Elections 2010 BUNGENI: Upinzani upo ndani ya kambi ya upinzani?

"Tuna asilimia 12.5 ya wabunge na hiyo inatupa nafasi ya kuunda kambi ya upinzani bungeni," alisema Mrema. Sasa swali sijui hawakujua kuwa asilimia 12.5 zao zingeweza kuwafanya washinde uspika? na hata wale CCM waliokuwa hawakufurahishwa na Anna Makinda kugombea waliona uroho wa chadema wa madaraka wakaona hawa wameshachuku KUB wakichukua na Uspika itakuwa balaa nadhani Chadema ni chama kinachoshabikia suala la uditekta wenye upeo wale ma great thinkers changieni bila unazi wa vyama.

what a crap!!!!!
 
CUF imeshachakachuliwa na CCM. Hao TLP, NCCR na UDP wamebaki majina tu na baadhi ya watu. Lakini sio vyama vyenye ushawishi tena Tanzania. Chadema wao wakaze buti wasiyumbushwe na hao wanaojitenga kwa sababu watajipendekeza wakiona mafanikio ya CHADEMA. Kwa sasa tuseme kwamba hao wameshanunuliwa na mafisadi ili kuigawa kambi ya upinzani. "They played very smart those shameful guys"
 
:A S-cry: Inatia uchungu mwanzoni unapogundua kuwa upo pekee yako wkt ulizani mpo wengi..... lakini bdae inabidi kuwa jasiri....nna hakika CHADEMA ndicho chama cha ushindani pekee. inachotakiwa kufanya ni kujipanga kufanya operation :horn:nyingi ktk kanda zote hasa vijijini, mjini wameshaiva kinamna bila CUF:blabla: CHADEMA inaweza.songa mbele:hungry::hungry::hungry::hungry::hungry:
 
CUF imeshachakachuliwa na CCM. Hao TLP, NCCR na UDP wamebaki majina tu na baadhi ya watu. Lakini sio vyama vyenye ushawishi tena Tanzania. Chadema wao wakaze buti wasiyumbushwe na hao wanaojitenga kwa sababu watajipendekeza wakiona mafanikio ya CHADEMA. Kwa sasa tuseme kwamba hao wameshanunuliwa na mafisadi ili kuigawa kambi ya upinzani. "They played very smart those shameful guys"

nafikiri hata zitto atakuwa anajilaumu sana kwa namna alivyowasupport nccr huko kigoma.
 
mwenzetu SLAA na Freeman na wale tulio wapinzani, ni vuzuri ukamjua mchumba asiyekufaa kuliko kufunga ndoa ukajagundua baadaye kuwa una mwenza asiyekufaa!
CHADEMA MMESOMA ALAMA NGAPI HAPO KWENYE RESULTS?
MIMI NA UJINGA WANGU:NIMEONA HATUNA MSHIRIKA TOKA UPINZANI NA TENA NI KIPINDI CHA KUTULIA VITA NDIYO IMEANZA NA SISI TUSIMAME WENYEWE,TUJENGE CHAMA WENYEWE NA KUITAFUTA 2015 KIMKAKATI KULIKO KAWAIDA!HATA KUMCHUKUA MTU ALIYETOKA CHAMA KINGINE TUWE MAKINI,TUWE STRATEGIC NA WENGINE TUWAKATAE!
 
cuf walishalishwa mlungula wa muafaka wa zenji nivyo usitarajie upinzani wa kweli
 
Yaliyotokea ni haya hapa:

Kutoka ndani ya uvungu wao...
Walikaa Chadema na CUF ili waone wataingiaje Bungeni. Kabla ya Uchaguzi wa Spika, Hamad Rashid alitaka kugombea Uspika, Chadema wakamwambia hapana wacha Agombee huyu Mwanasheria, wewe utarudi katika kambi ya upinzani kwa cheo chako kile cha awali, na kwa kufanya hivyo tutagawana madaraka. Hamad akawakubalia na kuondoa azma yake ya kugombea U-Spika alipofanya hivyo, Zito akaibuka na kusema Wataunda kambi Chadema peke yake bila kushirikisha vyama vingine. hilo nalo. Hapo ndipo Marando alipozikosa kura ambazo zingemvusha kwenye Uspika. Na hii imefanyika kutokana na ufinyu wa fikra (kama sio viongozi waandamizi wa Chadema kupewa chochote toka CCM) wakidhani kwamba umaarufu unatokana na kuongoza kambi ya upinzani bungeni bila kuwa na ushirikiano kutoka vyama vingine. Walichokisahau Chadema ni kuwa CUF walijaribu kutoshirikisha vyama vingine awali na kisha wakajirekebisha, na hapo wasiomjua Slaa ndipo walipomtambua. Ila kwa kwa hili la ubinafsi wa CHADEMA wameumaliza UPINZANI Tanzania. Tutafute kaburi tuuzike...

