CCM wamejivua Gamba: Je CCM siyo Nyoka tena bali sasa ni mjusi tu?

Pasco,

Mimi nitaamini kama kweli CCM wako serious..nikiona wanawachukulia hatua za kisheria wale wote waliotuibia and I mean Lowassa, RA, Chenge and company. But for now, I think its simply a ploy to insult intellectual ability za watanzania! To be honest, CCM must come out clean watu walioiba pesa za wananchi sio tuu waadhibiwe lakini kwanza wazirudishe! Then I will reinstate my faith in CCM politics. But for now? Hapana...




hakiya nani bado sijiungi nao kuna Gamba moja linaitwa Jakaya Mrisho Kikwete likitoka mimi na ukoo wangu wote tutajiunga na CCM
 
hakuna cha kujivua gamba hapi kama wameharibu ni kusepa tu kwa kweli hata ukijivua gamba wakati bado mchafu haitusaiddi kwa miaka hii 50 tunahitaji mabadiliko ya ukweli
 
Ukifuatilia taarifa za vikao vya CCM huko Dodoma hivi karibuni, utagundua kuwa Mwenyekiti wake JK hana ujasiri wa kuwataja waziwazi wale anohitaji kuwashughulikia (pengine kwa shingo upande), watu ambao wanaccm walio wengi wanaamini wanasababisha kazi ya JK iwe ngumu (magamba na mafisadi).

Lakini kuna usemi unaosema 'deeds talk louder than words' , huu ni muhimu sana, na pengine umemsaidia JK kueleweka kwa kile alichoshindwa kuweka wazi. Bila kujali mzunguko aliotumia kufika kwenye matokeo, matokeo ni kuwa baba mtu (Makamba) katolewa na mtoto (Januari) kaingizwa kwenye Sekretarieti ya sisiemu.

Je, kwa mtaji huu JK atakanusha kuwa kwa kusema GAMBA, alimaanisha MAKAMBA?
JF nawaombeni jibu.
 
Wanabodi,
Baada ya JF kushutumiwa kuwa inamilikiwa na Chadema, na CCM imejivua gamba, Jee hakuna haja ya kujitolea kutoa wito kwa wana JF wengi tujiunge na Chama Cha Mapinduzi?.

Natoa wito kwa wale wote wanaitakia mema nchi hii, naombeni sasatuipende CCM, CCM sasa ni CCM Mpya, imejivua gamba la ufisadi, sasa CCM inameremeta, inavutia, inapendeza hivyo wale tusio na vyama kama mimi, CCM ndio chama cha kujiunga nacho, kwani baada ya kuvua gamba, CCM ni safi.

Na kwa msiomjua nyoka, kumbe sumu ya nyoka, iko kwenye gamba!, nyoka akishajivua gamba, anakuwa hana sumu tena, huyo ni nyoka wa kumkaribia hata kumchezea kama yale majoka wa Kibisa!.

Shime tujiunge na CCM safi, CCM Mpya kwa wingi! na humu jukwaani tujaze posti za shangwe na mapambio kuisifu CCM, ili ipendeke baada ya kujivua gamba.

Pasco.

Phylosophy hiyo inafaa ccm tu; pasco mie kwa uelewa wangu wewe ni ccm na mwanaharakati (mchana huna chama usiku ccm) ila unalazimika maana ccm haiuziki na una akili ndio maana huwezi kujiondo akili zako; anayway ni mambo tu turudi ktk mada.
Kuna mafisadi 11; karibu wote walikuwa CC na NEC. Sasa wakitolewa 3 je ndio kujivua; what about wengine akiwemo Mweneyekiti wao? najua wanatakiwa waondoke maana hawa wamejichubua tu robo ya gamba la nyoka bado hawajajivua gamba mpaka tuone mafisadi wote wanashughulikiwa ndio tujue wamejivua gamba au la ni usanii tu full stop na mwacheni Dr afanye kazi yake
 
_dk%20wilbord%20slaa.jpg

Dk Slaa

Godfrey Nyang'oro, Urambo
KATIBU Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka Rais Jakaya Kikwete awataje watuhumiwa wa ufisadi na kisha kuwavua nyadhifa zao zote na kisha kuwafikisha mahakamani katika muda wa siku 90 kama kweli anataka kukivua gamba chama hicho.

