CHADEMA, hapa Lwakatare alikuwa anamaanisha nini?

Status
Not open for further replies.
Mimi naendelea kuutafuta ukweli kupitia wataalamu wanao jua kucheza na upandikizi wa maneno na picha bandia kuwa za ukweli.[/QUOTE]

Mkuu km video haitokua ya kuchonga basi Lwakatare amewazunguka CDM kwasababu ukimsikiliza kwa makini maongezi ni ya upande mmoja (yameandaliwa) kutoka kwa lwakatare (kama lecture), wakati yule jamaa mwingine alikua anachombeza vimaneno kurudia rudia yale yaliyosemwa na lwakatare. kwahiyo haionekani km ni mpango(majadiliano).

Kingine ni position ya kamera inaonekana ni fixed (haichezi) km vile ni kamera kubwa ambayo lwakatare anaiona na ipo karibu sana na Lwakatare km ingekua kamera ndogo ya kujificha isingeweza kupata picha ya ukubwa ule.

Kingine ni eneo ambalo mpango unafanyika linaonekana halina usiri wowote, hivi kwa hali ya kawaida inawezaka mpango mzito km huo ukapangwa eneo lenye watu wengi wenye shughuli tofauti?
 
MJINGA ni wewe unaetetea upumbavu....!! Acha kushikiwa akili, CHADEMA SI BABA AKO WALA MAMA AKO kiasi kwamba uchafu wake uone taabu kuusemea!! Binafsi, sishikiwi akili na mtu kama unavyoshikiwa wewe!!
umesoma taarifa ya Bashe jinsi walivyokuwa wanafuatwa na polisi? au umekuwa mtaji wa kudumu wa ccm?
 
Ikithibitika kuwa huu ugaidi unnafanyika CDM .....Msajili anatakiwa kuifutIa usajili CDM ASAP.
Na hicho ndicho wanachokitafuta CCM, kutengeneza propaganda zitakazopelekea CDM kufutwa ili 2015 wawe huru. Ila muweni makini sana, maana mnaweza kudhani kwamba mnajitengenezea nafasi ya kutawala milele, mkajikuta mnaishia kuuawa kwa aibu kama alivyouawa Ghadafi, na familia yake yote ikateketea. Si rahisi hivyo kuizuia hasira za wananchi siku watakaposema sasa inatosha. Mimi nafikiri tumieni njia za busara zaidi kuliko hizi za mkato mnazozitumia sasa.
 
NARUDIA KUSEMA KWAMBA MUVI HII IMETENGENEZWA.

Ushahidi wa kimakosa katka uandaaji wa muvi hii unanithibitishia kwamba, waandaaji walipanga kujirekodi.

1. Mpiga picha anaanza kwa kumtaarifu Lwakatare kitu kuhusu "...Mic..." then Lwakatale anauliza "...mmh..." kisha anasema "...hapo sawa..." Halaf Lwakatare anaanza kuhutubia. Hii sio incidence ya kiintelejensia maana camera iliyotumika inaonekana kuanza kaz pale tu Lwakatale anapoanza kuongelea njama, Na hapo ndipo natambua lengo la mpiga picha kusema "MIC", alimaanisha "akiishika kwa chini ataziba mic kwa hiyo aiweke juu ya kitu tu" MAANA MUDA WOTE CAMERA HAITIKISIKI HATA KIDOGO.

2. Mtiririko wa maongez yao umejaa STORY zaid za matukio ya awali. Huku Mpiga picha akionesha hajui lolote yaan ni kama mtu mgen Tz na kwenye CDM, hasa pale anapohoji vitu vidogo vidogo kuhusu ZZK.

