CCJ waibukia kwa Nyerere

Tatizo mwanafalsafa..unazungumza kama unajua kilichowaliza ni nini. Unaona watu wanalia kwenye kabuli unafikiri wanamlilia Nyerere! Hawa nimeanza kuwapenda kwani they are doing all the good things I would have done kama ningeanzisha chama.. Wanajua wanachokitaka, wanafalsafa inayowaongoza na kinyume na wengi wanavyofikiria hawahitaji kigogo kuwa nyuma yao! Ni ajenda inayoelewekak na ambayo wanajua itawavutia Watanzania.

Uongozi ni uwezo mara zote siyo ahadi, siyo kutoa misaada, siyo cheap popularity ni kuweza kuchukua msimamo na watu wakajua msimamo huo. CCJ (SisiJUU).. ni chama ambacho kinafuata hatua zote muhimu za kuongoza mapambano ya kifikra kwenye sanduku la kura..

Nakumbuka kisa cha kuteuliwa kwa Daudi kuwa Mfalme... Alipoenda Nabii Samwel kwenda kuwapaka mafuta watoto wa Yesse. Wakaletwa watoto saba wa kiume (vyama vilivyokomaa na vyenye uzoefu na majina makubwa).. Hadi alipokuwa tayari kumpaka mmoja wao mafuta BWANA akamwambia siyo "HUYU". Kila mmoja aliamini kabisa mfalme atakuwa ni mmoja wa hawa wazoefu na wanaosifiwa kijijini..

Hadi pale Samweli akashangaa mwishoa akamuuliza Yesse "Yesse watoto wako wote ni hawa". Ndipo Yesse kiuvivu akasema "yeah kapo kamoja kanachunga ng'ombe huko sidhani kama hako kanaweza kuwa kafalme". Samweli akamwambie "mlete".

Sasa.. tunaweza kucount watu out kwa sababu they don't fit in our own concept ya nani anaweza kutuongoza. Tunawapima na kuwaangalia majina yao wanajulikana vipi na kwa namna gani na wasiporidhisha tunasema hawa haiwezekani. Tungependa sana atakayetuongoza awe kutoka kwa wale Saba!!

Well.. friends.. Here comes David!

Mmh hapa umenoa Mwanakijiji...ndio makuburini?do you think Nyerere anawasikia au anawaunga mkono kwa kuanzisha hicho chama chao..Je is it true kwamba wanadhamira ya dhati na kama ni ndio why now kwani sio mwaka jana,juzi au mwakani?kama wanafuata nyayo za Mwalimu,mbona waanzishaji wenyewe hawajitokezi front?Kwenda kwenye Kaburi la mwalimu ni kujitia mkosi tu...Hivi mfu hasikii mpaka uende kwenye kaburi lake?unawatetea eti uongozi sio cheap popularity hivi kitendo cha kwenda kwenye kaburi la Mwl pamoja na media sio kutafuta cheap popularity?Jipange tena mkuu...ukija na chama chako halafu ukaenda kwenye Kaburi la Mwl nitakucheka sana.Umekosea kabisa kutoa mfano wa Daudi na kisa cha CCJ...hatudanganyiki.
 
yeah, GS nimekukubali sana hapo......... chama gani waanzilishi wake wanjifichaficha............ mara sijui kadi waweke picha ya marehemu.......... sasa wanatoa machozi ya mamba kaburini........ sio washirikina hawa kweli?????.............. hivi hawa wanajua kuwa mabingwa wa maigizo ya kumuenzi mwalimu ni CCM?................

mimi hawa kwanza nilishdoubt busara zao, timming yao imekuwa mbaya sana hadi sasa ni dhahiri kuwa wanatarajia kuhurumiwa tu pale watakapokosa kushiriki uchaguzi mkuu............ subiri uone hata manifesto yao itajaa duplication ya ile ya CCM hawana mawazo mbadala hawa............ hatuoni mikakati......... kugawa kadi ningi sio siasa........... hawa bado sana........ tena nasikia wako na mtu mmoja msanii wa kutupwa anaitwa seneta misele!!!!!!!!!!!! hahaha.......... wanacheza hawa...........

haya sasa watamjua JK na watajua kuwa CCM inajua siasa............... subirini muone.................

to my surprise........... sikuwahi kufikiri kama MM anaweza kuandika yale aliyooandika!!!!!!!!!!!!... nimeshangaa sana...................
 
Tatizo mwanafalsafa..unazungumza kama unajua kilichowaliza ni nini. Unaona watu wanalia kwenye kabuli unafikiri wanamlilia Nyerere! Hawa nimeanza kuwapenda kwani they are doing all the good things I would have done kama ningeanzisha chama.. Wanajua wanachokitaka, wanafalsafa inayowaongoza na kinyume na wengi wanavyofikiria hawahitaji kigogo kuwa nyuma yao! Ni ajenda inayoelewekak na ambayo wanajua itawavutia Watanzania.