Kauli hiyo ya Chadema kwa Rais Kikwete imekuja siku chache baada ya CCM kuchukua hatua katika kile ilichokiita kujivua magamba kwa kuwataka watuhumiwa wote wanaotajwa kuhusika katika kashfa kadhaa za ufisadi, kujiondoa wenyewe katika nafasi zao ndani ya chama hicho katika kipindi cha miezi mitatu vinginevyo watawajibishwa.
Jana, akiwa kwenye Uwanja wa Kaliua, Urambo Magharibi, Dk Slaa alisema kama kweli Rais Kikwete amedhamiria kukivua gamba chama chake, anapaswa kuuthibitishia umma kwa kufanya hivyo vinginevyo itakuwa ni ‘usanii.'
Kwa mujibu wa Dk Slaa, endapo watuhumiwa hao watatajwa na kuchukuliwa hatua ikiwamo kuvuliwa nafasi zao na uanachama na kupoteza ubunge au kufukuzwa serikalini, dhana hiyo ya kujivua gamba itakuwa na mantiki.
Dk Slaa alisema, Watanzania wanataka kuona fedha zao zilizoibwa na mafisadi zinarejeshwa na watuhumiwa kufikishwa mahakamani, hivyo haitoshi kusema neno kujivua gamba.
Mwanachama mwingine maarufu wa Chadema, Frederick Mpendazoe ambaye aligombea ubunge kwa tiketi ya chama hicho, Jimbo la Segerea katika Uchaguzi Mkuu uliopita, alisema endapo CCM kitashughulikia watuhumiwa hao wa ufisadi ndani ya siku 90 ni dhahiri kutafanyika uchaguzi kutokana na kile alichodai kwamba ni kuwa na wabunge wengi waliingia madarakani kwa njia ya rushwa.
Alidai kwamba CCM imepoteza mwelekeo kutokana na kuhodhiwa na watu wenye malengo ya kibiashara ambao huchochea ufisadi unaokigharimu sasa.
Mpendazoe ambaye aliwahi kuwa kada wa chama hicho tawala alisema miaka ya nyuma wakati wa Mwalimu Julius Nyerere, CCM kilikuwa madhubuti kutokana na kuwa na viongozi waliokuwa tayari kupambana na rushwa na ukosefu wa maadili ya uongozi, hali ambayo ni tofauti kwa sasa.
Mpendazoe ambaye alijiondoa CCM kutokana na kile alichodai kuwa ni fitina za mafisadi alisema uongozi ndani ya chama hicho tawala kwa sasa ni uwekezaji akisema asiye na fedha ni vigumu kupata uongozi.
Alisema kutokana hali hiyo, hata ile misingi ya waasisi iliyojengwa katika miaka ya 1960 na 1970 imebomolewa na mafisadi kushika hatamu za uongozi wa chama hicho tawala.
Mpendazoe alisema Serikali iliyopo ni ya kidemokrasia lakini imekuwa ikiyapa kisogo matatizo ya wananchi wa tabaka la chini na kukumbatia wafanyabiashara ambao wana nguvu ndani ya chama hicho.
Kuhusu muswada wa Sheria ya Marejeo ya Katiba, alisema hadi sasa serikali imeuondoa muswada huo bila kuweka mambo wazi na kuonya kama ukirejea kama ulivyo na tume ikiundwa na rais chama hicho kitaandamana.
 
