CCM kwa sasa ina machaguo mawili tu. Kumtosa Rais Samia na wenzie waliotufikisha hapa ianze upya au kuikosa Ikulu 2025

Mathanzua

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
15,877
20,732

CCM kwa sasa ina chaguzi mbili tu, kumtosa Rais Samia na wenzie waliotufikisha hapa ianze upya au kuikosa Ikulu 2025​

Nchi imechafuka, wananchi wamekasirika kwa kuwa wameujua ukweli kwamba CCM na Serikali yake si rafiki, ni adui yao,na haiwezi kabisa kuwafikisha Kanani, nchi ya maziwa na asali. CCM kwa sasa ina options mbili tu,au imtose Samia na wenzake waliotufikisha hapa ianze upya, au iikose Ikulu 2025.

Ni ukweli usiopingika, kwamba nchi yetu haijawahi kuwepo katika sintofahamu ya namna hii tangu tupate Uhuru wetu mwaka 1961. Ndio CCM na serikali zake mbali mbali zimetufanyia mambo mengi mabaya:Vijiji vya Ujamaa,sera ambayo iliingiza Watanzania kwenye umaskini uliotopea;kutaifisha mali za walioitwa wanyonyaji na hatimaye kuharibu uchumi wa nchi kabisa; mikataba mingi mibovu: MEREMETA, KAGODA, SYMBION, IPTL, ATCL, TRC nk., lakini nchi haijawahi kukosa amani na Wananchi wakalalamika na kuichukia serikali yao kiasi hiki.

Hii ni kwa nini? Ni kwa sababu wananchi wamekosa imani kabisa na mfumo mzima wa utawala. Hawana imani tena na utawala wowote wa CCM na Serikali zake,wanataka mabadiliko chanya. Unaweza ukauvuta mpira kwa kiasi fulani, lakini hatimaye unafikia ukomo wa kuvutika(elastic limit) na kukatika.Ndio, Watanzania wamefikia ukomo wa uvumilivu.CCM sasa ina chaguzi mbili tu ili angalau kujisafisha:au iachane na Samia na kufanya kama kile kilichofanyika Uingereza kwa kuachana na Waziri Mkuu Boris Johnson na kumuweka Waziri Mkuu wa sasa Rishi Sunak madarakani,au iparaganyike kabisa na kupotea kwenye ulingo wa siasa, huku ikisubiri uchaguzi mkuu 2025.Ndio uaminifu na heshima ya wananchi kwa CCM vimeshashuka sana, lakini angalau wananchi wataona kwamba CCM imetambua makosa yake na iko tayari kujirekebisha.

Ni nini kimeibua yote haya. Hakuna shaka yeyote kwamba mkataba mbovu wa DP World ambao kwa kipimo chochote ni mkataba mbovu,ndio uliofukua makaburi. Legal Human Rights Centre(LHRC) wamesema bila kumung'unya maneno, kwamba mkataba huu una matatizo mengi.

Katibu Mkuu wa CCM Comrade Chongolo(chini mwisho) ameeleza kwamba ipo haja ya kusikiliza wadau wengine na mawazo yao kufanyiwa kazi.Comrade Kinana naye ametoa msimamo unaofanana na Comrade Chongolo.

Sababu zinazotolewa na mamlaka za kutafuta muwekezaji kwenye Bandari zetu ni kama ifuatavyo:

1.Watanzania ni wezi.
Sababu hii si ya msingi sana,kwa kuwa kama walioajiriwa Bandarini ni wezii,wangefukuzwa na kuajiriwa wengine waadilifu.Isitoshe Watanzania tupo million sitini(60) na zaidi,naamini kusinge-kosekana Watanzania waaminifu.Naomba niseme hivi, sababu hii ambayo si ya kweli, imetudhalilisha sana Watanzania kwenye jamii ya kimataifa.Katika jamii yeyote wezi wapo,si ajabu.Sasa kusema kwamba Watanzania ni wezi,ni kutudhalilisha na kutukosea Watanzania heshima,kwa hiyo katika hili, tunaomba tuombwe radhi.