Tusubiri kuundwa kwa chama kipya kisicho na damu ya U-CCM-CCM.:sad:

Nawasilisha.
 
Mh. Zitto Kabwe ameoeleza vizuri sana leo asubuhi akiwa Star TV kwamba jana mh. Mbowe alifanya mazungumzo na CUF kwamba milango ipo wazi kuunda upinzani kwa pamoja. Aidha Mh. Zitto amesema yeye binafsi yupo tayari kuachia Cheo cha Naibu kiongozi wa upinzani kwa CUF wakikubali kuungana. Kama hivi ndivyo nani ana matatizo hapa? Hapa itabidi turejee historia kati ya vyama viwili Chadema na CUF nani ana historia ya kumpinga/kumuunga mkono mwenzake? Vinginevyo tutabaki kuumiza vichwa wakati wengine ni Kenge kwenye msafara wa mamba. Tusubiri tuone
 
Du Mwanamageuko kama ni kweli bora kuambiana au kuwahabarisha mapema kama wataendelea kutengana hawatawasilisha chochote ndani ya Bunge lazima mmoja anyenyekee
Upinzani baaado watagombana zaidi kama hawataungana
 
Baada ya CUF kuungana na CCM kuunda serikali ya mseto, ni vizuri watanzania wote waelemishwe kuwa chama pekee cha upinzania kilichobaki Tanzania ni Chadema. Kulikuwa na nafasi ya vyama vingine kama TLP, NCCR navyo kuwa vyama vya upinzani. Lakini baada ya TLP, NCCR na vyama vingine kuungana na CUF bungeni inamaanisha kuwa CUF, TLP, NCCR vyote vimeungana na CCM. Hivyo, kama ambavyo tumeendelea kutoa elimu ya uraia kwa watanzania, tuendelee kuwafahamisha na waelewe kuwa chama cha upinzani na ambacho kinatetea masilahi ya Watanzania nchini kwetu ni Chadema pekee. Ujumbe huu na uenee nchi nzima sasa.
 
Nadhani tusingeangalia upinzani baina ya vyama upinzani kwa hoja nyingi kama hivi. Nadhani kilichotokea leo ni kile ndugu mafisadi(ngoja tu niwaite hivyo) walichokuwa wanasali na kuomba kitokee! Waliweza kumtoa Sita, wakashindwa kumweka mtu wao Chenge, lakini wakampata Ana ambaye ni bora kwao mara elfu nyingi kuliko Marando! Imagine Marando kwa muujiza angepita, nadhani hata Chenge angekuwa anakacha mjengo ule. Kwa hivyo leo tuwapongeze hao kina anti-Sita, anti-mageuzi, MAFISADI kwa kufanikisha azma yao.

Pili Mwikimbi (kwenye thread nyingine) alituarifu maagizo SMZ iliyowapa CUF.Yaani pamoja na kuwa majority Bungeni CCM hawakujiamini kiasi kwamba walihitaji kura za CUF ili wamtose Marando. Bahati Mbaya Mwikimbi alishambulia kwa hoja lakini sasa nadhani tunaelewa kilichotekea ni kama alivyotabiri. Incidentally Mwikimbi ni neno la kichaga lenye kuimanisha 'atoaye maonyo', sema soothsayer, anayetabiri baya linalokuja(mtabiri - lakini sio Yahya!).

Mjadala huu ungekuwa na maana kama tungeelekeza hoja zetu juu ya hitima ya kuwa na huyu Ana ambaye amepandikizwa pale bungeni, je bunge litakuwa na uwezo wa kujiaminisha kwetu kama lilivyoanza kuwa chini ya Mzee aliyejiita wa Viwango?
 
WANAGOMBANISHWA NA NANI?KWA NINI VIJANA HAMTAKI KUTAFITI?HAMKUMBUKI KUWA VITA VYA PANZI NI FURAHA YA KUNGURU,KUNA MTU AMA TAASISI INAYOFAIDI SANA WAPINZANI WAKIGOMBANA NDANI YA CHAMA KIMOJA AU KATI YA VYAMA AU HATA AKITOKEA MTU MMOJA WA UPINZANI AKAAMUA KURUDI KUNDINI KAMA YULE DR WA FALSAFA ALIYEISUMBUA SAAAAAANA CCM HAPO MANZESE NA UBUNGO MIAKA YA 1995 NA HATIMAYE AKASALIMU AMRI AKAPIGA GOTI KAMA VILE ANACHUKUA PhD kwa Mkapa na ukawa ndiyo mwanzo wa mwisho. Kama tunaamini katika mabadiliko tuiangalie CCM KAMA ADUI WA MABADILIKO NA ADUI WA MAWAZO BTOFAUTI, NA ADUI WA UADILIFU NA ADUI WA UPINZANI
HAPA NASIMAMA EE MUNGU NISAIDIE!
 