Phylosophy hiyo inafaa ccm tu; pasco mie kwa uelewa wangu wewe ni ccm na mwanaharakati (mchana huna chama usiku ccm) ila unalazimika maana ccm haiuziki na una akili ndio maana huwezi kujiondo akili zako; anayway ni mambo tu turudi ktk mada.
mwanza_kwetu, hata mimi Mwanza kwetu. nashukuru kwa kunitambua kama mwanaharakati wa CCM, kwa vile mimi sio mwanachama wa chama chochote cha siasa, hivyo nina uhuru wa kupenda chama chochote na ndia maana niko hapa jf kuhamasisha wana jf wenzangu, tujiunge na CCM, imevua gamba lenye sumu, nimejifunza pia kumbe sumu ya nyoka inakaa kwenye gamba, na nyoka akishajivua gamba, anageuka kambale!, tujiunge na chapa kipya ndani ya gamba jipya na watu wapya na sera mpya ya kupinga ufisadi!.
 
Ndugu zangu nimefuatilia kwa makini siku za hivi karibuni wimbo mpya wa changu wa kujivua Gamba!
Ni kichekesho kutaka kuwaaminisha watanzania kuwa kitendo cha Makamba senior kutoka na kuingia Makamba junior ni kusafisha chama, au kumkumbuka mtoto kwa Kada Maarufu na kiongozi wa juu wa Zamani kidogo Yaani Nape mtoto wa Moses Mnawiye eti ni usafi chamani!!. Maigizo makubwa zaidi ni pale tunapoambiwa yule mtengeneza sera ya uchaguzi ya ccm 2010-15 ambaye alituhakikishia kupitia vyombo vya habari kuwa bei za vifaa vya ujenzi haziwezi kushuka kupewa Ukatibu mkuu ni usafi zaidi na matumaini kwa watanzania!.
Hivi ccm inakata tuamini kuwa ina ubavu wa kuwagusa mafisadi wa nchi hii ambao kwa hakika shekeli zao ndo zinaendesha chama??! Nadhani ccm inatakiwa iache kuigiza na badala yake ikubali kuwa haina tena uwezo wa kuwasaidia wanyonge na maskini wa taifa hili. Hivi kweli Makamba anaweza kuwa Gamba gumu kuliko RA??? Hivi kweli matatizo ya watanzania yalisababishwa na Makamba yule luteni wa Jeshi???, au tuseme Hosea wa Takukuru aliyesema richmond ni safi alitumwa na Makamba!!! This is a joke
Jamani ccm tusitaniane let us be serious
 
Nisicho Kielewa ni kuwa Inawezekanaje Fisadi aombwe kuwashughulika Mafisadi???
Mi naona ni muhimu kuchora mstari nyoofu, kama kikwete ni Fisadi basi aombwe aondoke madarakani na mafisadi wenzie ama Kikwete awe mr clean then awashughulikie Mafisadi. ki ukweli Mambo haya yanachanganya, kwani kumuomba kikwete awashughulikie Mafisadi ingali na yeye anaonekana ni fisadi si kitu ambacho ki uhalisia kinawezekana. so Dr slaa and others need to clarify this matter and put it in the right place!!


Inashangaza shangaza sana
 
Slogan yenyewe imekosa mashiko. Haina mantiki yoyote. Aliyebuni slogani hii si mbunifu kabisa, hii inatokana na ukungu uliowajaa. Hawaoni tena. Ila kwa muvi hii nina hakika chama cha magamba kitakufa bila wasi wasi.
Mungu ibariki Tanzania.
 
Warudishe pesa walizochukua mwaka 2005 ku fund campaign yao ndo tutaamini wamejivua gamba.
 
Wakuu ukisoma vizuri hiyo habari hapo juu, utaona Dr. Slaa katamka wazi kuwa kikwete ajivue gamba ndani ya ccm sababu kashirikiana na wenzake kufanya ufisadi. Hapo mwishoni amemtega kuwa awachukulie hatua za kisheria watuhumiwa wote au kama anashindwa aondoke. Huo ni mtego kwa sababu kikwete hataweza kuwachukulia hatua watu alioshirikiana nao kuiba.
 
watanzania wakati mwingine tuache unafiki...tulipewa nafasi ya kumuondoa Kikwete kwa njia ya kura, tukamrudisha madarakani....kama walichakachua matokeo kwa nini hatukuwa tayari kufa kwa kuandamana...kuwa hatukumchagua iwe vipi atangazwe mshindi....haya yote tuliyataka wenyewe..next time tuwe tayari kwa lolote endapo tutakuwa na uhakika kuwa aliyetangazwa mshindi si chaguo letu....inwezekana tukiamua....!
 
