Watanzania ni maneno maneno na kulialia, Vitendo 0. Katiba ni maneno tu! Je, 2023 tuendeleze maneno matupu na kulialia au tubadilike tufanye kitu?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,506
113,627
Wanabodi,
Screen Shot 2023-01-08 at 2.12.16 PM.png
Screen Shot 2023-01-08 at 2.12.35 PM.png

Leo 30/12/2022 tunapoanza safari ya kuuaga mwaka 2022 hapo kesho na keshokutwa kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 hivyo naomba nianze makala yangu hii ya "Kwa Maslahi ya Taifa" kwa kusema "kwaheri 2022, na Karibu 2023, kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya 2023 in advance, kwa rai moja tuu, "Mwaka 2023, Tubadilike, Tufanye Kitu!"

Nimegundua sisi Watanzania, kwa jina letu maarufu la Wabongo ni watu wa maneno maneno mengi, kulalamika sana na kulialia lia mwingi!, lakini tukija kwenye matendo, actions na kuchukua hatua, kusema ukweli kabisa, vitendo ni sifuri, zero, 0 nil!.

Kwenye hili la Katiba, Watanzania ni maneno maneno tuu meengii, na kulia lia kwingi!, lakini ukiangalia kwenye matendo, kuchukua hatua, to take actions ni hakuna kitu zaidi ya kelele!. Makala ya leo ni ya swali, huko nyuma tumekuwa tukipiga sana kelele miaka nenda, miaka rudi!, je na mwaka huu wa 2023, tuendeleze kulia lia kwa kupiga kelele kwa maneno maneno matupu au tubadilike tufanye vitendo, tuchukue hatua, tufanye kitu?. Yaani we have to do something!, au tuendelee tuu na maneno maneno, kulia lia na kupiga tuu kelele?.

Wengi huuanza mwaka mpya kwa kuweka malengo ya mwaka, “new year’s resolutions” kwamba mwaka huu nitafanya hili na lile, ila katika kupanga hayo malengo, sii wengi hufanya mapitio ya mwaka ulioisha, walipanga kufanya nini, wametekeleza nini, wamefanikiwa nini na wamekwama nini, ili baadhi ya yale malengo ya mwaka uliopita, ambayo hayakufanikiwa, yabebebwe katika mwaka unaofuata, au kama hayabebeki yafutwe, na sio kila mwaka unakuja na malengo mapya, mwisho wa mwaka hufanyi tathmini wala mapitio ya mwaka ulioisha, kisha unakuja na mengine mapya!, mwisho wa siku, unakuwa huwezi kupima mafanikio yako!.

Katiba ya nchi ndio Biblia ndio Msahafu wa uendeshaji wa nchi yetu. Kama ilivyo Ikulu ni mahali patakatifu, katiba ni kitabu kitakatifu kwa nchi yetu kama vilivyo vitabu vitakatifu vya Biblia Takatifu kwa Wakrusto na Quran Tukufu kwa Waislamu. Hii ndio sheria mama ya uendeshaji wa nchi yetu.

Tofauti pekee kati ya Biblia, Msahafu na Katiba, ni Msahafu haubadiliki, katiba inaweza kubadilishwa, ila mabadiliko yoyote ya katiba, lazima yawe ni mabadiliko halali ya haki.

Katiba ndio sheria kuu kuliko zote za nchi, viongozi wetu wakiisha chaguliwa, tunawaapisha kwa mujibu wa katiba, wanaapa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, na ikitokea hata rais wa JMT akikiuka katiba, anaondolewa madarakani!.

Sheria yoyote ikitungwa, ikiwa ni kinyume cha katiba, sheria hiyo inahesabika ni batili “null and void”, ikitungwa sheria ambayo ni batili, kwa kwenda kinyume cha katiba ya JMT, kisha ubatili huo, ukaja kuchomekewa ndani ya katiba yetu!, huku sasa tukuiteje?, maana kunakuwa sio kuibatilisha katiba, bali ni kuinajisi katiba!.