KWA UFUPI SIDANGANYIKI, Maana kama Yuda aliweza KUMSALITI YESU, Sembuse RWAKATALE. "CDM 4 LIBARATION"


kula like mkuu
 
Wadau, mimi niko ughaibuni na nimeona Clip ya kijasusi ikimhusisha Rwakatare ambaye inasemekana ni Afisa usalama wa chama kimoja cha siasa, bila shaka kama ilivyosemwa ni CHADEMA. Nimefanya uchambuzi wangu kama ifuatavyo: Mazingira ya Tukio: Hivi kweli ikiwa Rwakatare alikusudia kupanga njama kubwa kama hizo kwa maslahi ya chama chake, iweje akapangie kwenye mgahawa wa mamantilie ambapo wateja wanapishana wakinywa na kula, huku wahudumu wakiwa bize kuhudumia na hata mmoja wa wateja aliyekuja mgahawani wapo kusalimiana na hawa wapanga njama, huku wao wakiendelea kupanga njama hizo bila hofu. Inaingia akilini kweli hii??? ''Strange''. 2. Kamera ilipokuwa: Kwa wale waliosoma topic ya photography kwenye Geography wanaweza kuona jicho la kamera iliyochukua matukio hayo ilipokuwa. Kifupi ilichukuliwa ground photo na kamera ilikuwa mbele yake hivyo alikuwa akiiona. Sasa unawezaje kupanga njama kama hizo huku ukijua unarekodiwa??? Kama ilikuwa imewekwa mahala bila yeye kujua, basi coverage yake isingekuwa ndogo kisi kile kama passport size. Pia ingewa-cover na hao washirika wengine walao kwa kiasi kidogo, lakin picha ingekuwa pengine oblique na sio kama ilivyo sasa. 3: Watekelezaji/Washirika wa njama hii: Inawezekanaje ukampa mtu kazi ya kutekeleza njama kubwa kama hii, afu awe haijui kazi yenyewe. Inaonekana mara zote, anayeitwa Rwakatare akiwafundisha na kutoa maelekezo namna ya kufanya hiyo kazi, na wanaofundishwa wanaonyesha kutoijua kabisaaaaa hiyo kazi. Inawezekana kweli??? Pia anawafundisha nadharia ambazo ktk akili ya kawaida haziingii akilini, mfano ku-spray dawa kwenye gari pale litakapokuwa limefunguliwa vioo. Hiyo dawa itakuwa na mechanism gani ya kubaki kwenye gari hadi mhusika atakapokuja bila kutokea hapohapo kwenye uwazi ilipoingilia. 4. Mifano ya Mwangosi na Ulimboka: Rwakatare ametoa mifano ya Ulimboka na Rwakatare kwamba, hakuna haja ya kumfanya huyo jamaa kama walivyofanywa hawa kwani watu wata-sympathize. Mifano hii haihusiani na mipango anayojifanya kuipanga sasaivi kwani nani asiyejua kuwa Mwangosi alipigwa risasi adharani na polis. Nani asiyejua Mwangosi alikuwa mfuasi mkubwa wa CHADEMA. Nani asiyejua Ulimboka alikuwa akiungwa mkono na CHADEMA siku zote. Nani asiyejua Kubenea na hao wengine waliotajwa walikuwa na misimamo ambayo ilishabihiana sana na ile ya CHADEMA hivyo kuwa kitu kimoja hata kama hawakuwa wanachama. 5. Mannerism ya Rwakatare: Katika hii clip, jinsi Rwakatare anavyo-behave anaonyesha dhahiri anafanya maigizo na kwamba anarekodiwa. Hajakaa kidili hata kidogo. Anaopanga nao njama wanauliza maswali ya kiuandishi na sio maswali ya kufanikisha njama. Mfano wanamuuliza, ,,kwa hiyo huyu jamaa wa mwanachi katumwa na CCM'' swali kama hili halikuwa na nafasi ktk mipango kama hii. MY TAKE: CHADEMA wanapaswa ku-clear hili hadharani ikiwa kweli hawahusiki. Pili, Rwakatare anapaswa kusimamishwa haraka iwezekenavyo. Tatu, CHADEMA wanapaswa kutoa taarifa polisi na kuisaidia polis ktk upelelezi ikiwa kweli hawahusiki.

Mkuu gennessh!!!!

Heshima kwako.

Kwanza naheshimu analysis yako. Umejitahidi kiasi cha kutosha kuelezea jinsi clip hii fake inaidhalilisha baadhi ya watu walio tamka awali kwamba wana VIDEO za watu kupanga njama za mauaji. Sina haja ya kutaja majina kwani wao wenyewe walisha jitaja mara nyingi kwenye vyombo vya habari.

