Elections 2010 CCM sasa yadai JK hakukataa kura za wafanyakazi

matapishi yanaliwa tena! Sababu zitakuwepo tena nyingi sana..! Lakini mwisho wa yote hiyo October leteni matokeo yenu ya kifedhuli muone mziki

Mkuu shughuli itakuwa pevu inaonekana wameshaandaa Janjaweed 500 wanaowaita polisi. Kulikuwa hakuna haja ya maandalizi haya kama uchaguzi utakuwa huru na haki. Ninaamini kabisa kuwa haki si tu inapotendeka bali inapoonekana kutendeka kwa pande zote, huwa ni polisi namba 1 wa kulinda amani.

 
Last edited by a moderator:
...Alisema kwa kutoa ufafanuzi huo, anaamini alitekeleza kwa usahihi wajibu wake katika Chama, na si kutoa jibu lolote kwa niaba ya Ikulu au Serikali...





huyu bwana ni bingwa wa kuwa kigeugeu. alipokuwa CUF aliwatukana sana CCM. sasa amewageuka CUF anabariki kejeli dhidi ya mbayuwayu.


wahusika ikulu wamekaa kimya wakijipanga namna bora ya kuwaomba msamaha watanzania na hasa wafanyakazi, huyu jamaa wa hamaki, bila ya consultation, amekimbilia kupaka kinyesi mkakati wa ikulu wa kumwombea radhi jk kwa wafanyakazi.


amesahau yaliyompata mapuri na wanahabari? hamaki ya kingunge na maaskofu? hata kama anatetea maslahi ya chama chake, kukurupuka bila halmashauri si ishu?
 
NAIBU mkuu wa kitengo cha propaganda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Tambwe amesema Rais Jakaya Kikwete hajawahi hata mara moja kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali alielezea kutofurahishwa na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta).

Tambwe alisema hayo kupitia taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari akikanusha kauli ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk Wllibrod Slaa, aliyewataka Watanzania kumpuuza Tambwe kwa madai ya kwamba aliingilia shughuli za Serikali kwa kutoa taarifa iliyopingana naye kuhusu mgombea Urais wa CCM kukataa kura 350,000 za Wafanyakazi.

Tambwe hakufafanua zaidi juu ya msimamo wake kwamba Rais Kikwete hakuwahi kutamka kauli ya kuzikataa kura za wafanyakazi, lakini alisema taarifa ya Dk Slaa ilichapishwa bila ya yeye kuombwa maoni yake. Pia hakufafanua taarifa ya Dk Slaa ilivyosema kuhusu yeye.

“Nimesikitishwa kuona habari hiyo ikipewa nafasi bila ya kunipa nafasi ya kutoa ufafanuzi wangu dhidi ya kauli hiyo kama vyombo mahiri vya habari vinavyopaswa kufanya.

“Nilipokanusha uongo wa Dk Slaa nilifanya hivyo kwa niaba ya Chama, kwamba mgombea wetu wa urais hajawahi hata mara moja hajawahi kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali awali alisema hafurahishwi na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Tucta,” alifafanuan Tambwe.

Alisema kwa kutoa ufafanuzi huo, anaamini alitekeleza kwa usahihi wajibu wake katika Chama, na si kutoa jibu lolote kwa niaba ya Ikulu au Serikali.

Source: Mwananchi news paper

Mwalimu: Tunga sentensi kwa kutumia neno iba
Mwanafunzi: Mwalimu ameiba maembe manne.
Mwalimu: We mwanafunzi huna adabu, sentesi gani hiyo? Rudia tena mara moja! :confused2:
Mwanafuzi: Mwalimu hajaiba maembe manne!
 
NAIBU mkuu wa kitengo cha propaganda wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Richard Tambwe amesema Rais Jakaya Kikwete hajawahi hata mara moja kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali alielezea kutofurahishwa na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Shirikisho la vyama vya wafanyakazi nchini (Tucta).

