CCM Zanzibar: Uamsho ifutwe mara moja!

Ngida1

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
586
206
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeitaka serikali ya Mapinduzi kuifuta mara moja Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa kuwa inafanya kazi kinyume na malengo yake usajili.

Mbali na matusi ya nguoni na kumshutumu Maalim Seif kwamba anahusika na kundi la Uamsho walisema Maalim Seif hafai kuwa kiongozi kutokana na kuwa mbinafsi kwa kuwa ameisema serikali yake mbele ya viongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kuwaeleza kwamba jeshi la polisi na vikosi vya SMZ vinahitaji mafunzo ya kukabiliana na vurugu ili waweze kupata mafunzo ya kukabiliana na vurugu hizo bila ya kuvunja haki za binaadamu.

"Huyu Maalim Seif anawaambia UNDP kwamba jeshi letu la polisi linahitaji mafunzo ya kuwakamata wahalifu sisi tunamwambia polisi wetu na vikosi vyetu havihitaji mafunzo wewe ndio unahitaji mafunzo kwa sababu kwani wewe unalindwa na nani? Si hawa hawa polisi" alisema Khalifa."
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kwa hili ccm wameonyesha uzalendo kwa maslahi mapana kwa zanzibar! Uamsho wana lengo la kuivuruga zanzibar kwa mgongo wa dini!
Ccm wanaona maslahi yao yanakua hatarini ndo maana wanaweweseka na hii inawapa nguvu Ccm kutokana na kutotumia akili kwa hawa Uamsho na maalimu katika kudai zanzibar huru..

Kwanza uamsho lengo lao halikua dini hivyo wangesajili hii jumuiya kama ya uelimishaji masuala ya Zanziba na Misaa kwa Wazanziba alafu ndo wakinukushe bila kuchoma makanisa wala kukashifu ukristo maana ndipo wanapokwamia na hakuna atakayewavumilia hata kama watatendewa nini...

Tena kama wasingechoma makanisa hata mimi nilikua nipo tayari kwenda kupitia Tanga nikapambane na Ccm hadi muungano uvunjike pale Zenj maana hakuna anayetaka muungano ili Ccm na serikali yake ndo inaung'ang'ania tena bila kujali malalamiko ya wahusika
 
Aliyemfuta maalim uanachama wa CCM alikuwa kawaza mbali sana. Nadhani sasa mnaona madhara ya maalim. Alikuwa na njaa, sasa kala kavimbiwa anaanza kubeua.
 
CUF je wamesemaje? Wanaunga mkono kufutwa Uamsho? Manake ccm & cuf ni wamoja hawa, hadi wakatengeneza sirikali ya umoja wa kataifa kao!
 
Ccm wanaona maslahi yao yanakua hatarini ndo maana wanaweweseka na hii inawapa nguvu Ccm kutokana na kutotumia akili kwa hawa Uamsho na maalimu katika kudai zanzibar huru..

Kwanza uamsho lengo lao halikua dini hivyo wangesajili hii jumuiya kama ya uelimishaji masuala ya Zanziba na Misaa kwa Wazanziba alafu ndo wakinukushe bila kuchoma makanisa wala kukashifu ukristo maana ndipo wanapokwamia na hakuna atakayewavumilia hata kama watatendewa nini...

Tena kama wasingechoma makanisa hata mimi nilikua nipo tayari kwenda kupitia Tanga nikapambane na Ccm hadi muungano uvunjike pale Zenj maana hakuna anayetaka muungano ili Ccm na serikali yake ndo inaung'ang'ania tena bila kujali malalamiko ya wahusika
........

Kwani UAMSHO ndio wamechoma Makanisa? Mbona SMZ haikutaka Kuunda tume kuchunguza ni nani waliohusika! Au ndiyo UKITAKA KUMUUA MBWA NI LAZMA UMPE JINA BAYA KWANZA.
 
Naona yale makubliano ya kutokukosoana hadharani wameanza kuyageuka....ny way waifute UAMSHO....
 
ccm wanaona maslahi yao yanakua hatarini ndo maana wanaweweseka na hii inawapa nguvu ccm kutokana na kutotumia akili kwa hawa uamsho na maalimu katika kudai zanzibar huru..

Kwanza uamsho lengo lao halikua dini hivyo wangesajili hii jumuiya kama ya uelimishaji masuala ya zanziba na misaa kwa wazanziba alafu ndo wakinukushe bila kuchoma makanisa wala kukashifu ukristo maana ndipo wanapokwamia na hakuna atakayewavumilia hata kama watatendewa nini...

