CCM haitakufa na itaongoza milele: Nape Nnauye

Nape unabishana na waanzilishi wa chama wakati wewe umedandia njiani tu.!!!
 
Nappe amesema CCM haitakuja kufa na itaongoza milele.

Ameitoa kauli hiyo kufuatia kauli zilizotamkwa na wazee 3 ambao ni Butiku, Kitine na mzee Kaduma waliosema kuwa CCM inakaribia kufa bin kutokomea.

Source: ITV taarifa ya habari saa mbili jioni ya leo

Sina hakika na statement hii kama kweli nape kajanayo, lakini ninaamini dogo dishi limeyumba kiasi cha kukosa uhuru, na finally kashindwa kuwa objective, na wajibu wake kama k/tibu mwenezi siyo huo, wa mara kamjibu lowasa, mala hili nadhani issue kwake sasa ni kusutwa moyoni kwa ufisadi alionao
 
Wakuu pamoja na kupotea, mimi nadhani na ndio imani yangu, Nape ameongea sawa na kwamba kwa kuwa CCM sio mtu ni taasisi, na moja ya sifa ya taasisi ni succession and continuity, ccm ya Mwalimu sio hii kwa maana ya uongozi na viongozi, lakini nia, imani na malengo yake na kwa mujibu wa katiba yake bado ni yale yale, hivyo hoja ya ccm kuishi milele maana yake ndio hiyo na sio kwa maana kwamba ccm ni mtu na hivyo ataishi milele, hii ina maana viongozi na uongozi utakwenda na kubadilika ikiwa ni pamoja na kukidhi matakwa na haja ya wakati, lakini ccm itaendelea kuwepo.

Hivyo hakuna haja ya kutafsiri neno kwa neno maana mantiki iko wazi, Nape taf, endelea na jukumu lako la kutoa taaluma, na ni wazi kwamba tofauti ya mawazo na muono zitaendelea kuwepo, wazee wetu wana mtazamo tofauti na wa kizazi chetu, hata njia za mapambano ya kisiasa na media za mapambano ni tofauti, ila hii isitupe tabu, kubwa ni kwamba endelea kuelimisha vijana wenzako kuelewa chama ni nguzo na ni malengo na ni tegemeo la watanzania wa kawaida walio wengi, hata marafiki wa ccm kwa maana ya wapinzani sio kweli kwamba hawaitakii mema ccm ,ila wana tofautiana juu ya approach ya namna ya kufikia ufumbuzi wa kutatua matatizo ya watu wake, hivyo tafauti kati ya wazee na vijana itaendelea na ndio mana hata wale wanaopiga kelele kuh, azimio la arusha sio kwamba hawaelewi ukweli halisi wa maisha na mapambano ya ki uchumi, ila kwa kawaida ni lazima kuwepo na tofauti ya mitazamo na approach.

Endelea kutoa taaluma, muelekeo,tumaini na malengo ya chama chako, wacha wazee wawe na maoni yao na vijana muwe na ya kwenu, kubwa ni kutatua na kufikia solution ya matatizo ya Taifa hasa juu ya matatizo ya vijana.

Tuko na wewe na tunafuatilia kwa ukaribu mno juu ya mwenendo, muono na muonekano. kwa ujumla mapambano yaendelee, wale wanaojitahidi kuipiga madongo ccm ni haki yao kwa kuwa wana tofauti ya imani na muono, sisemi kwamba wako sawa kwenye chama chao, ila kwa kuwa lengo kuu la chama CHOCHOTE CHA SIASA NI KUSHINDA KILA UCHAGUZI NA KUUNDA SERIKALI, hivyo endelea na tutafanikiwa. Usivunjike moyo, wenye tofauti ya mawazo na mitazamo juu ya ccm na serikali zake ni lazima wawepo na hasa kwa vile tofauti za kimtazamo ni nyingi kutoka ndani ya ccm na nje ya ccm,hii ni ishara tosha kwamba demokrasia ya kweli ndio inayojengwa kwenye jamii, pamoja na kwamba hatujafikia tunapofikiria kufika ili demokrasia iwe absolute, kubwa ni ku focus on mission and goals za chama ,lakini pia kupata model nzuri ambazo zitaweza kusaidia ccm kufikia malengo yake kwa uhakika na kwa muda muafaka.
usife moyo na usipate tabu watu wanapoifanya hii ni vita yako binafsi dhidi ya wengine ama ndani ya ccm au nje ya ccm, Umetumwa na kukabidhiwa jukumu, endelea kulitekeleza na kulikamilisha kwa moyo na uwezo wako wote.