Tambwe alisema hayo kupitia taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari akikanusha kauli ya mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Mendeleo (Chadema), Dk Wllibrod Slaa, aliyewataka Watanzania kumpuuza Tambwe kwa madai ya kwamba aliingilia shughuli za Serikali kwa kutoa taarifa iliyopingana naye kuhusu mgombea Urais wa CCM kukataa kura 350,000 za Wafanyakazi.

Tambwe hakufafanua zaidi juu ya msimamo wake kwamba Rais Kikwete hakuwahi kutamka kauli ya kuzikataa kura za wafanyakazi, lakini alisema taarifa ya Dk Slaa ilichapishwa bila ya yeye kuombwa maoni yake. Pia hakufafanua taarifa ya Dk Slaa ilivyosema kuhusu yeye.

“Nimesikitishwa kuona habari hiyo ikipewa nafasi bila ya kunipa nafasi ya kutoa ufafanuzi wangu dhidi ya kauli hiyo kama vyombo mahiri vya habari vinavyopaswa kufanya.

“Nilipokanusha uongo wa Dk Slaa nilifanya hivyo kwa niaba ya Chama, kwamba mgombea wetu wa urais hajawahi hata mara moja hajawahi kukataa kura za kundi lolote la jamii, wakiwemo wafanyakazi, bali awali alisema hafurahishwi na vitisho vya baadhi ya viongozi wa Tucta,” alifafanuan Tambwe.

Alisema kwa kutoa ufafanuzi huo, anaamini alitekeleza kwa usahihi wajibu wake katika Chama, na si kutoa jibu lolote kwa niaba ya Ikulu au Serikali.

Source: Mwananchi news paper

Richard Tambwe asiwafanye Watanzania kuwa wajinga! Rais Jakaya Kikwete tulimsikia akisema kwa kauli yake. Mbona yeye hajakanusha kuwa alichosema 'Watanzania wajinga' hawakumwelewa? Mbona wakati anakataa kura za wafanyakazi hakumtuma Tambwe kutoa hotuba? Hivi ndivyo walishazoea kusema hiki wakikosolewa wanabadili maneno na kusema hawakueleweka.
 
Richard Tambwe asiwafanye Watanzania kuwa wajinga! Rais Jakaya Kikwete tulimsikia akisema kwa kauli yake. Mbona yeye hajakanusha kuwa alichosema 'Watanzania wajinga' hawakumwelewa? Mbona wakati anakataa kura za wafanyakazi hakumtuma Tambwe kutoa hotuba? Hivi ndivyo walishazoea kusema hiki wakikosolewa wanabadili maneno na kusema hawakueleweka.

Ndio maana kipindi kile cha May alipotoa hotuba nilisema wafanyakazi wa Tanzania wako 350,000 hawa ndio wanaoccupy 30% ya walipa kodi wasiozidi milioni mbili Tanzania (Dk Slaa). Sasa kwakawaida wafanyakazi wa Tanzania wana extended family wanazozisaidia ambapo tukisema 350,000 akiwa kila moja ana mke (mme) na watoto watatu maximum unakuwa na figure kama ya watu 5, pia weka na wazazi wawili inakuwa watu 7, weka na wadogo wawili wanaomtegemea unakuwa na watu 9. Weka na rafiki mmoja kipenzi unakuta watu 10, unakuta kila mfanyakazi mmoja anawatu 9 wanaomtegemea. Zidisha kwa 350,000 unapata kura 3,150,000 ambazo Kikwete hazitaki. Weka na kura 500,000 za watu wanaoona wafanyakazi wameonewa unakuta kura 3,650,000 Kikwete hazitaki.

Hivyo basi wafanyakazi wana nguvu kuliko Kikwete anavyodhani ni bora tu aombe radhi hadharani kuliko kuwatunishia misuli wafanyakazi kwani ndio wanaoamua hatima ya nchi venginevyo nchi hii hataitawala labda kwa maguvu
 
CCM wasithubutu kumtetea mgombea wao. Tulimsikia na tumekubali ombi lake "HATUTAMPA KURA ZETU". Wakati akisema vile alikuwa ame-underrate intelligence ya Watz. Sasa tutamuonyesha kuwa sisi sio 'bongolala'. Bila shaka alidhani hatapata upinzani wowote kwenye kinyang'anyiro cha urais.
 
