Kikwete ndie sahihi kwa urais na kwa ubunge wapewe wao.ila lengo ni kuharibu balance ya kura kwa manifaa ya ccm.

-Mazoea pia yalipunguza watu kufikiri sana.Kwani wengi walishazoea kuwa wether unapimpigia Kikwete au lah wapinzani hawawezi shida.kwani CCM ni wezi siku zote.

kuna mengi sana ila hayo yalichangia sana na mategemeo yangu ni kuwa Kikwete angepata kura nyingi zaidi kwani kila kitu kilikuwa upande wake.Kutoa kukubalika haswa na wenye uelewa.Hata yale mazingaombwe ya kutokea watu vituoni na magari ya ajabuajabu na raia kuwakimbiza.wengine kuokolewa na polisi halafu kimya yalichangia sana.Hata hivyo hizo factors kuna maeneo zilikuwa zikiapply kwa viwango tofauti ila resultant effects zilikuwa upande wa Kikwete.

Note:Jimbo la Zitto lilimezwa sana na NCCR effect huku yeye mwenyewe akimezwa "zittoism" zaidi. Kwani alikuwa msaada kwa NCCR hata kwa majimbo mengine kuliko CDM.Na Hakuna mwenye hakina kama sakata la kugombea uongozi lilikuwa okay rohoni kwake.Ila kwa sasa karivu vyote hivi haviwezi changia lolote la maana.
 
Acha ujinga wako wewe, Rais wa nyinyiem hakushinda kwa kura za kwenye sanduku bali za mezani, so data zako zote siyo valid na hilo liko wazi kabisa kwahiyo analysis yote ulofanya ni ubatili mtupu
 
Mchambuzi hongera kwa uchambuzi wako mzuri, lakini nadhani unakumbuka kwa jinsi matokeo yalivyochakachuliwa, ni vigumu mno kwa majimbo yote haya kuwa na ushindi wa kufanana kwa mwagombea wa uraisi na wabunge.
Taarifa za kiuchambuzi zinaonesha kuwa ushindi wa chadema katika majimbo haya ulikuwa mkubwa kuliko uliotangazwa licha ya kuchakachuliwa. Pili vipi yale majimbo ambayo ccm iliongoza ubunge na chadema uraisi nayo umwyaweka katika kundi gani?
Kwa vigezo ulivyovitaja hapa, ni wazi ccm watavitumia tena kumanipulate matokeo 2015.
 
Kwanza nikupongeze kwa data bila kujua usahihi wake ila ni directive.
Kuna Mengi.Ila mimi naweza sema elimu,dini, hofu, na mabaki ya umaarufu wa Kikwete, mazoea, smear compaign za ccm-b, ahadi binafsi za rais.

-Kuna maeneo watu hawakuwa tayari mpigia Dr. Slaa kwa vile alishaambiwa kuwa Padri.Na hii ni very serious hata kwa Wakristu wenyewe.Hata madhehemu yanayoogopa catholics,achilia mbali waislam ambao bado wanalia na vatican/mfumo Kristo.Bora zimwi likujualo/ulijualo Kikwete kuliko Slaa wasiye mjua na wengine wakisema bora wetu kwa vile tumedhulumiwa sana.

-Kuna maeneo watu hawakuwa wanajua kusoma na kuandika na hivyo walitegemea mawakala waliweza vipi pata nafasi ya kuwasaidia kwa stail elekezi.Au hata mpiga kura kuwajua wagombea ubunge wao na Kikwete ambaye vijijini nguo na vipeperushi vimejaa Picture zake ila kutomjua Dr. Slaa sana.

-Kipindi cha pili kikwete hakuwa amepoteza umaarufu ulimuingiza madarakani kipindi cha kwanza kwa kishindo huku akifunika kabisa madhaifu ya CCM.Bado kuna watu walikuwa hawajafikia mahalai pa kujiuliza maswali juu ya uwezo wake.

-Kikwete alitoa ahadi binafsi kila kukicha alikuwa disperate aliahidi mbingu na nchi.Tena kwa kujiamini na kwa vile watanzania hupenda viungo vya kudanganywa kidogo basi hapakuwa na time ya kumuuliza maswali.hata hivyo rais hakuweka nafasi ya maswali magumu ya pao kwa papo.

-wengine ni hofu ya kuitoa CCM.CCM wamefikisha ujumbe wa hofu kuwa wakiingia wapinzani amani itapotea.ubunge hawakuogopa kwa vile walishwahi ona mifano mingi.

