CCM na CHADEMA sasa turudi kujadili solutions za issues muhimu kwa taifa letu!

Huyo chaguo la watu alipata kura ngapi kwa uchaguzi uliosimamiwa na taasisi gani, alitangazwa na nani, aliapishwa lini na wapi, nifahamishe anaishi ikulu ya wapi. Na ni nani hasa?
Leta hoja za maana, siyo upuuzi kama huu.

Join Date : 24th May 2011
Posts : 3
Thanks0Thanked 0 Times in 0 Posts

Rep Power : 0
 
Whts the use of this Rocky?!

Mkuu hebu tutafutie matokeo ya urais hata uliompa ushindi Mkuu wa Kaya katika website ya tume ya uchaguzi utuwekee hapa. Ni miezi Nane sasa toka uchaguzi umalizike ila website iko tupu. Tukishayaona tutaongea
 
Oh c'mon Rocky, hutomtambua raisi mpaka atangazwe kwenye website? Na hao wa vijijini je?
I opt not to answer that foolish qn of yours!
 
Oh c'mon Rocky, hutomtambua raisi mpaka atangazwe kwenye website? Na hao wa vijijini je?
I opt not to answer that foolish qn of yours!

Hapo ndipo ninapouona uelewa wako wa mambo ulivyo mdogo
Matokeo yote ya urais yawe ya kitongoji au kijiji au kata au ya wilaya yote yanawasilishwa NEC na NEC ndio yeenye utaratibu wa kuyakusanya yote na kuyatangaza na kuutangazia umma kuwa rais ni nani na ndo maana mamlaka ya mwisho ya kutangaza Rais ni nani ni NEC wanayo
hakuna cha matokeo ya kijijini wala nini. Naomba tuu ukasome sheria iliyounda Tume ya Uchaguzi na uelewe ni nini majukumu yake kabla ya kukurupuka kusema foolish qn
 
NEC waliutangazia umma kupitia televisheni na redio tena live.
Mtu niliyemnukuu mwanzo alisema JK ni chaguo la NEC, labda ungemuuliza kwa nini basi hawakumtangaza kwenye website yao?
 
NEC waliutangazia umma kupitia televisheni na redio tena live.
Mtu niliyemnukuu mwanzo alisema JK ni chaguo la NEC, labda ungemuuliza kwa nini basi hawakumtangaza kwenye website yao?

Iliwachukua NEC wiki moja kuyakusanya matokeo yote kuyaingiza kwenye system yao ya computer na kuutangazia umaa kuwa rais fulani ameshinda
Why it takes eight solid months kuyaweka the same yale yale waliyotutangazia kwenye website at least tujue ni wapi na wapi walimchagua huyo rais
Hatuna ushabiki wa chama hapa ila inatia wasi wasi website ya tume ya uchaguzi kutokuw ana matokeo ya uchaguzi wa rais uliopita
Angalia tume za taifa z auchaguzi wa Rais za nchi za wenzetu kila kitu kiko wazi kwenye website yao hapa kwetu kuna nini
 
Mkuu WJM,

Agenda kubwa ni kuitoa CCM madarakani ambayo imeshindwa kuongoza na kuleta maendeleo. Miaka karibu ya 50 sasa tangia tumepata uhuru, ajabu hatuna cha kujivunia Kama taifa. CHADEMA wanafanya Kila kiwezekanacho wanainchi wajue uraia. Porojo za amani na utulivu wakati serikali haiweki miundo mbinu hazina nafasi tena. Ufisadi na wizi wa Mali ya umma ufikie mwisho. adui nambari moja wa Watanzania ni CCM ambacho mtaji wake ni ujinga wa Watanzania wenyewe.
Yaani hapa kwangu mimi umemaliza kabisaaaaaaaaaaaa
 
nguvumali,
ahadi zipi uzisemazo na porojo zipi tuziache?

Hakika kama huzijui porojo na ahadi zipi mtekeleze wewe thubutu kidogo kuanzisha thread kuomba watu wakufaamishe!!! Nafikiri utashangaa sana sana jinsi zilivo nyingi na pengine zitakusaidia kuacha kupiga kelele jukwaani kuhamasisha ukabila na kuanza kutekeleza hizo ahadi.
Mie nitakukumbusha moja....Raisi aliaidi MELI kuondoa tatizo sugu la usafiri DODOMA!!!!
 
Hili ni hoja muhimu sana Bw Malecela kaleta hapa. Viongozi wote wa vyama vya siasa( tawala au upinzani) ni lazima wazingatie umoja na amani wa taifa kwa kila wanalo tenda au kusema. Kuleta ukabila na udini ni kusaliti taifa. Wote tunafahamu kua mlango wa ukabila na udini ukishafunguliwa wazi basi haufungiki na majanga tu ndio yatazidi.