Taifa la Tanzania lina maadui wanne
1. umasikini
2. Maradhi
3. Ujinga
4. CCM
 
Na Waandishi wetu



PAMOJA na uamuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya vigogo, baadhi ya makada maarufu wa chama hicho wameibuka na kusema bado chama hicho kina wakati ngumu.

Makada hao wameeleza kuwa uamuzi uliofikiwa na chama hicho hautakisaidia chochote na kusema kuwa ni sawa na kuoga mwili bila kubadili nguo safi.

Hivi karibuni aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, na sekretarieti yake waling’olewa kama hatua ya chama hicho kuzaliwa upya kwa lengo la kurejesha imani na umaarufu wake kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla.

Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki, makada hao: Stephen Galinoma na David Butinini walisema uamuzi huo hautasaidia chochote ndani ya CCM zaidi ya kuongeza mpasuko na kuendelea kuvipa umaarufu vyama vya upinzani hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Galinoma alisema hatua ya CCM kujivua gamba ni moja ya mchakato mzuri katika wakati huu, ingawa uamuzi huo umekuja kwa kuchelewa mno, hivyo hautakuwa msaada kwa chama.

Galimona ambaye amepata kuwa mbunge wa Kalenga kwa tiketi ya CCM, alisema dalili za aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Makamba kukivuruga chama ilianza kujionyesha mapema, lakini uongozi wa juu haukuchukua hatua wala kusikiliza maoni ya wana CCM hadi chama kimefika mahala pabaya. “Tunashukuru chama sasa kimechukua hatua ya kumuengua katika nafasi hiyo pamoja na makada wengine ambao walikuwa wakikivuruga chama chetu..ila ukweli bado CCM ina wakati mgumu kujisafisha na kufanya Watanzania kurudisha imani yao kama mwanzo,” alisema Galimona.

Alisema makundi ndani ya CCM hayatamazilika kutokana na mizizi ya makundi hayo kuenea hadi ngazi za chini na kuwa baada ya kufanya mabadiliko hayo ngazi ya juu ni vizuri kuanza jitihada za kusafisha chama hicho ngazi ya mikoa, wilaya hadi vitongoji.

Aidha, alisema mabadiliko hayo yafanyike katika ngazi ya serikali kwa kuwapumzisha wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wazembe na ikiwezekana hata baraza la mawaziri kuvunjwa na kuundwa upya.
“Ukweli sasa CCM imechafuka sana tena uchafu huo umeshuka hadi huku chini sasa kusafisha juu pekee haitoshi ni sawa na kuchafua, kwani kuoga mwili huku nguo ni chafu ni sawa na kutooga kabisa. Hapa CCM imeanza kupunguza matawi kwa lengo la kuangamiza magugu bila kuchimbua mizizi yake ardhini,” alisema Galimona.

Kuhusu moto ambao viongozi wapya wameanza nao zikiwemo kauli za Nape Nnauye kuwa mafisadi ndani na CCM wakae chonjo, Galinoma alisema anawatakia mafanikio viongozi hao kutimiza mipango hiyo, japo matunda yake ni madogo.

Kwa upande wake, kada maarufu wa chama hicho Mkoa wa Iringa, Butinini alisema moto wa vyama vya upinzani hasa ule wa CHADEMA ni mkali zaidi na kuwa bila CCM kujitathmini upya na kujipanga vema moto huo unaweza kuiteketeza CCM.

Alitaka CCM kuwa makini na wapinzani wanaokimbia vyama vyao na kujiunga na CCM kuwa ni vizuri hao kuogopwa na kutoaminiwa haraka na kupewa nafasi za uongozi ndani ya chama, ili kuwachunguza taratibu.

Wakati huohuo, viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyoosheana vidole kutaka wajivue magamba kwa kutokuwa waadilifu.