-wapinzani dhaifu tayari walishaingia line kwa ccm na hivyo pale walipohisi kuwa CCM haina nguvu na wao hawawezi shinda walisema wazi kuwa Kikwete ndie sahihi kwa urais na kwa ubunge wapewe wao.ila lengo ni kuharibu balance ya kura kwa manifaa ya ccm.

-Mazoea pia yalipunguza watu kufikiri sana.Kwani wengi walishazoea kuwa wether unapimpigia Kikwete au lah wapinzani hawawezi shida.kwani CCM ni wezi siku zote.

kuna mengi sana ila hayo yalichangia sana na mategemeo yangu ni kuwa Kikwete angepata kura nyingi zaidi kwani kila kitu kilikuwa upande wake.Kutoa kukubalika haswa na wenye uelewa.Hata yale mazingaombwe ya kutokea watu vituoni na magari ya ajabuajabu na raia kuwakimbiza.wengine kuokolewa na polisi halafu kimya.Hata hivyo hizo factors kuna maeneo zilikuwa zikiapply kwa viwango tofauti ila resultant effects zilikuwa upande wa Kikwete.

Note:Jimbo la Zitto lilimezwa sana na NCCR effect huku yeye mwenyewe akimezwa "zittoism" zaidi. Kwani alikuwa msaada kwa NCCR hata kwa majimbo mengine kuliko CDM.Na Hakuna mwenye hakina kama sakata la kugombea uongozi lilikuwa okay rohoni kwake.

Asante kwa mchango wako mzuri mkuu. Takwimu zangu ni za tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) ambazo whether ni za kweli au za kupikwa, its the only stats available for us to make sense of what happened, unless tuamue kutojadili matokeo ya 2010 kwa vigezo vya takwimu hizi, na badala yake kuja na kitu for us to base our analysis ambacho kitakuwa still a representation of what transpired huko majimboni; ningependa kusikia mapendekezo yako juu ya hili ili tuweze kupata picha inayokaribiana na mambo yalivyojiri huko majimboni;

Vinginevyo, kimsingi nakubaliana na hoja zako nyingi lakini pia ningependa kusikia maoni yako juu ya personalities vis-a-vis issues when it comes to wapiga kura wetu nyakati za chaguzi, tukiachilia mbali mazoea, udini, fear factor, illiteracy na mengineyo uliyoyajadili. In the long run, tutakomaa iwapo tutaweza overcome haya yote na kuwa na ushaindani wa kisiasa based on issues, ndio maana kauli ya Dr. Slaa nimeipenda sana kwani hakuna kiongozi wa chama kingine cha Siasa (HATA CCM) ambae amewahi kutamka hili, licha ya imani kwamba CCM ni chama kilichokomaa, chenye hazina ya viongozi n.k; nia ya mjadala wangu ni kujaribu kujenga pale Dr. Slaa alipoanzia na kauli yake kwa uchaguzi wa 2015 and beyond;

Hoja yako kuhusu Zitto suggests kwamba his candidacy kupitia chadema 2015 may not be as strong; Na je, if we hold other things constant (such as uchakachuaji wa kura n.k), do you think Dr. Slaa kushindwa kwa idadi sawa ya asilimia kwenye majimbo ya Zitto na Mbowe ni coincidence? Pia hapa swali lingine linajitokeza kuhusu vigezo sahihi vya kutumika kuchagua viongozi wa vyama vyetu vya siasa ngazi ya taifa; mbali ya elimu, uzoefu na experience, je kigezo cha kwamba fulani anafaa kuwa kiongozi wa chama ngazi fulani kitaifa na kwamba anakubalika kiwe based on performance bungeni? majimboni kwao - kura za ubunge na urais? Nini mtazamo wako katika hili mkuu;
 
Mchambuzi nikupongeze kwa kuja hii mada. Nikiri kuwa wewe ni mmoja wa watu wachache wenye mada constructive kwa mustakabali wa taifa hili.
Mimi nitachangia kwa namna tofauti. Kama utakumbuka CHADEMA walichelewa kuteua mgombea wa ngazi ya Uraisi. Hii ni mojawapo ya weakness ambayo niliiona kwenye mchakato wa Uraisi ili oliopita kwa CHADEMA. Pamoja na uchelewaji huo waliteua weak Mwenza. Kwa hili CHADEMA wanatakiwa wawe makini kwa uchaguzi ujao Kama kweli wanataka kuchukua dola.
Kuhusu Dr. Slaa kukosa kura chache Jimbo la Zitto, pengine mtazamo aliokuwa nao Zitto limechangia. Zitto alikuwa against CHADEMA kusumamisha mgombea wa Uraisi pengine kwa nia njema tu, ya kuimarisha idadi ya wabunge wa chama chake.
 