"Tuna asilimia 12.5 ya wabunge na hiyo inatupa nafasi ya kuunda kambi ya upinzani bungeni," alisema Mrema. Sasa swali sijui hawakujua kuwa asilimia 12.5 zao zingeweza kuwafanya washinde uspika? na hata wale CCM waliokuwa hawakufurahishwa na Anna Makinda kugombea waliona uroho wa chadema wa madaraka wakaona hawa wameshachuku KUB wakichukua na Uspika itakuwa balaa nadhani Chadema ni chama kinachoshabikia suala la uditekta wenye upeo wale ma great thinkers changieni bila unazi wa vyama.
:smile-big: Hii post wanakuwa wanaipita kama kichaka kilichoshika moto!!" Tatizo ni mapenzi, yametuzidi mara nyingi hatuutazami ukweli bali kile tunachokitaka.:smile-big:
 
Kura za wabunge kwa wagombea wa nafasi ya Spika zimenifanya nihitimishe kuwa Kama bungeni kunatakiwa kuwa na kambi mbili basi CCM ina wabunge 265 na Upinzani una wabunge 53. Nimefikiri hivyo hasa pale ambapo CCm walikuwa wanaimba CCM! CCM! CCM! wakati Anna Makinda anakwenda kula kiapo. Kwa maoni yangu wapinzani waliopiga kura kwa CCM nao ni CCM tu.
 
Yaliyotokea ni haya hapa:

Kutoka ndani ya uvungu wao...
Walikaa Chadema na CUF ili waone wataingiaje Bungeni. Kabla ya Uchaguzi wa Spika, Hamad Rashid alitaka kugombea Uspika, Chadema wakamwambia hapana wacha Agombee huyu Mwanasheria, wewe utarudi katika kambi ya upinzani kwa cheo chako kile cha awali, na kwa kufanya hivyo tutagawana madaraka. Hamad akawakubalia na kuondoa azma yake ya kugombea U-Spika alipofanya hivyo, Zito akaibuka na kusema Wataunda kambi Chadema peke yake bila kushirikisha vyama vingine. hilo nalo. Hapo ndipo Marando alipozikosa kura ambazo zingemvusha kwenye Uspika. Na hii imefanyika kutokana na ufinyu wa fikra (kama sio viongozi waandamizi wa Chadema kupewa chochote toka CCM) wakidhani kwamba umaarufu unatokana na kuongoza kambi ya upinzani bungeni bila kuwa na ushirikiano kutoka vyama vingine. Walichokisahau Chadema ni kuwa CUF walijaribu kutoshirikisha vyama vingine awali na kisha wakajirekebisha, na hapo wasiomjua Slaa ndipo walipomtambua. Ila kwa kwa hili la ubinafsi wa CHADEMA wameumaliza UPINZANI Tanzania. Tutafute kaburi tuuzike...

Tusubiri kuundwa kwa chama kipya kisicho na damu ya U-CCM-CCM.:sad:

Nawasilisha.

Kwa upande wangu unaonekana mtu mzima uliyekosa akili, unafikiri kura 30 za CUF zingeweza kushindana na kura 250 za CCM.
CUF ni chama Tawala, taka usitake. NCCR, TLP,UDP hawana impact. kwahiyo chama cha upinzani ni CHADEMA, Chama tawala ni CCM+CUF
 
Huo sasa ni umbea taslimu.

CHADEMA 45 + CUF 34 + NCCR 4 + TLP, UDP 2 = 85

CCM = 251

Hapo uspika wa Marando uko wapi Mwanamageuko? au na wewe unataka kuchakachua JF?
 
Kwa upande wangu unaonekana mtu mzima uliyekosa akili, unafikiri kura 30 za CUF zingeweza kushindana na kura 250 za CCM.
CUF ni chama Tawala, taka usitake. NCCR, TLP,UDP hawana impact. kwahiyo chama cha upinzani ni CHADEMA, Chama tawala ni CCM+CUF

Asante PPM.
 
Chadema wanapaswa kuitumia fursa hii kuimarisha uimara wao na uaminifu wao kwa Wtz, naamini waliiongezea kura za uspika hapo ni vijana wale wa kigoma na CCM Halisi ambao ni wachache sasa Bungeni kwa sasa, Chadema wao ni wa Mrengo wa kushoto hawapaswi kushikana mkono watu wanafiki. Hata Mnyazi Mungu anaagiza aidha uwe baridi au moto lakini ansema walio vuguvugu ni chukizo sana kwake. Keep on going CHADEMA safari ni hatua na ndio hatua moja huongeza ingine.....
 
Back
Top Bottom