CCM: Tuna madiwani 16 Arusha

Naona hapa hamuelewani. Kwa nilivyoelewa swali na majibu kwa ujumla ni hivi:

V Kamata angeliweza kuwa Diwani wa Mbeya kama tu CCM (Chama chake) wangeliwajulisha Halmashauri ya Mbeya kuwa atakuwa Diwani wao kwa msimu huu wa bunge 2010 - 2015. Ila akishatambulishwa Mbeya, basi inakuwa imetoka na hawezi tena kubadilisha na kuwa wa Geita.

Regia angeliweza kuwa Diwani wa Dar es salaam, Dodoma au Kilombero na hata wa SIKONGE kwetu huku.

Ila yeye mwenyewe kwa UTASHI wake, aliamua kuwa wa Kilombero ingawa Katiba inamruhusu awe wa POPOTE pale Tanzania. Huu ndiyo nasema upuuzi wa Katiba hii na utatanishi wa Wabunge/madiwani wa kuchaguliwa.

Kibaya zaidi ni kuwa sijui watawezaje kuwa wakishiriki Vikao vya Bunge, halmashauri zao na kuwaona wananchi wao? Labda ndiyo maana Regia alilalamika kuwa majukumu ni mengi sana na akina Kiranga wakamwijia juu. Mtu kama Zitto anakuwa ni kasheshe zaidi maana unamkuta kwenye tume za bunge, udiwani, Naibu katibu wa chama, Bunge ............. Ndyo maana mambo yanakwenda shaghala baghala kwa Tanzania yetu ile. Mtu mmoja vyeo kibaoo.
Mkuu hata wewe kumbe unaweza kwenda low kiasi hiki? Nisaidie hicho kipengele cha katiba. Tuendelee kufunzana.
 
Mie Mnyamwezi wa Sikonge na Mnyakyusa wapi na wapi? Nawafahamu Mwakalinga family wengi tu ila mie siyo mtu wa huko wa Kyela na wala sijafika. Unaweza ukaweka ila utakuwa unaumbua watu wengine kabisa na siyo mie.

Veve Nyanda, Msula eve. Lelingange, kada kiti kampaninga kahurumzya, Fyonooo....... Nafikiri Kinyonga kaelewa :)
Asiyekujua atakubali, wanyamwezi na wasukuma hawana neno 'veve' wanasemaga 'bebe nyanda'.
 
Manispaa ya Arusha, the so called Jiji ina kata 17 tu. Ana maana hata Mbunge wa Arusha ni wa CCM?

Hesabu tena vizuri, inaelekea wana kata 19. Kumbuka kuna kata ziliongezwa mwaka 2010.

Madiwani wa Arusha ni 19 wa kuchaguliwa, mbunge mmoja wa kuchaguliwa. Madiwani wa kuteuliwa 7 (CCM 4 na CHADEMA 3) na wabunge viti maalum wanne (CHADEMA 2 na CCM 2). Jumla ndio inakuja 31.

Waliopiga kura walikuwa 16 wa CCM na mmoja wa TLP, jumla 17.
 
Mkulima

Asante kwa kujibu swali kuhusiana na idadi ya madiwani ktk vyama huhusika, sasa mwenye macho haambiwi tazama, akili ni nywere kila mtu na zake. Shauri lao wenyevipara kichwani.

Hahahahahah sisi wenye vipara hatuna akili sababu hatuna Nywele na si Nywere!
 
Wee MkamaP,

Acha kututukana wenye WASH & GO Kichwani bana.

Pamoja na kusoma yote, kumbuka kutumia akili za Mbayuwayu. Kwani Nywele ni kichwani tu?

Sema wengine wanazo nyingi, wengine ni kama Michael Jordan.....
Mkulima

Asante kwa kujibu swali kuhusiana na idadi ya madiwani ktk vyama huhusika, sasa mwenye macho haambiwi tazama, akili ni nywere kila mtu na zake. Shauri lao wenye vipara kichwani.
 
