CHADEMA lazima itashinda uchaguzi 2015 - Maige

Kwanini usingoje hadi jipu liwive?...Tutacomment nini sasa kwenye habari inayokuja kama tetesi!
 
Geita kuna Mengi ya kutujuza zaidi ya huyu Mpayukaji anayelilia Tonga hasa baada ya kujitia kitanzi cha madeni akidhani atasubiriwa mpaka auze twiga wote.Tupe taarifa za wale wakimbizi wa pale mahakama ya mwanzo Nyankumbu na maendeleo yao kisha tuambie nini kinaendelea na wale wadau wa Magwangala kule nyuma ya mgodo upite na Hospitali ya wilaya juu ya wizi wa vifaa vya gharama na matumizi mabaya ya ruzuku wanayopewa na Mgodi na usisahau kupita kwa Mkurugenzi wa wilaya juu ya kashfa za ngono katika ofisi ya elimu ya wilaya na matumizi mabaya ya madaraka ya Baraza la madiwani.Ukitoka huko Msalimie Vicky Kamata Mbunge wa viti maalum ambaye hajui hata Geita inafananaje.
 
Geita kuna Mengi ya kutujuza zaidi ya huyu Mpayukaji anayelilia Tonga hasa baada ya kujitia kitanzi cha madeni akidhani atasubiriwa mpaka auze twiga wote.Tupe taarifa za wale wakimbizi wa pale mahakama ya mwanzo Nyankumbu na maendeleo yao kisha tuambie nini kinaendelea na wale wadau wa Magwangala kule nyuma ya mgodo upite na Hospitali ya wilaya juu ya wizi wa vifaa vya gharama na matumizi mabaya ya ruzuku wanayopewa na Mgodi na usisahau kupita kwa Mkurugenzi wa wilaya juu ya kashfa za ngono katika ofisi ya elimu ya wilaya na matumizi mabaya ya madaraka ya Baraza la madiwani.Ukitoka huko Msalimie Vicky Kamata Mbunge wa viti maalum ambaye hajui hata Geita inafananaje.

AMA KWELI wewe MSEMAOVYO!!!!!


MIZAMBWA
NABII MTARAJIWA!!!
 
nenda adc sisi chadema atukutaki

Mara nyingi watu hawajui siasa za Tanzania zilipofikia sasa! Unajua mimi ninaanza kuwa na wasiwasi kama huyu Mh alitendewa haki kuondolewa kwenye Uwaziri! Nimejiunga facebook yake kuangalia malalamiko yake na kusema ukweli naanza kupata picha halisi na si muda tunaweza kuona jinsi mikono ya Ufisadi ilivyojikita kufanya lolote kama ukiingilia maslahi yao! haswa kwa kupitia media yetu uchwara! Wajameni mumpe nafasi ajieleze tusimhukumu wkati tunajua tunaongozwa na Mbayuwayu anayefaidia na kukirimiwa na ufisadi huu unaoutafuna nchi!
 
Maige anatakiwa akumbushwe kwamba CHEO NI DHAMANA na Si TAALUMA. Kwa mtazamo wangu ameaumia sana kwakua amechukua za watu bila kuwatimizia walichokua wanakitaka au amechungulia dili nene hivyo ni kama katemeshwa tonge mdomoni. Vyovyote viwavyo inamaanisha alitumia cheo kwa faida yake, ndugu zake na marafiki zake na hilo ni kosa kubwa sana la kimaadili. Amesahau kwamba alipewa kazi kimtandao kaondoka kimtandao.
 
Maskini, Cheo kinamchanganya, kwani alikuwa anafanya kazi gani before haya mauongozi, kutemwa tu uwaziri, anataka Chadema twiga kilishaeleweka?!, embu atulie nyumbani kwake asizidi kujiumiza kichwa zaidi, akachukue trekta akalime matunda apeleke ulaya!, asijiongezee kesi na kashfa kupitia uongozi Bongo
 
