Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,476
- 39,995
- Thread starter
- #81
WAAAT? hapo pekundu inaelekea hujakaa chini na kufikiria. Kwanza kuna transitional period katika govt yeyote.
Katika Tanzania hakuna Transition period hiyo ndefu kama nchi nyingine - Marekani kwa mfano, Uchaguzi hufanyika wiki ya kwanza ya Novemba, lakini Rais anaapishwa Januari 20! karibu miezi mitatu baadaye. Rais wa Tanzania akichatangazwa kashinda anatakiwa aapishwe ndani ya siku 7 (kwani hakuna mahakama inayoweza kuchunguza kuchaguliwa kwake hata kama mnafikiria kuna kura zimeibwa!) na ndani ya siku 14 anatakiwa awe na Waziri Mkuu. Kwa CCM hili ni rahisi sana, kwa chama kipya ambacho hakijawahi kushika madaraka huko nyuma kikishika madaraka kwa mara ya kwanza yafuatayo yatatokea:
a. Rais wake atatakiwa awe na Waziri Mkuu ndani ya siku 14 na Baraza lake
b. Atatakiwa awe na Mawaziri na Manaibu (kama inahitajika)
c. Atatakiwa awe na Mwanasheria Mkuu
Hizi ni nafasi ambazo mtu yeyote anayetaka kuwa Rais anatakiwa awe anazo kichwani kabla ya kutaka kugombea Urais!
Rais mpya anapoapishwa tu, wateule wote wa Rais ambao hufanya kazi kwa ridhaa ya Rais hupoteza nafasi zao (hapa tunaonda wateule ambao wakishateuliwa na Rais, hawezi kuwaondoa kirahisi).
Hivyo Rais mpya atatakiwa aidha kuwaombea mabalozi, wakuu wa mikoa, n.k walioteuliwa na serikali ya CCM waendelee na nafasi zao au wote wajiuzulu ili aweke watu wake. Kama hatokuwa na watu hao tayari option anayobakiwa nayo ni ama awaombe waendelee na nyadhifa zao, au aache nafasi hizo bila kujaza huku akitafuta watu wa kuzijaza. Yote mawili siyo hekima.
Ni kweli, lakini Obama alijua kabisa anapoingia madarakni nani atamwomba kushika nafasi gani. Wakati anajiandaa kuingia madarakani kulikuwa na negotiation na background checks n.k kwa watu mbalimbali ambao walikuwa washike nafasi mbalimbali za uongozi. Alipoingia madarakani alianza kujaza nafasi za msingi kwa urahisi kwa mfano Ulinzi, Mambo ya Nje, Fedha, Mnadhimu Mkuu n.k Hawa siyo watu aliowatafuta baada ya kuingia madarakani.Katika kipindi hicho, kuna negotiations kibao zinaendelea katika chama kilichoshinda kuweza kujipanga vizuri. Chadema haihitaji kuja na list ya viongozi wake. Kwani Obama alikuja na list ya viongozi? Si walichaguliwa katika hii transition period. Na kuna wengine waliobaki kutoka serikali ya Bush.
Kumbuka a civil servant hatakiwa kuwa na mshikamano wowote na chama chochote. Kwa mfano Mkuu wa Majeshi, IGP
Wakuu wa mikoa siyo civil servants, ni political appointees, Rais mpya akiingia wote hupoteza nafasi zao., wakoo wa mikoa, wilaya, etc. Wao ni kufanyia kazi policies za the ruling party. Ama sivyo, uchaguzi ungekuwa ni kazi bure kama kila chama lazima kije na viongozi wote.hahahhaa
well if it suits you.This is exactly why naona bado unaumia na CCJ.hahahaha!