CCM yaibwaga CHADEMA katika Umeya jiji la Mwanza

Kesho viongozi wa CDM watakua makini na maamuzi yao ya jazba.

VIVA CCM
Ni heri Chama kishindwe Uchaguzi kuliko kuwa na Wanachama wa aina ya Zitto Kabwe, refer to Hamad Rashid CUF, na Kafurila NCCR, je umeshasikia tena chokochoko kwenye hivyo vyama?
 
Ningeelewa huo ushindi ungekuwa ni ule unaotokana na kura za wananchi moja kwa moja. Meya anachaguliwa na madiwani (ambao wameshakuwa madiwani tangu 2010), kwa hiyo sioni kilichobadilika mana madiwani wa ccm na wale wasio wa CHADEMA wakiwa wengi obviously watamchagua diwani wa ccm. So what is new here?

Endelea kujifariji sisi tunasonga mbele kurudisha majimbo yetu.
 
Chama makini chenye sera nzuri za kuwaendeleza wananchi wake kiuchumi na kijamii.chama dume,safi sana
 
Kwa matokeo haya wakulaumiwa ni kamati kuu ya cdm na secretariat nzima ya cdm. Walifanya maamuzi ya jazba sana kuwafukuza udiwani wakina Chagulani matokeo yake ndio haya kupoteza uongozi wa halmashauri hii muhimu sana sana, bila kupepesa macho lawama ziende kwa Dr Slaa. Sasa hii yaonyesha nguvu za cdm mwanza ndio zitakuwa zimepungua hivyo na hii yaweza kukidhoofisha chama chetu, tujifunze kwa hili la mwanza na tusirudie makosa tena kama hayo.

Sijakubaliana na wewe kuheshimu katiba kwa mwanachama ni muhimu kuliko vyote.kumbuka ARUSHA yalitokea kama ya mwanza mbona hadi leo CDM ndiyo inanguvu zaidi ya CCM ni kwamba issue ya meya mwanza is the same scenario happened in AR CITY watanzania wame-capitalize kwa cdm wanapoona viongozi wanawajibishwa ni mtaji tosha cause that is the only maker of difference between two parties.

Amini usiamini umeya is nothing than uimara wa chama pasipo mapandikizi kama chabulani, zitto and the like.CDM will continue dictating terms in Mwanza.
 
Sad news!
Mgombea wa kiti cha umeya katika Halmashauri ya jiji la Mwanza kupitia CCM na diwani wa kata ya Mkolani Ndg Stanslaus Mabula, ameshinda kiti cha umeya kwa jumla ya kura 11 dhidi ya mgombea wa CHADEMA diwani wa kata ya Mahina Ndg Charles Chinchibera aliyepata kura 8.

Source: Mimi mwenyewe nipo eneo la tukio.
 
Hongera zenu CCM!

Ingawa sioni umuhimu wa ushindi huo kwani nchi nzima mna mameya na wenyeviti wa halmashauri zaidi ya 120, labda mngeangalia ktk wingi huo ni nini mchango wenu ktk kumwinua Mtanzania kutoka ktk lindi la umaskini na ujinga. Ila kama tu ni ninyi "kumiliki" halmashauri basi hamna chenu.

Ni wazi kuwa CHADEMA walikuwa na nafasi finyu sana kwa vile kura za CCM na CUF (pamoja na za akina Chagulani & Henry kama walipiga) zilikuwa ni nyingi kuliko za madiwani wa CHADEMA. Ila kama nilivyotoa rai juzi tunauomba uongozi wa CHADEMA makao makuu kuchunguza kiini cha migogoro ya chama hapo Mwanza. Lazima muitatue ili haki itendeka na CHADEMA isonge mbele. We just need a united Mwanza please!!!
 
Ni heri Chama kishindwe Uchaguzi kuliko kuwa na Wanachama wa aina ya Zitto Kabwe, refer to Hamad Rashid CUF, na Kafurila NCCR, je umeshasikia tena chokochoko kwenye hivyo vyama?

hao wote uliowataja wana akili mara laki 5 kuliko wewe na ukoo wako.
 
sinaskia nape na wenzake jana usiku walikuwa lakairo hotel wakipanga wanunue umeya kwa sh. Ngapi so wamefika bei.! Ccm hovyooooo.! Ndo chama linakufa hivyo ngoja hela chafu zamafisadi zipigwe pini tuone jeuri yenu magamba nyie

Mimi naona kama CCM sasa ndo inafufuka kwa kasi, sijui nyie wenzangu.
 
Jamiiforum mbona kwenye simu zetu mnatum\a meseji moja mara mbili alafu mnakata!!!!?

Hata mimi nimeiona hiyo nilijitoa kupata news za Simba kwasababu wanachelewa kutuma au wana rudia habari....mfano unaweza kutumiwa taarifa watakao anza kucheza leoni ........ wakati huo ni saa mbili ya usiku na machi imechezwa saa kumi jioni...
 
Ni heri Chama kishindwe Uchaguzi kuliko kuwa na Wanachama wa aina ya Zitto Kabwe, refer to Hamad Rashid CUF, na Kafurila NCCR, je umeshasikia tena chokochoko kwenye hivyo vyama?
hapo umenena. Kuna wengine kama sisi tunaendelea kutawaliwa kwa sababu ya ujinga wetu lakini likija suala la watu walio na 'malengo maalum', ndipo tunajifunza ilivyokuwa muhimu kuwafukuza hao madiwani na hata ni bora kupoteza kiti chama kikiwa na wanachama watiifu kuliko kuwa na kiti kikiwa na mamluki wasioweza hata kusimamia vision ya chama.
Nchi hii tuna matatizo mengi zaidi ya tunavyofikiri na huu ni ushahidi lakini haitakuwa sababu ya kukata tamaa maana historia itatuhukumu vibaya!

 
Back
Top Bottom