Mwisho wa safari ukweli utajuilikana tena bila ya kutumia nguvu mana mchele na pumba ni vitu tofauti, aidha siku zote ukweli unapowadia uongo hujitenga mana wanasema ukweli huwa una kawaida ya kujirudia rudia. Kwa lugha nyengine ukweli hauozi wala haurogwi.
 
Ilo genge la wezi mwisho wake 2015.anajifariji tu.kijana ndani ya chama kizee!nenda arumeru huko
 
anamfanyia Mungu dhihaka sasa asuburi moto wake
Mungu amesikia sala za watanzania tunaoibiwa,kudanganywa,kunyonywa
kudhulimiwa na kila aina ya uchafu wa chama hicho
naeishi milele na milele ni Mungu peke yake sio magamba.
 
CCM haina roho inakufa vipi? au sijaelewa maana ya kufa..

CCM inaweza kukosa mvuto (hilo halina shaka), linaweza kukosa mamlaka na ridhaa ya wananchi hilo halina shaka..litatokea
 
Hivi tulitegemea jibu la namna gani toka kwa mtu ambaye kwa ujasiri kabisa tena mbele ya kadamnasi akatamka kuwa
"ccm bado inatekeleza sera za ujamaa na kujitegemea"

Samahani kwa kusema hivi ila ni ukweli uliowazi kuwa Nape ni KITUKO mwingine tu asiyejua anachosimamia.

Lakini? Hivi angejibu nini pale??
 
Nappe amesema CCM haitakuja kufa na itaongoza milele.

Ameitoa kauli hiyo kufuatia kauli zilizotamkwa na wazee 3 ambao ni Butiku, Kitine na mzee Kaduma waliosema kuwa CCM inakaribia kufa bin kutokomea. Source: ITV taarifa ya habari saa mbili jioni ya leo

Nape kama kweli umesema hayo umekuwa OVER ZEALOT, Hakuna mamlaka yeyote under this SUN itakayo tawala milele. Jaribu kusoma vitabu vya historia na misahafu ya dini, utagunduia uliochongea/unachoamini ni sawa na mbingu na ardhi.
 
Nape ukweli anaufaham, sema yuko vitani hivyo kugeuka fasta sheria za jeshi si unazijua lazima ajifariji tu!
 
Huyu anaishi kwa kuuza maneno, ndio mtaji wake wala si wa kubishana naye ni kumpuuza tu, Si mwanasiasa wala nini!! Hana Mission wala Vision!!
 
Wakuu pamoja na kupotea, mimi nadhani na ndio imani yangu, Nape ameongea sawa na kwamba kwa kuwa CCM sio mtu ni taasisi, na moja ya sifa ya taasisi ni succession and continuity, ccm ya Mwalimu sio hii kwa maana ya uongozi na viongozi, lakini nia, imani na malengo yake na kwa mujibu wa katiba yake bado ni yale yale, hivyo hoja ya ccm kuishi milele maana yake ndio hiyo na sio kwa maana kwamba ccm ni mtu na hivyo ataishi milele, hii ina maana viongozi na uongozi utakwenda na kubadilika ikiwa ni pamoja na kukidhi matakwa na haja ya wakati, lakini ccm itaendelea kuwepo.

Hata makabila hufa na kuzaliwa mapya.
 
Back
Top Bottom