Elections 2010 CCM sasa yadai JK hakukataa kura za wafanyakazi

Wapenda mabadiliko, hebu pia tuangalie Ilani ya CCM 2010 - 2015 kuhusu wafanyakazi. Inasema hivi: Karibuni kusoma kipengele hiki na zaidi kwa maoni yenu.



Wafanyakazi

79. Katika kipindi cha 2010-2015, CCM itaendelea kuwa karibu na wafanyakazi na

kuhakikisha kuwa Serikali zinayatambua na kuyashughulikia kwa ukamilifu na

kwa wakati muafaka matatizo yao. Miongoni mwa hatua zitakazochukuliwa na

Serikali zitakuwa pamoja na hizi zifuatazo:-

(a) Kuendelea kuboresha mishahara ya wafanyakazi kwa kadri hali ya uchumi

wa nchi utakavyoruhusu.

(b) Kuimarisha na kufanya kaguzi za kazi, ikiwa ni pamoja na masuala ya afya

na usalama mahali pa kazi.

50

(c) Kusuluhisha na kuamua kwa wakati migogoro yote ya kikazi na kuimarisha

ushiriki na ushirikishwaji wa wafanyakazi mahali pa kazi.

(d) Kuhakikisha kwamba mishahara ya wataalamu wa ndani na nje wenye sifa

na kazi zinazofanana wanalipwa mishahara inayolingana.

(e) Serikali kuanzisha mchakato utakaohakikisha kwamba pamoja na

kuthamini mchango wa kila mfanyakazi na kufanya kazi katika taaluma

zao na kuziheshimu ni muhimu ione tofauti kubwa iliyopo kati ya malipo

ya wafanyakazi wa ngazi za juu na wale wa ngazi za chini.



Kwa maoni yangu ukisoma maandiko hayo hapo juu utaona kuwa ni blaa bla tupu. H
 
Ha ha ha! Ni Tambwe Hiza huyu huyu aliyemtukana mama yake?

Huyo huyo! Na huenda mpaka sasa analala na mama yake, kwa sababu akiwa CUF alisema kwamba akirudi sisiemu basi atalala na mama yake mzazi!
Laana iliyoje!
Jamani Tambwe Hiza anasumbuliwa na laana ya kulala na mama yake mzazi (maana alisema akirudi CCM basi atalala na mama yake mzazi). Kwa kuwa amerudi CCM basi amelala na mama yake mzazi. Na kwa kuwa amelala na mama yake mzazi basi laana inamtafuna. The best thing we can do for him is to ignore him completely.

Yes, ni kumsamehe na kumsahau tu.

Ila tukumbuke kwamba wafanyakazi popote pale duniani wawna nguvu ya kudondosha serikali, tusiwadharau kwa lolote lile. Kama tunakumbuka vema historia ya O-level kwa Tanzania, uhuru wa nchi nyingi hasa za Kiafrika ulitokana na juhudi kubwa za wafanyakazi. Morgan Tsvangirai wa Zimbabwe alikuwa kama Mgaya wa TUCTA, kabla hajajiingiza katika siasa.
Lisemwalo lipo.
 
Inanikumbusha yale mambo kiongozi awamu iliyopita....Nakanusha kwamba sijakanusha kwamba nilikanusha kukanusha kwangu....
 
CCM wasithubutu kumtetea mgombea wao. Tulimsikia na tumekubali ombi lake "HATUTAMPA KURA ZETU". Wakati akisema vile alikuwa ame-underrate intelligence ya Watz. Sasa tutamuonyesha kuwa sisi sio 'bongolala'. Bila shaka alidhani hatapata upinzani wowote kwenye kinyang'anyiro cha urais.
MzeePunch hawa CCM ni hatari sana, wana dharau na kiburi kisicho mfano. Kauli ile kila mtu alisikia leo hii wanakanusha. Kama ulisikiliza sana kauli za JK alionesha kuwa harakati zile za Kaimu katibu Mkuu- TUCTA (Mgaya) zilikuwa zake binafsi, ndio maana alimshambulia Mgaya kama Mgaya. Lengo lake alidhamiria kumtenga Mgaya na wafanyakazi. Anasahau kuwa Mgaya asingalisema hayo kama sio kwa kuwa kiongozi wa TUCTA. Nina imani wao ndo walioisajili TUCTA na katiba ya TUCTA inatoa nafasi ya kuchagua viongozi, viongozi hawa wana kibali cha kusema kwa niaba ya wafanyakazi wote. Ni lazima Mgaya aseme kwani wafanyakazi wakiomba kibali cha kuandamana au kugoma ili kila mfanyakazi aseme mwenyewe yanayomkereta watawaacha?

Ninaongea kwa uchungu kama mfanyakazi kutokana na haki zangu nyingi kushikiliwa na serikali ya CCM, malimbikizo, madai mbalimbali, kupanda vyeo na mishahara n.k. Ukiwauliza watakwambia, tulishalipa. Uongo mtupu.

I WILL VOTE FOR INTERGRITY & PATRIOTIC
 
Ama kweli Tambwe Hizza ametambuliwa kama pizza! Opportunistic huyu, msishangae hiyo ni style ya kujifagilia aonekane anaweza kutumwa kwa lolote na wakubwa zake hata kama kwa kufanya hivyo ndio kujimaliza kwake pumzi.
 