Uongozi ni uwezo mara zote siyo ahadi, siyo kutoa misaada, siyo cheap popularity ni kuweza kuchukua msimamo na watu wakajua msimamo huo. CCJ (SisiJUU).. ni chama ambacho kinafuata hatua zote muhimu za kuongoza mapambano ya kifikra kwenye sanduku la kura..

Nakumbuka kisa cha kuteuliwa kwa Daudi kuwa Mfalme... Alipoenda Nabii Samwel kwenda kuwapaka mafuta watoto wa Yesse. Wakaletwa watoto saba wa kiume (vyama vilivyokomaa na vyenye uzoefu na majina makubwa).. Hadi alipokuwa tayari kumpaka mmoja wao mafuta BWANA akamwambia siyo "HUYU". Kila mmoja aliamini kabisa mfalme atakuwa ni mmoja wa hawa wazoefu na wanaosifiwa kijijini..

Hadi pale Samweli akashangaa mwishoa akamuuliza Yesse "Yesse watoto wako wote ni hawa". Ndipo Yesse kiuvivu akasema "yeah kapo kamoja kanachunga ng'ombe huko sidhani kama hako kanaweza kuwa kafalme". Samweli akamwambie "mlete".

Sasa.. tunaweza kucount watu out kwa sababu they don't fit in our own concept ya nani anaweza kutuongoza. Tunawapima na kuwaangalia majina yao wanajulikana vipi na kwa namna gani na wasiporidhisha tunasema hawa haiwezekani. Tungependa sana atakayetuongoza awe kutoka kwa wale Saba!!

Well.. friends.. Here comes David!

mkuu, hapa umeteleza.................. kajipange vizuri........................ sorry.........
 
MMM,

I beg to differ... umeweka hekaya na sijaona tangible potentials au hata basi context ya hawa sisijuu kama ulivyoweka. we dont have a short memory and i remembr very well how you decorated sophia simba and how you lean towards your teams no matter what!!!

we need strategies, background and competency matrix of the leaders, apart from tears and a few demos

MMM, sorry but we need more!
 
mkuu, hapa umeteleza.................. kajipange vizuri........................ sorry.........
mwanakijiji pia ni mtu na kukosea ni sunna!!! labda ana mkono wake... lakini kwa wau wale, with limited profile, hata kwenye ten-cells!!!
 
Mmh hapa umenoa Mwanakijiji...ndio makuburini?do you think Nyerere anawasikia au anawaunga mkono kwa kuanzisha hicho chama chao..Je is it true kwamba wanadhamira ya dhati na kama ni ndio why now kwani sio mwaka jana,juzi au mwakani?

Kila mtu anapanda shamba lake apendavyo; kwanini haikuwa juzi au jana; kwanini haikuwa miaka 20 iliyopita. Vipi labda hawakuwa na mbegu wakati huo, au walikuwa wanasubiri alama za nyakati. Je hawana haki ya kuanzisha chama wakati muafaka wauonao wao au ni lazima waanzishe chama wakati wengine wangependa waanzishe. Walichofanya ni kuonesha uhuru wao wa kuamua kufanya wanachokitaka.

Siasa ni pamoja na timing, CCJ wameonesha timing yao ni nzuri kwa sababu ndiyo chama pekee ambacho kuanzishwa kwake kumewafanya CCM na uongozi wake kutoa maelezo mara kadhaa ya kukikandia, kuanzia Katibu na Msajili mwenyewe wote wanataka watu wapuuzie.. nashangaa kwanini? Kama hiki chama si kitu.. mbona hata Seif wa CUF(chama kikongwe) naye ametoa kauli yake.. wanaogopa nini?

kama wanafuata nyayo za Mwalimu,mbona waanzishaji wenyewe hawajitokezi front?

Tatizo ni kuwa siyo CCJ; tatizo ni watu ambao hawaamini kabisa kuwa wapo Watanzania wenye uwezo wa kufikiri nje ya sanduku walilowekewa. Tangu mwanzo watu wameanza kusema "kuna vigogo nyuma ya CCJ" na watu wanaamini hilo. Kwa sababu tunafikiri kuwa ili kuweza kuongoza mabadiliko tunahitaji majina ya vigogo. As a matter of your information, CCJ itawakataa baadhi ya vigogo ambao watataka kujiunga nao!!

Kwenda kwenye Kaburi la mwalimu ni kujitia mkosi tu...Hivi mfu hasikii mpaka uende kwenye kaburi lake?

Watu wanaenda kwenye sanamu ya Lincoln hapa US na wanatembelea makumbusho ya George Washington! kila siku kwa maelfu! Hakuna kosa kwenda kutembelea kaburi la muasisi wa Tanzania, as a matter of fact hata CUF, CHadema na wengine wangeweza kwenda hata kama hawatalia lakini kuonesha chochote wanachofikiria. CCJ wameonesha hawana wa kumuogopa na hawana haya kuonekana wanatambulishwa na Nyerere.

unawatetea eti uongozi sio cheap popularity hivi kitendo cha kwenda kwenye kaburi la Mwl pamoja na media sio kutafuta cheap popularity?

