Tusker Bariiiidi
JF-Expert Member
- Jul 3, 2007
- 5,520
- 2,091
Jengo na eneo lilipo pia huleta heshima kwa jamii... Mifuko mi-5...
Hilo jengo la dodoma limejengwa na wananchi, sio wana ccm. linapaswa kurudi serikalini haraka. cha kwanza ninacho waomba CDM wakishika madaraka ni kurudisha mali zote zilizoprwa na magamba.
Ubarikiwe mkuu,Wana JF nawashikuru kwa kuchangia. Nimefurahi kuona kuwa wengi humu mna wazo linalofanana na langu. Ikumbukwe kuwa posti hii imekuja kwa nia njema ili kuhamasisha jambo hili.
Ni ukweli usiopingika kuwa kuaminika kwako kunatokana pia na wewe ulivyojiweka. Huwezi kutoka katika kajumba ka nyasi tukakupa kazi ya kusimamia maghorofa. Kwa mliobahatika kufika pale makao makuu mtakubaliana nami kuwa sura ya kitaifa inayoonyeshwa na CHADEMA utaihitaji kuiminya sana ili iingie kwenye kajumba kale.
Naileta kwenu ninyi viongozi muanze mara moja kuhamasisha uchangiaji ili jengo linunuliwe au kujengwa mara moja. Hii haimaanishi mambo mengine yasiendelee. Yote kwa pamoja yanawezekana. Niiteni hata mimi nitachangia!!