Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,305
Great Thinkers,
Habari zenu na ni matumaini mu wazima wa afya na wale wanaumwa ni mategemeo yangu watajaaliwa afya na siha njema na Mwenyezimungu.
Tangu kukamatwa kwa viongozi wa chama kikuu cha "upinzani" kumetolewa kauli nyingi sana hapa jamvini na wapenda "chama" na nyingi ya kauli hizo ni za kuvuruga amani na utulivu zenye lengo la kuchochea machafuko na umwagaji damu! Bila kujielewa au kwa kuelewa wengi wamediriki hata kusema "watapindua" nchi na ndio uhuru wa kweli utapatikana! Nimejiuliza watu wenye kuweza kupindua nchi lazima watakuwa na majeshi yao sitaki kuamini kuna jeshi zaidi ya jeshi la ulinzi na usalama la Tanzania. Tumekuwa tukisikia watu wakipewa vyeo vya "kamanda" na "mpiganaji" nadhani hatuhitaji kupigana tunataka maendeleo yatakayo leta tija kwetu na kwa vizazi vijavyo.
Ndugu yangu Waberoya ameelezea nini kile wananchi wanacho kitaka katikama thread yake https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...a-maslahi-ya-taifa-they-are-just-another-tool japo wengi wenu mmeona kama ni kejeli kwa sababu hoja zake ni za kujenga na nyie sera yenu ni ya kubomoa na kuleta chuki na mifarakano wengi wenu hamkuipokea wala kuitafakari. Sisi tunahitaji utaifa kwanza! tunataka Tanzania iwe nchi yenye kutawalika! tunataka watoto wetu waje kuiridhi nchi ikiwa kwenye hali ya kutawalika!
Imefikia wakati napata wakati mgumu sana kutofautisha wanachama wa cdm na waumini wasabato masalia. Kuna fikra zenu na mawazo mnayoyatoa humu jamvini ni ya kufikirika zaidi kama yale ya kusafiri bila ya passport wala visa!
Nafasi mnayo ya kujenga Tanzania msije mkaandika historia ambayo itakuja kuwa chungu kwetu na kwa vizazi vijavyo. Tujifunze ustaarabu kidogooooo tujaribu kuipenda nchi na si kuwapenda "wapiganani" na vyama. Hii nchi itaendelea kuwepo lakini hawa "wapiganaji na makamanda" pamoja na vyama vyao vitakufa!
Ushauri wangu mdogo sana kwenu mlio na upofu wa kutoona uzuri wa maelewano/mshikamano/uhuru wa kwenda popote ni kuwa kuna nchi zina zilianza chokochoko kama zetu lakini mpaka leo hazitawaliki moja wapo ni Somalia.
Nimesikitishwa na ndugu jangu mmoja ambae ni memba nguli hapa JF kwenye FB status yake amewataadharisha Polisi na wanasiasa "watawala" wawe na busara na kuepusha maafa kwa kinachoweza kutokea kwenye issue ya Mhe Mbowe. Huyu ni mwandishi anatumia fani yake kama mwandishi kujaribu kujenga mazingira kuwa mamlaka ni za kionevu na busara zifanyike. Pengine ataandika makala ya kuelezea uonevu wa mamlaka zilizokuwa zinashughulikia hii issue naamini haitajenga ila kuongeza chuki! Natamani tupate waandishi wenye kujali maslahi ya nchi zaidi kama kuwaonya wawaonye wahusika wote. Mfano amwonye mtu ambae ana kesi aweze kuhudhuria kesi yake yeye au wakili wake kwani kwa kutokufanya hivyo kunaweza kukafanya akamatwe na kuleta machafu anayotaka yazuiwe kwa kukwepa kufata misngi ya sheria.
Mwandishi Nguli Ngugi wa Thiong'o amepata kusikiaka akisema pale Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam kuwa, "Ukitaka kujua nchi itakuwaje kesho basi waangalie vijana wake wa leo" Vijana wa leo wa cdm ambayo kesho wanataka kuchukua nchi wanataka Arusha isikalike wanasema eti leo wataandamana na kuingia bungeni kuchukua viti! Kwahiyo mtaona kesho nchi yetu itakuwaje!
Najua hampendi kuambiwa ukweli lakini sioni tofauti yenu kifikra na wasabato masalia mnatofautiana kuwa nyie ni wanachama wa chama cha siasa wao ni waumini wa dini.