Of course ni cheap popolarity thats why inaitwa Siasa! Watanzania wanamkumnbuka Baba wa taifa wakati huu, na here comes CCJ na kuwakumbusha.. guess what? CCJ gets points. Simple old fashioned Politics

Jipange tena mkuu...ukija na chama chako halafu ukaenda kwenye Kaburi la Mwl nitakucheka sana.Umekosea kabisa kutoa mfano wa Daudi na kisa cha CCJ...hatudanganyiki.

Well.... at the end historia ndio muamuzi, mtakapoamka itakuwa too late. Too much intellectualizing instead of politicizing!
 
yeah, GS nimekukubali sana hapo......... chama gani waanzilishi wake wanjifichaficha.

Nimeshalijibu hilo! waanzilishi siadi wameonekana kupiga picha, wameenda kuchukua cheti chao na mtawaona wakirudisha na kupata usajili wa kudumu. Nyie mtakaa kusubiri "vigogo".. hawapo! CCJ ni chama cha Watanzania chenye lengo la kuirudisha nchi mikononi mwa Watanzania kwa misingi ya itikadi na mafundisho ya Nmwalimu Nyerere na waasisi wa awali wa Taifa letu.

.......... mara sijui kadi waweke picha ya marehemu.......... sasa wanatoa machozi ya mamba kaburini........ sio washirikina hawa kweli?????.............. hivi hawa wanajua kuwa mabingwa wa maigizo ya kumuenzi mwalimu ni CCM?................

Well.. kama chama hakina cha kuusimamia, chama hufuata upepo. CCJ wameamua kumsimamia Nyerere, na watavaa tisheni za Nyerere, kuimba nyimbo na kutukuza uongozi wake pasipo haya au kuomba kibali. Vyama vingine ambavyo havitaki kumuenzi Nyerere vifanye hivyo kwa maangamizi yao wenyewe. Usanii wa CCM juu ya Nyerere ni furaha ya CCJ kwani mwanga na nuru havifanani.

mimi hawa kwanza nilishdoubt busara zao, timming yao imekuwa mbaya sana hadi sasa ni dhahiri kuwa wanatarajia kuhurumiwa tu pale watakapokosa kushiriki uchaguzi mkuu............ subiri uone hata manifesto yao itajaa duplication ya ile ya CCM hawana mawazo mbadala hawa............ hatuoni mikakati......... kugawa kadi ningi sio siasa........... hawa bado sana........ tena nasikia wako na mtu mmoja msanii wa kutupwa anaitwa seneta misele!!!!!!!!!!!! hahaha.......... wanacheza hawa...........

If I were you.. I will not count them out! na hiyo manifesto.. it'll be the most exciting document ya uchaguzi kuliko the combined manifestos all other parties.

haya sasa watamjua JK na watajua kuwa CCM inajua siasa............... subirini muone.................

siyo JK wala CCM wanaoweza kukizuia kwa sababu hakuna kitu kizuri kama kuwa underdog.. hakuna kitu kizuri kama kuonekana ni mpuuzi na kuwa ni chama ovyo.. wakati wao CCM na wengine wanakipuuzia.. CCJ inazidi kujijenga..

to my surprise........... sikuwahi kufikiri kama MM anaweza kuandika yale aliyooandika!!!!!!!!!!!!... nimeshangaa sana...................
l

well.. usije kujikuta unakosa uwezo wa kushangaa zaidi..
 
AIFANANISHA NA WINGU ZITO LINALOPITA

Elias Msuya

KATIBU Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Seif Sharif Hamad, amekiponda Chama cha Jamii (CCJ) akisema siyo tishio kwa chama chake wala kwa kambi ya upinzani nchini na ni sawa na wingu linalopita.

Maalim Seif ametoa kauli hiyo jana katika mahojiano maalum na Mwananchi jijini Dar es Salaam, ambapo pia alielezea hali ya vyama vya upinzani nchini ikiwa ni mahojiano yake ya kwanza tangu atoke hospitalini alikokuwa amelazwa hivi karibuni.

Hii ni mara ya kwanza kwa Maalim Seif kujitokeza kuzungumzia masuala ya kitaifa tangu akumbwe na maradhi ya mkamba (bronchitis) Machi 5, mwaka huu akiwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Dar es salaam akijiandaa kusafiri kwenda Muscat, Oman ambapo alilazwa Hospitali ya Hindu Mandal na akaruhusiwa Machi 11.

Kulazwa kwa Maalim Seif, kulizua hofu kubwa kwa baadhi ya watu baada ya kuenezwa kwa uvumi kuwa kiongozi huyo wa upinzani alikuwa amekufa, ambazo hazikuwa na kweli.

