CCM wamejivua Gamba: Je CCM siyo Nyoka tena bali sasa ni mjusi tu?

tuleteeni kanga na kofia
,mtuletee ze comedi na wasanii wa bongo fleva sisi wanafunzi wa VETA tutajiunga fasta na kuwa makada wa kuiwakilisha CCM popote mtakapotaka
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, kumbe sumu ya nyoka, iko kwenye gamba!, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.

mkuu wito wako mzuri ila naomba unitajie kwa majina waliovuliwa gamba. Hapa simaanishi waliosengenywa,nasema waliondolewa!na wao kutangaza kuwa kweli wameondoka! Yasije yakawa maneno kama ya jk,na mahaadi yao feki! Anyway,mi kadi yangu ya ccm bado ninayo na nahaidi kurudi ccm kama haya yatatekelezwa: 1. List of shame ya mwembe yanga ipelekwe mahakamani. 2. Rais jk aeleze wangapi walikamatwa na kwenda jela katika kesi ya dowans,epa na kagoda,achana na tangold na meremeta! 3. Nyumba zote zilizouzwa na magufuli kwa majaji na vigogo washtakiwe na kutaifisha nyumba za serikali. 4. Bil1.5 za mabango ya jk zimetokaje hazina? 5. Kwa nini Rex Attoney ndo wakili wa taasisi za serikali badala ya taasisi ya mwanasheria mkuu wa serikali! 6. Kwa nini Babu zetu waliofanya kazi EAC wanapigwa mabomu. 7. Kima cha chini cha mshahara kiwe sawa na mshahara wa housegirl/wapishi wa ofisi za ikulu! 8. NEC itoe takwimu halali za kura za uchaguzi mkuu oct2010. Baada ya hapo mi naenda Lumumba kulipia ada ya miaka ya nyuma na uanachama wangu uwe hai.
 
koma kabisa! NYOKA NI NYOKA, LABDA ANG'OLEWE MENO NDIO ATAFANANA NA YALE YA KIBISA!

WAPO KINA MANGOMANGO YULE ALIKUWA SPIKA UDSM TEYARI KASHAENDA.....LABDA ATAPEWA UKUU WA WILAYA....

NI WAKATI WA MAOPPORTUNIST KUINGIA CCM

NCHI HII HAIJAWAHI, NA HAITAWAHI KUJENGWA NA MAOPPORTUNISTS...

SIJAWAHI, SIKO HIYVO NA SIITAKUWA OPPORTUNIST.......NA NAWACHUKIA MAOPPORTUNISTS...HAWA WAKO HATA TAYARI WAKE ZAO WAPIGWE MITI ILI WAPATE NAFASI ZA UONGOZI.....
 
umuiya CCM zatakiwa pia 'kujivua magamba'

Na Gladness Mboma

MWENYEKITI wa Taifa CCM, Jakaya Kikwete pamoja na sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, Bw. Wilson Mukama wameombwa wayafikishe mageuzi katika ngazi zote
za chama na jumuiya zake ili kuwaondoa viongozi wote wazembe, wasio waadilifu na wafuasi wa mafisadi.

Mbali na ombi hilo pia wameombwa katika chaguzi zitakazokuja kiandae utaratibu utakaowazuia mafisadi na washirika wao wote kugombea na kupata nyadhifa ndani ya chama, na kuwa makini nao kwa kuwa hivi sasa wana hasira na chama.

Hayo yalisemwa jana na Shirikisho la Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia Vyuo Vikuu Mkoa wa Dar es Salaam, wakati likimpongeza Rais Kikwete kwa 'ujasiri na hatua madhubuti' alizochukua katika kufanya mabadiliko ya kiuongozi ndani ya CCM.

"Kama chama kitakubaliana na ombi letu la kuandaa utaratibu utakaozuia mafisadi na washirika wao wote kugombea na kupata nyadhifa ndani ya chama, hilo litarudisha imani kwa wafuasi na wanachama wa CCM, hali itakayokifanya chama kibaki kuwa kimbilio la wanyonge, wakulima na wafanyakazi," alisema Katibu wa Shirikisho hilo, Bw. Abubakar Asenga.

Alisema kuwa wanaunga mkono hatua zilizoanzishwa na chama za kupambana wazi na vitendo vya kifisadi na kwamba wale wote ambao wanatuhumiwa kwa kashfa nzito za ufisadi mkubwa na ubadhirifu wa mali za umma waachie nyadhifa zote ndani ya chama katika muda wa siku 90 walizopewa.

