CCJ waibukia kwa Nyerere

Kulialia mbele ya kaburi la Nyerere may seem like a cheap publicity stunt to some. Lakini it could be taken as a serious gesture of empathy by others.

No doubt to CCJ this is a calculated move to gain political mileage and ultimately votes. These people know their customers. All political parties do what they have to do to beat the competition.

Miaka nenda rudi kila nikiona kwenye kampeni za uchaguzi CCM wakigawa khanga, kapelo, t-shirts, maonyesho ya ndondi, kwaya, taarabu, nk nilikua nadhani hawako makini. Kumbe wao wanajua kile wapigakura wakitanzania wanachotaka.

Asilimia ya wapigakura wa kitanzania wanaotaka kusikia manifesto, sera, mikakati na kuichambua ni ndogo mno. Nadhani hata negligible. Idadi ya wale wanaotaka burudani, mandazi na vitumbua ni kubwa sana.

Hawa jamaa wa CCJ are definitely on to something.
 
Tatizo mwanafalsafa..unazungumza kama unajua kilichowaliza ni nini. Unaona watu wanalia kwenye kabuli unafikiri wanamlilia Nyerere! Hawa nimeanza kuwapenda kwani they are doing all the good things I would have done kama ningeanzisha chama.. Wanajua wanachokitaka, wanafalsafa inayowaongoza na kinyume na wengi wanavyofikiria hawahitaji kigogo kuwa nyuma yao! Ni ajenda inayoelewekak na ambayo wanajua itawavutia Watanzania.

Uongozi ni uwezo mara zote siyo ahadi, siyo kutoa misaada, siyo cheap popularity ni kuweza kuchukua msimamo na watu wakajua msimamo huo. CCJ (SisiJUU).. ni chama ambacho kinafuata hatua zote muhimu za kuongoza mapambano ya kifikra kwenye sanduku la kura..

Nakumbuka kisa cha kuteuliwa kwa Daudi kuwa Mfalme... Alipoenda Nabii Samwel kwenda kuwapaka mafuta watoto wa Yesse. Wakaletwa watoto saba wa kiume (vyama vilivyokomaa na vyenye uzoefu na majina makubwa).. Hadi alipokuwa tayari kumpaka mmoja wao mafuta BWANA akamwambia siyo "HUYU". Kila mmoja aliamini kabisa mfalme atakuwa ni mmoja wa hawa wazoefu na wanaosifiwa kijijini..

Hadi pale Samweli akashangaa mwishoa akamuuliza Yesse "Yesse watoto wako wote ni hawa". Ndipo Yesse kiuvivu akasema "yeah kapo kamoja kanachunga ng'ombe huko sidhani kama hako kanaweza kuwa kafalme". Samweli akamwambie "mlete".

Sasa.. tunaweza kucount watu out kwa sababu they don't fit in our own concept ya nani anaweza kutuongoza. Tunawapima na kuwaangalia majina yao wanajulikana vipi na kwa namna gani na wasiporidhisha tunasema hawa haiwezekani. Tungependa sana atakayetuongoza awe kutoka kwa wale Saba!!

Well.. friends.. Here comes David!

Mzee wa kijijini unataka kutuaminisha hawa jamaa wana kitu? Mbona watu wanakituhumu kwa mengi, cha vigogo, cha Lowassa nk....kama mtu anajua ukweli halisi wa CCJ, tafadhali tujuze. Hata mimi haya majina ya viongozi wao yananingónyesha, hawana profile yeyote. Siamini mtu unaibuka leo, ukafanikiwa kisiasa leo leo.
 
Hawa jamaa wasilete ya Kambona kwamba ana siri za Mwalimu Nyerere kumbe alikuwa hana kitu. Wanatangaza kuna vigogo wa CCM kumbe ni uongo mtupu.

Vigogo wa CCJ wayeyuka
Imeandikwa na Regina Kumba; Tarehe: 22nd March 2010





AHADI ya Chama cha Jamii (CCJ) kuwatangaza vigogo katika uzinduzi wa chama hicho, uligonga mwamba baada ya uzinduzi huo kufanyika jana bila hata kigogo mmoja kutoka Chama cha Mapinduzi (CCM).

Aidha mkutano huo wa uzinduzi uliofanyika makao makuu ya chama hicho yaliyopo Mwananyamala, Dar es Salaam ambapo yalihudhuriwa na watu wachache tofauti na matarajio yao kwamba uzinduzi huo ungehudhuriwa na watu wengi.

Mwenyekiti wa muda wa CCJ, Richard Kiyabo baada ya uzinduzi alipohojiwa na waandishi wa habari kuhusiana na vigogo waliowatangaza kuwa watakuwepo kwenye mkutano huo, alijibu kwamba vigogo kwa tafsiri ya CCJ ni wananchi wapatao milioni 40 wenye uwezo wa kumuweka kiongozi madarakani na kumuondoa wakati wowote.

Aidha alisema pia chama chake kilituma mialiko kwa mabalozi wa nchi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini; lakini hakuna aliyehudhuria hali iliyomfanya akitupie lawama Chama Cha Mapinduzi kuwa kimewazuia mabalozi hao wasihudhurie uzinduzi wa chama hicho.

Kabla Mwenyekiti wa Chama hicho hajazindua chama hicho, Katibu Mkuu Renatus Muabhi alitoa kadi kwa wanachama watano na baada ya hapo alitoa kadi nyingine 13 kiholela bila kuwarekodi wale anaowakabidhi.

Katika hotuba yake Kiyabo alisema CCJ ni chama kinachokusudia kuwafikisha Watanzania pale walipotazamia kufika na kwamba chama hicho sio cha vigogo kama kinavyodaiwa na watu wengi bali ni chama cha wananchi wote.

Pia alisema anataka kuhakikisha Watanzania wote wanakuwa na uwezo wa kula nyama tofauti na sasa inavyodaiwa kuwa wananchi hawapendi nyama wakati wanashindwa kununua kutokana na bei kuwa juu.

CCJ iliahidi kuwa ingewaweka wazi vigogo ambao ilidai wametoka CCM na kujiunga na chama hicho ambacho tayari kimepata usajili wa muda.
 
Nawapenda CCJ, nalipenda tamko lao kuhusu vigogo! Ni ukweli usiopingika vigogo wa nchi hii ni wananchi wanaowapa uongozi wale tunaowaita na kuwatambua kwamba ndio vigogo. Kwa uelewa wangu mdogo ni kwamba CCJ wamefika mahali wameona kwamba hao vigogo ndio walioifikisha nchi hapa ilipo - pabaya. Sasa iko haja ya kufanya mageuzi ili vigogo halisi wa nchi hii wajulikane na watambulike vilivyo kwamba ndio vigogo haswa. Ni darasa la aina yake toka CCJ, ni wenye akili nzuri peke yao ndio watakaoweza kuelewa fundisho hilo toka CCJ.
 
Ndiyo wameibukia Butiama. Nasikitika kuhusu yule mtu aliyepiga busu kaburi la Mwalimu Nyerere. Watu kule wanapaswa kutoa heshima zao bila kubusu kaburi.
 
Back
Top Bottom