Asiyekujua atakubali, wanyamwezi na wasukuma hawana neno 'veve' wanasemaga 'bebe nyanda'.

Quinine,

Achana na ubishi ambao hauongezi tija. Sikonge mbona anajulikana waziwazi hapa kwamba ni mtu wa Sikonge, Tabora? Kufahamiana kwake na Mwakalinga hakumfanyi awe mtu wa Mbeya.

Nafikiri muhimu tuendelee kujadili mambo ya katiba na kuacha haya ya kushambuliana.
 
Wee MkamaP,

Acha kututukana wenye WASH & GO Kichwani bana.

Pamoja na kusoma yote, kumbuka kutumia akili za Mbayuwayu. Kwani Nywele ni kichwani tu?

Sema wengine wanazo nyingi, wengine ni kama Michael Jordan.....

Nina hasira na MkamaP ina maana mimi, Mkapa, Kinana na vipara vyetu hatuna akili? Ole wake nikutane naye atajua kuwa niko uwt!
 
Wee MkamaP,

Acha kututukana wenye WASH & GO Kichwani bana.

Pamoja na kusoma yote, kumbuka kutumia akili za Mbayuwayu. Kwani Nywele ni kichwani tu?

Sema wengine wanazo nyingi, wengine ni kama Michael Jordan.....

Sikonge ,duuu nywele(masahihisho) ndo akili kama una kipala(masahihisho) maamuzi yako yatakuwa tata balaaa.
 
Asanteni kwa Masahihisho ya KIPARA na siyo KIPALA.

Wengine unyamwezi umetujaa na nashindwa kujua kwa nini mji wetu unaitwa TABORA na siyo Tabola. Na cha ajabu ni kuwa unatokana na jina la vile viazi vilivyopikwa, kukatwa na kukaushwa yaani MATOBOLWA. Wanajua akina Mtemi Milambo/Mirambo walioanzisha huo mji.

Kwa Said Mwema, duuu naona kama ni RISASI basi shabaha imeenda pale kwenye 10.

Mseven na yeye yuko juu sana kwa Kipara. Sijui tumuweke wapi.

Ila Vipara ni WAKALI? Lione li-Mpaka, mhhh!!! Said Mwema yeye pia kamwaga damu yake Arusha kama Mkapa kule Pemba.

Ahhh, hakuna mtu mwenye kifungu hiki cha 2/3 ya WAPIGA KURA ili tumalize huu mjadala? Itabidi uchaguzi wa MEYA wa Arusha urudiwe kama itaonekana ni kweli. Hakuna uhakika kuwa CCM au Chadema watashinda maana uchaguzi ni SIRI. Sioni haja ya CCM kushindwa kurudia huu uchaguzi. Kama hawana mtu mwenye BUSARA ya kutoa maelezo, wamuombe Kaka Samuel Sitta alimalize hili jambo. Huyu Sitta pamoja na mabaya yake yote, ni wazi kuwa ana busara sana na KATIBA anaijua vizuri sana. Angelikuwa ni YEYE PM wa Tanzania, nafikiri sasa hivi wale Wahanga wangelikuwa bado hai na tungelikuwa tunaongelea jambo jingine kabisa...... Au kwa sababu SITTA ana NYWELE?

Nimekusamehe hahahahah!!!! Said Mwema nilikuwa namheshimu sana sasa nadhani unaweza kuwa sahihi wenye vipara hawana akili huenda.

NB: Ni Kipara na si Kipala refer kamusi ya TUKI

Search Results for 'kipara' | Matokeo ya Utafutaji kwa 'kipara' | The Kamusi Project
 
Quinine,

Achana na ubishi ambao hauongezi tija. Sikonge mbona anajulikana waziwazi hapa kwamba ni mtu wa Sikonge, Tabora? Kufahamiana kwake na Mwakalinga hakumfanyi awe mtu wa Mbeya.