Ukweli ni kwamba jua linaelekea kuzama, na kila mbinu ambayo imetumiwa na MAGAMBA kufifisha juhudi za CHADEMA kuikomboa nchi hii kutoka mikononi mwa MAFISADI zinashindwa kwa nguvu kubwa. MAGAMBA wanacho kifanya sasa hivi, ni kujitahidi kuwaondoa CHADEMA kwenye agenda moja kuu ya KUIKOMBOA Tanganyika kwa kutengeza matujio ambayo yataifanya CHADEMA iwe inayashughulikia ili ijisahau.

Tunaona mambo mengi yanayo pandikizwa kwa CHADEMA kutoka taasisi mbalimbali kwa lengo la kuwaondolea CHADEMA concentration ya kujijenga kwa wananchi, ikiwa ni pamoja na kutoa elimu ya uraia na kujua haki zao. MAGAMBA wameshaona jinsi mipango yao na utekelezaji wake unavyo kubalika kwa wananchi. MAGAMBA wamesha PANIC kwa kujua kwamba wamesha chelewa sana. Hivyo kazi iliyo bakia kwao ni kujitahidi kuchepusha uelekeo wa CHADEMA kwa wananchi kwa kutengeneza MATUKIO ambayo yataifanya CHADEMA ijizatiti kuyajadili.

Lengo langu hapa ni kwamba, CHADEMA haina haja ya kuhangaika na hii Video Clip ya hawa walio kata tamaa ya kuongoza. Kama kweli clip hii ni ya kweli, ilikuwa inangoja nini kutolewa kama ushahidi kwa Police wakati Mwigulu alishaielezea kwamba anayo kwa muda mrefu sasa? Ukweli ni kwamba mchezo huu ulikuwa umetangazwa kabla ya stori kuandikwa na hadi leo hii igizo ndiyo limefanyika na clip ambayo haina sifa za ukweli imetolewa.

Kumbuka kwamba, humu kwenye jamvi watu walisema wazi kwamba, wanajuwa nani mtaalamu wa IT atakae itengeneza hiyo video! Na alitajwa kwa jina.

CHADEMA TAFADHALI MSIPOTEZE MUDA KUHANGAIKA NA VIDEO HII. KAMA VYOMBO VYA USALAMA VISHINDWA KUMWAMBIA MWIGULI AWASILISHE HIVYO VIELELZO VYA KUPANGA KUHUJUMU WATU HIYO SIO KAZI YENU.
 
Ccm bana,iweje lwakatare avae tshirt ya Cuf?

Hiyo T-shirt ina nembo ya PPF sioni neno CUF


U435P6lncjrkxbCzAAAAAElFTkSuQmCC
 
Na hicho ndicho wanachokitafuta CCM, kutengeneza propaganda zitakazopelekea CDM kufutwa ili 2015 wawe huru. Ila muweni makini sana, maana mnaweza kudhani kwamba mnajitengenezea nafasi ya kutawala milele, mkajikuta mnaishia kuuawa kwa aibu kama alivyouawa Ghadafi, na familia yake yote ikateketea. Si rahisi hivyo kuizuia hasira za wananchi siku watakaposema sasa inatosha. Mimi nafikiri tumieni njia za busara zaidi kuliko hizi za mkato mnazozitumia sasa.

Mkuu mi si mwana CCM, Mi ni mpiga kura ninayependa FAIR PLAY sina chama ....ikikosea CCM iadhibiwe, ikikosea CDM/CUF/NCCR waadhibiwe EQUALLY.
 
Haya mtaalamu hebu tiririka ili uniondolee kuta za mashaka ambazo kwa muda mfupi zimejengeka kwangu kufikia level ya lintel,hebu saidia mkuu.
Mkuu kwanza Mazingira ya hii picha ni ya Zamani na Nimetafuta Picha nyingi za Lwakatare hadi za wiki hii lakini hii sura iliyoko kwenye Video ni ya Mwaka 1999.Zaidi nimejaribu Ku-edit hiyo Video nimekuta zipo sauti mbili ambapo Original sector iko Erased hapo sauti inayotoka siyo ya Kile anachokiongea Lwakatale. Ki ukweli hiyo Video ilirekodiwa Bukoba Mjini mwaka 1999 na alikuwa anaongea Baadhi ya Madiwani waliomtembelea kwenye ofisi zake kipindi yeye ni Mbunge wa Bukoba Mjini.Over. Matahila naona walijipanga timu kuja kueneza uongo.
 