2.Watanzania hawana weledi wa kuendesha bandari.
Inawezekana hii ni kweli,lakini kama ni kweli,CCM na serikali zake mbali mbali tangu Uhuru wanahusika moja kwa moja katika tatizo hili kwa kuharibu Elimu yetu.

Kulikuwa na sababu gani za msingi kwa mfano za kutumia waalimu wa Darasa la Saba.Kulikuwa na sababu gani za kuwa na Elimu ya UPE(Universal Primary Education).Kwa nini mitaala mibovu.Kuna haja gani ya kubadilisha mitaala kila wakati na hivyo kukosa consistency.Kuna sababu gani ya msingi ya kuajiri waalimu wa Division IV tena,wa course ya ualimu ya mwaka mmoja tu(Voda Fasta).Kulikuwa na ulazima gani na haraka gani ya kuanzisha Shule za Kata,huku tukijua kwamba hazina vifaa,waalimu wanaofaa na mazingira mazuri ya kufundishia na mengine mengi?Jibu ni moja tu,nia ni kuharibu elimu,ili kusiwe na watu wenye weledi wa kusimamia rasilimali zao na maendeleo ya nchi yao.

Labda katika swala la Watanzania kutokuwa na weledi unaotakiwa kuendesha bandari,niongeze jambo lingine la msingi.Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwa na tabia ya kutoa ajira kindugu na kujuana.Sina shaka yeyote kwamba mfumo huu wa ajira ume-compromise sana weledi,na hii haijaathiri utendaji Bandarini pekee tu,lakini serikalini kwa ujumla na kwenye mashirika yote.Na hapa niseme wazi,CCM na serikali zake zote inahusika,kwa kuwa haijaisimamia serikali zake vizuri kudhibiti uovu huu.

Kumekuwa na harakati nyingi kutoka CCM na serikali yake kuutetea mkataba huu kati ya Serikali na DP World. Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mkataba huu kwa kipimo chochote haufai,kwa hiyo kimsingi hakuna sababu yeyote ya kuendelea kuutetea na kulazimisha kuutekeleza, kwa kuwa wananchi hawautaki,na sababu kwa nini hawautaki iko wazi,hauna maslahi kwa Taifa lao.Kuendelea kuutetea na kuonyesha nia ya kuutekeleza ni kuendelea kuwatia wananchi hasira na ningeishauri CCM iache.Naomba niwe muwazi,Watanzania hawakatai uwekezaji katika bandari zao,au hata bandari ya Dar es Salaam, wanachokataa ni uwekezaji usio na maslahi kwao na taifa lao.

Naomba nimalizie kwa kusema hivi, wananchi wa Mali,Sierra Leone na Niger walichoka na serikali zao kwa sababu ya kutowajibika ipasavyo kwao.Angalia clip ifuatayo.

Kama sisi Watanzania tunaona our government is delivering,basi tuna matatizo makubwa.
 
Attachments

  • VID-20230802-WA0000.mp4
    12.3 MB
Nchi imechafuka, wananchi wamekasirika kwa kuwa wameujua ukweli kwamba CCM na Serikali yake si rafiki, ni adui yao na haiwezi kabisa kuwafikisha Kanani, nchi ya maziwa na asali. CCM kwa sasa ina options mbili tu,au kumtosa Samia na wenzie wote waliotufikisha hapa ianze upya au kuikosa Ikulu 2025.

Ni ukweli usiopingika kwamba nchi yetu haijawahi kuwa katika sintofahamu ya namna hii tangu tupate Uhuru wetu mwaka 1961. Ndio CCM na Serikali zake mbali mbali zimetufanyia mambo mengi mabaya:vijiji vya ujamaa; kutaifisha mali za walioitwa wanyonyaji na hatimaye kuharibu uchumi wa nchi kabisa; mikataba mingi mibovu, MEREMETA, KAGODA, SYMBION, IPTL, ATCL, TRC nk. lakini nchi haijawahi kukosa amani na Wananchi wakalalamika kiasi hiki.

