VISIONEER
Senior Member
- Apr 29, 2011
- 141
- 20
Hata ccm ipewe miaka hamsini tena kutawala hatutaona maendeleo yeyote sanasana tutajikuta na wananchi tumetaifishwa, broda mbona mgumu kuelewa?, hata picha huoni
@ facebook:by william malecela on monday, may 23, 2011 at 4:11am
- mjadala wa suala la ukabila na udini ni mjadala ambao umeshapittwa na wakati. Sioni sababu kwanini baadhi ya viongozi wa ccm bado wanatumia karata hiyo linapokuja suala la chadema. Hatari yake ni kuwa jambo hili litafanya chama chetu kionekane kinawagawa watanzania kwa misingi ya dini, kabila na hata rangi vitu ambavyo ni vigeni kabisa ndani ya ccm.
Ccm ni chama ambacho kinahitaji wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule kuonesha uongozi katika kujadili issue na siyo watu. Kwa kuanza kujadili watu ccm kimejiingiza kwenye mtego ambao ni vigumu sana kutoka na ni mtego ambao mwisho tutajikuta tunanasa sisi wenyewe. Sasa turudi kwenye issue muhimu za taifa.
- kuna masuala mengi ambayo watanzania tunataka kuona tofauti katika maisha yetu na yanayohitaji majibu kutoka chama tawala. Tulienda kwenye uchaguzi na kuomba kura za watanzania ili tuwaongoze kwa miaka mitano ijayo na hilo ndilo tunatakiwa kufanya siyo kujitetea kila kukicha au kulalamikia upinzani. Kama tutawapatia watanzania uongozi wakati huu basi hoja nyingi za upinzani zitakufa zenyewe. Lakini tukisikia tena mambo ya chadema chama cha wachagga au cha wakristu kutoka viongozi wa ccm tutakuwa tunakaribisha mgawanyiko mkubwa kati ya wananchi. Ccm iachane na hoja hizi za udini na ukabila na iwe mwepesi kujitenga nazo wala isizilee au kuhusishwa nazo kabisa. Siasa za udini na ukabila zimepitwa na wakati twende kwenye siasa za issue:
yapo masuala ya:
utawala bora
elimu
utawala wa sheria
nishati
katiba mpya
n.k
- viongozi wetu wa ccm na chadema, mtaanza lini kuzungumzia haya badala ya kuhangaika na mambo ya ccj na siasa za chama cha wachagga? Hebu turudi sasa kwenye issues muhimu kwa taifa letu, kama hamuwezi jivueni magamba tuanze upya!
mungu ibariki tanzania!
william malecela.