Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 6,422
- 8,918
Baada ya kumsikiliza Bw. Lowasa (Waziri mkuu aliyepita) kwenye kipindi cha dakika 45 ITV kwa makini sana ninaweza kusema kwamba sijawahi tangu ufwatiliaji wangu wa siasa za hapa kwetu kusikia kiongozi akiongea mambo ambayo yamenigusa kama Bw. Lowasa.
Kwangu mimi ameonekana kama mtu anayeelewa ni nini hasa tatizo letu na kwa nini hatutoki hapa tulipo kwa mfano moja ya vitu alivyonigusa ni pale kwenye Mafuta, anasema kwamba ni lazima tununue mafuta kwa wingi PALE AMBAPO BEI YA MAFUTA INAPOKUWA CHINI (soko la Dunia) ili kuweza kufidia kwa wakati inapopanda, hiyo kwangu mimi ni reasoning ya hali ya juu na ninalazimika kusema sijawahi kusikia kiongozi wa Tz akiweza kuongea na kutoa reasoning kama hiyo, kingine ni kuhusu uwiano wa ukuaji wa Uchumi na mabadilko ya maisha ya mwananchi wa kawaida (trickle down effect) ameweza kuelezea nini kifanyike ili ukuaji wa uchumi uweze kumfikia mwananchi wa chini, hakuna kiongozi wa Tanzania niliwahi kumsikia akiongelea nini kifanyike kutatua matatizo wote wengine nawasikia ni kulialia tu na kulalamika bila kutoa au kushauri nini kifanyike!
Hivyo kwangu mimi pamoja na kusikia yote kuhusu huyu Bw. Lowasa ikiwemo tuhuma za mambo mbalimbali nafikiri ni mtu ambaye tukimtumia vizuri kwa njia yoyote ile, hata kwa usahuri tu, tunaweza kupata kitu!