Mwaka 2022 tuliipigia kelele najisi fulani ndani ya katiba yetu kwa kulialia na kuisema sema, hivyo tumefika hadi mwisho wa mwaka 2022 bila jambo lolote la maana kufanyika kuiondoa najisi hii, sasa tumeingia mwaka mpya wa 2023, je na mwaka huu 2023, tuendelee tuu kupiga kelele kwa kulialia na kusema sema tuu, bila kufanya tendo lolote, au mwaka huu 2023, tubadilike, badala ya kulia lia na kusema sema, twende hatua moja zaidi mbele kwa kutenda kitu? ( msiwe na wasiwasi kuhusu kutenda huku, sio kwa mikutano ya hadhara au kufanya maandamano, ni kutenda kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni).
Maneno Maneno Yangu Kuhusu Najisi Kwenye Katiba Yetu ya 1977
  1. Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
  2. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  3. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  4. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  5. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  6. Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
  7. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  8. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  9. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
  10. Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010
  11. "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
  12. Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. kwa vile Rais Samia ameisha jitanabaisha yeye ni kama Magufuli, hivyo anapaswa kulitimiza na hili!.
Sisi Watanzania tuna fani mbalimbali, kuna wenzetu kazi yao ni kufikiri na kupanga mikakati, hawa wanaitwa think tanks, kuna wenzetu ni viongozi, kazi yao ni kutuongoza, kuna wenzetu ni watendakazi, kazi yao ni kutenda kazi kwa kutumia nguvu zao, kuna wengine tukiwemo sisi waandishi wa habari na vyombo vya habari, wa kiasili, yaani “traditional media” kazi zetu kuu ni tatu, kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, hatuna kutenda!. Na tumegawanyika makundi mawili, waandishi wa habari watangazaji na vyombo vya utangazaji (broadcast media) ambao kazi yao ni kutangaza na kuongea tuu, hakuna kutenda lolote!, na waandishi wa habari wa magazeti (print media) ambao kazi yao ni kuandika tuu hakuna kutenda lolote!.

Lakini ujio wa mapinduzi ya kidigitali kwenye dunia yetu na ujio wa mitandao ya kijamii, haya makundi mawili ya vyombo vya habari, yaani broadcast media na print media, yameunganishwa na mtandao wa jamii, hivyo kule kwenye mtandao, hakuna print peke yake wala broadcast peke yake. Vyombo vya utangazaji vina kurasa zake za mitandao ya kijamii navyo sasa vinaandika, mtu unaweza kusoma, vyombo vya print, kama magazeti, navyo kwenye kurasa zake, vinatangaza, na kuweka magazeti mtandao, hivyo siku hizi, kupata habari, kuangalia TV au kusoma gazeti, sio lazima ukae nyumbani uwashe TV uangalie habari, ukijisajili tuu na mtandao fulani, wanaita ku subscribe, unaletewa tuu habari, kila inapotokea, hivyo mtu hana tena haja kusubiria taarifa ya habari saa mbili usiku, kila tukio linapotokea linatangazwa live, hivyo kufikia ule muda wa habari, kila kilichotokea, watu wanakijua, magazeti ya kesho yake, sisi tunayasoma leo, maana kwenye kurasa zao za mitandao, kila habari, inachapishwa pale pale inapotokea.

Ujio huu wa mitandao ya jamii, umemfanya sasa kila mtu kuwa ni mwandishi wa habari, kila mtu sasa ni mtangazaji, hali inayopelekea hata sisi ambao ni watangazaji wa kweli wa kusomea hii kazi, kujikuta hatufui dafu mbele ya watangazaji vijana wa kisasa kwenye mitandao ya jamii, hivyo ukiwauliza vijana wa kisasa, unamjua Pasco Mayalla?, atakuuliza, Pascal Mayalla ndio nani?, utamwambia ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Kiti Moto, atakuuliza kiti moto ndio nini?, naomba link yake ni kitazame nikivutiwa, nita subscribe, unajikuta huna cha kumwambia!, hivyo sisi waandishi wakongwe wa ki analojia, ili tuendelee kuwepo ni lazima tubadilike na kwenda kidigitali vinginevyo tunafutika jumla!, hivyo mwaka 2023, Pasco Mayalla nae anakuja kidigitali zaidi!.

Hivyo kwa vile mimi kazi yangu ni kuandika tuu na kutangaza tuu, nikikaa chini na kuutafakari mwaka 2022, nimeandika mangapi na kutangaza mangapi, kuhusu katiba na yapi yamefanyiwa kazi, nimejikuta nimekata shauri kwa mwaka huu 2023, ili kulisaidia taifa na kuisaidia jamii, na kulisaidia taifa, nisiishie kuandika tuu, na kutangaza tuu, ninapaswa nifanye kitu cha ziada kwa kwenda mbele zaidi kwa kufanya jambo la ziada zaidi ya kuandika tuu na kutangaza tuu.

