Bollo Yang
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 440
- 50
Mfa maji heshi kutapatapa! CHADEMA sasa wanatapatapa!!
Mimi sina ugomvi kabisa kwa vyama vya upinzani kushirikiana vyenyewe kwa vyenyewe -- na hata kuungana, iwapo sheria na kanuni zinaruhusu. Kinachonikera ni kwa chama cha upinzani kushirikiana au kuungana na chama kilichopo madarakani.
Bila shaka CUF wamelitambua hili na Prof Lipumba -- ambaye naamini kabisa ni kiongozi ambaye angefaa kabisa kuwa rais wa nchi hii -- amejikuta njia panda kutokana na yaliyojiri huko Visiwani kwa chama chake.
Na ndiyo maana juzi alionekana kumsapoti Mbowe alipokamatwa na polisi. CDM nawaomba wakutane pia na Profesa ili kuona taifa linaokolewa vipi kutoka kwa hao mafisadi, na ambao sasa pia wamekuwa wauaji wa raia.
Huwa nawaza: Jee sasa hivi Profesa akitangaza kuhamia CDM -- itakuwaje? nadhani watakaochanganyikiwa sana sana siyo CUF, wala CCM -- bali ni CDM! Just think about it!!!!!
Tunapongeza hatua mlizoamua kuzichukua CDM lkn tahadhari ni muhimu hasa kwa vyama kama CUF na TLP. NCCR wameonyesha kuwa katika njia moja nanyi hata kihoja. Umakini na busara za hali ya juu ni lazima vitumike katika hili. Twende nalo taratibu tusikurupuke.
Tahadhari ni muhimu saaana,ninapenda sana ushirika huu ingawaje tatizo langu bado liko palepale...kwamba CUF iliyokuwa inaikejeri CDM,leo wanaona CDM itawafaa?TLP kama chama sioni tatizo ila tatizo naliona kwa Mrema,huyu mzee katu sitakuja nimwelewe kamwe,ni zaidi ya kinyonga,ni zaidi ya popo,sidhani kama atakuwa na jema kwa CDM kwa 100%
Ushauri wangu,ni kweli tumeyasikia mengi,tumeyaona mengi,nawashauri CDM wawe waangalifu sana na waanzishe chombo maalumu cha kufatilia na kuripoti ushirika huu kwa ukaribu sana ili badala ya kujenga tusije kulia kilio cha kusaga meno
juzi kati tumetoka kuletewa thread humu ndani iliyokuwa ikisema- wakati sisi tunalala wenzetu wanakesha,amini usimini,tupende tusipende magamba yako kila mahali na nina uhakika hata kwenye ushirika huu wataingia ama phsically ama spiritually.... they are so opportunists!
Mbowe ndio anaomba kuangana na TLP, NCCR, CUF, vipi mkuu utaama chama au utakubali na wewe ndoa
Ngekewa said:Hamadi Rashid sie alieleta Serikali ya Mseto kule Zanzibar ambako mlitowa matusi ya nguoni, mlisahau msemo wa Waswahili " Msitukane wakunga na bado hamjazingoa.
hivi upo nchi gani? kwanini haufuatilii mambo ya nchi yako ? aliye kudanganya hivyo ni nani? pole sana be updated IQ ikutume kujadili hoja za msingi toa mpendekezo ya kujenga kulingana na upeo wako CDM wataungana na yeyeote maadamu ni kwa kulinda na kukuza demokrasia ya nchi kama unaelewa fuatilia UCHAGUZI wa mwaka janaChadema si mlisema chama cha upinzani Tanzania ni kimoja tu, sasa imekuaje tena mnaanza mchakato wa kushirikisha vyama vingine vya siasa, miezi sita tu taingia kuundwa kwa Baraza la Mawaziri Kivuli mpo hoi, Chadema-JF, sijui mtaama Chadema wakiungana na CUF,NCCR Mageuzi, UDP, TLP
Kafulila huyu si yule aliyewahi kuwa Chadema na baadae wanamfukuza ndio akaingia NCCR.
Sasa vipi wanakaa nae meza moja?
Nashangaa!!!!!!!!!!!!???
Kafulila huyu si yule aliyewahi kuwa Chadema na baadae wanamfukuza ndio akaingia NCCR.
Sasa vipi wanakaa nae meza moja?
Nashangaa!!!!!!!!!!!!???
Acha ujinga wako wewe!Sasa mtu kama Sugu, Lema au Wenje, wanaweza kweli kuchambua bajeti ya wizara yoyote zaidi ya maandamano
Kwenye siasa hakuna adui wala rafiki wa kudumu. Ingawa binafsi nawaona jamaa zangu wengi wa Kigoma ni wabishi tu wasio na msimamo hata kwa maamuzi ya pamoja.Kafulila ni kichwa kile, na wanajilaumu kwa nini walitumia jazba ile kumfukuza, walim-understate kwa kusema eti Kafulila ni mtu mdogo tu kama sisimizi ndani ya CDM lakini leo wanamwona ni mkubwa zaidi ya tembo ndani ya siasa za Tanzania.
Kuna gazeti moja limeandika likiwakariri wasomi wa Nchi hii wakipendekeza mishahara ya WABUNGE itofautiane kulingana viwango vya elimu, uzoefu. Nadhani si haki Sugu kulingana mshahara na Zitto!Sasa mtu kama Sugu, Lema au Wenje, wanaweza kweli kuchambua bajeti ya wizara yoyote zaidi ya maandamano