Mkimbizi
JF-Expert Member
- Aug 23, 2008
- 222
- 34
NAIBU mkuu wa kitengo cha propaganda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Tambwe amesema Rais Jakaya Kikwete hajawahi hata mara moja kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali alielezea kutofurahishwa na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta).
Tambwe alisema hayo kupitia taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari akikanusha kauli ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk Wllibrod Slaa, aliyewataka Watanzania kumpuuza Tambwe kwa madai ya kwamba aliingilia shughuli za Serikali kwa kutoa taarifa iliyopingana naye kuhusu mgombea Urais wa CCM kukataa kura 350,000 za Wafanyakazi.
Tambwe hakufafanua zaidi juu ya msimamo wake kwamba Rais Kikwete hakuwahi kutamka kauli ya kuzikataa kura za wafanyakazi, lakini alisema taarifa ya Dk Slaa ilichapishwa bila ya yeye kuombwa maoni yake. Pia hakufafanua taarifa ya Dk Slaa ilivyosema kuhusu yeye.
Nimesikitishwa kuona habari hiyo ikipewa nafasi bila ya kunipa nafasi ya kutoa ufafanuzi wangu dhidi ya kauli hiyo kama vyombo mahiri vya habari vinavyopaswa kufanya.
Nilipokanusha uongo wa Dk Slaa nilifanya hivyo kwa niaba ya Chama, kwamba mgombea wetu wa urais hajawahi hata mara moja hajawahi kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali awali alisema hafurahishwi na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Tucta, alifafanuan Tambwe.
Alisema kwa kutoa ufafanuzi huo, anaamini alitekeleza kwa usahihi wajibu wake katika Chama, na si kutoa jibu lolote kwa niaba ya Ikulu au Serikali.
Source: Mwananchi news paper