Elections 2010 CCM sasa yadai JK hakukataa kura za wafanyakazi

Mkimbizi

JF-Expert Member
Aug 23, 2008
222
34
NAIBU mkuu wa kitengo cha propaganda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Tambwe amesema Rais Jakaya Kikwete hajawahi hata mara moja kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali alielezea kutofurahishwa na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta).

Tambwe alisema hayo kupitia taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari akikanusha kauli ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk Wllibrod Slaa, aliyewataka Watanzania kumpuuza Tambwe kwa madai ya kwamba aliingilia shughuli za Serikali kwa kutoa taarifa iliyopingana naye kuhusu mgombea Urais wa CCM kukataa kura 350,000 za Wafanyakazi.

Tambwe hakufafanua zaidi juu ya msimamo wake kwamba Rais Kikwete hakuwahi kutamka kauli ya kuzikataa kura za wafanyakazi, lakini alisema taarifa ya Dk Slaa ilichapishwa bila ya yeye kuombwa maoni yake. Pia hakufafanua taarifa ya Dk Slaa ilivyosema kuhusu yeye.

“Nimesikitishwa kuona habari hiyo ikipewa nafasi bila ya kunipa nafasi ya kutoa ufafanuzi wangu dhidi ya kauli hiyo kama vyombo mahiri vya habari vinavyopaswa kufanya.

“Nilipokanusha uongo wa Dk Slaa nilifanya hivyo kwa niaba ya Chama, kwamba mgombea wetu wa urais hajawahi hata mara moja hajawahi kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali awali alisema hafurahishwi na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Tucta,” alifafanuan Tambwe.

Alisema kwa kutoa ufafanuzi huo, anaamini alitekeleza kwa usahihi wajibu wake katika Chama, na si kutoa jibu lolote kwa niaba ya Ikulu au Serikali.

Source: Mwananchi news paper
 
matapishi yanaliwa tena! Sababu zitakuwepo tena nyingi sana..! Lakini mwisho wa yote hiyo October leteni matokeo yenu ya kifedhuli muone mziki
 
Sio hao tu, Kikwete alikataa hata kura ya Tambwe mwenyewe, lakini kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria alionao Tambwe.....leo hii anajipa nafasi ya Salvatory Rweyemamu kwa kuwa msemaji wa ikulu!!
 
Pia alisema hata mika kumi natono ijayo hakutakuwa na uwezakano wa kuongeza mishahara kama ilivyopendekezwa na TUCTA,kama yeye anataka kurejea kwenye uongozi bila kutumabia jinsi atakavyo kuza pato la taifa hafai hata kidogo kuendelea na uongozi ,TAMBWE awe na adabu pia hawezi kumzungumzia kiongozi mkuu wa nchi ,anaanzia wapi,hawa CCM watu waajabu sana hawana mipaka wanamgeuza Raisi wa Nchi kama Msanii mmoja hivi
 
mimi hotuba nzima niliisikia... Sasa ma mbayuwayu leo wamekuwa malaika?? Ikulu tamu ila mtatoka tu kwa wizi wenu..%%^&^%&*^%$%
 
Tambwe Hiza CV yako ya SIASA hii hapa...Kugumbea ubunge
1995-NCCR MAGEUZI(Looser to Kihiyo)
1996-NCCR MAGEUZI(Cowardice by allowing Mrema to run)
2000-TLP(Looser to Hadija Kusaga)
2005-CUF(Looser to Zubeir Mtemvu)
2010-CCM(Looser to Zubeir Mtemvu again...damn in primaries!!!With your very uncle Makamba looking...argh)
2015-JAIL TERM FOR ADVOCATING FOR FISADIS!!!!!!!
 
Huyu Tambwe Hiza akapimwe akili kwanza maana hata kiziwi alisikia kauli ile
 
Hivi Tambwe ni msemaji wa serikali au wa CCM?...kwani Rais alikuwa akiongea kama Serikali (japo kwa TZ hakuna tofauti ya chama na serikali), au ndio J.K anamuandaa Tambwe kuchukua nafasi ya Salva Rweyemamu?...coz isije ikawa J.K ndio anajitenga na ma-sponsor wake wa enzi zileee za kipindi kile
 
Sio hao tu, Kikwete alikataa hata kura ya Tambwe mwenyewe, lakini kutokana na uwezo mdogo wa kufikiria alionao Tambwe.....leo hii anajipa nafasi ya Salvatory Rweyemamu kwa kuwa msemaji wa ikulu!!