Bw. Asenga alisema watuhumiwa hao wasipofanya hivyo, wao (vijana) wataunga mkono hatua za chama kuwang'oa, na kusisitiza kwamba CCM siyo kichaka cha kuhifadhi watu wasio waadilifu wala mafisadi, na akawashauri waachane na siasa wakafanye biashara.

Katibu huyo alisema kuwa wanaunga mkono mageuzi makubwa yaliyofanywa kiuongozi, pili dhamira ya kufanya mchakato wa marekebisho ya kimfumo ndani ya chama.

"Shirikisho linatoa pongezi za dhati kwa sekretarieti mpya chini ya Katibu Mkuu, Bw. Mukama, uteuzi wao ni faraja kubwa kwa chama, hasa kwa kuwa umezingatia hali halisi ya siasa za sasa na uwakilishi wa vijana ambao ndio wadau wakubwa," alisema.

Bw. Asenga aliwapongeza pia wote waliochukua hatua za kujiuzulu nafasi zao, ili kupisha mageuzi makubwa ndani ya chama licha ya kwamba ni maamuzi machungu, lakini yanayofaa kupongezwa na kuigwa.

Shirikisho hilo limewataka vijana nchini kupeleka maoni na mawazo yao katika matawi na kuacha kutumia utaratibu wa kuropoka hovyo.

Alisema kuwa mafisadi watakuwa wanawatumia vijana ili UVCCM ionekane haijatulia na kuwataka kukaa chonjo na kundi hilo ambalo kwa sasa lina hasira na chama.

Wakati huo huo, Spika wa Bunge wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Godluck Mangomango ambaye alidai alikuwa mwanachama wa CHADEMA amejiunga na shirikisho hilo kwa madai ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Bw. Mangomango alisema kuwa baadhi ya vijana waliokuwa wamejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA, sasa wameamua kurejea CCM baada ya kuwepo kwa mabadiliko.

my take: KUNA HAJA YA KUCHUNGUZA CHETI CHA HUYU JAMAA!! AMESOMA, HAJAELIMIKA.....NI OPPORTUNIST KAMA SHANGWE CHITAMBALA, LUCY MAYENGA etc...wilaya zenyewe ziko ngapi??? hamwoni hata mkulu mwenyewe ameshindwa kufanya teuzi mpya?,

tuleteeni kanga na kofia
,mtuletee ze comedi na wasanii wa bongo fleva sisi wanafunzi wa VETA tutajiunga fasta na kuwa makada wa kuiwakilisha CCM popote mtakapotaka
merytina, kumbe wewe ni mwanafunzi wa VETA?,
Hivyo vyote mbona vimeshatekelezwa?!, labda usema kingine!.
 
mkuu wito wako mzuri ila naomba unitajie kwa majina waliovuliwa gamba. Hapa simaanishi waliosengenywa,nasema waliondolewa!na wao kutangaza kuwa kweli wameondoka! Yasije yakawa maneno kama ya jk,na mahaadi yao feki! Anyway,mi kadi yangu ya ccm bado ninayo na nahaidi kurudi ccm kama haya yatatekelezwa: 1. List of shame ya mwembe yanga ipelekwe mahakamani. 2. Rais jk aeleze wangapi walikamatwa na kwenda jela katika kesi ya dowans,epa na kagoda,achana na tangold na meremeta! 3. Nyumba zote zilizouzwa na magufuli kwa majaji na vigogo washtakiwe na kutaifisha nyumba za serikali. 4. Bil1.5 za mabango ya jk zimetokaje hazina? 5. Kwa nini Rex Attoney ndo wakili wa taasisi za serikali badala ya taasisi ya mwanasheria mkuu wa serikali! 6. Kwa nini Babu zetu waliofanya kazi EAC wanapigwa mabomu. 7. Kima cha chini cha mshahara kiwe sawa na mshahara wa housegirl/wapishi wa ofisi za ikulu! 8. NEC itoe takwimu halali za kura za uchaguzi mkuu oct2010. Baada ya hapo mi naenda Lumumba kulipia ada ya miaka ya nyuma na uanachama wangu uwe hai.

