CCM wamejivua Gamba: Je CCM siyo Nyoka tena bali sasa ni mjusi tu?

Hii janja ya CCM kutufunga macha waTZ haikubaliki hata siku moja. Ukijaribu kuona wanachokifanya ni kwamba wanawabembeleza kina RA, EL na Chenge na wengine watoke kwenye Chama ili tu kuwa full waTZ nasema hii haikubaliki. Eti sijawahi kusikia wakiwaambia watoke kwenye Serikali au wafilisiwe kutokana na Kutupiga hela nyingi sana.

Embu angalia, hawa jamaa wote wametupiga hela nyingi sana wakiwa nje ya CCM mfano rostam amepiga hela za serikali akiwa nje ya CCM, Tanil Somaiya anapiga sana hela zaserikali lakini yuko nje ya CCM, Manji anapiga sana hela za serikali ila yuko nje ya serikali.

Angalia timu yote ya EPA iko nje ya CCM na Serikali lakini wanapiga sana hela zetu. Watanzania tuamke na kuiunga mkono harakati za CDM ili kuhakikisha CCM inakuwa chama cha upinzani na hatimaye hawa jamaa wafikishwe mahakamani.

Peoples power
 
Ni kweli hata sumu yake haipungui na akizaa huzaa nyoka.

Tabia ya kurithishana madaraka ambayo wenzetu wa Libya ni chanzo cha mgogoro haiwezi kuisha ,angalia sekretariat mpya Nape,January koo zilezile
Hapa lengo ni kumaintain ile cycle ya haves and have nots apart, na zaidi kujenga political dynasty ya watoto wa wakubwa!
 
beginning of the end,.kwa hiyo kikwete kawageuka deal makers wenzake!!jk is not serious,hivi anawezaje kumtosa RA!?na lile dili la dowans si ndo litafumuka kabisa??mi nahisi hawa akina EL,RA,CHENGE,MKONO na wengine wengi wataanza kuawa mmoja mmoja,.dead men tell no tales..stay tuned more to come
 
Jamani hakuna mpya CCM. Hizi ni njama za kuwadanganya wananchi. Wamewachagua viongozi walioshindwa Zanzibar kuwakilisha Zanzibar katika baraza lao. Hhahahahahahha - OVYO.

Nyoka huvua gamba lote kuanzia kichwani hadi mkiani, lakini hii danganya toto ya hawa sisiemu ya kuvua gamba kuishia shingoni na kubakiza gamba la kichwani bado ni kichekesho kama wanataka kuhurumiwa kwa dhambi zao wamtimue jkm, Mwenye kiti na wapambe wake wote wafikishwe mbele ya sheria kiukweli hapo tutaamini kweli wamedhamiria kubadilika, pia watuombe msamaha WATZ kwa kurudisha mali ya umma yote walivyodhurumu (viwanja vya mpira, majengo yaliyojengwa kwa jasho la watz wote,viwanja walivyodhurumu nk) kwa Halmashauri husika mfano Kirumba stadium iwe mali ya jiji la Mwanza kwa faida ya Manispaa zke na H/Wilaya zake
 
kwani gamba ni la nyoka tu.....? iliyozungumziwa ni process ya kuvua gamba ambayo wengi wanayo akiwemo na nyoka....kitendo cha kuvua gamba hakibadilishi aina ya mnyama "reincarnation" bali kitendo hicho kinasaidia ukuaji wake ...maana ikibaki na gamba inazuia ukuaji
hivyo basi...CCM IMEVUA GAMBA LA ZAMANI....NA SASA WAPINZANI WAPISHE NJIA
 
Huu ni aina nyingine ya usanii ili kujaribu kujenga tena imani kwa watanzania,lakini hiki chama hakiwezi kubadilika leo.., ni mpaka kitakapokosa madaraka ndio kitaweza kujivua gamba kwa amani ila sio sasa..!
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, kumbe sumu ya nyoka, iko kwenye gamba!, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.
 
Wazo lako sio zuri, kwani kujivua magamba kwa nyoka ndio mwisho wa kuuma? Kwani hatapata sumu tena? kwani katiba ya CCM imebadilika? Weweeee mtoto wa nyoka ni nyoka tu.
Kujivua magamba ni lugha ya kuwadanganya watoto lakini kwetu sisi tuliokomaa kisiasa hatudanganyiki na hilo.
CCM ni ile ile, watu ni walewale, washauri ni walewale, kwatiba ni ileile.
Pole.
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, sumu ya nyoka, iko kwenye gamba, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.
 