Hii ni kwa nini? Ni kwa sababu wananchi wamekosa imani kabisa na mfumo mzima wa utawala. Hawana imani na utawala wowote wa CCM tena na Serikali zake. Unaweza ukauvuta mpira kwa kiasi fulani, lakini hatimaye unafikia ukomo wa kuvutika. Watanzania wamefikia ukomo wa uvumilivu. CCM sasa ina chaguzi mbili tu ili angalau kujisafisha au iachane na Samia na kufanya kama kile kilichotokea Uingereza kwa kuachana na Waziri Mkuu Boris Johnson na kumuweka Waziri Mkuu wa sasa Rishi Sunak madarakani huku ikisubiri uchaguzi mkuu.Ndio heshima na uaminifu wa CCM kwa wananchi umeshashuka, lakini angalau wananchi wataona kwamba CCM imetambua makosa yake na iko tayari kujirekebisha.

Ni nini kimeibua yote haya. Hakuna shaka yeyote kwamba ni mkataba mbovu wa DP World ambao kwa kipimo chochote ni mkataba mbovu. Legal Human Rights Centre(LHRC) wamesema bila kumung'unya maneno kwamba mkataba huu una matatizo mengi.

Katibu Mkuu wa CCM Comrade Chongolo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Comrade Kinana nao wameonyesha wasi wasi wa wazi katika mkataba huu.

Nini kifanyike. Kumekuwa na harakati nyingi kutoka CCM na serikali yake kuutetea mkataba huu kati ya Serikali na DP World. Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mkataba huu kwa kipimo chochote haufai,kwa hiyo kimsingi hakuna sababu yeyote ya kuendelea kuutetea na kulazimisha kuutekeleza kwa kuwa wananchi hawautaki,na sababu kwa nini hawautaki iko wazi,hauna maslahi kwa Taifa lao.

Hapa naomba niwe muwazi,Watanzania hawakatai uwekezaji katika bandari zetu,au hata bandari ya Dar es Salaam, wanachokataa ni uwekezaji usio na maslahi kwao.

Naaani wa kumtosa? Naaani wa kuthubutu kumgusa mwenyekiti? Hajazaliwa bado!! 👇👇👇 Ishi humo!!
 
Attachments

  • Screenshot_20221205-182804.jpg
    Screenshot_20221205-182804.jpg
    131.8 KB · Views: 4

Kwa upinzani huu nchini ,ccm hata wakimsimamisha Hamprey Polepole, Shaka Hamdu Shaka au Sophia simba wanashinda kwa kishindo mno bila wasiwasi na bila kutumia nguvu.

Wapinzani gani sijui hawa, wabinafsi wanatamaa na majivuno kama yote. Watapigwa vizuri kwenye ubinafsi wao kwenye sanduku la kura kisha waendelee kulalama kumbe tatizo ni wao wenyewe.
 
Thubutu. Nani wa kumweka pembeni mwenyekiti wakati ndiyo final sayer. Labda aamue kuachia mwenyewe. Au Mungu aweke mkono wake kama alivyofanya kwa wana wa Israel
 
Nchi imechafuka, wananchi wamekasirika kwa kuwa wameujua ukweli kwamba CCM na Serikali yake si rafiki, ni adui yao na haiwezi kabisa kuwafikisha Kanani, nchi ya maziwa na asali. CCM kwa sasa ina options mbili tu,au kumtosa Samia na wenzie wote waliotufikisha hapa ianze upya au kuikosa Ikulu 2025.

Ni ukweli usiopingika kwamba nchi yetu haijawahi kuwa katika sintofahamu ya namna hii tangu tupate Uhuru wetu mwaka 1961. Ndio CCM na Serikali zake mbali mbali zimetufanyia mambo mengi mabaya:vijiji vya ujamaa; kutaifisha mali za walioitwa wanyonyaji na hatimaye kuharibu uchumi wa nchi kabisa; mikataba mingi mibovu, MEREMETA, KAGODA, SYMBION, IPTL, ATCL, TRC nk. lakini nchi haijawahi kukosa amani na Wananchi wakalalamika kiasi hiki.