CCM wasithubutu kumtetea mgombea wao. Tulimsikia na tumekubali ombi lake "HATUTAMPA KURA ZETU". Wakati akisema vile alikuwa ame-underrate intelligence ya Watz. Sasa tutamuonyesha kuwa sisi sio 'bongolala'. Bila shaka alidhani hatapata upinzani wowote kwenye kinyang'anyiro cha urais.

Ishu ni hivi JK hataki kura za wafanyakazi ndio maana amekataa kuongeza mishahara yao hivyo tuseme wote wasimpigie kura hana kura 3,650,000, amewahadaa waislamu na mahakama ya kadhi ijapokuwa swala bado halina ufumbuzi. Hivyo kuna probability kama kura 2,000,000 kati ya 5,000,000 kikwete anazikosa. Tukija kuna watu wasioridhika na utendaji wa ufisadi ambao hawa sina haja ya kuwataja maana wako wengi wawazi wengine ni wanafiki but ana kura kama 5,650,000 Kikwete hatazipata. tukichukulia wapiga kura ni kama ni 40% of the total population (ni assumption) inamaana katika 40,000,000 ni watu 16,000,000 watapiga kura. Toa milioni 5.6 unakuta wanabakia wapiga kura milioni 11 sijui CCM watatokea wapi sioni mahala kwani katika milioni 11 wapo CUF, CCM, Chadema, NCCR, na wengineo watakaopiga kura kwa itikadi ya chama tu. ndio unapoona hizi kura wafanyakazi ni muhimu kuliko CCM wanavyofikiria.
 
Miongoni mwa mambo yanayoipa kiburi CCM ni imani ilishamiri miongoni mwa viongozi wa chama hicho kuwa Watanzania hawana kumbukumbu,hawajui kutofautisha zuri na baya,wavumulivu kupita kiasi,na ni viumbe wa kupelekeshwa tu.Yayumkinika kuhitimisha kwamba imani hiyo ya viongozi hao inasababishwa na mambo makuu mawili:Kwanza,dharau,kiburi,ubinafsi,na kubwa zaidi ya yote,ufisadi.Sababu ya pili,ni namna Watanzania wengi wanavyoendelea kukiamini chama ambacho kilishawatelekeza miaka kadhaa iliyopita.

Katika sababu hii ya pili,mfano mzuri ni ule wa mume anayemnyanyasa mke kupindukia lakini mapenzi ya mke huyo yanazidi kudumu akitarajia mumewe atapatwa na akili au huruma.Kwa bahati mbaya,utiifu huo wa mke kwa mume mnyanyasaji huishia kutafsiriwa na mume huyo kuwa mkewe “amenasa kwenye zege”,hana ujanja wa kuomba talaka au kukabiliana na manyanyaso ya mume huyo.

Ni katika mantiki hiyo ndipo leo tunasikia kioja cha mwaka ambapo “msema chochote” wa CCM,Tambwe Hizza (ambaye bado anaugulia maumivu ya kubwagwa kwenye kura za maoni huko Temeke) akikurupuka na kudai Rais Jakaya Kikwete hajawahi kutamka kuwa “hataki kura za wafanyakazi”.

Huyu Tambwe ni mhuni,hana nidhamu kwa Watanzania (kama alivyokuwa mhuni kwa kuapa kumtukana mama yake mzazi),na anafikiri bado tunaishi katika zama zile ambapo kama mwananchi hakuhudhuria mkutano uliohutubiwa na kiongozi husika,basi tegemeo pekee ni magazeti ya CCM ya Uhuru na Mzalendo au “midomo ya serikali” yaani Radio Tanzania na Daily News.Na vyombo vyote hivyo vya habari vilikuwa na unyenyekevu wa kuchefua kwa namna vilivyokuwa vikifanya kila liwezekanalo kupendezesha hotuba au kauli za watawala wa enzi hizo.