1. List of shame ya mwembe yanga ipelekwe mahakamani- Tumeshazipeleka zile kesi za utangulizi mahakamani, zikishaamuliwa ndipo tutazipeleka zilizobakia. Hatupendi kuingilia uhuru wa mahakama, hukumu za kwanza zinatarajiwa kutolewa 2016, hivyo 2015 mtatupa miaka mingine mitano tumalizie kazi hii nzuri tulioianza.
2. Rais jk aeleze wangapi walikamatwa na kwenda jela katika kesi ya dowans,epa na kagoda,achana na tangold na meremeta! -Wengi tuu wako jela, ila kwa vile tunaheshimu haki za binaadamu, tumepanga hatutawataja kwa majina ili kuwalindia heshima zao.
3. Nyumba zote zilizouzwa na magufuli kwa majaji na vigogo washtakiwe na kutaifisha nyumba za serikali- infact zile nyumba hatukuziuza kwao, bali tumewapa kama zawadi kwa kuheshimu mchango wao kwa taifa. Tulijifanya tumewauzia ili wanachi wasipige kelele sana, ndio maana zile bei ni za chini, na ni serikali, imewapa mikopo kuzinunua na hawatakiwi kulipa mkopa huo.
4. Bil1.5 za mabango ya jk zimetokaje hazina?- No hazikutoka hazina, tulipewa na Shemeji Ghadaffi, hivi hamjua amemuoa yule aliyekuwa mke wa yule mbabe wa Zenj, baada ya mke mwenyewe kumlalamia mumewe kwa Ghadaffi kuwa hawezi kazi!.
5. Kwa nini Rex Attoney ndo wakili wa taasisi za serikali badala ya taasisi ya mwanasheria mkuu wa serikali!- Kwenye mikataba yoke ya inayohusu serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni sehemu ya serikali, hivyo hawezi kuwa wakili wa serikali. Samani ilikuwa ni Mkono Companya sasa ndio Rex. Tumeipa Rex kwa sababu, siu unajua tena uhusiano wa mkulu na mama balozi?, isitoshe kale ka mkwana ka mwanetu mpenzi, pia kameajiriwa pale, sasa bila kuipa kampuni hii kazi hizi kubwa kubwa, watakalipa nini kabinti ketu?, next time tutaipa IMMA etc etc, nawe kama una kakampuni kako ka uwakili, kalete tuu.
6. Kwa nini Babu zetu waliofanya kazi EAC wanapigwa mabomu, wanapigwa mabamo kwa vile wameshajizeekea wakisubiri woto tuu, hivyo kuwalipa haki zao, kutapunguza fungu la vinywaji na vitafunwa na safari za muheshimiwa kwenye ile bajeti yetu.
7. Kima cha chini cha mshahara kiwe sawa na mshahara wa housegirl/wapishi wa ofisi za ikulu!- tukiwalipa watu vizuri hivyo, tutaharibu!, watu ili waweze kukunyenyekea, hakikisha wananjaa siku zote ili ukiwapatia tuu T-shirt, kofia na kanga, watakushukuru na kuendelea kukupigia kura zao.
8. NEC itoe takwimu halali za kura za uchaguzi mkuu oct 2010- Zile zilizotolewa ndizo halali zenyewe, hata hao wanalalama, wanalijua hilo, maana mawakala wao walikuwepo kwenye vituo vyote ndio maana hawana zaidi ya matokeo yale.

Kama umeridhika jiunge haraka, kama wewe ni msomi wa ngazi ya chuo kikuu, tutakuzawadia ka wilaya, kama una masters, tunakupa mkoa na wenye Ph.D ndio watashika wizara. Ila hata kama haujasoma sana, T-shirt na kofia hutakosa.
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, kumbe sumu ya nyoka, iko kwenye gamba!, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.
Tujiunge na nini? Jiheshimu mtu wangu.
 
Dk.Slaa amtupia mishale Kikwete

*Amtaka naye ajivue gamba CCM
*Adai amekuwa akitetea mafisadi

Na Moses Mabula, Tabora

Majira

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete anapashwa ajivue gamba CCM kwa kuwa yeye na washirika wake wameshrikiana kufanya ufisadi ndani ya Serikali.

Dkt. Slaa alisema hayo katika mkutano wa hadhara wakati akihutubia wananchi kwenye Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora.

Alisema kuwa Rais Kikwete amekuwa akiwatetea maswahiba wake wanaotuhumia kuiingizia Serikali hasara ya mamilioni ya shilingi licha ya kuelezwa bayana lakini amekuwa akikaa kimya bila kuwachukulia hatua zozote zile za kisheria.

"Kikwete naye inafaa ajivue gamba ndani ya CCM kwa kuwa naye ni muhusika, asiwadanganye Watanzania kwamba eti CCM imejivua gamba wakati naye ni gamba katika CCM," alisema Dkt. Silaa huku akishangiliwa na umati wa watu na kuongeza:

"Huyu naye Chiligati eti anawatangazia Watanzania kwamba amewapa siku tisini wale wote wanaotuhumiwa na ufisadi, wawe wameondoka wenyewe ndani ya CCM na kumwacha Mkuu wake wa kazi Rais Kikwete kumtangaza naye awe ameondoka ndani ya hizo siku tisini" alisisitiza Dkt. Slaa.

Akimgeukia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema Dkt. Slaa alisema kwamba achague mambo mawili siasa au upolisi.

Alisema kuwa Mkuu huyo wa Polisi amekuwa akikipigia debe Chama Cha Mapinduzi na kusahau kazi aliyotumwa na Watanzania ya kulinda usalama wa watu na mali zao lakini hivi sasa amegeuka kuwa mwanasiasa ndani ya Jeshi la Polisi.

Alieleza kwamba iwapo ameshindwa kufanya kazi ya Upolisi ni vyema
akawatangazia Watanzania haraka kuwa yeye ameshindwa kazi hiyo na mwanasiasa.

Kuhusu watu wanaotuhumiwa kuwa mafisadi Dkt. Slaa alimtaka Rais Kikwete kuwachukulia haraka hatua za kisheria na kuwafikisha mahakamani na kwamba kama hawezi basi naye aondoke madarakani kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi kwa wananchi waliomchagua kuingia madarakani.

1. List of shame ya mwembe yanga ipelekwe mahakamani- Tumeshazipeleka zile kesi za utangulizi mahakamani, zikishaamuliwa ndipo tutazipeleka zilizobakia. Hatupendi kuingilia uhuru wa mahakama, hukumu za kwanza zinatarajiwa kutolewa 2016, hivyo 2015 mtatupa miaka mingine mitano tumalizie kazi hii nzuri tulioianza.
2. Rais jk aeleze wangapi walikamatwa na kwenda jela katika kesi ya dowans,epa na kagoda,achana na tangold na meremeta! -Wengi tuu wako jela, ila kwa vile tunaheshimu haki za binaadamu, tumepanga hatutawataja kwa majina ili kuwalindia heshima zao.
3. Nyumba zote zilizouzwa na magufuli kwa majaji na vigogo washtakiwe na kutaifisha nyumba za serikali- infact zile nyumba hatukuziuza kwao, bali tumewapa kama zawadi kwa kuheshimu mchango wao kwa taifa. Tulijifanya tumewauzia ili wanachi wasipige kelele sana, ndio maana zile bei ni za chini, na ni serikali, imewapa mikopo kuzinunua na hawatakiwi kulipa mkopa huo.
4. Bil1.5 za mabango ya jk zimetokaje hazina?- No hazikutoka hazina, tulipewa na Shemeji Ghadaffi, hivi hamjua amemuoa yule aliyekuwa mke wa yule mbabe wa Zenj, baada ya mke mwenyewe kumlalamia mumewe kwa Ghadaffi kuwa hawezi kazi!.
5. Kwa nini Rex Attoney ndo wakili wa taasisi za serikali badala ya taasisi ya mwanasheria mkuu wa serikali!- Kwenye mikataba yoke ya inayohusu serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni sehemu ya serikali, hivyo hawezi kuwa wakili wa serikali. Samani ilikuwa ni Mkono Companya sasa ndio Rex. Tumeipa Rex kwa sababu, siu unajua tena uhusiano wa mkulu na mama balozi?, isitoshe kale ka mkwana ka mwanetu mpenzi, pia kameajiriwa pale, sasa bila kuipa kampuni hii kazi hizi kubwa kubwa, watakalipa nini kabinti ketu?, next time tutaipa IMMA etc etc, nawe kama una kakampuni kako ka uwakili, kalete tuu.
6. Kwa nini Babu zetu waliofanya kazi EAC wanapigwa mabomu, wanapigwa mabamo kwa vile wameshajizeekea wakisubiri woto tuu, hivyo kuwalipa haki zao, kutapunguza fungu la vinywaji na vitafunwa na safari za muheshimiwa kwenye ile bajeti yetu.
7. Kima cha chini cha mshahara kiwe sawa na mshahara wa housegirl/wapishi wa ofisi za ikulu!- tukiwalipa watu vizuri hivyo, tutaharibu!, watu ili waweze kukunyenyekea, hakikisha wananjaa siku zote ili ukiwapatia tuu T-shirt, kofia na kanga, watakushukuru na kuendelea kukupigia kura zao.
8. NEC itoe takwimu halali za kura za uchaguzi mkuu oct 2010- Zile zilizotolewa ndizo halali zenyewe, hata hao wanalalama, wanalijua hilo, maana mawakala wao walikuwepo kwenye vituo vyote ndio maana hawana zaidi ya matokeo yale.

Kama umeridhika jiunge haraka, kama wewe ni msomi wa ngazi ya chuo kikuu, tutakuzawadia ka wilaya, kama una masters, tunakupa mkoa na wenye Ph.D ndio watashika wizara. Ila hata kama haujasoma sana, T-shirt na kofia hutakosa.

Kwenye nyekundu: Wewe umeshajiunga tayari?
Nimependa mchanganuo wako: PhD=> wizara, Masters=>Mkuu wa mkoa, Bachelor=>Mkuu wa milaya, FormVI=>Kata FormIV=Kijiji. STD VII and below =>T-shirt, Kofia,kanga n.k
 
Tujaribu kuwa wa kweli kabisa, hata kwa sekunde moja tu! .... inaingia je akili kufikiri kikwete haja upa ufisadi wa taifa hii NGUVU KUU??

Anatoa wapi ujasiri kufikiri ... amekuwa anaupiga vita ufisadi wa nchi hii!! Kivipi??

Matarajio yake ni kweli ...avue viongozi vipenzi marafiki zake gamba ...na watanzania ..waamini yeye hana gamba??

Nashindwa kuelewa kabisa ... hii tamthilia!!!
 
Nisicho Kielewa ni kuwa Inawezekanaje Fisadi aombwe kuwashughulika Mafisadi???
Mi naona ni muhimu kuchora mstari nyoofu, kama kikwete ni Fisadi basi aombwe aondoke madarakani na mafisadi wenzie ama Kikwete awe mr clean then awashughulikie Mafisadi. ki ukweli Mambo haya yanachanganya, kwani kumuomba kikwete awashughulikie Mafisadi ingali na yeye anaonekana ni fisadi si kitu ambacho ki uhalisia kinawezekana. so Dr slaa and others need to clarify this matter and put it in the right place!!

umuiya CCM zatakiwa pia 'kujivua magamba'

Na Gladness Mboma

Wakati huo huo, Spika wa Bunge wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. Godluck Mangomango ambaye alidai alikuwa mwanachama wa CHADEMA amejiunga na shirikisho hilo kwa madai ya mabadiliko yaliyofanywa na Rais Kikwete.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Bw. Mangomango alisema kuwa baadhi ya vijana waliokuwa wamejiondoa CCM na kujiunga na CHADEMA, sasa wameamua kurejea CCM baada ya kuwepo kwa mabadiliko.

my take: KUNA HAJA YA KUCHUNGUZA CHETI CHA HUYU JAMAA!! AMESOMA, HAJAELIMIKA.....NI OPPORTUNIST KAMA SHANGWE CHITAMBALA, LUCY MAYENGA etc...wilaya zenyewe ziko ngapi??? hamwoni hata mkulu mwenyewe ameshindwa kufanya teuzi mpya?,

Hao mara nyingi ni reserve ya CCM kuwa wakifanya usanii basi wao wanajitokeza na kuonyesha kuwa wamekuwa convinced ili wapate wachache kutoka kwenye public. Pia kama ulivyosema ni ma opportunist ambao wanakuwapo kwenye opposition strategically kwamba ikitokea opportunity basi wanajitokeza ili waonekane. Mwache aende maana watu wengi wanapenda kumezea mate ving'avyo bila kujua kuwa siyo vyote ni dhahabu. Wanafiki kama hao siku zote wanaishia kuwa loosers maana by themselves they can not bring effective change na kwasababu wako weak are able to be bought and being used at a very cheap price. Matokeo yake ndiyo hivyo soon ataanza kuonekana kama zuzu mbele ya wenzake maana atakuwa parrot kusema kile anachoambiwa na siyo anachofikiri.
 
1. List of shame ya mwembe yanga ipelekwe mahakamani- Tumeshazipeleka zile kesi za utangulizi mahakamani, zikishaamuliwa ndipo tutazipeleka zilizobakia. Hatupendi kuingilia uhuru wa mahakama, hukumu za kwanza zinatarajiwa kutolewa 2016, hivyo 2015 mtatupa miaka mingine mitano tumalizie kazi hii nzuri tulioianza.
2. Rais jk aeleze wangapi walikamatwa na kwenda jela katika kesi ya dowans,epa na kagoda,achana na tangold na meremeta! -Wengi tuu wako jela, ila kwa vile tunaheshimu haki za binaadamu, tumepanga hatutawataja kwa majina ili kuwalindia heshima zao.
3. Nyumba zote zilizouzwa na magufuli kwa majaji na vigogo washtakiwe na kutaifisha nyumba za serikali- infact zile nyumba hatukuziuza kwao, bali tumewapa kama zawadi kwa kuheshimu mchango wao kwa taifa. Tulijifanya tumewauzia ili wanachi wasipige kelele sana, ndio maana zile bei ni za chini, na ni serikali, imewapa mikopo kuzinunua na hawatakiwi kulipa mkopa huo.
4. Bil1.5 za mabango ya jk zimetokaje hazina?- No hazikutoka hazina, tulipewa na Shemeji Ghadaffi, hivi hamjua amemuoa yule aliyekuwa mke wa yule mbabe wa Zenj, baada ya mke mwenyewe kumlalamia mumewe kwa Ghadaffi kuwa hawezi kazi!.
5. Kwa nini Rex Attoney ndo wakili wa taasisi za serikali badala ya taasisi ya mwanasheria mkuu wa serikali!- Kwenye mikataba yoke ya inayohusu serikali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ni sehemu ya serikali, hivyo hawezi kuwa wakili wa serikali. Samani ilikuwa ni Mkono Companya sasa ndio Rex. Tumeipa Rex kwa sababu, siu unajua tena uhusiano wa mkulu na mama balozi?, isitoshe kale ka mkwana ka mwanetu mpenzi, pia kameajiriwa pale, sasa bila kuipa kampuni hii kazi hizi kubwa kubwa, watakalipa nini kabinti ketu?, next time tutaipa IMMA etc etc, nawe kama una kakampuni kako ka uwakili, kalete tuu.
6. Kwa nini Babu zetu waliofanya kazi EAC wanapigwa mabomu, wanapigwa mabamo kwa vile wameshajizeekea wakisubiri woto tuu, hivyo kuwalipa haki zao, kutapunguza fungu la vinywaji na vitafunwa na safari za muheshimiwa kwenye ile bajeti yetu.
7. Kima cha chini cha mshahara kiwe sawa na mshahara wa housegirl/wapishi wa ofisi za ikulu!- tukiwalipa watu vizuri hivyo, tutaharibu!, watu ili waweze kukunyenyekea, hakikisha wananjaa siku zote ili ukiwapatia tuu T-shirt, kofia na kanga, watakushukuru na kuendelea kukupigia kura zao.
8. NEC itoe takwimu halali za kura za uchaguzi mkuu oct 2010- Zile zilizotolewa ndizo halali zenyewe, hata hao wanalalama, wanalijua hilo, maana mawakala wao walikuwepo kwenye vituo vyote ndio maana hawana zaidi ya matokeo yale.

Kama umeridhika jiunge haraka, kama wewe ni msomi wa ngazi ya chuo kikuu, tutakuzawadia ka wilaya, kama una masters, tunakupa mkoa na wenye Ph.D ndio watashika wizara. Ila hata kama haujasoma sana, T-shirt na kofia hutakosa.

Pasco for this case I dont fit any where kwenye chama chenu kwani with my PhD na hao typology ya watu wenu the best offer I can accept ni presidential post if you are willing to give me that basi niko hapa niite nami nitaitika. Ila huku CHADEMA kwasababu kuna vichwa vinavyonizidi na kuweza kuni challenge am willing kuwa mbeba mikoba yao na kuwasaidia kufuta vumbi za miguu ya viongozi wangu maana ni privillage kwani ni mizuri kama nini miguu yao waletao habari njema je ni wathamani kama nini mimi servant wakufuta vumbi miguu hiyo yenye kuleta habari njema Tanzania?
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, kumbe sumu ya nyoka, iko kwenye gamba!, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.

MKUU PASCO upo sawa kabisa, yaani kwa umri tulio nao tunaaminishwa kuwa sumu ya nyoka ipo kwenye gamba hivyo nyoka akishalivua gamba unaweza cheza nae BLUES kama nyoka wa KIBISA. Eti CCM imekuwa mpya yaani kwa kumtoa ROSTAM na CHENGE katika CC na kuwapa siku 90 kupima kama waendelee ktk uongozi au la ndio chama kuwa kipya na kimejisafisha? Hivi kweli JK na CCM yake wanataka kutuaminisha kuwa nchi hii MAFISADI ni RA, EL NA MZEE WA VIJISENTI TU? Basi kama wao ndio mafisadi pekee na ndio tatizo ndani ya CCM kweli nakubaliana na kauli ya MAREHEMU KOLIMBA kuwa CCM imepoteza DIRA na MUELEKEO ndio maana wamerukia HOJA ya CDM ya vita vya UFISADI na KATIBA MPYA na kutaka kuzibinafsisha kuwa ni HOJA zao halafu kama ilivyo ADA WAZICHAKACHUE na kuibuka na HITIMISHO la AJABU kwa TAIFA. NINI kujivua GAMBA hata wakijichuja DAMU, hao ni walewale tukumbuke HATA SIKU MOJA SHETANI AKIZEEKA HAGEUKI KUWA MALAIKA.
 
My litle daughter she is at baby class; she always tell me she is a CHADEMA showing me two fingers. I dont know why she likes CDM and also I dont know how to convince her to change her mind by merely telling her Makamba and other gambas are no longer there because she dont know them.
 
Tujiunge na nini? Jiheshimu mtu wangu.

chigwiye, sababu mbona nimezitoa, kwamba kumbe tatizo la CCM lilikuwa ni gamba tuu, na kumbe sumu ya nyoka inakaa kwenye gamba, sasa gamba limevuliwa CCM safi inang'ara na kumeremeta, haina sumu tena, ndio maana nikauliza, kwanini sisi tusio na vyama tusijiunge?..
Hebu niambie nimekosa heshima wapi?, au kwako heshima ni kujiunga Chadema tuu?!.
 
MKUU PASCO upo sawa kabisa, yaani kwa umri tulio nao tunaaminishwa kuwa sumu ya nyoka ipo kwenye gamba hivyo nyoka akishalivua gamba unaweza cheza nae BLUES kama nyoka wa KIBISA. Eti CCM imekuwa mpya yaani kwa kumtoa ROSTAM na CHENGE katika CC na kuwapa siku 90 kupima kama waendelee ktk uongozi au la ndio chama kuwa kipya na kimejisafisha? Hivi kweli JK na CCM yake wanataka kutuaminisha kuwa nchi hii MAFISADI ni RA, EL NA MZEE WA VIJISENTI TU? Basi kama wao ndio mafisadi pekee na ndio tatizo ndani ya CCM kweli nakubaliana na kauli ya MAREHEMU KOLIMBA kuwa CCM imepoteza DIRA na MUELEKEO ndio maana wamerukia HOJA ya CDM ya vita vya UFISADI na KATIBA MPYA na kutaka kuzibinafsisha kuwa ni HOJA zao halafu kama ilivyo ADA WAZICHAKACHUE na kuibuka na HITIMISHO la AJABU kwa TAIFA. NINI kujivua GAMBA hata wakijichuja DAMU, hao ni walewale tukumbuke HATA SIKU MOJA SHETANI AKIZEEKA HAGEUKI KUWA MALAIKA.
Naloli, tangu nimeposti hii post, imeshachangiwa posti 25, hii posti yako ndio ya kwanza inayotoa majibu ya hicho ninachouliza. Thanks for that, ila pia inanisaidia mimi kuelewa level ya uelewa wa wana jf wa kisasa vinginevyo ukimwaga nondo za kufa mtu humu jf, unaweza vuna mabua (matusi na kejeli).
 
Back
Top Bottom