CCM toeni tamko kwamba dirisha kwa mwanachama yeyote kutia nia kuwania urais kupitia CCM limefunguliwa rasmi

Mganguzi

JF-Expert Member
Aug 3, 2022
1,032
2,769
Nimeona chama changu Cha mapinduzi na Seketarieti ya chama, kamati kuu na mawaziri wote wakiongozwa na waziri mkuu ,wanapita huku na huku kukusanya pesa za fomu ya urais 2025.

Ni kama Wana uoga Fulani kwa sababu muda wenyewe Bado sana!

Wameanza hata kumpigia kampeni mgombea mmoja kwamba ndio chaguo la wote! Na nimemsikia waziri mkuu akisema hata fomu ya urais itachapishwa Moja!

Naiomba cc ya chama ikiongozwa na mwenyekiti wetu, wafuate katiba ya chama chetu! Hata kama wao wanaona aliyepo anafaa lakini fungueni dirisha watu wachukue fomu wachuane ili huyo mtu wenu asije kuonekana kama hakuwa na sifa ila alibebwa!

Sio kweli kwamba nchi nzima wote hakuna mwenye nia ya kugombea ama kutia nia hata Mimi ninayo dhamira ya kutia nia.

Kama mmeruhusu watia nia waanze kuzunguka huku na huko kutafuta uungwaji mkono na hata kuchangiwa fomu basi na waomba mtoe tamko rasmi wote tuanze kutangaza nia nakuomba uungwaji mkono mapema kama mlivyoanza nyinyi.

Kinyume chake mkiendelea kuvunja katiba makusudi kwa ubabe ,sisi wengine haki yetu ya kikatiba ya kugombea nafasi ya urais tutaitafuta mahakamani.

Tutakwenda mahakamani kama wanachama hai wa CCM kudai haki yetu ya kikatiba na kupinga uvunjifu wowote wa katiba yetu.
 
Kuna mambo mawili hayaguswi

Mwenyekiti Wa CDM
Kutoa fomu zaidi ya moja CCM katika nafasi ya urais.
 
Nimekuuliza pamoja na hiyo Katiba,wewe ni mgeni na utaratibu wa Chama kuhusu Rais aliyepo kipindi hicho?
Rais aliyepo madarakani ndio anagombea kwa mara ya kwanza hii awamu alikuwa anaimalizia ya mwendazake ! Rasmi atatakiwa kugombea na kupitishwa na chama 2025 ,kwa mara ya mwisho uchaguzi wa chama ulifanyika 2015 miaka kumi iliyopita ,
 
IMG-20240312-WA0002.jpg
 
Ccm chapisheni fomu nyingi za urais samia wewe ulikuwa rais toka 2015 miaka 10 umenamaliza 2025 samia atasitaafu 2025 mwezi wa 11 tareh 5 tunaomba utulivu kwenye chama
 
nyie ccm mlitakiwa kuzidishiwa ugumu maana kila siku mnashangilia na kusifu.na safari hii sukari ifike kilo 10000 mseme mama anaupiga mwingi
 
Rais aliyepo madarakani ndio anagombea kwa mara ya kwanza hii awamu alikuwa anaimalizia ya mwendazake ! Rasmi atatakiwa kugombea na kupitishwa na chama 2025 ,kwa mara ya mwisho uchaguzi wa chama ulifanyika 2015 miaka kumi iliyopita ,
Tatizo lenu mumekariri mambo msiyoyajua.

Unaweza nijibu Kwa nini inaitwa awamu ya 6 na sio ya 5 kabla hatujaendelea?
 
Back
Top Bottom