Sioni kama chama hicho ni tishio kwa chama chetu, (ni kama wingu). Hata viongozi wake walikuwa hawajulikani, alisema Maalim Seif na kuongeza:

Ni chama ambacho kimekuzwa tu na vyombo vya habari, kwakuwa kilijitangaza kuwa kitazoa (vigogo) wa CCM ambao hata hivyo wameshakiruka. Ndiyo, watapata wanachama kwa kipindi hiki lakini, hakitafika mbaliâ

CCJ yenyewe imekuwa ikikanusha kuhusishwa na vigogo wa CCM, lakini haijaweza kutuliza habari zinazokihusisha chama hicho na makada wa chama hicho tawala. Tayari vigogo kadhaa wameshakanusha habari za kuhusishwa kwao na CCJ, akiwemo Spika Samuel Sitta, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere, Joseph Butiku, mawaziri wakuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba na John Malecela.

Kwa sasa CCJ ina usajili wa muda ilioupata Machi 2 na inahaha kusaka angalau wanachama 2,000 kutoka Bara na Visiwani katika kipindi cha miezi sita ili kiweze kupata usajili kamili. Lakini katika muda mfupi, chama hicho kimeshatangaza kuwa kimevuna wanachama 7,700 katika mikoa 11.

Akizungumzia maridhiano yaliyofikiwa kati ya chama chake (CUF) na CCM mwishoni mwa mwaka jana, Maalim Seif alitetea uamuzi wake wa kumuunga mkono Rais Karume akisema: “Sitishiki kubadili msimamo wangu na kumuunga mkono Rais Karume. Hapo ndipo tulipotaka tufikie.Politics is not staticâ (siasa siyo mawazo mgando), hatuwezi kushikilia misimamo hiyo hiyo muda mrefu, lazima tufikie makubaliano ya amani.

Hata hivyo, Maalim Seif aligoma kuweka bayana nini walichozungumza baina yake na Rais Karume katika vikao vyao hivyo vilivyokuwa vya faragha.

Kuhusu Serikali ya umoja wa kitaifa itakayoundwa baadaye mwaka huu visiwani Zanzibar, Maalim Seif alisema serikali hiyo itakuwa ni endelevu tofauti na serikali za makubaliano yaliyofikiwa nchini Kenya na Zimbabwe.

Tuangalie mazingira ya kila nchi, Kenya na Zimbabwe zilifikia makubaliano ya serikiali ya umoja wa Kitaifa kutokana na shinikizo la Kimataifa. Kofi Annan alihamia Kenya, hata Rais Kikwete alikwenda huko lakini, Zanzibar ni tofauti. Wazanzibar wenyewe bila (shinikizo) lolote wameamua. Hata Rais Karume na mimi tulikutana bila yoyote kutoka nje, hivyo serikali hiyo haitakuwa na migogoro tena,alisema.

Alisema kuwa Rais Karume ameonyesha nia njema katika maridhiano hivyo hatarajii kuona tena malumbano yaliyokuwepo awali.

Akizungumzia maandalizi ya uchaguzi mkuu wa mwaka huu, Maalim Seif alisema kuwa CUF imejipanga vizuri na kwamba yeye mwenyewe atagombea kiti cha urais Zanzibar.

“Mimi nilishasema tangu zamani kuwa nitagombea urais. Ni kweli chama kitakaa na kutoa fomu za wagombea lakini, mimi nimeonyesha nia yangu ya kuendelea kugombea.

Tumejipanga vizuri hata upande wa bara, kuhakikisha kwamba hata ikiwa hatupati rais basi tunakuwa na nguvu bungeni,alisema Seif ambaye amekuwa akigombea urais wa Zanzibar tangu uchaguzi mkuu wa kwanza mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1995.

Kuhusu uandikishaji wa wapiga kura visiwani Zanziba, kiongozi huyo wa chama kikuu cha upinzani alionyesha kutokuwa na wasiwasi na kauli za Rais Aman Karume licha ya kasoro zinazojitokeza.

Uandikishaji umerudia mara ya pili, 'ile spirit' (roho) ya maridhiano bado iko on 'trek' (mbioni), hivyo sina shaka na Rais Karume kwa sababu ameshatoa maagizo kwa watendaji wake kuwa kila mwenye sifa ya kuandikishwa aandikishwe.

Lakini, baadhi ya watendaji hao, ama kwa makusudi au 'inefficiency' wamekuwa wakiwabagua wanachama wetu. Kwa mfano Nungwi kuna wanachama 866 hawakuandikishwa kwa sababu ya kutokuwa na vitambulisho, Konde nako kuna wanachama wetu 427. Bado tunafanya tathmini.