Last edited by a moderator:
Asante kwa mchango wako mzuri mkuu. Takwimu zangu ni za tume ya taifa ya uchaguzi (NEC) ambazo whether ni za kweli au za kupikwa, its the only stats available for us to make sense of what happened, unless tuamue kutojadili matokeo ya 2010 kwa vigezo vya takwimu hizi, na badala yake kuja na kitu for us to base our analysis ambacho kitakuwa still a representation of what transpired huko majimboni; ningependa kusikia mapendekezo yako juu ya hili ili tuweze kupata picha inayokaribiana na mambo yalivyojiri huko majimboni;

Vinginevyo, kimsingi nakubaliana na hoja zako nyingi lakini pia ningependa kusikia maoni yako juu ya personalities vis-a-vis issues when it comes to wapiga kura wetu nyakati za chaguzi, tukiachilia mbali mazoea, udini, fear factor, illiteracy na mengineyo uliyoyajadili. In the long run, tutakomaa iwapo tutaweza overcome haya yote na kuwa na ushaindani wa kisiasa based on issues, ndio maana kauli ya Dr. Slaa nimeipenda sana kwani hakuna kiongozi wa chama kingine cha Siasa (HATA CCM) ambae amewahi kutamka hili, licha ya imani kwamba CCM ni chama kilichokomaa, chenye hazina ya viongozi n.k;

Hoja yako kuhusu Zitto makes his candidacy kupitia chadema 2015 kuwa questionable; Na je, if we hold other things constant (such as uchakachuaji wa kura n.k), do you think Dr. Slaa kushindwa kwa idadi sawa ya asilimia kwenye majimbo ya Zitto na Mbowe ni coincidence? Pia hapa swali lingine linajitokeza kuhusu vigezo sahihi vya kutumika kuchagua viongozi wa vyama vyetu vya siasa ngazi ya taifa; mbali ya elimu, uzoefu na experience, je kigezo cha kwamba fulani anafaa kuwa kiongozi wa chama ngazi fulani kitaifa na kwamba anakubalika kiwe based on performance bungeni? majimboni kwao - kura za ubunge na urais? Nini mtazamo wako katika hili mkuu;

Ukiangalia kwa makini hizo fators zangu zinajibu kwanini majimbo ya Mbowe na Zitto Slaa hakupata ushindi tena mnene.Ungechora drafti ukatembea nayo majimboni halafu ukaweka asilimia ya kura kupitia hizo factors unaweza ona jinsi zinajibu yote.Kuna sehemu nyingine zitakuwa karibia na zero nyingine zikapanda. Hiyo idadi sawa inaweza kuwa coincidence kwa baadhi ya maeneo ila kwa sehemu hizi ulizotaja ni ishara ya wanamazingaombwe kufanya kazi "hawa walijwekea margin ya uchakachuaji ili "kutoinua eyebrows" kwa wambea kama sisi.Yaani inaitwa TOP-DOWN APPROACH. watanzania ni wavivu sana hasa linapokuja suala la number.Labda ikiwa hela ndio watakuwa makini.Ila nalo pia kama hela ninyingi zaidi ya mtu alivyodhani kuwa hawi tena mwangalifu kw akiburu.Ukimpatia mtanzania set ya number atumie kutengeneza majibu hawezi maliza bila kurudia hata kama ni nyingi.Kwangu mimi naona ni tatizo la kupika data halafu kuzitafuta kura.Pia pressure ya kufanya vitu in the shortest time,ni ngumu hao jamaa kufikiri sana.
 
Kwa sababu vyama vyetu havina tofauti ya kiitikadi, watu huangalia mhgombea na siyo chama gani anatokea.
Ungefananisha na uchaguzi wa 2005, labda ungeona hili jambo clearly.
Nguvu ya umma/ ujamaa na kujitegemea bila wakulima na wafanyakazi kwenye uongozi, viongozi wote ni mabepari wanaojifanya wajamaa, kwa hiyo hizo kura zinareflect masinia ya pilau.
 
