CHADEMA jengeni ofisi

mangifera

Member
Oct 15, 2011
47
34
CHADEMA ni chama kinachoaminika sana na jamii na kinatarajiwa kuchukua madaraka pindi hawa magamba wakipigwa chini.
Lakini kusema kweli kale kanyumba mnakotumia kama makao makuu pale kinondoni kanatutia wasiwasi. Ni nini kinachowafanya msijenge?!! Ni ukata? mbona wabunge mnao wa kutosha na ruzuku ni nyingi. Kama vipi mwaweza hata kuchangishana mkawa na mjengo wa maana ili muwe na sura ya kuongoza nchi!!
 
Hiyo ni kweli kabisa. Kale ka nyumba kanatia aibu bwana! Tujenge li jengo la maana libebe maofisi ya heshima, tuko tayari kuchangia ofisi ya kisasa.
 
Kweli pale kichefuchefu, ila mkuu harakati huzaliwa katika mazingira km hyo tuvute subra nadhan itajengwa ofice nzur
 
Wakianza kujenga ofisi ndo nitaanza kuwaamini kama chama chenye nia ya kuwatoa CCM madarakani.
 
kweli hata mikoani wajenge pia,nami nko tayari kuleta roli la mchanga. Tujitolee.
 
Ofisi zitajengeka kwa kutumia maandamano na kulia lia kuilaumu serikali?
 
Ndugu zangu,

Nakubaliana na nanyi kwamba ofisi yetu ni ndogo na haiakisi mjonekano wa chama kwa wakati huu.

Naomba tuelewane kwamba chadema kwa sasa inatumia kila shilingi iliyopo kufanikisha elimu ya uraia inayolenga kuokoa wananchi hivi punde, ni ukwelu usiopingika kwamba chama chetu kwa sasa kina vijana wengi bungeni ambao ninyi ni mashahidi wa jinsi wanavyopigwa vita na chama dola, ccm, na hivyo vijana wetu wanatumia rasilimali zao zote kuhakikisha wanawafikieni na kuwatia moyo na kuwapa elimu ya uraia ili kuendelea kuwanusuru na madhambi ya ccm. Hii yote inahitaji fedha.

Ofisi yetu ni ndogo japo kwa hakika ni kituo bora cha demokrasia hapa Tanzania na napenda kuwahakikishia ndugu zangu kwamba tunajitahidi kuitumia kadri tuwezavyo ili itutoshe na itufae wote.

Mipango ni mingi na mikakati ni mingi na katika yote haya nawaomba mvute subira kwani chama chenu daima kiko mstari wa mbele kusikiliza hoja zenu na kuzifanyia kazi. Sisi chadema tunalichukua hili na napenda kuwahakikishia kwamba litafanyiwa kazi na kupewa uzito unaostahili.

Ni mimi,
Pangu Pakavu
Nawasalimia.

Kweli pale kichefuchefu, ila mkuu harakati huzaliwa katika mazingira km hyo tuvute subra nadhan itajengwa ofice nzur
 
siyo siri!lori mbili za mawe niko tayari!Chadema acheni mzaha!jengeni ofisi yenye hadhi ya chama!
 
Sidhani kama hoja yenu ina uzito, chama sio ofisi bali chama ni kuwafikia wananchi, sera nzuri za kuinua uchumi wa nchi.
swali; c.c.m wanalojengo zuri kule makao makuu dodoma, mbona nchi bado masikini miaka hamsini ya uhuru? (kilomita 20 kutoka ikulu hakuna maji ya bomba)
 
Ofic nzuri ya chama ipo kwenye mioyo ya watanzania,kama majengo ndo kukua kwa chama basi yatajengwa baadae lkn kwa sasa kazi moja kutoa elimu ya uraia iwaingiea sawasawa wtz ya kujitambua
 
CHADEMA ni chama kinachoaminika sana na jamii na kinatarajiwa kuchukua madaraka pindi hawa magamba wakipigwa chini.
Lakini kusema kweli kale kanyumba mnakotumia kama makao makuu pale kinondoni kanatutia wasiwasi. Ni nini kinachowafanya msijenge?!! Ni ukata? mbona wabunge mnao wa kutosha na ruzuku ni nyingi. Kama vipi mwaweza hata kuchangishana mkawa na mjengo wa maana ili muwe na sura ya kuongoza nchi!!

chadema inahitaji kujihimarisha kwenye information technology kuliko kwenye issue ya majengo. ukiweza kuwasiliana na wananchama wako wote ktk wakati mufaka na kuweza kupokea feedback wakati wowote na kuzifanyia kazi ni kitu muhimu hata kama unawasiliana chini ya mti.
 
Sidhani kama hoja yenu ina uzito, chama sio ofisi bali chama ni kuwafikia wananchi, sera nzuri za kuinua uchumi wa nchi.
swali; c.c.m wanalojengo zuri kule makao makuu dodoma, mbona nchi bado masikini miaka hamsini ya uhuru? (kilomita 20 kutoka ikulu hakuna maji ya bomba)

Hilo jengo la dodoma limejengwa na wananchi, sio wana ccm. linapaswa kurudi serikalini haraka. cha kwanza ninacho waomba CDM wakishika madaraka ni kurudisha mali zote zilizoprwa na magamba.
 
nakubaliana na hoja hii, niko tayari kutoa mchango, CHADEMA anzisheni mchakato wa kuchangisha michango ya kujenga ofisi nzuri. Inaonekana support ipo ya kutosha. We need to show how real its by the slogan PEOPLES POWER
 
Ofisi sio jengo ni utendaji. Nani atabisha kuwa Jengo Letu La Bunge ni bora kuliko majengo yote ya Bunge Africa? Lakini hebu tujiulize tena juu ya ubora wa sera zinazotungwa humo kwa ushabiki na kulinda chama badala ya wananchi. Ndio humo Wassira anakochapa usingizi as if nyumbani hana kitanda.

Hata hivyo ningependa kuona CDM inapata jengo zuri zaidi ya ile nyumba.
 
Ofisi zitajengeka kwa kutumia maandamano na kulia lia kuilaumu serikali?

Hapana. Itajengwa kwa rushwa na ufisadi, kwa kuuza twiga, kwa kuhongwa suti, kwa pesa za RADA, kwa mrabaha wa 3% ya madini, kwa kuhudhuria kila msiba huku mambo ya maana yanalala, itajengwa kwa 10% tutakayopata baada ya kufanikisha DOWANS kulipwa, kwa kuombaomba kwa hisani kama tulivyoomba vyandarua, kwa nyongeza ya posho za wabunge, kwa udini na mahubiri ya chuki.

Umeshaelewa sasa itakavyojengwa eeeh?
 
Back
Top Bottom