Japo vyombo vya habari vya serikali (Habari Leo,Daily News na TBC) bado vimeendelea kukumbatia siasa za chama kimoja kwa kuipendelea CCM waziwazi na kupuuza kuwa vinaendeshwa kwa fedha za walipakodi (ambao takriban milioni 35 kati yao sio wanachama wa CCM) lakini angalau siku hizi tuna vyombo binafsi vya habari pamoja na social media (blogs,youtube,facebook,twitter,nk) na hiyo inasaidia kwa kiasi kikubwa “kutofautisha mchele na pumba”.

Lakini kutokana na dharau zao na kutojali,Tambwe na CCM wanajifanya hawajui kuwa hotuba ya Kikwete kuhusu tishio la mgomo wa wafanyakazi ipo mtandaoni.Mtandaoni kuna video zenye hotuba hiyo,na uzuri wa mtandao ni kwamba unahifadhi kumbukumbu vyema sana.Kwahiyo hata kama CCM wangetaka “kufuta maneno hayo ya JK” bado wangekabiliwa na kigingi katika kufuta kumbukumbu zilizozagaa mtandaoni.Pengine wanafahamu sana kuhusu hilo lakini wanajipa matumaini kwa kuamini kuwa “Watanzania ni wanyonge sana na hawaweza kusaka kumbukumbu za kauli hiyo ya Kikwete”.Au pengine ni jeuri tu ya madaraka na imani kwamba kiongozi ana ruhusa ya kuahidi chochote,kusema lolote na kufanya chochote na asihukumiwe na umma.

Leo Tambwe anasema Kikwete hajawahi kutamka kuwa hahitaji kura za wafanyakazi.Je atakanusha pia kuwa Kikwete hajawahi kusema mimba za wanafunzi wa kike ni kiherehere chao?Au hakuwahi kutamka kuwa hajui kwanini Tanzania ni masikini?Au hajawahi kutamka kuwa anawafahamu wala rushwa lakini anawapa muda wa kujirekebisha?Au hakuwahi kuahidi kuwa maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana?Au Tambwe pia atakabusha kuwa Kikwete hakutumia mfano wa MBAYUWAYU?

Kwani Tambwe au CCM,au hata JK mwenyewe,hawakukanusha habari zilizoandikwa na gazeti la Mwananchi chapisho la mtandaoni Mei 3, 2010 na kupewa kichwa cha habari "JK: Nipo Tayari Kukosa Kura Zenu" na kumnukuu "(Kikwete) alifafanua kuwa kima cha chini cha mshahara cha Sh315,000 kwa mwezi kinachopigiwa debe na Tucta, serikali haiwezi kukitekeleza na kama hilo ni shinikizo kwake ili wafanyakazi wampatie kura kwenye Uchaguzi Mkuu ujao, hahitaji kura zao". (BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI HIYO)

Ni dhahiri hili zoezi la kukanusha kauli halitafanikiwa.Liliwezekana katika zama ambapo Watanzania uhuru na access ya habari ilikuwa kwa ridhaa ya watawala lakini sio sasa ambapo blogs,webforums,facebook,twitter,youtube,nk zinapatikana kila kona ya dunia alimradi kuna internet connection.

Dharau na jeuri ya CCM iliwafanya wajisahau kwenye usingizi wa pono huku JK akitoa baadhi ya kauli zisizotarajiwa kutoka kwa mwanasiasa anayetarajia kuomba tena ridhaa ya wananchi kuwaongoza tena.Wakati huo walikuwa na uhakika wa asilimia zaidi ya 100 kuwa JK na CCM yake kurejea madarakani ni suala la muda tu na sio “if watarejea”.Lakini ghafla,baada ya Chadema kumtangaza Dkt Wilbroad Slaa kuwa mgombea wake wa nafasi ya urais,CCM wametahayari.Hawakuona umuhimu wa kukanusha kauli hiyo ya JK mpaka baada ya kumsikia Dkt Slaa akiwaeleza wafanyakazi kuwa “anahitaji kura ambazo Kikwete hazihitaji”.Ghafla,CCM wanakugundua kuwa kauli hiyo haikuwa mwafaka,lakini kwa dharau zao badala ya kuomba radhi au kutafuta suluhu wanakimbilia kukanusha.