Babuwaloliondo,

Nashukuru sana kwa mchango wako. Kuhusu suala la uchakachuaji wa matokeo nilitoa majibu yangu kwa nadhani kwa mchangiaji aitwaye babuyao kwamba, nililifikiria sana suala hili kabla ya kuja na mada hii lakini nikaona kwamba kwa ujumla wake, Chadema will play it safer kwa kuyafanyia kazi matokeo haya kuliko kuyadharau kwamba hayana uhalali kutokana na taarifa zilizosambaa kwamba matokeo yalichakachuliwa, hasa kwa vile haijulikani ni wapi matokeo yalichakachuliwa; nikazidi kusisitiza kwamba either way, still Chadema needs numbers za kufanyia kazi as they prepare for 2015, na takwimu za matokeo ya uchaguzi wa 2010 ni moja ya numbers muhimu sana kuzifanyia kazi katika miaka hii mitatu iliyobakia;

Pia nilitoa majibu kwa mchangiaji mwingine i.e. ‘nicholas', ambae nae aligusia suala la uchakachuaji ambapo nilimjibu kwamba, kwamba takwimu hizi ni za kweli au nyingi ni za kupikwa (kwani kuna sehemu ya takwimu hizi ni za kweli), these are the only stats available for us to make sense of what transpired huko majimboni, and unless tuamue kutojadili matokeo ya 2010 kwa vigezo vya takwimu hizi, lakini kufanya hivyo won't make things better for us hasa kama hatutafanikiwa kuja na kitu cha kutusaidia to base our analysis ambacho kitakuwa still a representation of what transpired huko majimboni; ksms nilivyomwomba Nicholas, ningependa pia kusikia kusikia kutoka kwako juu mapendekezo katika hili, ili tuweze kupata picha inayokaribiana na mambo yalivyojiri huko majimboni;

Kuhusu swali lako kwamba je naweka katika kundi gani majimbo ambayo CCM ilishinda ubunge lakini Chadema ikashinda Urais, hili ni swali la msingi sana lakini sikuwa na majibu yake ya moja kwa moja, hivyo nikaamua kuliweka suala hili ndani ya Nadharia Tete kuu mbili; Nadhani watu wengi wame overlook maswali yangu na nadharia tete zangu ambazo nilitegemea ndizo zingetupatia msingi wa mjadala kwani hata mimi natafuta majibu; badala yake, wengi naona wametazama zaidi uchambuzi wangu wa majimbo na kutoa maoni yao mbalimbali; Ningependa kuweka nadharia tete kuu mbili kama ifuatavyo, kwa imani kwamba kwa pamoja tutaweza kupata mwanga zaidi ndani ya mada hii ya kichokonozi:

NADHARIA TETE YA KWANZA:

Wananchi huchagua wabunge kwa matarajio kwamba kiongozi huyo atajuhusisha zaidi na local issues and grievances; wananchi hawategemei mtu watakayemchagua kuwa mbunge wao ajihusishe sana na masuala ya kitaifa, isipokuwa kama masuala hayo yana uhusiano wa MOJA KWA MOJA na majimbo yao.

NADHARIA TETE YA PILI:

Wananchi wa Tanzania huchagua Rais kutokana na mapenzi fulani waliyonayo juu ya nchi yao ya Tanzania ambapo wapo tayari kujitolea kwa hali na mali katika kuilindana kuitetea nchi yao ya Tanzania. Mapenzi haya kwa Tanzania yanahusishwa moja kwa moja na CCM kwasababu CCM ndio imeizaa TANZANIA, tofauti na TANU ambayo iliikomboa nchi ya TANGANYIKA, taifa ambalo lilipotea pamoja na TANU. Mapenzi na Uzalendo wa wapiga kura kwa TANZANIA unaenda sambamba na kuichagua CCM kwani ni kwa sababu ya CCM, wao wanajihisi ndio watanzania, na wanajivunia kuwa WATANZANIA, hasa kutokana na ujenzi wa Taifa uliofanywa na CCM katika maeneo kama vile amani, umoja, udugu na mshikamano.
 
Mchambuzi nikupongeze kwa kuja hii mada. Nikiri kuwa wewe ni mmoja wa watu wachache wenye mada constructive kwa mustakabali wa taifa hili.
Mimi nitachangia kwa namna tofauti. Kama utakumbuka CHADEMA walichelewa kuteua mgombea wa ngazi ya Uraisi. Hii ni mojawapo ya weakness ambayo niliiona kwenye mchakato wa Uraisi ili oliopita kwa CHADEMA. Pamoja na uchelewaji huo waliteua weak Mwenza. Kwa hili CHADEMA wanatakiwa wawe makini kwa uchaguzi ujao Kama kweli wanataka kuchukua dola.
Kuhusu Dr. Slaa kukosa kura chache Jimbo la Zitto, pengine mtazamo aliokuwa nao Zitto limechangia. Zitto alikuwa against CHADEMA kusumamisha mgombea wa Uraisi pengine kwa nia njema tu, ya kuimarisha idadi ya wabunge wa chama chake.

Mkuu Obi,

nashukuru sana kwa mchango wako mzuri; nimependa sana hoja zako kwani pamoja na ukweli kwamba matokeo yale yalikuwa na utata, umeamua kuliweka hilo pembeni ili ku work backwards na takwimu tulizonazo kwani pengine kwa kufanya hivyo, tutaweza kujua kura zilichakachuliwaje; sikupenda kulisema hili sasa hivi lakini nimeonelea niliseme kwani kuna baadhi ya wachangiaji ambao wana dismiss mada hii kwa hoja kwamba matokeo yale yalikuwa batili hivyo uchambuzi wangu utakuwa batili; hawajui kwamba kama tukiamua kukomaa na kuchimba bongo zetu na mada hii, tunaweza kujua nini kilitokea katika uchakachuaji, na ndio maana nimeita uzi huu mada ya uchokonozi;

Baada ya kusema haya, niseme tu kwamba nakubaliana na wewe kuhusu Chadema kuchelewa kuteua mgombea Urais; asante sana kwa kunikumbusha kwani kwa hilo nilipitiwa, na hii ni factor muhimu sana ambayo tunahitaji kuijadili katika mazingira ya wananchi kupigia kura WATU vis-a-vis kupigia kura MASUALA yanayosimamiwa na watu hawa; kwa hoja yako, inaashiria kwamba pengine Chadema hawakuwa na muda wa kutosha kujipanga nini kisemwe kwenye campaign trail, lakini [ia hawakuwa na muda wa kutosha kupima nini wananchi wanataka kusikia na nani aseme nini n/k; siwezi kusema Chadema walikurupuka, lakini ningependa kujua zaidi kwanini Chadema walichelewa kuteua mgombea 2010/nini ilikuwa ni sababu ya msingi, tukiachana na sababu ndogo ndogo;

Kuhusu suala la Zitto kutounga mkono Chadema kusimamisha mgombea Urais, hili pengine litasaidia kutupa eneo la kuanzia katika kuchunguza kuanguka kwa Dr. Slaa Kigoma Kaskazini; kuna hoja nyingine nimeisikia kwamba - Zitto hana umaarufu sana Kigoma kama watu wengi wanavyofikiria, na umaarufu wake unabebwa zaidi na NCCR kuliko Chadema; kama hoja hii ni ya kweli basi inatoa majibu kwanini Kikwete alimshinda Dr. Slaa Kigoma Kaskazini, kwani upinzani dhidi ya CCM kigoma miaka ya mwanzo ya tisini (enzi za kina DR. Kaborou), ulianza na NCCR Mageuzi, na waasisi wake wengi kwa sasa (hata baadhi ya viongozi wa sasa) ni Pro - CCM;

Mkuu Obi, nashukuru sana kwa kuongezea mwanga kitendawili changu;
 
Kwa sababu vyama vyetu havina tofauti ya kiitikadi, watu huangalia mhgombea na siyo chama gani anatokea.
Ungefananisha na uchaguzi wa 2005, labda ungeona hili jambo clearly.
Nguvu ya umma/ ujamaa na kujitegemea bila wakulima na wafanyakazi kwenye uongozi, viongozi wote ni mabepari wanaojifanya wajamaa, kwa hiyo hizo kura zinareflect masinia ya pilau.

Mkuu Kobello,

Nashukuru kwa mchango wako; unaposema kwamba wapiga kura tanzania hutazama personalities kwa sababu vyama havina itikadi zinazoeleweka wazi, lakini hasa zinazouzika kwa wananchi walio wengi, nakubaliana na wewe kwa hili mia kwa mia; lakini pale Dr. Slaa anaposema kwamba kwa kawaida Chadema inajadili masuala na sio watu, kwa mtazamo wako, Chadema ifanye nini kuboresha kile anacholenga kukijenga Dr. Slaa, hasa katika mazingira ya itikadi bora na sio bora itikadi? Kwani ni dhahiri kwamba kwa Sasa Chadema hawana itikadi bora, bali bora itikadi; same applies to CCM;

Nimependa pia hoja yako kuhusu mwamko wa wapiga kura uchaguzi wa 2005, kwani unazidi kushindilia hoja yako kwamba mwenendo wa wapiga kura wengi Tanzania ni kuchagua WATU, na sio chama wala masuala yanayosimamiwa na Chama; Kuna ukweli katika hili, lakini je, nini mtazamo wako kuhusu upigaji kura kwa wabunge kwa vigezo nilivyojadili vya LOCALISM vis-a-vis vigezo vya NATIONALISM kwa nafasi ya Urais?
 
Back
Top Bottom