Desprospero
JF-Expert Member
- Feb 1, 2023
- 887
- 2,201
LEO ni siku ambayo nchi mbili huru kwa maana ya Tanganyika na Zanzibar ziliungana na kuzaa nchi moja Tanzania lakini nchi hiyo ikiwa na muundo wa Serikali mbili. Serikali ya Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Ni jambo jema watu wamoja tena ndugu waliokuwa wametengwa na wakoloni wanapoamua kuwa kitu kimoja. Ukuta wa Berlin uliowatenganisha ndugu wamoja wa Ujerumani ulipobomolewa Wajerumani walitoa machozi ya furaha kama Zanzibar na Tanganyika walipoungana. Kongole kwa Hayati Julius Nyerere na Abeid Aman Karume.
Hata hivyo, tunapoadhimisha siku hii muhimu ni vizuri tukatafakari nia na shabaha ya waasisi hawa walitaka kujenga Jamii ya aina gani? Ukweli ni kwamba baada ya TANU na ASP kuungana na kuzaa CCM waasisi hawa walitamani kujenga jamii ya watu wenye usawa, jamii isiyo na wanyonyaji kwa maana ya makupe. Na hapa ndipo ilipojikita siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Ni siasa hii ya Ujamaa iliyozaa Azimio la Arusha.
Hata ndani ya Katiba yetu ya mwaka 1977 bado inaelezwa bayana kuwa Tanzania inafuata siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. Swali ambalo wana-CCM wanatakiwa kujibu bila unafiki ni je, nchi hii bado ni ya kijamaa?
Ni uongo na unafiki kama jibu litakuwa ni NDIYO maana ngoma inayopigwa (Katiba) ni Ujamaa lakini uchezaji ni Ubepari. Ile dhima ya usawa katika jamii imetoweka na ndiyo madhara tuliyoanza kuona na yumkini kuna hatari kubwa ya nchi hii kuingia katika machafuko mabaya sana huko tuendako na ni CCM itabeba lawama na laana!
Pengo kati ya matajiri na masikini inapanuka kila uchao. Kikundi kidogo sana Cha mabepari wanahodhi ukwasi wa kutisha huku kundi kubwa wakiishi maisha dhalili mno. Hii ni hatari sana. Sasa tunashuhudia tabaka la watawala wanavyojitenga na watawaliwa wasiojua hata mlo wao wa kesho.
Dhana ya Kujitegemea imeondoka na tunadhani tuko salama tunaposifiwa na mabepari wa mtaa wa Brettonwood, New York WB na IMF eti uchumi wetu unakuwa kwa kasi. Haya mashirika mumiani wakikusifia jifikirie mara mbili. Mikopo yao inayoondoa Kujitegemea ni ndoano hatari sana hapo baadaye.
Mwalimu Nyerere aliwapinga wazi wazi na kanini yao ya GDP kwa hoja nzito kwamba eti kupata pato la kila mwananchi ni kuchukua pato lote na kisha kugawia idadi ya wananchi. Huu ni upumbavu maana mali imehodhiwa na watu 100 then unataka kuwagawia na kina Mama Lishe, bodaboda, vinyozi, mafundi mchundo nk. Ujinga uliovuka mawingu.
Kuendelea na mfumo huu wa Ubepari ni sawa na kumwagia nyumba yako petroli. Ninaambiwa mshauri wa masuala ya uchumi wa Rais Samia Suluhu Hassan ni mtaalamu wa fani hiyo tena mwanamke. Sijui ni kwa nini ameteua ushauri huu katili. Laiti kama angesikia vilio vya wananchi walio wengi wanateseka angeachana na ushauri huu kwa Samia na kama hashauriki angeachana naye na kurudi UDSM kufundisha
Kama kweli tunaenzi Muungano basi tuyaenzi na mawazo, maono na visheni kali ya waasisi wake. Tujenge Taifa la watu wenye usawa wanaofaidi keki ya nchi yao kwa pamoja. Kinyume na hapo ipo siku (haiko mbali) masikini watakuwa tayari kutafuta mbadala.
Kheri ya Muungano!
#BringBackOurMoney. CAG report.