Tunaamini kauli ya Rais Karume kwa sababu alishasema kuwa kama watu hawakuandikishwa hakutakuwa na uchaguzi,alisema Maalim Seif.

http://www.mwananchi.co.tz/newsrids.asp?id=18625
 
Watu wanaenda kwenye sanamu ya Lincoln hapa US na wanatembelea makumbusho ya George Washington! kila siku kwa maelfu! Hakuna kosa kwenda kutembelea kaburi la muasisi wa Tanzania, as a matter of fact hata CUF, CHadema na wengine wangeweza kwenda hata kama hawatalia lakini kuonesha chochote wanachofikiria. CCJ wameonesha hawana wa kumuogopa na hawana haya kuonekana wanatambulishwa na Nyerere.

agreed, lakini sio kulialia na kuabudu kaburi, kulipigia magoti etc. hii ni cheap popularity na we have had enough in the past few decades!!! We need brave hearts kama Kagame

Kwa mwendo huu wa machozi, watalia sana hadi mwisho wa october... maana vya kulilia viko vingi mno
albinos
EPA
madini
matumizi makubwa ya serikali
usimamizi mbovu wa maendeleo kwenye halmashauri
dominance ya donors kenye plans zetu
barabara feki
bidhaa feki
viongozi feki
na kulialia feki!!
 
agreed, lakini sio kulialia na kuabudu kaburi,

kweli unaamini walikuwa wanaabudu kaburi? maana unachosema ni imani tu.

kulipigia magoti etc. hii ni cheap popularity na we have had enough in the past few decades!!! We need brave hearts kama Kagame

Ukimuuliza Kagame shujaa wake ni Nyerere, the same goes with Museveni!

Kwa mwendo huu wa machozi, watalia sana hadi mwisho wa october... maana vya kulilia viko vingi mno
albinos
EPA
madini
matumizi makubwa ya serikali
usimamizi mbovu wa maendeleo kwenye halmashauri
dominance ya donors kenye plans zetu

Angalia wao wanalia kuliko hawa wanaocheka cheka!
 
kweli unaamini walikuwa wanaabudu kaburi? maana unachosema ni imani tu.

as far as i am concerned, hakuna wanachofanya pale zaidi ya kuabudu.. walishafanya hata CCM wakaenda pale, wakachangamsha mji na kuondoka patupu! Kumbuka si gestures au maneno, ni matendo

Ukimuuliza Kagame shujaa wake ni Nyerere, the same goes with Museveni!
agreed completely, lakini wao walienda na kuyafanya waliyoyaamini kwa vitendo na si kulialia. BTW, Kagame alishawahi kumtukana nyerer hadharani kuhusu failures zake, unakumbuka?

Angalia wao wanalia kuliko hawa wanaocheka cheka!
I am focused on hao wanaolialia, with fake faces... at least wanaocheka tumeshajua ni watu wa namna gani,
 
as far as i am concerned, hakuna wanachofanya pale zaidi ya kuabudu.. walishafanya hata CCM wakaenda pale, wakachangamsha mji na kuondoka patupu! Kumbuka si gestures au maneno, ni matendo

Matendo si ndiyo hayo; wameenda na kuanzisha chama, wanapita na kupata wanachama na wakipata usajili wa kudumu wataandika katiba yao ya kudumu na baadaye ilani yao ya Uchaguzi.

agreed completely, lakini wao walienda na kuyafanya waliyoyaamini kwa vitendo na si kulialia. BTW, Kagame alishawahi kumtukana nyerer hadharani kuhusu failures zake, unakumbuka?

Mbona unafanya big deal kulia? Kulia ni hisia ya mwanadamu na hakuna (siyo wewe wala mimi) ambaye anaweza kumuamulia mtu mwingine atoe machozi wakati gani, wapi, na kwa sababu gani. Wapo wengine wakiikosa JF wanajisikia kulia (au kulia lia kwa maneno yako); na wapo wengine wakiambiwa wanapendwa donge linakwama shingoni. Hilo la Kagame sijui ni wapi maana ni yeye juzi juzi tu hapa ameomba tuende kumuanzishia JKT ili kuwa intergrate vijana wa Rwanda, kitu ambacho sisi tulikifanya Kenya hawakukifanya wala Zimbabwe! JKT tunaambiwa ilikuwa ni failure (kwa sababu JKT imetokana na Azimio vile vile)!

I am focused on hao wanaolialia, with fake faces... at least wanaocheka tumeshajua ni watu wa namna gani,

Hujui fake faces zao; huna msingi wa kudai hilo isipokuwa hisia zako tu. Why are they fake compared to CCM, Chadema CUF, TLP au any other party? Unataka tuamini kuwa vyama hivi vingine ndiyo "real"?
 
Makucha ya CCJ hadharani leo - gazeti la Mwananchi

CHAMA cha Jamii (CCJ) leo kinaanza kuonyesha hadharani ubavu wake kitakapofanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara, jijini Dar es Salaam, kikiwa kimealika vigogo wa CCM kushuhudia.

Katibu Mwenezi wa CCJ, Dickson Ng'hily alitamba kuwa uzinduzi huo utatia fora na kuonyesha jinsi chama hicho kinachotafuta usajili wa kudumu kwa udi na uvumba, kilivyojiandaa kuichukua nchi.
Akionekana kujiamini, alisema katika uzinduzi huo ambao utafanyika Mwananyamala 'A', amewaalika vigogo wa CCM kushuhudia.

"Tumevialika vyama vyote vya siasa... CCM tumemwaliki mwenyekiti (Rais Jakaya Kikwete), Katibu Mkuu Yusuf Makamba na mweka hazina wao," alisema Ngihily.

Mbali na wanasiasa hao, Ng'hily alisema amemwalika Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa ili ashuhudie wakitangaza kujikusanyia zaidi ya wanachama 7,000.

Lengo la bashasha hizo, alisema, ni kuudhihirishia umma uwezo wa CCJ ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasilisha majina ya wanachama wake kwa msajili.

"Kesho tutampelekea Mheshimiwa Tendwa majina ya wanaotuunga mkono ili kukamilisha taratibu za kupata usajili wa kudumu," alisema Ng'hily akidai lengo la chama hicho ni kuwahi kushiriki uchaguzi ujao.

Kwa CCM inavyohangaika, kwa serikali inavyohangaika, kwa Tendwa anavyohangaika na sasa hata Hamad naye anavyoanza kuhangaika, mmh yangu macho. Walituma maombi kwa Tenda, wakapata usajili wa muda baada ya wiki tatu na sasa Jumatatu watatinga kwa Tenda kwa usajili wa kudumu, mmh CCJ wameweza kuweka indiketa ingawaje wanakoelekea bado sikujui. Lakini kwa kasi ya mwendo wao wa Tsunami, ni heri kuwapisha kwani ni hatari kujaribu kuwazuia, waweza kujikuta unazolewa na maji au unageuzwa hasusa. Si ajabu kuna waheshimiwa wakabwaga manyanga kwa hofu.
 
Mag3 ndiyo maana nimewaambia watu hapo juu kuwa hakuna chama chenye bahati kama CCJ, kwanza kinapata matangazo ya bure (yaani CCM wametoa tamko, Chadema wametoa tamko, TLP na CUF), zaidi ya yote, wachunguzi na magazeti yamekitangaza bure kabisa, tungeweka kwenye gharama ya fedha, matangazo ya TV, Radio na magazeti ambayo CCJ imepata bure yangefikia mamilioni ya hela ya madafu!

Sasa mwananchi wa kawaida kwa kweli hajali hoja za kisomi za "why now, why CCJ, who is behind bla bla" mwananchi anaona mbona hiki chama kinawasumbua wakubwa, there has to be something. Halafu jamaa kuwaudhi wanaenda hadi kwenye kaburi la mwalimu, wanaoneshwa kuguswa na kumkumbuka muasisi wa taifa lao wanaapa kuwa ajenda yao ni kusafisha ufisadi n.k mwananchi wa kawaida anaona "hiki ndio chama".

Utaoan kuwa CCJ hawajaja na takwimu za matatizo yetu au kutangaza juu ya orodha mpya ya ufisadi!

Angalia wanatangaza hivi juu ya lengo la kuundwa kwao:
SISI WANANCHI WAZALENDO tuliokutana hii leo tarehe ... ... ... jijini Dar es Salaam kutekeleza wajibu wetu Kikatiba wa kuunganisha pamoja mawazo yetu na kuunda chama cha siasa kinachozingatia changamoto zote zinazoikabili nchi yetu tangu baada ya uhuru na kichachobeba matarajio ya wananchi ya leo na kesho, kwa jina la CHAMA CHA JAMII, kwa kifupi CCJ, ambacho lengo lake kuu ni kuleta mageuzi ya kitaifa ya kidemokrasia, kiuchumi, kijamii na kisiasa kwa faida yetu sote sasa na ya vizazi vijavyo.

Wanafikia lengo hilo kwa sababu kadhaa baadhi ni kuwa:

KWA KUWA matumizi bora na endelevu ya utajiri wa rasilimali yanawezekana tu katika Taifa ambalo lina uongozi wenye uchungu na nchi na unaozingatia maadili kama yalivyoainishwa na kusimamiwa kidete na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere; Taifa ambalo linawaandaa vijana wake vizuri kielimu na kimaadili; ambalo wanawake wana fursa sawa na wanaume; na ambalo mchango wa kila raia awe kijana, mzee, mlemavu n.k unatambuliwa na kuthaminiwa; na

na kuwa

Kwa kuwa adui mkubwa wa haki na maendeleo ni UFISADI, yaani rushwa, ubadhirifu wa mali ya umma na uporaji wa rasilmali za Taifa, adui ambaye hana budi kupigwa vita kwa nguvu zote

Yaani hilo limo kwenye Katiba yao! siyo CCM wala chama kingine cha ajenda hii kwenye Katiba yake!

Na angalia malengo yake:

[FONT=Comic Sans MS, cursive]IMANI, MALENGO NA MADHUMUNI[/FONT]

  1. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Chama Cha Jamii kinaamini kwamba:[/FONT]

      1. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Binadamu wote huzaliwa huru, na wote ni sawa;[/FONT]
      2. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa na kuthaminiwa utu wake;[/FONT]
      3. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Hifadhi na ustawi wa jamii yetu vitapatikana kwa matumizi bora na endelevu ya utajiri wa rasilimali tulizonazo, serikali kuwajibika kwa wananchi ambao ni msingi wa mamlaka yote katika nchi, na kupiga vita ufisadi kwa nguvu zetu zote;[/FONT]
      4. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Umoja ni nguvu ya pekee ya wananchi katika kujenga jamii yenye usawa na uhuru na katika kuondoa umaskini, ujinga, maradhi na kupambana na ufisadi.[/FONT]

  1. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Malengo na Madhumuni ya Chama:[/FONT]

  • [FONT=Comic Sans MS, cursive]Malengo na Madhumuni ya CCJ yatakuwa kama ifuatavyo:-[/FONT]

      1. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kuhakikisha kwamba utajiri wa rasilimali tulizonazo unatumika kwa maendeleo ya wananchi kwa kuondoa umaskini, ujinga, na maradhi;[/FONT]
      2. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kuhakikisha kwamba uwekezaji unatekelezwa kwa kumnufaisha mwananchi kutokana na rasilimali alizonazo na zinazomzunguka na kamwe usitoe fursa kwa wageni kuhodhi rasilimali hizo bila ushiriki wa wananchi. [/FONT]
      3. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kuhakikisha kwamba shughuli za uchumi haziruhusu ulimbikizaji wa mali au njia kuu za uchumi katika mamlaka ya watu wachache binafsi;[/FONT]

      1. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kujenga umoja wa kitaifa kwa kutoa fursa sawa na za kutosha kwa wananchi wote wake kwa waume bila kujali rangi, kabila, dini au hali ya mtu;[/FONT]
      2. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kuhakikisha kwamba aina zote za dhuluma, vitisho, ubaguzi, uonevu, rushwa au ufisadi zinatokomezwa nchini; [/FONT]
      3. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kuhifadhi na kuendeleza mazingira kwa ajili ya uhai na afya ya binadamu na viumbe vingine na kwa faida ya vizazi vijavyo ;[/FONT]
      4. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kulinda haki ya kila raia ya kujielimisha au kutafuta elimu katika fani anayopenda hadi kufikia upeo wowote.[/FONT]
      5. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kuhakikisha kuwa mfumo wetu wa uchaguzi ni huru na unaotoa fursa stahili kwa wananchi kuchagua viongozi wanaowataka bila kurubuniwa kwa rushwa na takrima za aina yote yote ile;[/FONT]
      6. [FONT=Comic Sans MS, cursive]Kudumisha maadili ya uongozi (uadilifu, uwajibikaji kwa wananchi na kutenda haki) katika chama na serikali kama yalivyoainishwa na kusimamiwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika uongozi wake kitaifa uliotukuka.[/FONT]

      • [FONT=Comic Sans MS, cursive](10) Kushinda katika chaguzi zote zinazofanyika nchini kwa kutumia ushawishi wa nguvu ya hoja na kuunda Serikali Kuu na Serikali za Mitaa katika pande zote mbili za Muungano ili kuiwezesha CCJ kutafsiri malengo na madhumuni yake kama yalivyoainishwa kwenye ibara hii kwa vitendo[/FONT]

sasa ni mtu gani wa kawaida akisoma hayo ambaye hatovutiwa? Je tunaweza kuona kwanini vyama vingine vinakiogopa chama ambacho kimechelewa kuanza?
 
Binadamu wote tumeumbwa na feeling na tuna emotion hiv yo tuna react hajalishi wewe ni kamanda au ni infantry. Na wakipata hasira zitawajengea feeling ya kuwafanay wawe na uchungu na kuwa focused zaidi. Mimi nadhani ni jambo zuri kuwa wameenda kujazwa hasira Butiama. Hakuna aliyepata picha ya mkutano wao wa hadhara???
you are wrong..atadanganya watanzania wsio na upeo.
kama kulia, kuna mambo mengi ya kuliza watu na yanayotia uchungu kuliko tukio la kuweka maua kwenye kaburi la hayati mwalimu.
nawapa pongezi hawa CCJ kwa usanii,kwani nina hakika watapata watu
 
Hujui fake faces zao; huna msingi wa kudai hilo isipokuwa hisia zako tu. Why are they fake compared to CCM, Chadema CUF, TLP au any other party? Unataka tuamini kuwa vyama hivi vingine ndiyo "real"?
I understand unachotaka niamini... kamwe sitafagilia chama simply kimekuja wakati wa uchaguzi... i wont, and you know what? ni chama kilichokuja kulamba mabaki ya wanamchujo wa vyama vingine na kuwasimamisha, ni chama chenye tamaa ya kura na si vingivevyo. let me tell you some mkuu, kuandika sera na mikakati ni rahisi sana, kutumia tool kufanikisha sera ni kazi ngumu kiasi, kutafsiri sera na mikakati ni kazi zaidi, na kusustain maazimio ndio ngumu kabisaaaa!!! you cant come in six months expecting to change something that is 45 years and still in the making

nafananisha na kiwavi, kiumbe anayekuja baada ya watu kupanda na kupalilia, nafananisha na nzige, nafananisha na mende nk. Yes kimepata freerides kutokana na publicity ya vyama vilivyopo sasa, and you know why? because we have lots of fake people in politics, we have boot lickers, and butt lickers, let alone buddy lickers!!

Do you know who gave CCJ platform ya kupata hiyo acknowledgment from other parties? Yes, ni media, ni lobbyists etc... Should we go further?? probably next time maana kuna zile funds za good governance ambazo baadhi yetu tunazifaidi tukidhani tunajenga kumbe ni divide and rule... ONE DAY YOU WILL UNDERSTAND, OR MAYBE YOU KNOW EXACTLY WHAT I MEAN,

Let me tell you some mkuu, i am not against CCJ, but i am against their cheap politics.. na kulialia is what i recall about CCJ, do you know the reason?? its the first image from CCJ that caught my eyes!!
 
Duh Hawa jamaaa wapo nyuma kweli.......... Yani ndo wanagundua hilo leo au ndo publicity??? :((

wewe ambaye uko mbele nini umegundua na kuwa kwako mbele?nyie ndio mnaoshinda humu JF kupiga makelele bali hujui kwa nini uko humu na kwa nini unachangia...think first!!
 
I understand unachotaka niamini... kamwe sitafagilia chama simply kimekuja wakati wa uchaguzi... i wont, and you know what? ni chama kilichokuja kulamba mabaki ya wanamchujo wa vyama vingine na kuwasimamisha, ni chama chenye tamaa ya kura na si vingivevyo. let me tell you some mkuu, kuandika sera na mikakati ni rahisi sana, kutumia tool kufanikisha sera ni kazi ngumu kiasi, kutafsiri sera na mikakati ni kazi zaidi, na kusustain maazimio ndio ngumu kabisaaaa!!! you cant come in six months expecting to change something that is 45 years and still in the making

nafananisha na kiwavi, kiumbe anayekuja baada ya watu kupanda na kupalilia, nafananisha na nzige, nafananisha na mende nk. Yes kimepata freerides kutokana na publicity ya vyama vilivyopo sasa, and you know why? because we have lots of fake people in politics, we have boot lickers, and butt lickers, let alone buddy lickers!!

Do you know who gave CCJ platform ya kupata hiyo acknowledgment from other parties? Yes, ni media, ni lobbyists etc... Should we go further?? probably next time maana kuna zile funds za good governance ambazo baadhi yetu tunazifaidi tukidhani tunajenga kumbe ni divide and rule... ONE DAY YOU WILL UNDERSTAND, OR MAYBE YOU KNOW EXACTLY WHAT I MEAN,

Let me tell you some mkuu, i am not against CCJ, but i am against their cheap politics.. na kulialia is what i recall about CCJ, do you know the reason?? its the first image from CCJ that caught my eyes!!

kwani lazima ujiunge na CCJ.si ubaki huko huko CCM kwani nani anataka uingie CCJ?hatutaki wanachama kama wewe..kaa huku huko uliko
 
kigogo, i am not for any party, i am for tanzania... I expected alot kutoka ccj lakini hadi sasa nasubiri. remember the best thing to do tanzania now is to address our needs and not to get more political. Na ujue kw si lazima kuwa mwanachama fulani ndo uipende nchi
 
broken-heart.jpg

Leon Bahati

CHAMA cha Jamii (CCJ) leo kinaanza kuonyesha hadharani ubavu wake kitakapofanya mkutano wake wa kwanza wa hadhara, jijini Dar es Salaam, kikiwa kimealika vigogo wa CCM kushuhudia.

Katibu Mwenezi wa CCJ, Dickson Ng'hily alitamba kuwa uzinduzi huo utatia fora na kuonyesha jinsi chama hicho kinachotafuta usajili wa kudumu kwa udi na uvumba, kilivyojiandaa kuichukua nchi.
Akionekana kujiamini, alisema katika uzinduzi huo ambao utafanyika Mwananyamala 'A', amewaalika vigogo wa CCM kushuhudia.

"Tumevialika vyama vyote vya siasa... CCM tumemwaliki mwenyekiti (Rais Jakaya Kikwete), Katibu Mkuu Yusuf Makamba na mweka hazina wao," alisema Ngihily.

Mbali na wanasiasa hao, Ng'hily alisema amemwalika Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa ili ashuhudie wakitangaza kujikusanyia zaidi ya wanachama 7,000.

Lengo la bashasha hizo, alisema, ni kuudhihirishia umma uwezo wa CCJ ikiwa ni siku moja kabla ya kuwasilisha majina ya wanachama wake kwa msajili. "Kesho tutampelekea Mheshimiwa Tendwa majina ya wanaotuunga mkono ili kukamilisha taratibu za kupata usajili wa kudumu," alisema Ng'hily akidai lengo la chama hicho ni kuwahi kushiriki uchaguzi ujao.
 
Back
Top Bottom