Tafrani hiyo ilitokea juzi baada ya CCM wilaya kuitisha kikao cha Halmashauri Kuu maalumu kwa lengo la kupongeza hatua iliyochukuliwa na chama hicho ngazi ya taifa ya kujivua gamba kwa kuwatosa baadhi ya viongozi.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa kuzuka kwa mvurugano huo kunatokana na baadhi ya wajumbe kushinikiza viongozi wa chama ngazi ya wilaya wajivue magamba kwa kujiuzulu kutokana na kuchangia chama kutofanya vema katika baadhi ya maeneo kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Habari hizo zilieleza kuwa wajumbe katika kikao hicho waliwapasha viongozi wao kuwa mahiri kupongeza maamuzi ya kitaifa yaliyofanyika huku miongoni mwao wakiwa hawana uadilifu.

Katika malumbano hayo, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kahama Mjini, Mathias Misungwi, aliwaeleza viongozi hao kama wanaunga mkono hatua zilizochukuliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nao wajivue magamba kwa kujiuzulu nyadhifa zao. Misungwi alisema viongozi wote wa CCM ngazi ya wilaya kuanzia Mwenyekiti wa CCM wilaya pamoja na watendaji wake wote wanastahili wapime uadilifu wao kwa kutambua kuwa utekelezaji wao kuanzia kipindi cha mchakato wa kura za maoni, uchaguzi mkuu hadi sasa hauna maslahi na chama hivyo kuwapasa kujivua magamba yao kwa kuachia ngazi.
 
