Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698
Leo May 5, mbunge Kilindi, Omary Kigua ametoa hoja ya kuahirisha shughuli zake za kawaida ili kujadili dharula ya ongezeko la bei ya mafuta.

Kigua amesema kuna changamoto ya kupanda kwa haraka sana kwa mafuta ya taa, dizeli na petroli ambapo hivyo vikipanda ni kimepandishwa kila kitu na Tanzania nzima kelele ni suala la mafuta na Bunge linalo wajibu mkubwa wa kuisimamia Serikali katika jambo husika.

Kigua amesema anaamini Serikali ya Tanzania itafanya jambo kama ambavyo Serikali nyingine duniani zinavyochukua hatua kwasababu wananchi hawawezi kulalamika halafu Serikali isichukue hatua yoyote.

Spika Tulia amesema pamoja na kwamba Waziri Mkuu ameshachukua kutua, hoja hiyo ambayo imeungwa mkono na wabunge wengi itajadiliwa na wabunge kama kazi yao ya kuishauri Serikali ifanye nini kwenye jambo husika.

MUSUKUMA;- Mafuta yaliyopanda juzi yamenunuliwa mwezi wa pili
Mbunge Joseph Kasheku amemshukuru Spika kwa kukubali kuwasikiliza na amesema kwa wao wanaotoka majimbo ya vijijini na kununua mafuta kwenye vidumu wananunua 5,000 kwa lita.

Musukuma ameiomba Serikali ieleze ukweli kwani mafuta yaliyopanda juzi yamenunuliwa mwezi wa pili. Musukuma amesema wafanyabiashara yeye akiwa mmojawapo wanacheza na namba.

Musukuma amesema iliwahi kushuka bei ya korosho na Serikali ilipeleka Jeshi ku-rescue suala la korosho na mpaka leo hakuna mtu anachezea bei ya korosho kwasababu wanajua Serikali inaweza kuingia kuchukua biashara.

Musukuma amesema kuna kuna kodi ziliwekwa kodi za mafuta, iangaliwe namna ya kuziondoa kwa dharula ya miezi mitatu ili mafuta yarudi kuwa chini.

Musukuma amemaliza kwa kusema nchi inakubalika kukopa kimataifa na inakopa hivyo wakope kufidia gharama ili mafuta yaweze kushuka, hakuna mtanzania atamudu na kudai hata wabunge linawapiga kwasababu wanalipwa mileage za kwenda vijijini na ya kwake inaishia Shinyanga.

Musukuma: Mheshimiwa spika mimi pia ni msafirishaji, yaani kwasababu watanzania tuna nidhamu ya kuiheshimu Serikali na kuwapa muda, hebu jiulize msafirishaji aliyekuwa anapeleka abiria kwa shilingi 30,000 Mwanza, leo mafuta yamefika 3,400 nauli bado 30,000 Hili haliwezekani, tukubaliane tuishauri Serikali na ije na kauli nzuri.

SONGE;- Serikali itafute fedha kupeleka ruzuku kwenye mafuta
Simon Songe: Naishauri Serikali mambo mawili, kwanza kutafuta fedha kwaajili ya kupeleka ruzuku kwenye mafuta walau kupunguza gharama za mafuta na kupunguza gharama za vitu vingine ambazo vinaenda kupanda bei.

Tuna tozo nyingi tumeweka kwenye mafuta kwaajili ya nchi na kwaajili ya bajeti tuliyoipitisha, sisi ndio wabunge na sisi ndio tulioipitisha, kuna haja ya kuangalia baadhi ya tozo tuweze kuziondoa kwa dharula kwa miezi miwili.

MHAGAMA;- Mafuta yamepanda kwa 92%
Joseph Mhagama: Kati ya mwezi January 2021 mpaka Mei 2022 mafuta ya petroli yamepanda kwa asilimia 92 kutoka Tshs 1,695 mpaka elfu tatu mia mbili na kitu.

Tozo mbili za fuel levy na exercise duty kwa pamoja zinachangia Tshs 792, waziri au Serikali waangalie ni namna gani tutatoka, tunajua umuhimu wa tozo za ujenzi wa mabarabara na maji hizo zibaki lakini nyingine tunaweza kupunguza matumizi ya Serikali tukaenda kuboresha maslahi ya watanzania.

KAKUNDA;- Kwanini Serikali isikope kupunguza maumivu
Joseph Kakunda: Nilikuwa Kenya na nilikutana na waziri wa fedha, nikamuuliza mmepata wapi fedha kwenye bajeti yenu za kutoa ruzuku karibu Tshs bilioni 900, akasema wamezikopa IMF. Kwanini sisi Serikali yetu isikope kwaajili ya kupunguza maumivu kama hayo.

Ningependa kuishauri Serikali yangu, wananchi wanahitaji kupata matokeo ya haraka. Kama kuna mbinu mbadala za kuagiza mafuta ambazo zitashusha bei ya mafuta kwa haraka basi zitumike badala ya mbinu ambayo sasahivi imesababisha ongezeko la bei ya mafuta.