Katika hali isiyo ya kawaida waziri huyu aliyetemwa ambae anaonekana kama kondoo wa kuchinjwa kinyuma na walipigwa chini wengine ameonekana akiwa anasononeka sana na kuvuliwa kwake kwa uuzaji wa TWIGA na Wanyamapori ambao yeye anakiri akipata muda atasema wale wanyama walikuwa wa nani liwalo na liwe, Akiendelea kukinyamba chama chake kwa kutanabaisha kuwa safari imefika kikomo na sikio la kufa halisikii dawa.....akiwa kama abiria ndani ya basi ajualo linaenda kupinduka sasa Maige kufanya uamuzi wa busara kuamua kushuka kwenye basi hilo......ntawajuza lini na wapi ngojea niendelee kupelemba habari hizi kwakina baadae ni dadavue humuhumu jamvini.....JF reporter Geita

maneno yenye RED yanatosha kumfikisha kwa pilato....sheria za nchi zipo wazi kwa mtu aliyeona uovu lakini akauficha
 
Haapa ndo naona mapungufu yake, huyu uwaziri aliupenda kuliko hata mama yake, mbona wenzake akina Ngereja wako kimya hata huwezi jua kama wapo Tz, huyu ni mtoto asiye na maadili.
 
Tatizo hawa jamaa wakipigwa chini ndo wanakuja na hizo ooooooooooo ntasema yote! Kwa nini hakusema kabla! Kwa nini angojee mpaka yamkute. Na asiposema kabisa! Yeye anafikiri CCM watamwacha mpaka aseme. Asitishie watu huyo! utoto unamsumbua! He was not born to be minister! Ilikuwa bahati basi nayo imemponyoka! Asubiri bahati nyingine labda atabahatisha!
Yaani woooooooooote weshafikiri kuwa CDM ndo kimbilio la malapulapu! Kuna vichwa tunavisubiri sio hawa!
 
Wana JF, P/se sisi wana Shy/Kahama twaomba mpe nafasi asikilizwe Mbunge Wetu, sisi yanayoendelea huku Shy kwa maana ya majimbo yetu ya Khma, Msalaa, Solwa na mengineyo tunayajuwa pamoja na Mambo aliyofanyiwa Mbuge wetu Maige. Sisi vijana kwa Wazee tunamwamini Mbunge wetu, na tumempa instructions kwamba ahamie CDM na yeye amekubali na siku itafika tu atatangaza na tumrudishe huyohuyo kwa CDM na wala si CCM maana tunamwamini. Sasa tunaomba sisi wananchi wa Msalala tusikatishwe tamaa ya ushauri tuliompa. Tunaomba apokelwe CDM bila mashariti yoyote, yeye ataanika wazi wale aliowagusa maovu yao. Amezunguka sana vijiji vikubwa vya msalala lakini kila anakopita wanamtaka ahame kwenda CDM. Jamani tusimhukumu kwamba yeye mwizi atawaambia. Nyumba kama nyumba lazima ya dola $ 700 mil mbona hata JK, Mkapa, na mawaziri wengi tu wanazo? tumpokeeni jamani, ni mchapa kazi kwetu na bado tunamwitaji
 
mwandishi/mleta mada mwenyewe mzabina zabina hivi,yaani anaandika utadhani kabanwa na mlango.toa taarifa iliyokamilika wafikiriaji wakuu wapime
 
Hatupokei wezi, anajua kwa vile 2015 tunahamia magogoni ndiyo ahamie? kama yeye si fisadi alishindwa nini kuwazuia au kufichua anayehujumu rasilimali za nchi kwa manufaa binafsi? Kuitaka CDM ni tamaa zake za madaraka? He is just a dreamer hatakiwi huku.

Pole pole mkuu, Mwache aje. Kwanza atahitajika kueleza yote ajuayo kuhusu ufisadi huo, pili atahitajika kutubu mbele ya umma wa watanzania, tatu tutakuwa tumepata ushahidi wa kutosha hivyo atafunguliwa mashitaka pamoja na wale wote atakao wataja.
 
Kama unajua ukweli wowote ili ukweli huo ukuweke huru tena huru kweli kweli sema sasa, nakushauri tu kwa nia njema sema sasa. Kwa kifupi suala la kutosema ukweli wote limemgharimu sana EL, Mwakyembe, Sitta na bado litawagharimu wengine kama wewe.
 
Mi sitamuelewa mpaka hapo atakapotutajia wale twiga wetu kutoroshwa ulikuwa ni mpango wa nani kama si yeye
 
Back
Top Bottom