Kwanza Mazingira ya hii picha kwa jinsi yalivyo utaelewa kabisa kwamba ni ya siku nyingi sana na pili anagalia sura ya Lwakatale aliyonayo kwa sasa na fananisha na hiyo ya Video utaelewa tofauti. Hapa kwenye Server yangu nimetafuta picha nyingi hadi za wiki hii na sura ilioko kwenye video hapo juu ni ya Lwakatale ya Mwaka 1999.Kwa hiyo wanabodi msichangie upuuzi wa magamba.Net inasumbua ila ikikaa sawa naweka sura zake toka mwaka 1995 hadi sasa.

Mkuu unasema picha ni ya 1999, Je mwaka huo ndo Mwangosi alikufa? Au hadi sauti unaikana? Mbna unakwepesha ukweli kwa kutoa uongo mwingine?
 
Majibu yote yapo hapo, kweli wamemumbuka, duh! Njia ya muongo ni fupi sana, haiwezekani uwe kachero alafu muende kufanya kama bongo movie.

NGOJA ni ISHUSHE kabla hawaja weka NYINGINE, Bada ya kwenda ku EDIT haya MAKOSA yao.
Mkuu hili ndo la msingi, tuweke kumbukumbu vyema kwani hawakawii kuibuka na new edition kwa kuzingatia kasoro tulizo waeleza hapa! Pole zao hadanganywi mtu hapa... na hiki kichaka cha karanga hakiwafichi ng'o!
 
Mkuu unasema picha ni ya 1999, Je mwaka huo ndo Mwangosi alikufa? Au hadi sauti unaikana? Mbna unakwepesha ukweli kwa kutoa uongo mwingine?

kwa upeo wako nadhani unafikiri kujua kutumia jf pekee ndo teknolojia. Pole sana mkuu. Umechelewa sana
 
Haihitaji kuwa na degree kujua huu mchezo wa kuigiza unaoendelea hapa..unaweza kupanga misheni ya kumdhuru au kumuua mtu kwa staili hii? unajirekodi na sehemu ya wazi kama hii!! Chadema wanatakiwa ku act quickly huu ni mchezo mchafu na Lwakatare anaweza kuwa ametumika kurusha hili wakiamini ni kuihujumu chadema bahati mbaya,njia ya mwongo ni fupi na hii yaonekana ilirekodiwa kwenye simu na bahati mbaya sana hii imepostiwa tu hapa lakini ilikuwa vema kujua ni lini imerekodiwa hii..Hope imeshafika makao makuu CHADEMA!!"The truth always comes to the surface! lets wait"
 
1. Video ni ya kweli, haijatengenezwa kwa teknolojia yoyote!
2. Imetumika spy pen na ilikaa kwenye mfuko wa shati la alokuwa anaongea na Lwakatare.
3. Hapana shaka siasa hizi zimekuwa zikiendeshwa na vyama vyetu na watu wanapotezwa kwa mapenzi kwa vyama lakini wanasahau kuwa mikakati hii bila kujalisha inaandaliwa na watu gani, ina lengo la kuondoa maisha ya watanzania kitu ambacho ni DHAMBI KUBWA.
4. Lwakatare ni dhaifu sana, yeye kama mkuu wa kitengo cha usalama hajui namna ya kuongea kwa coded language na hata haelewi kuwa 'sasa am recorded'? Hakuishtukia spy pen?
5. Mashabiki wa CHADEMA waache ushabiki kwenye masuala nyeti na ya msingi, kama watanzania tusimame pamoja kukataa uhuni na ukatili wa namna hii, si kitu cha kuchekea wala kutetea. Lwakatare kama mkuu wa kitengo kupanga mikakati hii inashangaza sana!

BTW, this' what they normally (both CCM n CHADEMA) do. Wanaua sana!