Huyu Tambwe asitufanye sisi wafanyakazi kama kuku! maana kuku bana ukianika mpunga wako huja kuudonoadonoa, utamfukuza hapo kwa hata kumrushia jiwe anaweza pia hata umia lakini atakimbia hatua chache na atarudi tena na kufikiri alifukuza jana yake, maana na kuwa anasahau muda mfupi sana! Tambwe aelewe kuwa kauli mbaya huvuma mbali, kama yeye mla kunde amesahau, sisi wazoa maganda bado hatujasahau matusi yale ya JK!
 
SON: DAD, I HAVE TO DO A SPECIAL REPORT FOR SCHOOL. CAN I ASK YOU A QUESTION?

FATHER: SURE SON, WHAT'S THE QUESTION?

SON: WHAT IS POLITICS?

FATHER: WELL, LET'S TAKE OUR HOME FOR EXAMPLE. I AM THE WAGE EARNER, SO LET'S CALL ME MANAGEMENT. YOUR MOTHER IS THE ADMINISTRATOR OF THE MONEY, SO WE'LL CALL HER GOVERNMENT. WE TAKE CARE OF YOUR NEEDS, SO LET'S CALL YOU THE PEOPLE. WE'LL CALL THE MAID THE WORKING CLASS AND YOUR BABY BROTHER WE WILL CALL THE FUTURE, DO YOU UNDERSTAND????

SON: I'M NOT REALLY SURE, DAD. I'LL HAVE TO THINK ABOUT IT.

That night, awakened by his baby brother's crying, The boy went to see what was wrong. Discovering the Baby had seriously soiled his diaper, the boy went to His parents' room and found his mother sound asleep. He then went to the maid's room where, peeking through
the key hole, he saw his father in bed with the maid. The boy's knocking went totally unheard by his father and the maid, so the boy returned to his room and went back to bed. The next morning:

SON: DAD, NOW I THINK I UNDERSTAND POLITICS.

FATHER: THAT'S GREAT SON, EXPLAIN IT TO ME IN YOUR OWN WORDS.

SON: WELL, DAD, WHILE MANAGEMENT IS SCREWING THE WORKING CLASS THE GOVERNMENT IS SOUND ASLEEP. THE PEOPLE ARE BEING COMPLETELY IGNORED AND THE FUTURE IS FULL OF SHIT.

 
Mimi nayataka maneno ya ile hotuba aliyoitumia kukataa kura zetu wafanyakazi, niiweke kuwa mlio kwenye simu yangu iwe inanikumbusha kila ninapopigiwa, na kila anayenipigia simu akumbushwe, pengine itasaidia japo kidogo. Anahitaji kupelekewa funzo huyu jamaa, na si ajabu tukifanya hivi kwa wingi itakuwa mwisho kusemewa mbovu namna hii, pengine tutapata rais mwenye heshima kwa wananchi.
 
Mimi nayataka maneno ya ile hotuba aliyoitumia kukataa kura zetu wafanyakazi, niiweke kuwa mlio kwenye simu yangu iwe inanikumbusha kila ninapopigiwa, na kila anayenipigia simu akumbushwe, pengine itasaidia japo kidogo. Anahitaji kupelekewa funzo huyu jamaa, na si ajabu tukifanya hivi kwa wingi itakuwa mwisho kusemewa mbovu namna hii, pengine tutapata rais mwenye heshima kwa wananchi.
Nakumbuka Mwanakijiji aliweka video yake..Jaribu kutafuta mada za mwezi wa 5 unajua tena Moi Mosi..
 
Nakumbuka Mwanakijiji aliweka video yake..Jaribu kutafuta mada za mwezi wa 5 unajua tena Moi Mosi..
Video zote zilizoletwa na Michuzi pale YouTube zilishaeditiwa na kuondolewa meneno yale. Halafu ile nakala ya hotuba iliyoandikwa siyo nakala halisi ya yaliyotoka mdomoni mwake; kwenye hotuba ya kuandikwa wametumia maneno "....................basi nakubali nimeshazikosa kura zenu," lakini kwenye hotuba yenyewe live alisema ".....................basi sina haja ya kura zenu." Sehemu hiyo iliondolewa katika clips zote za video zilizoko pale Youtube. Labda kama MKJJ aliipata ile ya moja kwa moja kutoka ITV kabla ya editing.
 
Yaani JF ingekuwa inaruhusu matusi huyo Tambwe leo nahisi ningemaliza mambo yangu humu yote maana ningemtukana hadi alipolalia...hawezi kutufanya sisi watanzania mazezete....mimi ni mwanaCCM lakini kwa hili nasubiri kauli ya Kikwete nifanye maamuzi. Nataka aje hadharani kusema hakukataa kura zetu afu nimuonyeshe ile video atolee ufafanuzi kama yule aliyesema maneno yale alikuwa Kikwete pacha wake. Baada ya hapo tutafahamiana vizuri.
 
Hata iweje mimi na familia yangu hatumjui kikwete kwenye kura alishanitukana nikiwa sebureni na watoto.
 
Watanzania msijeshangaa siku moja akaja huyo Tambwe au Makamba wakadai kuwa JK hajawahi kuahidi maisha bora kwa kila mtanzania, ari mpya, kasi mpya. Tambwe na Makamba, hakikishe mnamkumbusha JK kurudisha fomu za kugombea urais maana ni msahulifu sana.
 
Back
Top Bottom