Tatizo ni sisi wapiga kura kuwachagua watu wanaotumia karata za ukabila na udini. hawa watu hawastahili kura.
 
@ Facebook:by William Malecela on Monday, May 23, 2011 at 4:11am

- Mjadala wa suala la Ukabila na udini ni mjadala ambao umeshapittwa na wakati. Sioni sababu kwanini baadhi ya viongozi wa CCM bado wanatumia karata hiyo linapokuja suala la Chadema. Hatari yake ni kuwa jambo hili litafanya chama chetu kionekane kinawagawa Watanzania kwa misingi ya dini, kabila na hata rangi vitu ambavyo ni vigeni kabisa ndani ya CCM.

CCM ni chama ambacho kinahitaji wakati huu kuliko wakati mwingine wowote ule kuonesha uongozi katika kujadili issue na siyo watu. Kwa kuanza kujadili watu CCM kimejiingiza kwenye mtego ambao ni vigumu sana kutoka na ni mtego ambao mwisho tutajikuta tunanasa sisi wenyewe. Sasa turudi kwenye issue muhimu za taifa.

- Kuna masuala mengi ambayo Watanzania tunataka kuona tofauti katika maisha yetu na yanayohitaji majibu kutoka Chama Tawala. Tulienda kwenye uchaguzi na kuomba kura za Watanzania ili tuwaongoze kwa miaka mitano ijayo na hilo ndilo tunatakiwa kufanya siyo kujitetea kila kukicha au kulalamikia upinzani. Kama tutawapatia Watanzania uongozi wakati huu basi hoja nyingi za upinzani zitakufa zenyewe. Lakini tukisikia tena mambo ya Chadema chama cha Wachagga au cha Wakristu kutoka viongozi wa CCM tutakuwa tunakaribisha mgawanyiko mkubwa kati ya wananchi. CCM iachane na hoja hizi za udini na ukabila na iwe mwepesi kujitenga nazo wala isizilee au kuhusishwa nazo kabisa. Siasa za udini na ukabila zimepitwa na wakati twende kwenye siasa za issue:

Yapo masuala ya:
Utawala bora
Elimu
Utawala wa Sheria
Nishati
Katiba Mpya
n.k

- Viongozi wetu wa CCM na CHADEMA, mtaanza lini kuzungumzia haya badala ya kuhangaika na mambo ya CCJ na siasa za chama cha Wachagga? Hebu turudi sasa kwenye issues muhimu kwa taifa letu, kama hamuwezi jivueni magamba tuanze upya!

MUNGU IBARIKI TANZANIA!

William Malecela.

Falsafa ya Chama

1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

CCM wao wanaamini nini? Gamba?
 
Yaani hapa kwangu mimi umemaliza kabisaaaaaaaaaaaa

Mukome kutoa matusi kwa watz; KUTUITA WAJINGA, nyie mlizunguka, mkatangaza sera zenu, kura zenu hazikutosha!!! Wamlaumu nani hiyo ndiyo demokrasia ama kwenu DEMOKRASIA INAPATIKANA PUNDE DR. MITUTU AINGIE JUMBA LA MAGOGONI?????
MTAISHIE KUPIGA SOGA, JK NI RAIS WETU SOTE LABDA UUKANE UTZ:dance::dance::dance:
 
nilidhani na leo ummjibu kama juzi...''Nepotism''..

ki u ukweli chaedema inazungumzia kila siku suluhisho la taifa hili lakini ccm hawasemi kitu kazi kusingiziana na kupigana vijembe....kwa miaka 50 hatuna maemdela ya ukweli....sasa hivi nchi nzima imejaa magofu tupu.....magofu kwenye kilimo...magofu kwenye miondo mbinu...magofu kwenye elimu nk.......na yote hii ni sababu ya ccm maana kila mtu ana mipango yake lakini hawaisimamii kazi kuja na misamiati mipya tu.tuko hatua za mwisho......mchakato unaendelea.......jitihaza za serikali ziko wali.........nk

malecela william ccm hawana nia ya dhanti ya kumaliza matatizo ya nchi hii au kuja na mbadala wa matatizo hayo.....

Kwe;i nakubali kzi ya CCm siyo kupambana na CDM kwenye majukwa ila wanatakiwa kutimiza ilani ya uchaguzi , zile sera zao waziweke katika utendaji na hakuan mtu atakye wasikia CDM tena, lakini kama kazi yao ni kwenda kuiba Maiti walizoziuwa unategemea nini? Hawafikirii namna ya kuwasaidia watu ila kuwauwa na sasa kwa mtutu, hii ni hatari kwa kweli.
Mungu Ibariki Chadema, Mungu Ibariki Tanzania!!!!!!!
 