Nimeandika makala kadhaa katika blogu yangu kuhusu umuhimu wa CCM kuwaomba radhi Watanzania kwa madudu mbalimbali waliyotufanyia badala ya wao kuendelea kujigamba kuhusu “mafanikio yaliyopatikana katika utawala wao”.Yani wanataka kutuambia kuwa hata kushamiri kwa ufisadi ni mafanikio?Kwanini wasingetumia busara ya kutueleza “mafanikio” yao kisha wakaonyesha uungwana kwa kueleza maeneo ambayo kimsingi “wametuangusha”?Hawawezi kufanya hivyo kwa vile wanatudharau,wanatuona wajinga tusiojua kutenganisha mema na mabaya,wasahaulifu tusiokumbuka hata mahitaji yetu muhimu.

Tayari chama hicho tawala kimeshaonyesha “mchecheto” kwa kukacha kushiriki mdahalo wa wagombea urais kabla ya “kulialia” kuwa Chadema inacheza rafu “kwa kuanza kampeni kabla ya muda wake”.Ukichanganya na songombingo linaloendelea ndani ya chama hicho katika mchakato wa kupata wagombea wa nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao ni dhahiri kuwa kwa mara ya kwanza CCM inaanza kuona dalili za kung’olewa madarakani.Na huenda moto mkubwa zaidi ukawaka ndani ya chama hicho baada ya mchujo wa wagombea baadaye mwezi huu.

Tahayari iliyowakumba CCM inaweza kuwa silaha nzuri kwa Dokta Slaa na Chadema kwa ujumla.Kwa kauli kama hizi za akina Tambwe,ni rahisi kwa Chadema kuwaonyesha Watanzania namna gani chama hicho kinavyowadharau.Ndio!Kwani kama si dharau ni nini basi pale mtu anapokutukana halafu baada ya kitambo akaibuka na kukanusha kuwa hajakutukana japo ushahidi upo bayana?CCM inajikaanga kwa mafuta yake yenyewe.Dharau na jeuri yao inaweza kuwa mtaji mzuri wa anguko lake.

Kwa wale wote wenye uchungu wa dhati kwa nchi yetu na waliochoka kufisadiwa na CCM,kitendo cha chama hicho kukanusha kuwa JK hajawahi kukataa kura za wafanyakazi kinapaswa kutafsiriwa kama namna Watanzania “watakavyoingizwa mkenge tena kama mwaka 2005” ambapo chama hicho kiliahidi mambo chungu mbovu lakini badala yake matokeo ni kushamiri kwa ufisadi.Kama mwenyekiti wa chama hicho anaweza kutoa kauli hadharani kisha chama chake kikaibuka kudai kuwa hajatoa kauli hiyo,je kwanini tusiamini kuwa mgombea urais wa chama hicho (JK) ataishia kupuuza ahadi anazotoa sasa na wakati wa kampeni,na CCM ikiulizwa ikaishia kukanusha kuwa hajwahi kuahidi hivyo?

Watanzania sasa tumepatiwa nafasi adimu ya kuondokana na CCM.Katika chaguzi zilizotangulia tulikuwa hatuna uhakika na wagombea waliosimamishwa kuchuana na mgombea wa CCM lakini safari hii tumebahatika kupata mtu ambaye rekodi yake inajidhihirisha bayana.Na kwa namna ambayo haijawahi kutokea katika historia ya chaguzi nchini mwetu ambapo CCM inaonekana ikianza kutahayari waziwazi baada ya mwamko ulioletwa na Chadema na Dkt Slaa,huo ni uthibitisho tosha kuwa mafisadi wamegundua kuwa siku zao zinahesabika.

Tusirejee makosa ya huko nyuma ya kujaa kwenye mikutano lakini kura zinakwenda CCM.Safari hii,acha watoe rushwa zao (na mzipokee tu kwa vile ni fedha walizowafisadi) lakini kura ziende kwa Dkt Slaa.Dawa ya kung’oa ufisadi ni kung’oa mmea unaolea ufisadi,na mmea huo ni CCM.