Tena kama wasingechoma makanisa hata mimi nilikua nipo tayari kwenda kupitia tanga nikapambane na ccm hadi muungano uvunjike pale zenj maana hakuna anayetaka muungano ili ccm na serikali yake ndo inaung'ang'ania tena bila kujali malalamiko ya wahusika
......

kwa hiyo uamsho walijisajili kama kikundi cha dini kwa hila?
 
Uamsho hawana haja ya kufutwa wafanye mambo mawili kama wanataka kuwa wanasiasa wajisajili rasmi; waingie ulingoni wamwage sera zao; nina uhakika wakigeuka kuwa chama cha siasa wataishia maeneo ya Malindi tu; vinginevyo wabakie kama uamsho kupigania wazinzabari waishi maisha ya kumcha Mungu; Uamsho kinaweza kuwa chombo kizuri sana kikitumika kwa misingi iliyoanzishiwa; Zanzibar kuna matatizo mengi sana ya kijamii ambayo Uamsho wanaweza kuisaidia serikali kuyapiga vita ukahaba; ushoga; madawa ya kulevya; ukimwi ni matatizo yanayoleta changamoto sana kwa wazanzibari!

Chama
Gongo la mboto DSM
 
Hilo lipo wazi kabisa UAMSHO = CUF wafuasi wake ni walewale na malengo yao ni yaleyale ya kutoyatambua mapinduzi ya Zanzibar..mi nadhai kifutwe ili ibaki CUF
 
Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, kwa hili ccm wameonyesha uzalendo kwa maslahi mapana kwa zanzibar! Uamsho wana lengo la kuivuruga zanzibar kwa mgongo wa dini!....

Laiti Uamsho, Ponda, et al. wangekuwa na muono wa kuwaunganisha watanzania wote bila kuegemea too much udini nchi hii ingeshakombolewa kutoka makucha ya magamba.

Inapotokea mtu anaongea issue inayogusa maslahi ya wananchi wote lakini katika kuongea huko hawezi ongea maneno kumi bila kutaja dini yake inakuwa khatari sana.
 
Ndoa ya CUF na CCM ishaingia sumu tayari, sidhani hata kama taleke rejea itafaa tena.
 
Aliyemfuta maalim uanachama wa CCM alikuwa kawaza mbali sana. Nadhani sasa mnaona madhara ya maalim. Alikuwa na njaa, sasa kala kavimbiwa anaanza kubeua.......

Ha ha ha ha ha! Kubeua kwa njia gani mkuu? Anaanza kuchafua hali ya hewa kama kipindi kileeeee. Chumba chote kimechafuka.
 
Hivi suala la kuchoma makanisa limeishia wapi? CCM - Zanzibar kwani leo ndio wanaona tatizo la Uamsho? Serikali yao ilikuwa wapi tangu Uamsho waanze? Walipochoma makanisa wakasema ni wahuni. Wahuni waliokamatwa ni akina nani na je hawana uhusiano na Uamsho?
Kwa kweli suala la Uamsho linaonyesha jinsi Serikali ya Tanzania ilivyo dhaifu au jinsi inavyoyaogopa baadhi ya makundi katika jamii. Uamsho walipigiwa kelele, Serikali ikaamua kwenda kulala na kuona wanaotaka Uamsho wapigwe marufuku ni HAMNAZO.
 
Laana ya ubaguzi imeanza kuwatafuna wa zanzibar, CCM Zanzibar inawatenga Uamsho zanzibar.Hapo sasa!
 
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar kimeitaka serikali ya Mapinduzi kuifuta mara moja Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) kwa kuwa inafanya kazi kinyume na malengo yake usajili.

Mbali na matusi ya nguoni na kumshutumu Maalim Seif kwamba anahusika na kundi la Uamsho walisema Maalim Seif hafai kuwa kiongozi kutokana na kuwa mbinafsi kwa kuwa ameisema serikali yake mbele ya viongozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP) kwa kuwaeleza kwamba jeshi la polisi na vikosi vya SMZ vinahitaji mafunzo ya kukabiliana na vurugu ili waweze kupata mafunzo ya kukabiliana na vurugu hizo bila ya kuvunja haki za binaadamu.

"Huyu Maalim Seif anawaambia UNDP kwamba jeshi letu la polisi linahitaji mafunzo ya kuwakamata wahalifu sisi tunamwambia polisi wetu na vikosi vyetu havihitaji mafunzo wewe ndio unahitaji mafunzo kwa sababu kwani wewe unalindwa na nani? Si hawa hawa polisi" alisema Khalifa."

Another Somalia.

Zanzibar ina dini moja inakuwaje wanatofautiana na kutaka kuingia vitani?
 
Back
Top Bottom