Falsafa ya Chama

1. Falsafa ni fikra na mtazamo wa Chama ambayo ni kuamini katika "Nguvu na Mamlaka ya Umma" (The People's Power) katika kumiliki, kuendesha, kubuni, na kuendeleza maamuzi, mawazo, rasilimali, uchumi na siasa ya nchi yao.
2. Aidha falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo msingi na chimbuko la kuundwa dola ya nchi, na kuwa, Umma ndiyo wenye madaraka ya mwanzo na ya mwisho katika kuamua hatima ya nchi na taifa pasipo kuingiliwa, kudanganywa au kughilibiwa na viongozi, watawala au wageni.
3. Ujenzi na udumishaji wa Demokrasia na Maendeleo nchini vitatokana na Nguvu na Mamlaka ya Umma wa Watanzania. Nguvu na Mamlaka ya Umma itabainishwa, kuainishwa na kulindwa katika Katiba ya nchi na Umma ndiyo utakuwa chimbuko la Katiba hiyo.
4. Historia inaonyesha kuwa "UMMA" wa Watanzania haujawahi kuwa na sauti, mamlaka na madaraka juu ya maamuzi ya hatima ya maisha ya watu. Uhuru, nguvu, mamlaka na madaraka wakati wote, tokea enzi za ukoloni mpaka leo, vimekuwa vikihodhiwa na kumilikiwa na watu wachache ambao wana mamlaka ya kuongoza SERIKALI na kuwakandamiza wananchi.
5. CHADEMA tunaamini kuwa mifumo na miundo ya utawala wa nchi yetu havijawapo kwa ajili ya kuutumikia umma, bali umma ndiyo huzitumikia serikali hizo ambazo ni mali ya watu wachache wanaopoka "Nguvu ya Umma". Sambamba na hilo, umma wa Watanzania umekuwa hauna mamlaka ya mwisho ya kuhoji maamuzi ya serikali yanayowaathiri watu, na hivyo kujikuta hauna mamlaka juu ya rasilimali, sheria, utawala, na uendeshaji wa nchi. Aidha, Katiba ya Nchi imekuwa miliki ya Serikali kwa kutumia Bunge ambalo linatawaliwa na mawazo kongwe ya ukiritimba wa enzi za mfumo wa Chama kimoja cha siasa nchini.
6. CHADEMA tunaamini na kutambua kuwa "kuchaguliwa" kuunda utawala wa kuongoza nchi hakumaanishi wachaguliwa kujitwalia mamalaka ya UMMA na kisha kuyatumia mamlaka hayo kuwakandamiza "waliowachagua" kwa sababu tu ya kutetea maslahi binafsi badala ya maslahi ya umma.
7. Hivyo basi, falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" ndiyo njia ya msingi ya kubadilisha fikra na uongozi unaokandamiza umma, ili kuibua fikra mpya na kuweka uongozi unaoweza kumilikiwa, kuhojiwa, na kuwajibishwa na umma kwa kutumia vyombo vilivyopatikana kwa utashi wa wengi kupitia chaguzi huru na za haki.
8. Falsafa ya "Nguvu na Mamlaka ya Umma" inalenga kuwaamsha, kuwahamasisha, kuwaelimisha, kuwashawishi na kuwaandaa Watanzania wachukue hatua ya kuimiliki, kuitawala, kuilinda na kuifaidi nchi yao tofauti na kipindi cha miaka mingi chini ya mfumo wa chama kimoja cha siasa na miaka kumi na nne ya mwanzo ya mfumo wa vyama vingi.

CCM wao wanaamini nini? Gamba?

hii falsafa ya peoples power kama ulivyoieleza hapa mbona ni kama UJAMAA fulani? au UMMA ni kitu gani? kwa Tanzania ya leo ambayo imepitia katika mifumo mbalimbali ambapo kwa sasa kuna tofauti katika kipato/maisha elimu hata uelewa wa watu unafikiri unaweza kuundwa umoja - UMMA kama unavyoeleza? na kuwa mfumo.
shida ninayoiona hapa ni kwamba nguvu ya umma inakuwa na maana wakati CDM inapigania kuchukua dola, lakini ikishakamata dola hii nguvu ya umma inaweza kutafsiliwa tofauti. watu wanaweza jenga hoja against kiongozi yoyote wasiomtaka na wakatumia nguvu ya umma kuandamana na kumtoa.
Je hii falsafa inafanya kazi wapi? any reference? maanake sijasikia kama kuna nchi inaendeshwa kwa nguvu ya UMMA, nchi nyingi zinaendeshwa na mabepari/mabeberu
 
Back
Top Bottom