Elections 2010 CCM Dar watangaza maandamano na kuahirisha ndani ya dakika 5

tunasubiri tamko la chadema kuhusu kuandamana tuko tayari wakuu, semeni neno moja tu na roho zetu zitapona
 
Chadema mko wapi???? Dar slaaa. Nasi chadema tunataka maandamano ya kukupongeza wewe na uamuzi wa chadema. Please, do it right now!!!!!! Tunaaka mikoa yote ili huyu mwizi asifikiri kuwa ataendelea na upuuzi wake. Please!!!!!!!!!!!!!! Please!!!!!!!!!!!!!!!!!! Please!!!!!!!!!!!!!!!!!!. Kama police hawataki, watuuuwe ili nchi hii iwe ya wahindi. Do it!!!!!!!!!!!!!!!1 ongea dr. Slaa kama raisi wetu. Hii ni nguvu ya uma na siyo mafisadi.
 
Wadau nini kimetokea kwa CCM mkoa wa Dar es Salaam kutangaza maandamano na kuahirisha ndani ya dakika tano?. Kiufupi katika siku chache ambazo nimeangalia Channel Ten taarifa ya habari nimekutana na kioja. katibu wa CCM Mkoa wa Dar Bw. Kilumbe Ng'enda ameonekana akitangaza maandamano ya wana CCM wa Dar kulaani kile alichokiita kudhalilishwa kwa M/kiti wa CCM na wabunge wa Chadema. Wakati nikiwa na hasira kwamba kumbe na chadema nao wangeandaa maandamano kupinga uchakachuaji wa NEC ghafla msomaji wa habari akaja na Breaking News kwamba maandamano hayo yameahirishwa hadi wakati mwingine. Nini kimetokea? Tafakari

SOURCE CHANNEL TEN NEWS at 1900 HRS TODAY 20th Nov 2010

Tunasubiria waandamane, patachimbika nchi nzima. Wanafikiri watu millioni 5 watawashinda watu millioni 40? hawa kweli hawafikirii, tunawalia timing tu hawajui, wakitoka tu hilo ni kosa la jinai. Watu wana machungu wao wanafanya mizaha ee?
 
..Hata kutokee kitu gani..

Half life ya ccm imefikiwa ...hakuna cha kukiokoaa chama hiki...Kinakufa..!

Hakika ..its destined for extinction!!!!
 
mhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhhh CCM
 
WanaJF hao ambao wangeandamana mnadhani ni wana sisiemu!!!!!!!!!!!Ni watu wa mshiko ambao wakijua kwamba wameitiwa maandamano karibu wote watayeyuka na kuwaacha hawa viongozi wenye uchu wa madaraka peke yao!!!!!!!!!!!!!!!! Sisiemu imebaki na wanachama wazee ambao hawawezi hata kukubali kuandamana wakikumbuka wenzao wa EAC wanavyoburuzwa watakuwa tayari hata kumshauri mkwere amwachie Dr (PHD) kama ni choe ndicho kinagombaniwa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Kama watakuwa wamepata mshiko ndiyo ingekuwa vituko!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Vijana ndiyo population kubwa ya mijini ndiyo maana CDM iliteka miji yote!!!!!!!!!!!! Wanachama wa sisiemu ni wazee wako vijijini!!!!!!!!!!!!!! Ndiyo maana mwenye hekima mmoja alishtuka alipokumbuka kwamba wataaibika!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
This time they are in for it!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Mbona walijaribu UBUNG na KWE wakashindwa??????????????? CDM very strategic-ni wasomi wale-kabla ya kutoka nje walikwishasoma na kuelewa kabla hata spika wa sisiemu- wamshukuru mr 6 amewanusuru!!!!!!!!!!!!!!
 
nionavyo ni kama vile ccm wanakimbia kivuli cha maovu yao kwa wananchi ili hali wamesahau kuwa taswira halisi ndio wao wenyewe. wanapingana na kivuli chao wenyewe. hivi, wanashindwa kwenda kuandamana kudai watoto wa maskini walio wengi wanasoma kwenye shule taabani huko vijijini - sekondari za kata, watoto wa maskini wanakesha kuombeleza mikopo ya elimu ya vyuo, hawaamndamani kuhoji iweje leo thamani ya shilingi imeteremka kias hiki, na mengine mengi maana hivo ni vivuli vya maamuzi yao kwenye serikali yao. kwa mtu mwenye kufikiria wangeenda kwenye idara mbalimbali za serikali na ofisi za umma wakafikia kwenye parking za magari nje ya ofisi hizo na kujionea v8 za milion 200 zilizopangana kwenye parking nje ya idara nyingi za serikali ili hali mahospitalin mama zetu wanajifungulia chini na huduma duni kabisa! kwann wasingeandamana kwa kuhoji haya!!!!!
 
Let them try to do it, we will show them how to do it........ma - rope himiza wanao waandamane plz.
 