CCM sasa wageukana
• Wakejeli tambo za chama kujivua gamba

na Waandishi wetu


amka2.gif
PAMOJA na uamuzi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani baadhi ya vigogo, baadhi ya makada maarufu wa chama hicho wameibuka na kusema bado chama hicho kina wakati ngumu.
Makada hao wameeleza kuwa uamuzi uliofikiwa na chama hicho hautakisaidia chochote na kusema kuwa ni sawa na kuoga mwili bila kubadili nguo safi.
Hivi karibuni aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Yusuph Makamba, na sekretarieti yake waling’olewa kama hatua ya chama hicho kuzaliwa upya kwa lengo la kurejesha imani na umaarufu wake kwa wanachama wake na wananchi kwa ujumla.
Wakizungumza na Tanzania Daima kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki, makada hao: Stephen Galinoma na David Butinini walisema uamuzi huo hautasaidia chochote ndani ya CCM zaidi ya kuongeza mpasuko na kuendelea kuvipa umaarufu vyama vya upinzani hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Galinoma alisema hatua ya CCM kujivua gamba ni moja ya mchakato mzuri katika wakati huu, ingawa uamuzi huo umekuja kwa kuchelewa mno, hivyo hautakuwa msaada kwa chama.
Galimona ambaye amepata kuwa mbunge wa Kalenga kwa tiketi ya CCM, alisema dalili za aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Makamba kukivuruga chama ilianza kujionyesha mapema, lakini uongozi wa juu haukuchukua hatua wala kusikiliza maoni ya wana CCM hadi chama kimefika mahala pabaya.
“Tunashukuru chama sasa kimechukua hatua ya kumuengua katika nafasi hiyo pamoja na makada wengine ambao walikuwa wakikivuruga chama chetu..ila ukweli bado CCM ina wakati mgumu kujisafisha na kufanya Watanzania kurudisha imani yao kama mwanzo,” alisema Galimona.
Alisema makundi ndani ya CCM hayatamazilika kutokana na mizizi ya makundi hayo kuenea hadi ngazi za chini na kuwa baada ya kufanya mabadiliko hayo ngazi ya juu ni vizuri kuanza jitihada za kusafisha chama hicho ngazi ya mikoa, wilaya hadi vitongoji.
Aidha, alisema mabadiliko hayo yafanyike katika ngazi ya serikali kwa kuwapumzisha wakuu wa mikoa na wilaya na wakurugenzi wazembe na ikiwezekana hata baraza la mawaziri kuvunjwa na kuundwa upya.
“Ukweli sasa CCM imechafuka sana tena uchafu huo umeshuka hadi huku chini sasa kusafisha juu pekee haitoshi ni sawa na kuchafua, kwani kuoga mwili huku nguo ni chafu ni sawa na kutooga kabisa. Hapa CCM imeanza kupunguza matawi kwa lengo la kuangamiza magugu bila kuchimbua mizizi yake ardhini,” alisema Galimona.
Kuhusu moto ambao viongozi wapya wameanza nao zikiwemo kauli za Nape Nnauye kuwa mafisadi ndani na CCM wakae chonjo, Galinoma alisema anawatakia mafanikio viongozi hao kutimiza mipango hiyo, japo matunda yake ni madogo.
Kwa upande wake, kada maarufu wa chama hicho Mkoa wa Iringa, Butinini alisema moto wa vyama vya upinzani hasa ule wa CHADEMA ni mkali zaidi na kuwa bila CCM kujitathmini upya na kujipanga vema moto huo unaweza kuiteketeza CCM.
Alitaka CCM kuwa makini na wapinzani wanaokimbia vyama vyao na kujiunga na CCM kuwa ni vizuri hao kuogopwa na kutoaminiwa haraka na kupewa nafasi za uongozi ndani ya chama, ili kuwachunguza taratibu.
Wakati huohuo, viongozi wa CCM Wilaya ya Kahama wamejikuta katika wakati mgumu baada ya kunyoosheana vidole kutaka wajivue magamba kwa kutokuwa waadilifu.
Tafrani hiyo ilitokea juzi baada ya CCM wilaya kuitisha kikao cha Halmashauri Kuu maalumu kwa lengo la kupongeza hatua iliyochukuliwa na chama hicho ngazi ya taifa ya kujivua gamba kwa kuwatosa baadhi ya viongozi.
Habari kutoka ndani ya kikao hicho zinadai kuwa kuzuka kwa mvurugano huo kunatokana na baadhi ya wajumbe kushinikiza viongozi wa chama ngazi ya wilaya wajivue magamba kwa kujiuzulu kutokana na kuchangia chama kutofanya vema katika baadhi ya maeneo kwenye uchaguzi mkuu uliopita.
Habari hizo zilieleza kuwa wajumbe katika kikao hicho waliwapasha viongozi wao kuwa mahiri kupongeza maamuzi ya kitaifa yaliyofanyika huku miongoni mwao wakiwa hawana uadilifu.
Katika malumbano hayo, Mwenyekiti wa UVCCM Kata ya Kahama Mjini, Mathias Misungwi, aliwaeleza viongozi hao kama wanaunga mkono hatua zilizochukuliwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa nao wajivue magamba kwa kujiuzulu nyadhifa zao.
Misungwi alisema viongozi wote wa CCM ngazi ya wilaya kuanzia Mwenyekiti wa CCM wilaya pamoja na watendaji wake wote wanastahili wapime uadilifu wao kwa kutambua kuwa utekelezaji wao kuanzia kipindi cha mchakato wa kura za maoni, uchaguzi mkuu hadi sasa hauna maslahi na chama hivyo kuwapasa kujivua magamba yao kwa kuachia ngazi.
 
Matukio mengie yametokea siku za hivi karibuni kwenye siasa za nchi yetu. Nadhani tukio kubwa ninalokumbuka ni lile la CCM kujivua gamba kwa kuwaondoa madarakani akina Yusufu MAKAMBA na kuweka damu mpya ya akina January MAKAMBA.

Je ni kweli sasa CCM siyo nyoka tena bali sasa amekuwa ni mjusi tu asiyekuwa na madhara kwa watanzania tena? Swali hilo ndio sijaweza kulijibu; na ndiyo maana naanzisha thread hii ili baada ya wiki moja niweza kufahamu kama kweli magezui yaliyofanyika ndani ya CCM ni ya kweli au ni danganya toto tu. jambo moja linalokera zaidi ni kuwa gamba lililovuliwa na CCM ni lile la ufisadi, ambalo kwa mujibu wa sheria za nchi ni kosa la jinai. Je ni kweli mafisadi waliovuliwa CCM watafikishwa kwenye vyombo vya sheria; yaani kuna anayeweza kuniaminisha kuwa Januari atamfikisha Yusufu kwenye vyombo vya sheria ili hali Januari huyo amefika hapo kupitia mgongo wa Yusufu?