WAITARA;- Zambia dizeli 2,470
Mwita Waitara: Nchi kama Zambia, dizeli ni 2,470 lakini tunajua mizigo yao wanapitisha hapa, dizeli Tanzania imetangazwa bei ya EWURA zaidi ya Tshs 3000, wamezungumza bei ya mafuta Zanzibar na wanajaribu pia kutugawa.

Ni jambo ambalo Serikali lazima ichukue hatua za dharula.

KASALALI;- Kuondoa tozo hakuepukiki
Mageni Kasalali: Naiomba Serikali katika hatua ambazo imeanza kuchukua, jambo la kuondoa tozo za Serikali kwenye mafuta ni jambo ambalo haliepukiki. Umefika wakati ni lazima sasa tuache kugeuza mafuta kuwa sehemu pekee ya kutafuta pesa, ni lazima tufikire njia nyingine kwa huu muda.

TAARIFA;- Saasisha ataka Serikali iuze madini yaliyokamatwa kusaidia uchumi
Sasisha: Pamoja na tozo hizi za kitaasisi, kuna fedha ambazo zipo kwenye madini, yale madini ambayo yamekuwa yakikamatwa kama faini sasahivi ni wakati sahihi Serikali iuze iweze kuingiza huku kama sehemu ya kusaidia uchumi wetu ikiwa ni pamoja na dhamana zinazowekwa mahakamani, ziletwe ziingie huku.

SHANGAZI: Tozo zilikuwepo miaka sita iliyopita na hazijawahi kuwa tatizo
Rashid Shangazi: Matumizi yetu kwa mwezi ni kama lita milioni 300, tungekuja na mpango wa 'stabilization fund'. Serikali ije iombe kibali kwa Bunge, wakakope japo bilioni 300, kila lita moja tuiwekee ruzuku ya Tshs 1,000 kila lita.

Hii itatusaidia kwamba hatutakwenda kugusa tozo pamoja na kodi nyingine kwasababu hizi tozo zilikuwepo miaka sita iliyopita na hazijawahi kuwa tatizo. Kwahiyo leo sio kwamba mafuta yamepanda bei tatizo ni hizi tozo, tozo zinatusaidia kwenye mambo mengine kama kupeleka umeme vijijini, barabara, maji nk.

WIZARA
Kwa upande wake, waziri Makamba amesema Biashara ya mafuta ni biashara ambayo ina vita ya wenyewe kwa wenyewe ambapo kuna madaraja 3 ambao ni wenye vituo, watu wa kati na kuna wale 'Supplier' na huu mfumo umekuwa sehemu ya ugomvi.

Pia amesema kuna mambo kadhaa ambayo serikali haina mamlaka nayo lakini yamekuwa yakichangia kupanda kwa gharama za mafuta nchini akitaja bei za soko la dunia, gharama za kusafirisha mafuta, na gharama za kufanya biashara yenyewe hapa nchini.

Makamba amesema mpango wa sasa ni kuanzisha mkakati wa kuwa na hifadhi ya mafuta ya kimkakati (strategic reserve) mpango huo utaanza ndani ya wiki mbili zijazo.

BUNGE;-Spika ampa siku tano Makamba
Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson amempa siku tano kuanzia leo Alhamisi hadi Jumanne ya 10 Mei 2022, Waziri wa Nishati, January Makamba kutoa taarifa bungeni kuhusu hatua za dharura ambazo serikali inazichukua kupambana na ongezeko la bei ya mafuta.
 
Wanabodi,

Moja ya kazi za Bunge ni Kuisimamia serikali. Bunge la Mhe. Job Ndugai, lilituhumiwa kuwa ni Bunge dhaifu kuwahi kutokea, hivyo Spika Job Ndugai kuhesabika ni Spika dhaifu kabisa kuwahi kutokea, hivyo kupachikwa jina la "Bora Spika" Kwa kuanzia mimi niliisikia sauti hii Voices from within: Nimesikia sauti, Dr. Tulia Ackson ndiye Spika ajaye! Sauti hiyo imenieleza Ndugai, japo atatamani aendelee lakini...

Job Ndugai alipojiuzulu tukasema Kujiuzulu kwa Ndugai ni mpango wa Mungu kwa Tanzania ili tupate Spika Bora. CCM itateua Spika Bora au Bora Spika kama kawa?

Kwa vile Dr. Tulia alikuwa ni Naibu Spika wa Spika dhaifu, alipochaguliwa kuwa Spika, kuna watu walidhani Bunge la Tulia litakuwa ni Bunge Dhaifu kama Bunge la Ndugai.

Nilitoa ushauri huu Je, Wajua, Naibu Spika, Chini ya "Bora Spika", Anaweza Kuwa "Spika Bora?". Dr. Tulia, "Ukitulia, Una Fursa ya Kuwa Spika Bora Sana!" Hongera Sana!