Chama hakina dira tangu enzi za Mzee Horace Kolimba sasa wewe unafikiri kwa nini CCM kisiwe kikilazimika kuiga kila kitu barabarani???

Sasa hivi kilichobaki ni kwamba kukitokea tu aina yoyote ya UTANI JUU YA MADAI YA KATIBA MPYA YA WALALAHOI bila udalali basi hapo ndipo nasi vijana tutakapoamua kijivulia gamba la CCM kabisa kikafie mbali huko.

Hata hivyo kwa wale ambao huenda wakawa wanafikiria mkwa yote tuyasema yo ni mzaha tu basi hadi hapo watabaki kujilaumu wenyewe. Mabadiliko tunayoyataka nchini kamwe hayazuiliki hata kwa kutumia nguvu ya giza.

CCM, wenzenu huku waaala bado hatujaona gamba lolote mnalodai kujivua siku za hivi karibuni. Hadi hapo ndio kwaaanza mmepata alama 02 / 100. Chapeni kazi zaidi na zaidi kufanya mabadiliko makubwa ki-mfumo ndani na nje ya CCM ndipo angalaaaau tuweze kuwasikilizeni hapo baadaye kidoooooooooogo tuweze kuanza kuwafikirieni.

Nasema mpaka hivi sasa wala sijaona mabadiliko ya kiasi cha kuweza kuzungumzi hapa; wake up!!!!!!!!!!!!!!
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, sumu ya nyoka, iko kwenye gamba, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.

Isije kuwa umepewa chochote kuja na hii!! I will be very dissapointed!!

Anyway, back to your point..................!!

Nyoka inasemekana huwa anajivua gamba mara saba katika maisha yake..... CCM wamejivua mara mmoja tu kama wao na wewe mnavyotaka tuamini. Na sumu ya nyoka huwa haiishi baada ya kujivua gamba mmoja!! Kujivua gamba kwa nyoka huwa ni sehemu ya kukua kwake!!

Gamba la CCM ni mafisadi ambao wao wamedai wamewapa siku 90 wajiondoe..... lakini mpaka sasa wako kimya. Je una uhakika gani wataachia ngazi baada ya siku 90???

Uzuri CCM wamekiri wenyewe kuwa ni nyoka na sasa wamevua gamba ili waongezeke size may be kuwa chatu au nduli ili watumeze....... sasa nafikiri ni time yetu Watanzania kumpiga huyo nyoka kichwani badala ya kumchezea ngoma kama unavyosuggest!!
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, kumbe sumu ya nyoka, iko kwenye gamba!, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.

Pasco,

Mimi nitaamini kama kweli CCM wako serious..nikiona wanawachukulia hatua za kisheria wale wote waliotuibia and I mean Lowassa, RA, Chenge and company. But for now, I think its simply a ploy to insult intellectual ability za watanzania! To be honest, CCM must come out clean watu walioiba pesa za wananchi sio tuu waadhibiwe lakini kwanza wazirudishe! Then I will reinstate my faith in CCM politics. But for now? Hapana...
 
Kama umetumwa na wavua magamba wenzio(MAFISADI)kawaambie hakuna hata mmoja wa kumshika masikio humu JF.Hivi mnaweza kusema mmejivua gamba kwa kuwashutumu watu watatu tu?,Chenge,Rostam,Lowasa ni hao tu?,inamaana hawakushirikiana na wengine!?,vp kuhusu KAGODA,EPA na mengine mengi wahusika walishachukuliwa hatua gani?,yaani mtu anaiba mnasema mumnyang'anye uraia ndio suluhu hiyo kwa wananchi masikini walioibiwa fedha zao.Vp mikataba mibovu ya madini au ndio kusema ccm hamna wasomi,tuamini lipi zaidi ya tamaa yenu mbaya!?,Juzi mkaguzi mkuu wa hesabu za Serikali alitoa ripoti yake kuwa kwa mwaka mmoja umefanyika ubadhirifu(wizi)wa bilioni 48 kwa kulipa wafanyakazi hewa!!,vp kama hizo bilioni 48 zingeingizwa ktk wizara ya Afya?,mama zetu wajawazito wangekufa kweli kwa kukosa huduma?matokeo yake Serikali ya ccm(MAFISADI)inawanunulia wamama WAJAWAZITO bajaji Tena vijijini kwenye barabara mbovu,,hii ni sahihi kweli?wao wamejikopesha milioni 90 kila mbunge ktk bunge lenye idadi ya Wabunge 350?Na hivi wabunge ni zaidi ya Wananchi?Kumbuka mswaada mmbovu walioupitisha Wabunge wa ccm ktk kikao cha bunge hivi majuzi,hivi Wanamaker akili kweli?,wanapotisha sheria mbovu hata ile inayomkandamiza hata yule aliekupigia kura!?,kupitisha sheria mbovu kwa sbb ya maslahi ya chama kwa ushabiki"maandazi"ni hatari sn.Matatizo yapo mengi wewe endelea kubaki na ccm yako hakuna mjinga humu Jf wa kukubaliana na pumba ulizotoa
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, kumbe sumu ya nyoka, iko kwenye gamba!, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.