Nafikiri muhimu tuendelee kujadili mambo ya katiba na kuacha haya ya kushambuliana.
Kama ni ubishi usio na tija wewe unakuwasha nini, ukitaka tuvue majoho ya ustaarabu endelea, wewe endelea kuwadanga wengine na mahesabu yako ya chekechea hata Hai walikuwa wanafanya hesabu hizo hizo za kujumlisha na kutoa mwisho CCM wakapata jawabu la sifuri kwa kuanzia nyambaf.
 
Hizza amewehuka. Hana tofauti na mtu aliyeingiwa na pepo, ilhali punde tu ametoka kwa mganga.

Jiulize kama CCM wana madiwani wengi kwanini uchaguzi ulifanyika kwa kuvizia?

Pili kwanini walijaribu kumtumia mamluki Chatanda? Hata kama amemsafisha bado ni mamluki tu maana TAMBWE kaongopa katika kanuni.

Si kweli kuwa mbunge wa viti maalum ni mjumbe wa halmashauri yoyote. Ingekuwa hivyo CDM isingekuwa na mashaka maana ingewazoa wabunge wake wa viti maalum kila kona ya nchi na kwenda kuwajaza Arusha.

Tatu, kama kweli wana madiwani wengi kwanini hawataki uchaguzi urudiwe ili washinde kihalali tena ushindi wa waziwazi.?

Nne,kwanini TAMBWE anaudanganya umma kuwa CCM ina madiwani 16, wakati anafahamu fika kuwa diwani wao wa kata ya Sombetini amejiuzulu na ameshakabidhi barua kwa mkurugenzi wa halmashauri na nakala anayo Makamba?

Tano, kwanini hataki kukubali kuwa TLP waliwapa kura na kitendo cha naibu meya ambaye ni tlp kujiuzulu kitapunguza kura zao?

Saba, kama kweli CCM ina madiwani wengi kwanini waliungana na tlp, maana kama wako wengi kura zao tu zingetosha.

Nane, kama mameya wote wanatekeleza ILANI na sera za CCM kwanini walisimamirha mgombea Arusha? Maana wasingesimamisha mgombea wakijua yoyote atakayechaguliwa atatekeleza sera na ilani yao.

CCM wamewehuka, wanaweweseka, wana kihoro, OLE WAO!!
 
Wewe ni hopeless kabisa eti tumuulize Mwanakijiji inavyoonekana hata ukipigwa na mkeo huwa unamshitaki kwa MKJJ hovyoooo, kwanza takwimu zako feki hujui wabunge nao ni madiwani kwenye mikoa yao.

wewe ndio HOPELESS, kumbe unajua kuwa wabunge wa viti maalumu ni madiwani kwenye mikoa yao, halafu bado unarapoqt ujinga? Kama unafahamu hilo MARY chatanda alipigaje kura ARUSHA wakati mkoa wake ni Tanga? Acha wehu.
 
Hizza amewehuka. Hana tofauti na mtu aliyeingiwa na pepo, ilhali punde tu ametoka kwa mganga.

Jiulize kama CCM wana madiwani wengi kwanini uchaguzi ulifanyika kwa kuvizia?

Pili kwanini walijaribu kumtumia mamluki Chatanda? Hata kama amemsafisha bado ni mamluki tu maana TAMBWE kaongopa katika kanuni.

Si kweli kuwa mbunge wa viti maalum ni mjumbe wa halmashauri yoyote. Ingekuwa hivyo CDM isingekuwa na mashaka maana ingewazoa wabunge wake wa viti maalum kila kona ya nchi na kwenda kuwajaza Arusha.

Tatu, kama kweli wana madiwani wengi kwanini hawataki uchaguzi urudiwe ili washinde kihalali tena ushindi wa waziwazi.?

Nne,kwanini TAMBWE anaudanganya umma kuwa CCM ina madiwani 16, wakati anafahamu fika kuwa diwani wao wa kata ya Sombetini amejiuzulu na ameshakabidhi barua kwa mkurugenzi wa halmashauri na nakala anayo Makamba?

