Cameron threat to withhold UK aid to anti-gay nations ........ WATANZANI MPOO

TANZANIA imetoa msimamo kuwa haiko tayari kuhalalisha vitendo vya kishoga kwa vigezo vya kupata misaada ya maendeleo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe alitoa msimamo huo leo Jijini Dar es Salaam akisema huko ni kwenda kinyume na sheria na utamaduni wa nchi yetu inayotambua ndoa ya mme na mke kama kiini cha familia. Alitoa msimamo huo kufuatia kauli ya Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron kuwa wana mpango wa kusitisha misaada kwa nchi ambazo katiba na sheria zake hazitambui mashoga na ndoa zao. "Nchi yetu inaheshimu sheria na utamaduni wake hivyo hatupo tayari nchi nyingine kutuwekea masharti kama hayo ya kuwa na uhusiano wa jinsi moja, hili ni tamko hatarishi linaloweza kuvunja uhusiano na nje", Waziri Membe aliwaambia waandishi wa habari.
 
Back
Top Bottom