Nimekuelewa Pasco kazi njema, watajiunga watoto wa STD 4 kama walivyofanya dodoma.
 
Kama huna cha kuandika usitujazie server bila sababu. mimi kati ya kifo na ccm, mimi nachaguwa kifo.
 
Pasco,

Mimi nitaamini kama kweli CCM wako serious..nikiona wanawachukulia hatua za kisheria wale wote waliotuibia and I mean Lowassa, RA, Chenge and company. But for now, I think its simply a ploy to insult intellectual ability za watanzania! To be honest, CCM must come out clean watu walioiba pesa za wananchi sio tuu waadhibiwe lakini kwanza wazirudishe! Then I will reinstate my faith in CCM politics. But for now? Hapana...
u have spoken my worlds.I appreciate
 
Isije kuwa umepewa chochote kuja na hii!! I will be very dissapointed!!
Mr. Zero, kumbe takuwa very dissapoited kama nimepewa chochote kuipigia debe CCM, naomba usiwe dissapointed, sijapewa chochote na yoyote.

Baada ya kuzisikia shutuma za CCM kuwa JF ni ya Chadema, huku humu JF kuna kina sisi kibao tusio na vyama, na haswa baada ya CCM kujivua gamba na kugeuka chama kipya, na baada ya kufundishwa kumbe sumu ya nyoka inakaa kwenye gamba, ukivua tuu gamba, sumu imekwisha, hivyo sasa CCM ni chama safi, nimejitolea tuu kuhamasisha watu wajiunge na CCM, kwa sababu kumbe tatizo la CCM lilikuwa gamba tuu ambalo limechakaa, sasa ni gamba jipya, kwanini tusijiunge?.
 
Kama huna cha kuandika usitujazie server bila sababu. mimi kati ya kifo na ccm, mimi nachaguwa kifo.
Saigon, hakuna ulazima wa kuichagua CCM iwapo unaona bora kufa kuliko kuichagua CCM, nakushukuru uko hai, hukuichagua, lakini tukubali, tukatae, CCM ndio hii iliyopo, wewe kufa unangoja nini, au uliambia CCM lazima uichague wewe?, wako walioichagua na ndio hiyo, halafu sasa imekuja kuwashika wale wengine ambao hawakuichagua kwa sababu ya gamba chafu, sasa imevua gamba, ina meremeta, inang'aa hivyo kuna ubaya gani tukijiunga kwa vingi, ili kuwadhibitishia, tatizo lilikuwa gamba tuu!.
 
CCm wanapakaza masizi kwenye nyuso zetu wakigeuza kuwa eti ndio mafuta ,Gamba ni mfumo mzima wa utawla wa chama na serikali yake tutajiunga kwanza wakitutajia orodha ya mafisadi na watutajie ufisadi wao na kiasi gani cha fedha wanacho
Mafisadi yote yatakaposwekwa ndani
Watakapofuta mikatamba ya madini yote mibovu
CCM na serikali watakaporudisha fedha walizoiba EPA,DECI
CCM watakapoacha kupeana vyeo kwa upendeleo
Watakapo saidia vijana waweze kujiajili au kuajiliwa kwa kuongeza viwanda na kununua bidhaa zao
Vyoo vya nyasi na madarasa ya nyasi kwa wanafunzi vitakapotokomezwa
Maji yatakomfika kila mwananchi
Dar es salaam itakapkuwa safi na wanachi kufuata utawala wa sheria kuondoa magereji bubu na kuondoa malori yote barabarani
Wazee kutunzwa vizuri na kupewa pensheni zao
Wanafunzi vyo vikuu kutokusumbuliwa na mikopo yao
Vinginevyo Pasco jiunge mwnenyewe na tunakutakia kila la heri
 
Back
Top Bottom