CHADEMA + CUF: Maandamano ya kitaifa

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
AZMA YA KUTOSITISHA MAAANDAMANO YA KUPINGA MAUAJI YANAYOFANYWA NA POLISI
Imetolewa na Julius MtatiroNaibu Katibu Mkuu-Chama Cha Wananchi CUF – Tanzania Bara10/6/2011Chama Cha wananchi CUF kinasisitiza kuwa maandamano ya kupinga vitendo vya kinyama vya mauaji vinavyofanywa na jeshi la polisi dhidi ya wananchi wasioikuwa na hatia nchini yatakayofanyika tarehe 12/6/2011 yako palepale licha ya jeshi la polisi kupinga kwa sababu zisizokuwa na mashiko wala mantiki ya kikatiba. Kwa nini tutaandamana1. Tamko la Umoja wa Mataifa la haki za Binadamu la mwaka 1945, (The UN declaration of Human Rights of 1945) ambalo Tanzania ikiwa ni mjumbe rasmi wa Umoja wa Mataifa imeridhia,linatoa haki ya kuandamana ikiwa watu au chama kinataka kuonesha hisia zake kwa jamii husika ni muhimu kwa watanzania wote. 2. Katiba yetu ya jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977, ambayo tayari ina viraka zaidi 14 inatoa haki kwa Raia wa Tanzania vikundi au taasisi kutoa mawazo au hisia zao ibara ya 20 kifungu 1 3. CUF ni chama chama siasa chenye kauli mbiu HAKI SAWA KWA WOTE, hivyo basi kitendo walichofanya Polisi cha kufyatua risasi ni cha kinyama kilichokatisha haki ya kuishi ya mtanzania mwenzetu huko wilayani Urambo Mkoa wa Tabora, CUF, tutaandamana ili kupinga kitindo hicho na vitendo kama hivyo. Tutaandamana ili polisi wote waliohusika katika mauaji ya wananchi wasio na hatia wafikishwe mahakamani na wachukuliwe hatua za kisheria. 4. Moja ya malengo ya kuanzishwa kwa chama cha wananchi (CUF) ni pamoja na kuwaunganisha watanzania, kukataa aina yoyote ya uonevu, ukandamizaji, unyanyasaji, ubaguzi, na uadhalilishaji wa kisiasa au wa kiuchumi. Hivyo basi CUF kama chama chenye usajili wa kudumu nchini, kilichosajiliwa kutokana na malengo yake, kinacho haki na wajibu wa kuungana na wananchi kupinga unyanyasaji na uonevu unaofanywa na jeshi la polisi nchini. 5.Kifungu cha 43(1) cha sheria za Polisi na Polisi Wasaidizi sura ya 322 kama ilivyoandikwa upya mwaka 2002 kinaeleza kuwa waandamanaji wanapaswa kutoa taarifa ya maandamano kwa ofisa wa Polisi masaa 48 kabla ya maandamano. Aidha kifungu cha 43 (3) kinaeleza kuwa Ofisa wa polisi hawezi kukataza maandamano chini ya kifungu cha 43(2); isipokuwa iwapo atajiridhisha kuwa mkusanyiko huo utasababisha uvunjifu wa amani au kuathiri usalama wa nchi au kuvunja utulivu wa nchi au kutumika kwa malengo yasiyo halali. Kwa manti hiyo kukataza maandamano bila Polisi kusema maandamano ya CUF yatavuruga vipi amani ni uzembe wa dhahiri na kamwe chama hakiwezi kusitisha maandamano kwa kutekeleza uzembe.6.Hoja ya Kova kwamba maandamanao ya CUF kesi za Urambo na Nyamongo zimeshafikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria haina mashiko ya kwani kesi zote hizo si za mauaji bali ni kesi kukuasanyika kinyume na sheria.HIVYO CUF TUTAANDAMANA NA KUJARIBU KUTUZUIA NI KUVUNJA AMANI YA NCHI.NGUVU ZA POLISI KUTUZUIA ZITUMIKE KUTULINDA.
WOTE TUNAWAALIKA KATIKA MAANDAMANO.HAKI SAWA KWA WOTE.Julius Mtatiro,10/06/2011
watz itikadi za vyama tuziweke pembeni linapo jitokeza jambo mhimu kama hili rakudai haki ninashanga kuona hadi nyani anatuzidi akili huyu mnyama wanaushilikiano anaposhambuliwa na aduwi wenzake hutowa msada bira kujali chuki za nyumaKwauzembe wetu tunawapa polisi nguvu zakuendeleya kutunyanyasa usipo nyanyaswa leo yatakukuta kesho usimzalau aliye vunjiwa haki musaidie Wawo polisi wanashilikiana jee? Sisi tusishilikiyane mimi wewe tusijali upo chama gani wanao pigwa lisasi ni watz wenzetu naunga hoja
 
mtatiro kila siku tunakuona wewe tu vipi huko kafu hakuna viongozi wengine???? sijawahi kumsikia maalim!!
 
haya sasa...sinema nyingine inaanza! CUF wanaweza? Alafu Polisi ni wajanja. Yani wanazuia Ijumaa wakijua kuwa hakuna muda wa kwenda mahakamani ku-challenge decision yao. Haya bwana...kazi iendelee
 
Chadema yasemekana imekosa sababu ya kufanya maandamano dsm. Wakati mambo ya kutetea watanzania dsm yapo mengi.yapuuza imani yake katika maandamano ya dsm.kiongoz mmoja wa cdm akesha ofc za igp kumwambia 'ukiruhusu cuf waandamane na cc tutaandamana fanyeni lolote muwezalo kuhakikisha cuf awaandamani,'igp hamshangaa amwambia aliekutuma siku zake zina hesabika.
 
CUF wala hawana mpango wa maandamano bali wanachombeza ili ionekane kwamba wao wakinyimwa na CDM wanyimwe. Kwani ile CUF wametalikiwa na bwana wao?
 
Imekaa kiumbea zaidi,karibi Jf na ujifunze kuandika vizuri
CDM haifanyi maandamano kwa ajili ya kanda fulani ,ni swala la ratiba tu,subiri utaona mda utakapofika
 
Habari ya kutunga hiyooooooo! Ila uwezo wako wakutunga jambo ni mdogo sana ongeza juhudiiiii!
 
mtatiro kila siku tunakuona wewe tu vipi huko kafu hakuna viongozi wengine???? sijawahi kumsikia maalim!!

Unajua ndoa ya CCM na CUF ni kule Zanzibar tu. CUF huku bara wanahaha wafanyeje maana hata uchumba hawajauanza.
 
Limbukeni mkubwa wewe,unafikra mgando,unawaza kwa kutumia makamasi badala ya ubongo,kijana wa NAPE umetumwa haya nenda kachukue posho kwenye ofisi ya CCM kwa kazi uliotumwa ya kuandika upuuzi
 
Mleta mada hii ni mpuuzi .Bora watu waache ujinga wa kujaza thread za kipuuzi tujadili hoja za mashiko jamani
 
Back
Top Bottom