Tano, kwanini hataki kukubali kuwa TLP waliwapa kura na kitendo cha naibu meya ambaye ni tlp kujiuzulu kitapunguza kura zao?

Saba, kama kweli CCM ina madiwani wengi kwanini waliungana na tlp, maana kama wako wengi kura zao tu zingetosha.

Nane, kama mameya wote wanatekeleza ILANI na sera za CCM kwanini walisimamirha mgombea Arusha? Maana wasingesimamisha mgombea wakijua yoyote atakayechaguliwa atatekeleza sera na ilani yao.

CCM wamewehuka, wanaweweseka, wana kihoro, OLE WAO!!

Majibu mbona ni rahisi tu. Sisiem wanatapatapa tu, na viongozi wao hawana busara na utu hata kidogo. Lkn ipo siku mambo yatakuwa kama Kenya, wote wanaokiuka haki za binadamu watasimama kizimbani.
 
Hesabu tena vizuri, inaelekea wana kata 19. Kumbuka kuna kata ziliongezwa mwaka 2010.

Madiwani wa Arusha ni 19 wa kuchaguliwa, mbunge mmoja wa kuchaguliwa. Madiwani wa kuteuliwa 7 (CCM 4 na CHADEMA 3) na wabunge viti maalum wanne (CHADEMA 2 na CCM 2). Jumla ndio inakuja 31.

Waliopiga kura walikuwa 16 wa CCM na mmoja wa TLP, jumla 17.

Hizi kura 16 ni pamoja na mchakachuzi Maria Chitanda. CHADEMA ina madiwani wangapi katika Jiji hilo?
 
Hizza amewehuka. Hana tofauti na mtu aliyeingiwa na pepo, ilhali punde tu ametoka kwa mganga.

Jiulize kama CCM wana madiwani wengi kwanini uchaguzi ulifanyika kwa kuvizia?

Pili kwanini walijaribu kumtumia mamluki Chatanda? Hata kama amemsafisha bado ni mamluki tu maana TAMBWE kaongopa katika kanuni.

Si kweli kuwa mbunge wa viti maalum ni mjumbe wa halmashauri yoyote. Ingekuwa hivyo CDM isingekuwa na mashaka maana ingewazoa wabunge wake wa viti maalum kila kona ya nchi na kwenda kuwajaza Arusha.

Tatu, kama kweli wana madiwani wengi kwanini hawataki uchaguzi urudiwe ili washinde kihalali tena ushindi wa waziwazi.?

Nne,kwanini TAMBWE anaudanganya umma kuwa CCM ina madiwani 16, wakati anafahamu fika kuwa diwani wao wa kata ya Sombetini amejiuzulu na ameshakabidhi barua kwa mkurugenzi wa halmashauri na nakala anayo Makamba?

Tano, kwanini hataki kukubali kuwa TLP waliwapa kura na kitendo cha naibu meya ambaye ni tlp kujiuzulu kitapunguza kura zao?

Saba, kama kweli CCM ina madiwani wengi kwanini waliungana na tlp, maana kama wako wengi kura zao tu zingetosha.

Nane, kama mameya wote wanatekeleza ILANI na sera za CCM kwanini walisimamirha mgombea Arusha? Maana wasingesimamisha mgombea wakijua yoyote atakayechaguliwa atatekeleza sera na ilani yao.

CCM wamewehuka, wanaweweseka, wana kihoro, OLE WAO!!

Hawa kina Hiza, Makamba na Chitanda wote ni wa Tangaline. Hivyo, lao ni moja hatuwashangai hata wakisema nini.
 
wewe ndio HOPELESS, kumbe unajua kuwa wabunge wa viti maalumu ni madiwani kwenye mikoa yao, halafu bado unarapoqt ujinga? Kama unafahamu hilo MARY chatanda alipigaje kura ARUSHA wakati mkoa wake ni Tanga? Acha wehu.
Usidandie treni kwa mbele nani kasema Chatanda ni mbunge wa Arusha soma post za watu kabla ya kutapika Zee jinga zaidi.
 
Back
Top Bottom