I must do something more!. Hii something more ni nini?, naomba kwa sasa nisiiseme baada ya kumuomba sana Mungu anifundishe kunyamaza, hivyo just watch me closely 2023!.

Ndipo yale maneno ya rais kijana wa Marekani, John F. Kennedy aliyowaeleza Wamarekani, “usijiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize wewe umeifanyia nini Marekani?”. Hivyo tunapoukaribisha mwaka mpya, wa 2023, kama kila mmoja wetu atajitafakari kwa kujiuliza “jee ameifanyia nini Tanzania” akijikuta hajaifanyia kitu chochote cha maana huko nyuma, basi mwaka huu wa 2023, abadilike kwa kupanga malengo yenye mipango mkakati kwa kujiuliza, “jee ataifanyia nini Tanzania?”, Inawezekana kama kila mtu atatimiza wajibu wake kikamilifu.

Mwaka huu wa 2023, tupunguze maneno maneno, na kuongea ongea sana, tupunguze maandishi kuandika andika sana, hayo maneno maneno tunayoongea ongea sana, badaya ya kuishia kuongea ongea tuu, na kuandika andika tuu, tufanye jambo, tufanye na vitendo, tutende,!. Hivyo jambo langu kuu la kwanza kwa mwaka huu 2023 ni Katiba!. Japo kuna mambo mengi muhimu ya kuyashughulikia, lakini kwangu mimi kwa mwaka huu, naona muhimu kuliko yote ni hili la Katiba!, kwenye hili la Katiba, sasa tufanye kitu, tusiishie kuongea tuu na kuandika tuu, tufanye kitu cha ziada!, jee tufanye nini?, ungana nami wiki ijayo, nikiianzisha safari ya Katiba!, “it can be done, play your part” .
Kwa heri 2022, karibu 2023
Happy New Year!, Heri ya Mwaka Mpya!.
Paskali.
 
Asante sana mleta mada naunga Mkono nuio la "Mwaka 2023 tufanye kitu". Hii inaweza kuwa na ufafanuzi wa aina mbalimbali.

Binafsi ufafanuzi wa nuio hili ni kuwa, Mwaka 2023 uwe mwaka wa kufanya kitu kitakachotuwezesha kama Taifa kuweka misingi na kuitumia kujitegemea kiuhalisia kiuchumi, kidiplomasia, kiteknolojia, kisiasa, na mengine kama haya.

Nami naungana na wote tuombeane kuingia mwaka 2023 kisha tuumalize kwa Amani, afya njema na furaha. Amen.
 
Ungeanza wewe mwnyw kuonyesha uzalendo wako kwa taifa lako Kwa vitendo

Kwa kupinga blah blah za rafiki yako makamba kila kukichakutukatia umeme akijitetea kwasababu zisizo na mashiko akidhani watanzania wote hatuna akili
 
Mkuu wewe binafsi umetoa mchango gani katika kufanikisha upatikanaji wa katiba mpya? Tatizo hili jukumu tumewaachia baadhi ya vyama vya upinzani. Sisi wengine tunawatazama tu na mwisho wa siku tunakuja na mabandiko kama haya kuwananga wapinzani.
Nina uhakika ungefanikiwa kupenya EALA usingekuja na hili bandiko.
 
Yaweza kuwa ni THREAD Bora ya mwisho wa mwaka 2022.

Nilikuja na ID ya kimkakati April Ili kuamsha umma kupitia jukwaa hili juu ya KATIBA mpya.

Hali niliyoikuta ilikuwa mbaya sana, Upinzani na KIJANI walikuwa wameungana KUSIFU na kuimba MAPAMBIO ya Eti "Anaupiga mwingi''"

Nilipambana sana na kusaidia Upinzani kurudi ktk LINE na nafasi Yao .

Niliomba pia watu wafumbuliwe macho kuwa KUNDI la S.gang ni PROPAGANDA iliyoanzishwa kuwagawa wananchi Ili waliopo walihujumu TAIFA vizuri.

Naweza Sema mafanikio yatakayopigwa kupelekea 2023/2024 yamechagizwa na MAPAMBANO niliyoyaanza na wenzangu tangu April 2022.