Kilichotumika ni miwani, angalia 'angle' ya hizo shots.
 
Bado ndo nina download video ila tusiamini haya maneno.Technology imekua sana na mtu hawezi shindwa ku edit video kwa kuwawekea sauti za wewe utakacho waseme.
 
Lwakatare/CHADEMA,

Tafadhalini jitokezeni aidha mkubali na kuomba radhi au mkanushe na kuchukua hatua stahili, ukimya wenu utasambaza mengi yasiyotegemeka.

Ndimi.
 
Mkuu unasema picha ni ya 1999, Je mwaka huo ndo Mwangosi alikufa? Au hadi sauti unaikana? Mbna unakwepesha ukweli kwa kutoa uongo mwingine?

Hiyo sauti sio yake.Kama nilivosema kwamba Nimejaribu ku-edit hiyo Video na nimekuta Original Sector ya Sauti iko Erased kwa hiyo kama original imeondolewa ina maana Track haiwezi kuwa Original vile vile i mean hiyo imechanganywa vipande vipande na aliyeifanyia ujinga kama huo.Magamba hao Riz 1 na Mwenzake Nepi.
 
kwa kipindi cha miaka miwili mitatu sasa kumekuwa na matukio ya kinyama na ya uvunjaji haki za binadamu dhidi ya watanzania wachache wenye moyo wa uzalendo wa kuleta haki na usawa kwa jamii ya kitanzania iliyonyanyasika kwa kipindi kirefu.

Hivi majuzi Absalom kibanda mwenyekiti wa jukwaa la wahariri ameteswa na kufanyiwa unyama wa hali ya juu huku jamii ikibaki na maswali yasiyokuwa na majibu.

Aliteswa mpiganaji DR ULIMBOKA wakati yupo kwenye harakati za kuitetea sekta ya afya hapa nchini.

kijana ISSAH alimwagiwa tindikali huko igunga huku kukitokea mauaji ya kusikitisha ya mwandishi DAUDI MWANGOSI mkoani iringa na mwananchi asiye na hatia huko morogoro.

Watu wenye uchungu na nchi yao wamechoka wameona sasa basi..

Tukio la KIBANDA ni mwendelezo wa matukio yanayofuata.. Hivi karibuni mtasikia tukio lingine kubwa dhidi ya mwandishi mwandamizi wa mwananchi communications Ltd......sikiliza video.

Huyu anayeongea ni mchora dili mkuu kwa maelekezo ya mwenyekiti na katibu wake mkuu.

Hii ni part 4, part zingine zimekwisha tekelezwa Ila ZITAWEKWA HAPA WAKATI MAHSUSI UKIFIKA......
hizo part nyingine kwa nini usiwape polisi wako wazifanyie kazi,unagoja watu waue alafu utuletee tufanye nini, huo ujinga wenu umekuwa pembe la ngombe alifichiki. mwisho wenu ni 2015 na lazima jela inawahusu na kurudisha fedha yote mliofisadi.
 
Mkuu kwanza Mazingira ya hii picha ni ya Zamani na Nimetafuta Picha nyingi za Lwakatare hadi za wiki hii lakini hii sura iliyoko kwenye Video ni ya Mwaka 1999.Zaidi nimejaribu Ku-edit hiyo Video nimekuta zipo sauti mbili ambapo Original sector iko Erased hapo sauti inayotoka siyo ya Kile anachokiongea Lwakatale. Ki ukweli hiyo Video ilirekodiwa Bukoba Mjini mwaka 1999 na alikuwa anaongea Baadhi ya Madiwani waliomtembelea kwenye ofisi zake kipindi yeye ni Mbunge wa Bukoba Mjini.Over. Matahila naona walijipanga timu kuja kueneza uongo.

Mkuu nakubaliana na wewe 100%. Nimefanya kama ulivyofanya nimekutana na kitu kilele.

Hizo ndio video za Mwigulu Nchemba nadhani ameanza kuzirusha.

Katika hali ya kawaida Lwakatale sio mwehu akapange mikakati kama hiyo Mgahawani.
 
  • Thanks
Reactions: ESI
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom