Chadema Mwanza

Jeho

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
5,053
5,503
Leo wanafanya mkutano wa hadhara Mecco kaskazini pamoja na uzinduzi wa ofisi, hii ni kwa mjibu wa matangazo yanayoendelea kutangazwa muda huu. Eneo utakapofanyikia ni katika viwanja vya majanini kuanzia saa 8:30 mchana. Madiwani wa chadema watakuwapo pamoja na meya wa jiji la Mwanza ndugu Manyerere. Nawasilisha
The unseen is illustrated by the seen.
 
Hivi kulikuwa na haja ya kutaja hilo neno kweli? Sidhani kama Mecco ni kubwa kiasi hicho hadi ielezewe kwa pande nne za dira. Anyway, hata sumaku ikining'inizwa ina-point Kaskazini.
 
Hivi kulikuwa na haja ya kutaja hilo neno kweli? Sidhani kama Mecco ni kubwa kiasi hicho hadi ielezewe kwa pande nne za dira. Anyway, hata sumaku ikining'inizwa ina-point Kaskazini.

Hiyo ni kwa mjibu wa Chadema, labda wao wameamua wawe na tawi liitwalo mecco kaskazini, na hapa ninapoandika tawi la mecco kaskazini lipo mbioni kuzinduliwa.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Mkutano umeshaanza lakini mahudhurio na F -ve. Hakuna watu wengi labda itakuwa wananchi wameshaanza kuwachoka.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Manyerere ameanza kuongea na anasema kuchukua nchi mwaka 2015 si swala la kuuliza.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Charles Chinchibela ambaye ni diwani kata ya mahina na naibu meya amekaribishwa na msitahiki meya ili aseme machache. Na anasema, wameamua kuanzisha matawi kila mtaa utakuwa na tawi, na sababu iliyopelekea uamuzi huo ni kwa sababu zamani watu walikuwa wanadai Chadema hawana hata ofisi kwa hiyo hawatakiwi kupewa nchi. Lakini sasa wanawategea tanzi wananchi ili kisiwepo kisingizio cha ofisi ili 2015 iwe kura tu kwa chadema.
The unseen is illustrated by the seen.
 
Manyerere kasema kwa wale wanaohitaji kadi za chama anawanunulia mwenyewe, na watu ambao anawanunulia ni 30.
 
Kingine alichosema ni kujisifu tu, na alisema kwamba wao(chadema) wanafanya yale ambayo Ccm alishindwa kufanya. Mfano juzi alisaini mikataba 17 ya ujenzi wa barabara 17 hapa jijini. Na pia kasema barabara hizo zitajengwa kwa mawe.
 
Back
Top Bottom