Tusichoke kutenda mema, maana tutalipwa Kwa wakati wake TUSIPOZIMIA ROHO.

Ikumbukwe kuwa namba za kukamilika Kwa mchakato wa KATIBA mpya Bado zinasoma 2026, tupo kwenye right track.

Aaamen.
 
Tatizo madai ya Katiba Mpya yamehodhiwa na chama tawala, na hili limetokea kwa sababu ya matokeo ya hii Katiba mbovu iliyopo, imempa Rais ambaye ndie mwenyekiti wa CCM mamlaka ya kuongoza kila kitu.

Utamu wa madaraka wanaoupata kutokana na uwepo wa hii Katiba mbovu, unawafanya wawe wagumu kuruhusu mambo yaende kwa urahisi ili kuwezesha upatikanaji wa Katiba mpya ufikiwe kirahisi, hapa hutumia mbinu za kikatili kuwafunga wapinzani midomo ikiwemo kuwabambikia kesi.

Ajabu Mayalla umekuja na malalamiko, kwamba watanzania ni watu wa kulia lia, tunalalamika sana, sasa hebu tupe mbinu, tufanyeje ili kuwezesha kuwanyan'ganya tonge mdomoni hawa waliolewa madaraka? hawa wanaotumia mbinu za kikatili ili kutufunga midomo?

Vinginevyo, kuja na malalamiko tu kama ulivyofanya, bila kuwa na solution unakuwa hujalitendea haki tatizo ili kulimaliza, ulichofanya unakuwa ni sawa tu na kulitangaza tatizo ambalo tayari lipo lizidi kufahamika, sasa tupe mbinu mjomba...
 
kwenye hili la Katiba, sasa tufanye kitu, tusiishie kuongea tuu na kuandika tuu, tufanye kitu cha ziada!, jee tufanye nini?, ungana nami wiki ijayo, nikiianzisha safari ya Katiba!, “it can be done, play your part” .
Katiba mpya itapatikana siku Ccm wakitaka (baada ya uchaguzi wa mwaka 2025), huo ndio ukweli....

Ila Ccm inaweza kuwa-zawadia mambo kadhaa ikiwemo tume huru ya uchaguzi ili kuwapooza.

JokaKuu zitto junior Mag3
 
Nakubaliana na wewe mkuu.
Watanzania wengi hawataki kutumia akili zao kujiongeza.
Wanapendelea utegemezi tu.
Waafikiri Katiba Mpya itawajaza mapesa mfukoni kama sera za mzee Mapesa, Cheyo.

Watu awafanyi kazi, kulalama toka asubuhi mpaka jioni, utafikir wamezaliwa na serikali.
Shame on Tz!
 
Wanabodi,

Leo 30/12/2022 tunapoanza safari ya kuuaga mwaka 2022 hapo kesho na keshokutwa kuukaribisha mwaka mpya wa 2023 hivyo naomba nianze makala yangu hii ya "Kwa Maslahi ya Taifa" kwa kusema "kwaheri 2022, na Karibu 2023, kwa kuwatakia heri ya mwaka mpya 2023 in advance, kwa rai moja tuu, "Mwaka 2023, Tubadilike, Tufanye Kitu!"

Nimegundua sisi Watanzania, kwa jina letu maarufu la Wabongo ni watu wa maneno maneno mengi, kulalamika na na kulialia, lakini tukija kwenye matendo, Vitendo zero, sifuri, 0 nil!. Kwenye hili la Katiba, ni maneno maneno tuu, na kulia lia, ukiangalia matendo, ni hakuna kitu zaidi ya kelele!, makala ya leo ni ya swali, Jee na mwaka huu wa 2023, tuendeleze kulia lia kwa maneno maneno matupu au tubadilike tufanye vitendo, tufanye kitu, to do something, au tuendelee na maneno maneno na kulia lia tuu?.

Wengi huuanza mwaka mpya kwa kuweka malengo ya mwaka, “new year’s resolutions” kwamba mwaka huu nitafanya nini, ila katika kupanga hayo malengo, sii wengi hufanya mapitio ya mwaka ulioisha, walipanga kufanya nini, wametekeleza nini, wamefanikiwa nini na wamwkwama nini, ili baadhi yay ale malengo ya mwaka uliopita, ambayo hayakufanikiwa, yabebebwe katika mwaka unaofuata, au kama hayabebebi yafutwe, na sio kila mwaka unakuja na malengo mapya, mwisho wa mwaka hufanyi tathmini wala mapitio ya mwaka ulioisha, kisha unakuja na mengine mapya!, mwisho wa siku, unakuwa huwezi kupima mafanikio yako!.

Katiba ya nchi ndio Biblia ndio Msahafu wa uendeshaji wa nchi yetu. Kama ilivyo Ikulu ni mahali patakatifu, katiba ni kitabu kitakatifu kwa nchi yetu kama vilivyo vitabu vitakatifu vya Biblia Takatifu kwa Wakrusto na Quran Tukufu kwa Waislamu. Hii ndio sheria mama ya uendeshaji wa nchi yetu.

Tofauti pekee kati ya Biblia, Msahafu na Katiba, ni Msahafu haubadiliki, katiba inaweza kubadilishwa, ila mabadiliko yoyote ya katiba, lazima yawe ni mabadiliko halali ya haki.

Katiba ndio sheria kuu kuliko zote za nchi, viongozi wetu wakiisha chaguliwa, tunawaapisha kwa mujibu wa katiba, wanaapa kuilinda na kuitetea katiba ya JMT, na ikitokea hata rais wa JMT akikiuka katiba, anaondolewa madarakani!.

Sheria yoyote ikitungwa, ikiwa ni kinyume cha katiba, sheria hiyo inahesabika ni batili “null and void”, ikitungwa sheria ambayo ni batili, kwa kwenda kinyume cha katiba ya JMT, kisha ubatili huo, ukaja kuchomekewa ndani ya katiba yetu!, huku sasa tukuiteje?, maana kunakuwa sio kuibatilisha katiba, bali ni kuinajisi katiba!.

Mwaka 2022 tuliipigia kelele najisi fulani ndani ya katiba yetu kwa kulialia na kuisema sema, hivyo tumefika hadi mwisho wa mwaka 2022 bila jambo lolote la maana kufanyika kuiondoa najisi hii, sasa tumeingia mwaka mpya wa 2023, je na mwaka huu 2023, tuendelee tuu kupiga kelele kwa kulialia na kusema sema tuu, bila kufanya tendo lolote, au mwaka huu 2023, tubadilike, badala ya kulia lia na kusema sema, twende hatua moja zaidi mbele kwa kutenda kitu? ( msiwe na wasiwasi kuhusu kutenda huku, sio kwa mikutano ya hadhara au kufanya maandamano, ni kutenda kwa mujibu wa katiba, sheria, taratibu na kanuni).
Maneno Maneno Yangu Kuhusu Najisi Kwenye Katiba Yetu ya 1977
  1. Hongera sana Pascal Mayalla, Ndio Mwandishi Pekee Uliyemuuliza Swali Rais Magufuli
  2. Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
  3. Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
  4. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  5. Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
  6. Samia Mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa Hili, Atabarikiwa!, Taifa Litabarikiwa!. Asante Mungu kwa Samia, Mungu Mbariki Samia, Mungu Ibariki Tanzania
  7. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
  8. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
  9. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
  10. Hukumu ya Mgombea Binafsi Juni 17, 2010
  11. "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
  12. Trends, Visions: Watanzania msitatizwe na kauli zake kuhusu Katiba, baada ya Nyerere, ni Magufuli ndiye ataacha legacy kubwa ikiwemo Katiba Mpya!. kwa vile Rais Samia ameisha jitanabaisha yeye ni kama Magufuli, hivyo anapaswa kulitimiza na hili!.
Sisi Watanzania tuna fani mbalimbali, kuna wenzetu kazi yao ni kufikiri na kupanga mikakati, hawa wanaitwa think tanks, kuna wenzetu ni viongozi, kazi yao ni kutuongoza, kuna wenzetu ni watendakazi, kazi yao ni kutenda kazi kwa kutumia nguvu zao, kuna wengine tukiwemo sisi waandishi wa habari na vyombo vya habari, wa kiasili, yaani “traditional media” kazi zetu kuu ni tatu, kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, hatuna kutenda!. Na tumegawanyika makundi mawili, waandishi wa habari watangazaji na vyombo vya utangazaji (broadcast media) ambao kazi yao ni kutangaza na kuongea tuu, hakuna kutenda lolote!, na waandishi wa habari wa magazeti (print media) ambao kazi yao ni kuandika tuu hakuna kutenda lolote!.

Lakini ujio wa mapinduzi ya kidigitali kwenye dunia yetu na ujio wa mitandao ya kijamii, haya makundi mawili ya vyombo vya habari, yaani broadcast media na print media, yameunganishwa na mtandao wa jamii, hivyo kule kwenye mtandao, hakuna print peke yake wala broadcast peke yake. Vyombo vya utangazaji vina kurasa zake za mitandao ya kijamii navyo sasa vinaandika, mtu unaweza kusoma, vyombo vya print, kama magazeti, navyo kwenye kurasa zake, vinatangaza, na kuweka magazeti mtandao, hivyo siku hizi, kupata habari, kuangalia TV au kusoma gazeti, sio lazima ukae nyumbani uwashe TV uangalie habari, ukijisajili tuu na mtandao fulani, wanaita ku subscribe, unaletewa tuu habari, kila inapotokea, hivyo mtu hana tena haja kusubiria taarifa ya habari saa mbili usiku, kila tukio linapotokea linatangazwa live, hivyo kufikia ule muda wa habari, kila kilichotokea, watu wanakijua, magazeti ya kesho yake, sisi tunayasoma leo, maana kwenye kurasa zao za mitandao, kila habari, inachapishwa pale pale inapotokea.

Ujio huu wa mitandao ya jamii, umemfanya sasa kila mtu kuwa ni mwandishi wa habari, kila mtu sasa ni mtangazaji, hali inayopelekea hata sisi ambao ni watangazaji wa kweli wa kusomea hii kazi, kujikuta hatufui dafu mbele ya watangazaji vijana wa kisasa kwenye mitandao ya jamii, hivyo ukiwauliza vijana wa kisasa, unamjua Pasco Mayalla?, atakuuliza, Pascal Mayalla ndio nani?, utamwambia ni mtangazaji maarufu wa kipindi cha Kiti Moto, atakuuliza kiti moto ndio nini?, naomba link yake ni kitazame nikivutiwa, nita subscribe, unajikuta huna cha kumwambia!, hivyo sisi waandishi wakongwe wa ki analojia, ili tuendelee kuwepo ni lazima tubadilike na kwenda kidigitali vinginevyo tunafutika jumla!, hivyo mwaka 2023, Pasco Mayalla nae anakuja kidigitali zaidi!.

Hivyo kwa vile mimi kazi yangu ni kuandika tuu na kutangaza, nikikaa chini na kuutafakari mwaka 2022, nimeandika mangapi na kutangaza mangapi, kuhusu katiba na yapi yamefanyiwa kazi, nimejikuta kwa mwaka huu 2023, ili kuisaidia jamii, na kulisaidia taifa, nisiishie kuandika tuu, na kutangaza tuu, ninapaswa nifanye kitu cha ziada kwa kwenda mbele zaidi kidigitali zaidi na kufanya jambo la kuandika tuu na kutangaza tuu, I must do something more!. Hii something more ni nini?, naomba kwa sasa nisiseme, but watch me!.

Ndipo yale maneno ya rais kijana wa Marekani, John F. Kennedy aliyowaeleza Wamarekani, “usijiulize Marekani imekufanyia nini, jiulize umeifanyia nini Marekani?”. Hivyo tunapoukaribisha mwaka mpya, wa 2023, kama kila mmoja wetu atajitafakari kwa kujiuliza “jee ameifanyia nini Tanzania” akijikuta hajaifanyia kitu chochote cha maana huko nyuma, basi mwaka huu wa 2023, abadilike kwa kupanga malengo yenye mipango mkakati kwa kujiuliza, “jee ataifanyia nini Tanzania?”, Inawezekana kama kila mtu atatimiza wajibu wake kikamilifu,

Mwaka huu wa 2023, tupunguze maneno, kuongea sana, tupunguze maandishi kuandika sana, hayo maneno tunayoongea sana, badaya ya kuishia kuongea tuu, na kuandika tuu, tufanye na vitendo, tutende,!. Hivyo jambo langu kuu la kwanza kwa mwaka huu 2023 ni Katiba!. Japo kuna mambo mengi muhimu ya kuyashughulikia, lakini kwangu mimi kwa mwaka huu, naona muhimu kuliko yote ni la Katiba!, kwenye hili la Katiba, sasa tufanye kitu, tusiishie kuongea tuu na kuandika tuu, tufanye kitu cha ziada!, jee tufanye nini?, ungana nami wiki ijayo, nikiianzisha safari ya Katiba!, “it can be done, play your part” .
Kwa heri 2022, karibu 2023
Happy New Year!, Heri ya Mwaka Mpya!.
Paskali.
Hongera kwa makala yako Braza. Kiukweli Watanzania maneno maneno na ujanja ujanja. Ukiwa serious na jambo unachukiwa. Napenda hata style ya uongozi wa Mama kwa Sasa kawasoma. Mwanzoni walikuwa wanampa headache kwa kuwa aliwazingatia. Naona kashatujua mambo yetu ya uswahilii na maneno maneno kaamua kutupa kisogo anachapa kazi.
 
ningekuwa nauwezo wakubadilisha katiba ningeweka.kusinge kuwepo nauchaguzi waraisi.kupiga kura tunapoteza pesabure.tanzania inabidi iongozwe kidicteta.ndio maendeleo tutayaona.
 
Mkuu wewe binafsi umetoa mchango gani katika kufanikisha upatikanaji wa katiba mpya? Tatizo hili jukumu tumewaachia baadhi ya vyama vya upinzani. Sisi wengine tunawatazama tu na mwisho wa siku tunakuja na mabandiko kama haya kuwananga wapinzani.
Nina uhakika ungefanikiwa kupenya EALA usingekuja na hili bandiko.
Mkuu tamsana, kwanza sii kweli kuwa ningefanikiwa Kawe ama EALA, nisinge kuja na bandiko hili!, ningefanikiwa kuingia Bungeni, then hili la katiba ningeliamshia mle mjengoni!, angalia kama ningeingia Bungeni ningeingia kufanya nini mule mjengoni
Na ningeingia EALA angalia ningekwenda kufanya nini
  1. Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki-3: Ujue Mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
  2. Ubunge EALA, Wito Kwa CCM, Msiangalie Ukwasi, Tuteulieni, Wazalendo wa Kweli wa Taifa Hili, Wenye Uwezo na Uzoefu wa Kimataifa Kutuwakilisha Ipasavyo
  3. Ijue Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Fursa za Mtangamano
  4. Ijue Mahakama ya Afrika Mashariki, Kwanini Hukumu Zake Hazina Rufaa na Kwanini Zina Puuzwa na Baadhi ya Nchi Washirika Sisi Tanzania Tukiwemo?
  5. Lijue Bunge la Afrika Mashariki na Jee Uchaguzi wa Wabunge wa CCM EALA Ulikuwa ni Uchaguzi Kweli Au Kiini Macho cha Uchaguzi?
NB. Everything happens for a reason, ukikitaka kitu fulani, ukajiona unafaa, wakatokea wengine wanaofaa zaidi yako hivyo wewe ukakosa, unashukuru kwa yote and you never know, unaweza kuwa umekoseshwa ili ufanye mengine makubwa zaidi!.
P
 
Ni maajabu gani ungeenda kufanya huko bungeni wakati hata sheria mbaya ya vyombo vya habari imekushinda kuipigania? Kimsingi ww huwezi kwenda kinyume na mfumo uliokulea. Watu wanaoweza kupigania katiba mpya ni watu walio nje ya ufaidika wa dola. Ww ni kama umeshajisalimishwa kwa dola, hivyo utadai katiba kwa njia ya maongezi, wakati hakuna uwezekano wa kupatikana katiba mpya ya kweli bila machafuko.
 
Ni hivi, bila machafuko hakuna katiba mpya yenye utashi wa wananchi. Hiyo ya kupangwa na dola ndio hiyo hiyo tunayoipigia kelele kila siku.
Huu ni uchochezi!. Katiba mpya inaweza kupatikana kwa
1. Dialogue- kwa njia ya mazungumzo na kufikia consensus
2. Inaweza kupatikana kwa njia ya lobbying and advocacy
3. Inaweza kupatikana kwa pressure groups to press on issues
Njia hizo tatu za amani zikishindikana ndio tunakuja kwenye mapambano
4. Legal redress, kuitumia mapambano ya kisheria kuitumia Mahakama kuiamuru serikali kubadili katiba
5. Inaweza kupatikana kwa confrontations only if hizo njia nyingine zote za amani zimeshindikana!. Kushawishi kudai katiba kwa mapambano kabla ya kujaribu njia za amani, ni uchochezi!.
P
 
Back
Top Bottom