Hivi huyo Banyamulenge harudi kwao tu? Kazi za wabongo yeye amekomalia tu, tumemkweza kiasi cha kutosha tumemlisha kiasi cha kutosha sasa basi rudi kwenu salva na virago vyako. JK amekuwa kama kasungura wa EL Sizitaki mbichi hizi!
 
ngoja niitafute video ya siku ile wakati mzee anambayuwayuka niweke hapa msikie alivyonena.. Huyu ?Tambwe ni chizi
 
Maskini Tambwe Hizza hata alipokuwa CUf kazi yek ilikuwa kutumwa kutukana CCM na viongozi wake ndio maana hata lipohamia CCM wanachama wa CCM wakakataa kumpigia kura katika uchaguzi wa kura za maoni. Sasa kutumwa na CCM kumsafisha JK katika hili. Kila raia wa nchi alisikia kwa masikio yake Rais wa nchi alisema nini kwa kuwa ni wajibu wetu kama raia wema kufuatilia hotuba za viongozi wetu wa kitaifa. Hatuhitaji kufundishwa na Tambwe Hizza nini alichotamka Rais!!!!
 
NAIBU mkuu wa kitengo cha propaganda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Tambwe amesema Rais Jakaya Kikwete hajawahi hata mara moja kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali alielezea kutofurahishwa na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta).

Tambwe alisema hayo kupitia taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari akikanusha kauli ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk Wllibrod Slaa, aliyewataka Watanzania kumpuuza Tambwe kwa madai ya kwamba aliingilia shughuli za Serikali kwa kutoa taarifa iliyopingana naye kuhusu mgombea Urais wa CCM kukataa kura 350,000 za Wafanyakazi.

Tambwe hakufafanua zaidi juu ya msimamo wake kwamba Rais Kikwete hakuwahi kutamka kauli ya kuzikataa kura za wafanyakazi, lakini alisema taarifa ya Dk Slaa ilichapishwa bila ya yeye kuombwa maoni yake. Pia hakufafanua taarifa ya Dk Slaa ilivyosema kuhusu yeye.

"Nimesikitishwa kuona habari hiyo ikipewa nafasi bila ya kunipa nafasi ya kutoa ufafanuzi wangu dhidi ya kauli hiyo kama vyombo mahiri vya habari vinavyopaswa kufanya.

"Nilipokanusha uongo wa Dk Slaa nilifanya hivyo kwa niaba ya Chama, kwamba mgombea wetu wa urais hajawahi hata mara moja hajawahi kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali awali alisema hafurahishwi na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Tucta," alifafanuan Tambwe.

Alisema kwa kutoa ufafanuzi huo, anaamini alitekeleza kwa usahihi wajibu wake katika Chama, na si kutoa jibu lolote kwa niaba ya Ikulu au Serikali.

Source: Mwananchi news paper

Huyu Tambwe apelekwe Mirembe kwa vichaa. Yaani anafikiri watanzania wamelala. Nilisikiliza ile hotuba potofu na kujigamba na nilishangaa mno kwa Rais wa nchi ambaye hafahamu nguvu ya working class in politics. Sasa mimi ni mfanyakazi na nitahakiksha wale ndugu zangu wanaonitegemea wanampigia kura mgombea ambaye angalao hata kwa maneno ananiona ninafaa. Naombeni Chadema mnitafute nitoe mawazi yangu kwenye kampeni strategy yenu. Hakikisheni mna ule mkanda wa ile hotuba siku ile, for evidence. Nasikia hasira mimi.

Katika CCM wale wote wanaohama vyama vyao na kukimbilia huko
hutupwa kwenye IDARA YA PROPAGANDA, kwa mfano yeye Hiza na yule
Msabaha aliyetokea CUF.
 
Back
Top Bottom