Hii ni kwa nini? Ni kwa sababu wananchi wamekosa imani kabisa na mfumo mzima wa utawala. Hawana imani na utawala wowote wa CCM tena na Serikali zake. Unaweza ukauvuta mpira kwa kiasi fulani, lakini hatimaye unafikia ukomo wa kuvutika. Watanzania wamefikia ukomo wa uvumilivu. CCM sasa ina chaguzi mbili tu ili angalau kujisafisha au iachane na Samia na kufanya kama kile kilichotokea Uingereza kwa kuachana na Waziri Mkuu Boris Johnson na kumuweka Waziri Mkuu wa sasa Rishi Sunak madarakani huku ikisubiri uchaguzi mkuu.Ndio heshima na uaminifu wa CCM kwa wananchi umeshashuka, lakini angalau wananchi wataona kwamba CCM imetambua makosa yake na iko tayari kujirekebisha.

Ni nini kimeibua yote haya. Hakuna shaka yeyote kwamba ni mkataba mbovu wa DP World ambao kwa kipimo chochote ni mkataba mbovu. Legal Human Rights Centre(LHRC) wamesema bila kumung'unya maneno kwamba mkataba huu una matatizo mengi.

Katibu Mkuu wa CCM Comrade Chongolo na Makamu Mwenyekiti wa CCM Comrade Kinana nao wameonyesha wasi wasi wa wazi katika mkataba huu.

Nini kifanyike. Kumekuwa na harakati nyingi kutoka CCM na serikali yake kuutetea mkataba huu kati ya Serikali na DP World. Hata hivyo kama nilivyokwisha sema mkataba huu kwa kipimo chochote haufai,kwa hiyo kimsingi hakuna sababu yeyote ya kuendelea kuutetea na kulazimisha kuutekeleza kwa kuwa wananchi hawautaki,na sababu kwa nini hawautaki iko wazi,hauna maslahi kwa Taifa lao.

Hapa naomba niwe muwazi,Watanzania hawakatai uwekezaji katika bandari zetu,au hata bandari ya Dar es Salaam, wanachokataa ni uwekezaji usio na maslahi kwao.

Alposema anakwenda kuifungua nchi baadhi yetu hatukumuelewa. Na mpaka muda huu hatumuelewi pia.

Watanzania hatupendi kutoka katika eneo letu linalotupa amani, kwa kingereza wanaita comfort zone.

Hatukubali changamoto mpya na akili yetu ni ile ile ye juzi na jana. kwamba leo inahitaji kuchangamka vichwani mwetu hilo hata hatulioni.

Samia anafanya kile ambacho marehemu JPM angekifanya ikiwa angekuwa hai mpaka muda huu, ndio maana ya KAZI IENDELEE.

Tazama hata baadhi ya watendaji wa wizara ni wale wale wa awamu ya tano,,

Kadogosa ni yule yule wa TRC awamu ya tano. Hamza Johari ni yule yule wa TCAA awamu ya tano, hiyo ndio maana ya kuendeleza kazi iliyokwisha kuanza.

Kuleta mwekezaji bandarini ni kuendana na ushindani wa bandari zinazotuzunguka. Tukumbuke kuwa wateja wa mataifa yanayotumia bandari yetu hutoa mrejesho wa aina mbovu za huduma wanazozipata pale TPA.

Ni lazima serikali ijiongeze katika suala zima la ufanisi. Hivyo kwa watu tunaotazama masuala kwa kina hatuoni namna ambavyo serikali itakwenda kushindwa huko mahakamani na kwenye utekelezaji mzima wa wizara ya uchukuzi.

Hayo mengi mnayokuja nayo yanatokana na jinsia yake, hakuna aliyetegemea kuwa safari ya JPM ingemalizika March 2021.
 
Nchi ilichafuka baada ya CHADEMA kuwasaliti UKAWA wenzao wakati ule "mshenga" mh.Gwajima alipowezesha "usajili" na Mh.Mbowe kubadilisha "gia angani" baada ya "KULAMBISHWA YA KAIZARI MWACHIE KAIZARI"
 
Nchi ilichafuka baada ya Dr.Slaa na Prof.Lipumba kugundua kuwa mh.Mbowe "alilambishwa ya KAIZARI MWACHIE KAIZARI"...Lipumba akakimbilia Rwanda

Nje ya CCM hakuna siasa......
 
Back
Top Bottom