Watu Wazima Ovyoo: CCM Wakanusha JK Hakukataa Kura za Wafanyakazi | KULIKONI UGHAIBUNI
 
Mimi nitawashangaa wafanyakazi iwapo watajifanya wamesahau uhuni wa chama cha madhalimu hawa(CCM) na kumchaguwa Kikwete...I don't care nani watampa kura so long as watainyima CCM, kazi kwenu wefanyakazi.
 
Nimefurahia sana CCM kuamua kufanya kura za maoni ndani ya chama kwa staili mpya. Kwani kura hizo za maoni kitaalam zitazaa makundi ndani ya CCM kati ya wale waliopeta na wale walioshindwa ndani ya chama. Mwisho wa siku (hasa siku ya uchaguzi) tutapata "drop-outs" kutoka CCM na kupigia kura upinzani.

.... in any misfortune there are blessings.
 
Hapa ndio kazikubali?

Tuesday, May 4, 2010

Rais Kikwete: TUCTA waongo

“TUCTA ni waongo! Tucta ni wanafiki! Tucta wana hiana!... wafanyakazi watakaogoma tarehe 5, watakuwa wamekiuka sheria na watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria na kanuni za Serikali. Na wale wafanyakazi wataokwenda kazini lakini wasifanye kazi, pia watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.

“Kiongozi bora ni yule anayewaeleza wananchi wake ukweli hata kama ukweli huo utakuwa unauma.”


Hiyo ni kauli nzito ya Rais Jakaya Kikwete, alipozungumza na Taifa kupitia wazee wa mkoa wa Dar es Salaam jana, kuhusu mgomo ulioitishwa na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kuanzia kesho, kwa madai kuwa Serikali imepuuza mapendekezo ya kuongezwa kwa kima cha chini ya mshahara kufikia Sh 315,000 kwa mwezi.


Rais alisema Serikali haiwezi kulipa kima cha chini cha Sh. 315,000 kutokana na mapato inayopata.


“Nimewasikia Tucta, wanasema huu ni mwaka wa uchaguzi, hawatanipigia kura kama sitalipa kima cha chini wanachokitaka,
nipo tayari kuzikosa kura za wafanyakazi kuliko kuwadhulumu Watanzania walio wengi, wakakosa dawa, maji, barabara, elimu, pembejeo za kilimo na huduma nyingine,” alisisitiza Rais akionesha dhdhiri kukerwa na msimamo wa Shirikisho hilo.

Alisema pamoja na mazungumzo yanayoendelea sasa kwa lengo la kuboresha maslahi ya wafanyakazi ikiwamo mishahara, viongozi wa Tucta kwa makusudi, wameamua kuitisha mgomo wa wafanyakazi huku wakitoa madai ya uongo, kwamba Serikali haisikii na viongozi wa Serikali hawawajali wafanyakazi.


Alieleza kushangazwa na kauli za viongozi wa Tucta wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), kauli ambazo kimsingi alisema zinajenga taswira kwamba hakuna mazungumzo yoyote yanayoendelea baina ya Serikali, waajiri na wafanyakazi, kupitia vyama vyao ya kushughulikia maslahi yao na kujenga hisia mbaya kwa wafanyakazi kwamba Serikali haiwathamini.


“Si kweli, Serikalii inawajali na kuwathamini sana wafanyakazi. Zipo hatua ambazo imechukua na inaendelea kuchukua katika kuboresha maslahi ya wafanyakazi.


“Tuliingia madarakani kima cha chini ya mshahara kikiwa Sh 65,000 lakini sasa ni Sh 104,000. Kwa makusudi viongozi wa Tucta wanawadanganya wafanyakazi kwamba Kikwete ameongeza Sh 4,000 tu tangu amekuwa Rais wa nchi, jambo ambalo ni uongo mkubwa,” alisema Rais Kikwete.


