CHADEMA: A mob psychology na ole wenu

Kama si kwa huruma ya JK leo SLAA angekuwa kizuizini.

CDM endeleen kuleta makelele ila nawaonya kuwa nchii hi ina jeshi la kumlinda rais na katiba.

Uchaguzi umeisha makelele ya nini sasa?wanainchi wasiendee shambani wahudhurie maandamano mwisho wa siku wale mavuno yapi?

CDM munatumia kuwaongaa waandishi wa habari uchwara waandike upuuzi wenu ila hamtafua dafu

Mwisho SLAA kazeeka anasumbuliwa na magonjwa ya kizee atawapoteza
Kuna siku utatumwa kukata hicho kichwa chako.............NA KWA JINSI UNAVYOJIELEZA.............UTAKATA KWELI NA HUO NDO UTAKUWA MWISHO WAKO
 
KAULI YA KATIBU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU

VITENDO VYA JESHI LA POLISI KWA RAIA

NA

KUKAMATWA KWA WABUNGE WA CHADEMA


Katibu wa Wabunge wa Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA nalaani vitendo vinavyofanywa na Jeshi la Polisi kwa kusababisha mauji ya raia na kukwepa kufanya uchunguzi kamili na huru kuhusu wahusika wa vifo hivyo na kuingilia haki za msingi za jamaa za marehemu na wananchi wa eneo husika kushiriki katika maziko ya wakazi wenzao na hatimaye kupatiwa haki nyingine zinazostahili kutokana na madhila yaliyotokea.

Aidha nakemea hatua ya jeshi la polisi ya kuwakamata wabunge wa CHADEMA, Tundu Lissu na Esther Matiko wakiwa katika kazi ya kuwatumikia wananchi na natoa mwito waachiwe mara moja; wao pamoja na wote waliokamatwa nao.

Tundu Lissu (Mb) ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Sheria na Katiba aliitwa na wahanga wa tukio husika pamoja na chama kwenda kusimamia haki za msingi za familia za marehemu baada ya polisi kukataa kufanya uchunguzi na pia kuminya mazingira ya haki kupatikana.

Akiwa katika kutekeleza wajibu huo, jana (23 Mei 2011) alitaarifiwa na familia za marehemu na wananchi wengine kwamba polisi ina mpango wa kuchukua miili ya marehemu usiku na kuipeleka kusikojulikana na kuombwa kuungana nao katika kuwapa huduma za kisheria katika hatua zote. Aliambatana na familia za marehemu, wananchi na viongozi wa chama kufuatilia suala hilo ndipo alipokamatwa yeye na wengine na kuwekwa rumande kuanzia jana mpaka hivi sasa.

Esther Matiku ambaye ni mbunge wa viti maalum kupitia mkoa wa Mara anayetokea Tarime akiwa katika eneo lake la kazi leo (24/05/2011) alijulishwa na wananchi wa Nyamongo kwamba maiti ambazo walizichukua polisi kwa nguvu zingine wamezitelekeza njiani na kuitwa kwa ajili ya kushuhudia na kuchukua hatua zinazostahili kwa niaba ya wananchi. Akiwa katika kushughulikia suala hilo naye alikamatwa na jeshi la polisi na kuwekwa rumande mpaka hivi sasa.


Ifahamike kwamba matukio ya Nyamongo na Tarime kwa ujumla ni matokeo ya uongozi wa serikali kushindwa kusimamia vizuri sekta ya madini ikiwemo kuacha kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati wa miaka kadhaa sasa kutokana na vitendo vya ukiukwaji wa sheria na mikataba vinavyofanywa na kampuni Barick Africa Gold na vile vinavyofanywa na polisi na vya kifisadi vinavyofanywa na viongozi wengine wa kiserikali wanaonufaika na hali hiyo yenye athari kwa wananchi katika maisha yao kutokana na mauji, uchafuzi wa mazingira, upotevu wa mapato ya umma na watanzania wa eneo husika kutokunufaika kwa rasilimali.

Naungana mkono na wananchi na wadau wote waliotoa mwito kufanyika kwa uchunguzi huru wa vifo (inquest) ili hatua stahili ziweze kuchukuliwa na kwa nafasi yangu nyingine kama Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitatoa tamko karibuni lenye kueleza kwa kina udhaifu wa serikali ulivyosababisha mauji hayo na kutaka wahusika akiwemo waziri kuwajibika.

Aidha, kwa mara nyingine narudia tena kutoa pole kwa familia za marehemu ambao wanapitia kipindi kigumu wakati huu kutokana na matukio yanayoendelea; Mwenyezi Mungu awape uvumilivu wa kusimamia haki na ukweli kwa mustakabali wa taifa.

Imetolewa tarehe 24 Mei 2011 na:

John Mnyika (Mb)
Katibu wa Kambi Rasmi ya Upinzani
Na Wabunge wa CHADEMA
 
Bora wamfunge tu huyo mpuuzi slaa, kakosa kiti cha urais sasa anataka kuleta fujo, hii ndio tatizo la makabila yanayo penda fujo.

uliyaandika haya wakati njaa inakuuma naimani umeshakula na umeshiba sasa unajuta kwa nini uliyaandika hayo.
 