Nadhani bado tunaishi na nyoka uvunguni mwetu; wakati wowote atatung'ata tu!!

Ni vizuri zaidi kabla hujafanya jambo kwanza lifikirie halafu ndio ulifanye. Nikikusoma hapo juu naona kama vile umechanganyikiwa, huamini kilichotokea au kuna mgogoro ktk uwezo wa kuelewa. CCM iliposema itajivua gamba haikumaanisha kuwa wajumbe wa Secretariat ni mafisadi. CCM ilihitaji kuwa na Secretariat itakayoweza kuwashughulikia mafisadi ndani ya Chama. Mwenyekiti wa CCM alitoa mfano wa kujivua gamba "kama vile" nyoka anavyojivua gamba lake na kurudi ktk hali mpya na yenye nguvu zaidi. Ufisadi sio tabia ya CCM, bali kuna "vibaka" waliojipenyeza ndani ya CCM ndio wanaofanya Ufisadi huo. Kazi ya Secretariat mpya ni kuwashughulikia "Vibaka" hao. Unahitaji kuwa na kikosi kizuri cha polisi ili uweze kuwakamata waharifu. Hivi ndivyo CCM ilivyofanya.

Mchakato wa kuwashughulikia "vibaka" ndani ya CCM ndio umeanza. Nakushangaa kwanini unabeza mapema hivi? Kwanza mulianza kubeza kuwa CCM haiwezi kujivua gamba. Sasa imejivua, munasema, hapana, hawawezi kuwashughulikia 'mafisadi" ndani ya siku 90. Hivi hizi siku 90 zimeishapita?

Chadema najua imewauma saana kwa CCM kufanya maamuzi haya makubwa. Wengi wenu hamuelewi kuwa viongozi wenu wanakula na hao mafisadi, na ndio maana ktk mkutano wa Tabora walibadilisha ajenda ya KATIBA na kuiweka ya "MAFISADI". Mabadiliko haya yalifanywa na viongozi dakika za mwisho kwa kushawishiwa na hao mafisadi ili waliingize jina la Jakaya Kikwete ktk orodha hiyo mpya. Hivi ni kweli Jakaya Kikwete hakutajwa ktk orodha aliyoisoma Dr. Slaa plae Mwembe Yanga? Sasa kurudia tena jina la Jakaya Kikwete ktk orodha mpya, kuna upya gani hapa?

Siku zote huwa nasema huyu mzee Dr. Slaa sasa amefikia ukomo wa kufikiria, maana anakurupuka kama vile hana akili timamu. Hivi ile orodha aliyoisoma Tabora ni kweli mpya? Hivi anataka kumdanganya nani hapa? Nasi tupo humu ndani ya JF hatuhoji chochote juu ya hilo, tunaona mambo yote anayosema mzee huyu ni sawa tu? Tumekuwa MAZUZU? Its time for change. First of all we have to change our mindset.
 
CHADEMA yamshukia Nape


na Mwandishi wetu

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimemtaka Katibu wa NEC Ikitikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kufuta kauli yake aliyoitoa kuwa mafisadi wanatumia baadhi ya vyama vya siasa kuwapakazia watu wengine akiwemo Rais Jakaya Kikwete na familia yake kuhusika katika vitendo vya kifisadi. Akizungumza jana kwenye ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Oganizesheni na Mafunzo wa CHADEMA, Singo Benson, alisema kauli ya Nape haina mashiko na ameanza vibaya katika wadhifa huo.

"Tunamtaka Nape aweke wazi hao mafisadi ambao wanatutumia ili kuwapakazia watu akiwemo Rais Kikwete na familia yake kuhusika moja kwa moja katika tuhuma za ufisadi…, asiogope ataje majina yao," alisema Benson.
Alisema Nape hajafanya utafiti wa kina, ili kupata takwimu sahihi zitakazomsaidia pindi anapojieleza mbele ya umma wa Watanzania.