Alitoa mfano wa mazungumzo yaliyofanyika mwezi uliopita, ambapo pande hizo tatu; Serikali, waajiri na wafanyakazi, walikutana mara tatu Aprili 6, Aprili 26 na Aprili 27 kujadiliana kuhusu kima cha chini ya mshahara na wakashindwa kuafikiana kutokana na viongozi wa Tucta kuleta mapendekezo ya viwango vitatu vya kima cha chini cha mshahara baada ya Serikali kukataa kima cha chini cha awali cha Sh 315,000.


Alisema mazungumzo hayo yakapangwa kuendelea Mei 8 mwaka huu. “Wakati mazungumzo yamepangwa kufanyika tena Mei 8, ili wao waje na mapendekezo yao mengine ya kima cha chini cha mshahara, na sisi Serikali tulete mapendekezo yetu ili tujadiliane, viongozi hawa wa Tucta wanashindwa kusema ukweli na wanakana hata kile walichokisema na kupendekeza wao wenyewe ndani ya vikao halali,” alisema.


Rais alisistiza kuwa Serikali kwa upande wake, imekuwa ikiheshimu mapendekezo ya nyongeza ya kima cha chini cha mshahara katika sekta binafsi kupitia bodi nane za kisekta, na ndiyo maana kutokana na mazungumzo hayo, Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, alitangaza kima kipya kwa sekta binafsi Aprili 30, mwaka huu, ambacho kilianza kutumika Mei Mosi.


Alisema pia Serikali kupitia majadiliano hayo, imekubali kuongeza kima cha chini cha mshahara kwa watumishi wa umma, ongezeko ambalo litatangazwa katika bajeti ijayo ya mwaka wa fedha wa 2010/11, tofauti na kauli zinazotolewa na viongozi wa Tucta kwa wafanyakazi.


Aliongeza kuwa Serikali ina wafanyakazi 350,000 na endapo italipa kima cha chini cha mshahara cha Sh 315,000 italazimika kutumia Sh bilioni 6,852.93, fedha ambazo ni nyingi kuliko mapato ya Serikali, kwani katika bajeti ijayo, Serikali imepanga kukusanya Sh bilioni 5,757.3, na ili iweze kulipa kiasi hicho, italazimika kukopa jambo ambalo ni kichekesho.


“Kama tutalipa mishahara hii kama wafanyakazi wanavyotaka maana yake ni kwamba tutawaridhisha wafanyakazi hawa 350,000, lakini tutawadhulumu Watanzania milioni 39,650,000.


Hatutakuwa na pesa ya kuwanunulia dawa, kuwajengea barabara, kununua madaftari, kununua pembejeo za kilimo wala kuwapa maji safi na salama jambo ambalo siwezi kukubali litokee,” alisema.


Rais Kikwete katika hotuba hiyo iliyorushwa moja kwa moja na baadhi ya vituo vya redio na televisheni, alizungumzia pia mkutano mkubwa wa uchumi kwa Bara la Afrika, utakaofanyika kwa siku tatu Dar es Salaam kuanzia kesho, kwamba utasaidia kukuza na kutangaza jina la Tanzania.


Alisema viongozi na wakuu wa nchi 11 wamethibitisha kushiriki mkutano huo utakaoshirikisha zaidi ya watu 959 kutoka nchi 85 Duniani.


Alisema Tanzania kwa upande wake itanufaika kutangaza fursa ilizonazo katika vivutio vya utalii na uwekezaji
 
Asante mkuu kwa sred ndeeeefu ila pale ULIPO SEMA BONYEZA HAPA MHN SIJAONA PAKUBONYEZA NAKUOMBA UTIE KIBONYEZO!!!
 
tulikusikia saaaana kiwete ukisema hutaki kura zetu sie wafanyakazi..! usikataeee....! unatulima kodi kubwa mnooo kwa mishahara yetu..!
 
Jamani Tambwe Hiza anasumbuliwa na laana ya kulala na mama yake mzazi (maana alisema akirudi CCM basi atalala na mama yake mzazi). Kwa kuwa amerudi CCM basi amelala na mama yake mzazi. Na kwa kuwa amelala na mama yake mzazi basi laana inamtafuna. The best thing we can do for him is to ignore him completely.
 
Back
Top Bottom