Huyo aliyetangaza alikuwa anataka kujikomba kwa Kikwete na alikuwa anatumia tumbo katika kufikiria. Lakini wenye akili kidogo wameona kuwa hilo ni bomu ambalo litawalipukia CCM kwani Chadema nao watadai haki ya kufanya maandamano na kutoa shutuma chafu sana dhidi ya Kikwete, Makame, Kiravu, Ikulu na Usalama wa Taifa. Ubaya ni kwamba makada uchwara wa CCM hawajui haki za msingi za raia, kazi za bunge na haki za wabunge katika kuwawakilisha wananchi. Wao wanamchukulia raisi kama mfalme kumbe ni mwajiriwa wa wananchi. Hivyo wanataka watu walambe miguu ya raisi kama wao wanavyolamba. Ukweli ni kuwa raisi ni mwajiriwa wa raia na anawajibika kwao ikiwa ni pamoja na kwa wawakilishi wa raia bungeni. Ningependa kuwashauri makada-njaa kuwa wafunge mikanda yao kwani miaka hii wataenyeshwa ile mbaya na wengi wao watapatilizwa kisiasa katika muenyo huo.
 
UKIONA TWIGA ANAANZA KULA MAJANI YA CHINI UJUE JUU YA MTI KUMETANDA JOKA KUBWA

Nakuambia WANADEMOKRASIA na WANADIPLOMASIA ambao siku zote wana ufuhamu mkubwa na mambo mengi mno duniani, WANAELEWA FIKA MAANA YA UJUMBE waliutuma wana-CHADEMA kule Dodoma. Na kwa kitendo hicho, utawala DHALIMU utaanza kumomonyoka kama nyumba ya karata. Mtu kashikwa pabaya hapa!!!

Itakua ni kosa kubwa CCM kwenda Barabarani kwa siku yoyote ile. Kwani, wakitangulia huko barabarani kwenda kudai HAKI huko, basi ninauhakika kwamba CHADEMA na wale wapiga kura 15 milioni ndio haswa WATAMALIZIA KABISA picha zima. Kamanda Kombe, tayarisha vijana zaidi na barabara zote ziwe wazi kupitika na WADAI HAKI tu.

Ila, kwa UTULIVU mkubwa ambao Wa-Tanzania wameonyesha na kuendelea na michakato mbali mbali za kuleta MABADILIKO ya kweli TAnzania mpaka sasa inatoa TASWIRA zifyatazo:


1. Wameamua kuwapa WALIOWAPOKONYA HAKI yao Adhabu isiyokifani Kisaokolojia akilini. Hii na silaha hatari mno wailoutumia wananchi.


2. Wanatuma pia UJUMBE MZITO kimataifa ya kwamba nyuma ya UKIMYA WAO HUU, licha ya rais kupatikana kwa kura CHINI ya ROBO ya wote waliojiandikisha kufanya hivyo, kwamba Jumuiya ya Kimataifa ITUMIE AKILI kubanini kwamba kuna UDIKTETA wa ajabu uliofichama ndani ya NEMBO ya AMANI tuliyonayo Tanzania kwa miaka mingi sasa LAKINI BILA HAKI YA KUTOFAUTIANA na uongozi kwenye FIKRA na MAONI. Na Kwamba, wengi sasa tu (hadi wa ngazi za Maprofesa) WAMEPOTEZWA KIMYA KIMYA GIZANI kwa kuthubutu kufanya hivyo.


3. Pia, kwa ukimya huu Wa-Tanzania wameamua KUMNYIMA KAKA MBABE fursa ya kutumia DOLA kuwarudi.
 
Hao ndio CCM! Ingelikuwa ni CHADEMA, DP, CUF, NCCR, TLP au UDP ndio wanataka kuandamana ungelisikia kiongzi wa jeshi anasimama kukemea UVUNJIFU WA AMANI :embarrassed: BADALA YA KUANDAMANA CHADEMA WANAANDAMANA CCM.... Aaaaaagh WATANZANIA:pray2:
 
Tatizo la ccm hawataki kusikia ukweli ambao ndo njia pekee inayo kufanya kuheshimika. Wasiache kuandamana afu waone tension watakazo zianzisha zitakavyo watesa kwa kipindi chote.
 
Wangewasha moto mkubwa sana , ambapo kuuzima ingekuwa balaa, yaani kiufupi SISI CHADEMA tungeandamana NCHI NZIMA, na hapo ndo ingekuwa MSHIKEMSHIKE

Ndo manake nchi nzima tunaandamanaaa..Eti mwenyekiti wao kadhalilishwa...hivi CCM ina mwenyekiti??hahaaaa ..yaani hii imewauma CCM mpaka wanataka kutoka roho
 
Kwanza CCM wengi ni wazee, na wajaribu tu waone kama watarudi na meno nyumbani
 
Back
Top Bottom