Katika mkutano huo CHADEMA pia kimeitaka serikali kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote wa ufisadi kutokana na majina yao kuwa wazi.

Alisema majina hayo ya mafisadi yako wazi na chama hicho kimefanya utafiti wa kina na kuwabaini kuhusika katika matukio ya ufisadi dhidi ya taifa, hivyo serikali iwafikishe mahakamani na kuhukumiwa kama wahalifu wengine.
"CCM wamekiri mafisadi wapo na sisi tukawataja kwa majina kilichobaki wao ni kuwafikisha mahakamani ili washtakiwe kutokana na kuhusika na ufisadi wa taifa moja kwa moja.

Aidha, alisema kujiuzulu pekee kwa mafisadi hao hakutasaidia bali kinachohitajika ni kutaifishwa mali walizokula na baadaye kushtakiwa.

Juzi Nape alisema wamebaini watuhumiwa hao kutumia baadhi ya vyama vya siasa na viongozi wa dini kufanikisha azma yao.

Nape alikaririwa akisema wamebaini kuwa baada ya kuchukua uamuzi wa kuwaondoa mafisadi kwenye NEC kule Dodoma, wameanza kutumia baadhi ya vyama vya siasa kuhujumu chama, kibaya zaidi wanaelekeza hujuma zao kwa mwenyekiti wa CCM Taifa.
 
Dk.Slaa amtupia mishale Kikwete


*Amtaka naye ajivue gamba CCM
*Adai amekuwa akitetea mafisadi


Na Moses Mabula, Tabora


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Willibrod Slaa amesema Rais Jakaya Kikwete

anapashwa ajivue gamba CCM kwa kuwa yeye na washirika
wake wameshrikiana kufanya ufisadi ndani ya Serikali.

Dkt. Slaa alisema hayo katika mkutano wa hadhara wakati akihutubia wananchi kwenye

Uwanja wa Chipukizi mjini Tabora.

Alisema kuwa Rais Kikwete amekuwa akiwatetea maswahiba wake wanaotuhumia kuiingizia

Serikali hasara ya mamilioni ya shilingi licha ya kuelezwa bayana lakini amekuwa
akikaa kimya bila kuwachukulia hatua zozote zile za kisheria.

"Kikwete naye inafaa ajivue gamba ndani ya CCM kwa kuwa naye ni muhusika, asiwadanganye

Watanzania kwamba eti CCM imejivua gamba wakati naye ni gamba katika CCM," alisema
Dkt. Silaa huku akishangiliwa na umati wa watu na kuongeza:

"Huyu naye Chiligati eti anawatangazia Watanzania kwamba amewapa siku tisini wale wote wanaotuhumiwa na ufisadi, wawe wameondoka wenyewe ndani ya CCM na kumwacha Mkuu wake wa kazi Rais Kikwete kumtangaza naye awe ameondoka ndani ya hizo siku tisini" alisisitiza Dkt. Slaa.


Akimgeukia Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema Dkt. Slaa alisema

kwamba achague mambo mawili siasa au upolisi.

Alisema kuwa Mkuu huyo wa Polisi amekuwa akikipigia debe Chama Cha Mapinduzi na

kusahau kazi aliyotumwa na Watanzania ya kulinda usalama wa watu na mali zao lakini
hivi sasa amegeuka kuwa mwanasiasa ndani ya Jeshi la Polisi.

Alieleza kwamba iwapo ameshindwa kufanya kazi ya Upolisi ni vyema

akawatangazia Watanzania haraka kuwa yeye ameshindwa kazi hiyo na mwanasiasa.

Kuhusu watu wanaotuhumiwa kuwa mafisadi Dkt. Slaa alimtaka Rais Kikwete kuwachukulia

haraka hatua za kisheria na kuwafikisha mahakamani na kwamba kama hawezi basi naye
aondoke madarakani kwa kuwa ameshindwa kufanya kazi kwa wananchi waliomchagua
kuingia madarakani.

 
Back
Top Bottom