Kwa mujibu wa Katiba kila raia ana haki ya FREDOMA OF MOVEMENT, EXPRESSION AND ASSOCIATION. Hivyo wananchi wana haki ya kuchagua kwenda shamba au kuhudhuria maandamano.
Si lazima ulazimishe kiingereza
 
Mwenyewe unaona umeshawiiiiishi, pumba tupu hizi, hata wa kijijini hawezi kushawishika na mawazo chakavu kama yako.vua gamba ndugu yangu labda utaamka kwenye usingizi wako wa kisiasa. Utabaki hivyohivyo wanachukua nchi 2015.
 
Kama si kwa huruma ya JK leo SLAA angekuwa kizuizini.

CDM endeleen kuleta makelele ila nawaonya kuwa nchii hi ina jeshi la kumlinda rais na katiba.

Uchaguzi umeisha makelele ya nini sasa?wanainchi wasiendee shambani wahudhurie maandamano mwisho wa siku wale mavuno yapi?

CDM munatumia kuwaongaa waandishi wa habari uchwara waandike upuuzi wenu ila hamtafua dafu

Mwisho SLAA kazeeka anasumbuliwa na magonjwa ya kizee atawapoteza

Jee Ungemwambia Mandela hivyo? au hata Mwalimu? mawazo mgando yanawasumbua wengi. Kwanza madini yenyewe tunapata asilimia 3%. sasa ndio ndugu zetu wauwawe hovyo. :mod:
 
Kama si kwa huruma ya JK leo SLAA angekuwa kizuizini.

CDM endeleen kuleta makelele ila nawaonya kuwa nchii hi ina jeshi la kumlinda rais na katiba.

Uchaguzi umeisha makelele ya nini sasa?wanainchi wasiendee shambani wahudhurie maandamano mwisho wa siku wale mavuno yapi?

CDM munatumia kuwaongaa waandishi wa habari uchwara waandike upuuzi wenu ila hamtafua dafu

Mwisho SLAA kazeeka anasumbuliwa na magonjwa ya kizee atawapoteza

UTUMBO MTUPU! unalipwa na mafisadi wewe!
Nani mwenye nguvu kati ya Rais anayeanguka majukwaani hovyo na Rais wa wananchi anayehimili vitisho na vimbunga vya jeshi linalolinda Mafisadi??
Tafakari changanua chukua hatua
 
Mimi ni blogger sasa kuna simu nimepokea hivi punde kutoka kwa jamaa aliyejitambulisha kuwa anaitwa Richard amesema yeye ni mtu wa karibu na uongozi wa CHADEMA amenipa taarifa ya kusisimua sana kuwa mwanaharakati Tundu Lissu anajiandaa kuishtaki serikali Umoja wa mataifa kwa kile inachodaiwa kukamatwa kwake huko Tarime lakini sambamba na hilo anataka kuwasilisha malalamiko kwenye AMNEST INTERNATIONAL kuhusu kile kinachoendelea kwenye migodi nchini Tanzania.........Tungoje tuone
 
Mimi ni blogger sasa kuna simu nimepokea hivi punde kutoka kwa jamaa aliyejitambulisha kuwa anaitwa Richard amesema yeye ni mtu wa karibu na uongozi wa CHADEMA amenipa taarifa ya kusisimua sana kuwa mwanaharakati Tundu Lissu anajiandaa kuishtaki serikali Umoja wa mataifa kwa kile inachodaiwa kukamatwa kwake huko Tarime lakini sambamba na hilo anataka kuwasilisha malalamiko kwenye AMREF INTERNATIONAL kuhusu kile kinachoendelea kwenye migodi nchini Tanzania.........Tungoje tuone

Hapo kwenye red sijakuelewa?
 
Nilisema kabla kuwa tukio hili litakuwa fundisho kwa serikali ya Tanzania.
 
kila la kheri , huyu jamaa ni mtetezi wa haki za binadamu kwa hiyi anajua anachokifanya
 
Tumuombee mwanaharakati wetu jamani. Lakini pia nasikia amepigwa na polisi kuna ukweli wowote jamani?
 
mimi ni blogger sasa kuna simu nimepokea hivi punde kutoka kwa jamaa aliyejitambulisha kuwa anaitwa richard amesema yeye ni mtu wa karibu na uongozi wa chadema amenipa taarifa ya kusisimua sana kuwa mwanaharakati tundu lissu anajiandaa kuishtaki serikali umoja wa mataifa kwa kile inachodaiwa kukamatwa kwake huko tarime lakini sambamba na hilo anataka kuwasilisha malalamiko kwenye amref international kuhusu kile kinachoendelea kwenye migodi nchini tanzania.........tungoje tuone

so what?
 
Nadhani ni AMNEST International.

Umoja wa mataifa yuko Dr Asha Rose Migiro kwa hiyo ataweka chini ya carpet. Waanze kuwaandikia mabalozi wa nchi za nje walioko Tanzania na kuwaeleza in details ni kwa jinsi gani haki za binadamu zinakiukwa.

offcourse yule hawezi kuiadhibu nchi yake na wakubwa wake
 
Back
Top Bottom