Mohammed Hamad
JF-Expert Member
- Jan 17, 2011
- 3,988
- 1,304
- Thread starter
- #21
Hivi unaelewa vizuri ni kitu gani kinafanya nchi ziwe na amani? Kwa mtizamo wako Tanzania kuna amani? Haki ndio msingi mkuu wa amani haki inapotoweka hiyo amani haipo tena
Hizo ni siasa mkuu unless unaishi ughaibuni amani ipo na itaendelea kuwepo Mungu awaangamize wale wenye kuombea mabaya nchi yetu. Kwanini nasema amani ipo? Nimeamka asubuhi nimetoka nyumbani mpaka ofisini sijashuhudia mauaji ya kurushiana risasi njiani wala sijakuta watu wamevamiwa na majeshi wakabakwa "haya yalipata kutokea visiwani" walipokuwa wakihubiri mnayohubiri leo. Lakini sasa hivi watu wamekaa kwa utulivu na amani. Unadhani hao mnaowashabikia kwa kutumia fujo wakiingia madarakani hawataendelea kulipana posho za mamilioni bila kuzikatia kodi? hamjui hizi kodi kwenye mishahara yetu midogo ndio zinazolipia mishahara ya waalimu? halafu utakuta jibaba zima linasimama linasema waalimu wanalipwa kidogo ilhali wanalipana mamilioni hawayalipii kodi ebooo! wanataka serikali ipate wapi pesa wakati wadau wanakwepa kodi?