Sasa hiki ndio kinatokea Leo,

Bunge la Dr. Tulia, sasa limeanza kuisimamia Serikali kiukweli ukweli!, leo limesimamisha shughuli zake zote kujadili hoja ya dharura ya Mhe. Omari Kigua, kujadili kupanda kwa bei ya mafuta ya petrol na dizeli.​

Hongera Sana Spika Tulia, Bunge sasa linaisimamia serikali

Keep Watching Bunge Live

na Kazi iendelee!

Paskali.
 
Leo May 5, mbunge Omary Kigua ametoa hoja ya kuahirisha shughuli zake za kawaida ili kujadili dharula ya ongezeko la bei ya mafuta.

Kigua amesema kuna changamoto ya kupanda kwa haraka sana kwa mafuta ya taa, dizeli na petroli ambapo hivyo vikipanda ni kimepandishwa kila kitu na Tanzania nzima kelele ni suala la mafuta na Bunge linalo wajibu mkubwa wa kuisimamia Serikali katika jambo husika.

Kigua amesema anaamini Serikali ya Tanzania itafanya jambo kama ambavyo Serikali nyingine duniani zinavyochukua hatua kwasababu wananchi hawawezi kulalamika halafu Serikali isichukue hatua yoyote.
Hiyo bei ya kawaida tu! Mbona US bei ghali kuliko huku? Alisikika panya .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Leo May 5, mbunge Omary Kigua ametoa hoja ya kuahirisha shughuli zake za kawaida ili kujadili dharula ya ongezeko la bei ya mafuta.

Kigua amesema kuna changamoto ya kupanda kwa haraka sana kwa mafuta ya taa, dizeli na petroli ambapo hivyo vikipanda ni kimepandishwa kila kitu na Tanzania nzima kelele ni suala la mafuta na Bunge linalo wajibu mkubwa wa kuisimamia Serikali katika jambo husika.

Kigua amesema anaamini Serikali ya Tanzania itafanya jambo kama ambavyo Serikali nyingine duniani zinavyochukua hatua kwasababu wananchi hawawezi kulalamika halafu Serikali isichukue hatua yoyote.
wao wanashida gani si wana miposho ya kumwanga , wananchi hawawahusu kabisaaaa, waendelee kusifiana tu na kuupiga mwingi.

Wananchi wapambane tu na hali zao kama wakiona noma wahamie Burundi maana sio kesi
 
Mh hili ni jambo geni. Zamani hoja kama hizi zilikua zinaletwa na upinzani kisha chama tawala kinakua kinahalalisha hoja iliyoletwa hata kama ni kandamizi.

Sasa kwa hili bunge itakuaje? Wanaweza leta mbadala rahisi wa dizeli na petroli?

Au atakuja mbunge kusema hata hivyo tunanunua mafuta kwa bei rahisi kuliko nchi fulani?
 
Trust me, Wabunge wa CCM wa mwendazake Hawawezi kujadili na wakaja na kitu tangible. Trust me. Wakenya wanafanya kwa vitendo wao wanarukaruka tu

IMG-20220505-WA0078.jpg
 
Leo May 5, mbunge Omary Kigua ametoa hoja ya kuahirisha shughuli zake za kawaida ili kujadili dharula ya ongezeko la bei ya mafuta.

Kigua amesema kuna changamoto ya kupanda kwa haraka sana kwa mafuta ya taa, dizeli na petroli ambapo hivyo vikipanda ni kimepandishwa kila kitu na Tanzania nzima kelele ni suala la mafuta na Bunge linalo wajibu mkubwa wa kuisimamia Serikali katika jambo husika.

Kigua amesema anaamini Serikali ya Tanzania itafanya jambo kama ambavyo Serikali nyingine duniani zinavyochukua hatua kwasababu wananchi hawawezi kulalamika halafu Serikali isichukue hatua yoyote.

Spika Tulia amesema pamoja na kwamba Waziri Mkuu ameshachukua kutua, hoja hiyo ambayo imeungwa mkono na wabunge wengi itajadiliwa na wabunge kama kazi yao ya kuishauri Serikali ifanye nini kwenye jambo husika.

Kuna bunge au baraza la CCM?

Wafanyabiashara wakubwa wa mafuta ni hao hao wabunge fake
 
Mh hili ni jambo geni. Zamani hoja kama hizi zilikua zinaletwa na upinzani kisha chama tawala kinakua kinahalalisha hoja iliyoletwa hata kama ni kandamizi.

Sasa kwa hili bunge itakuaje? Wanaweza leta mbadala rahisi wa dizeli na petroli?

Au atakuja mbunge kusema hata hivyo tunanunua mafuta kwa bei rahisi kuliko nchi fulani?
Sanasana watasema hata Marekani bei ni kubwa
 
Huo mjadala uwe kweli na immediate impact, sio wanajadili tu halafu mambo yanabaki vile vile huku bei ya mafuta ikizidi kupanda na kuwaumiza watumiaji.

Rais kuruhusu bei za vitu kupanda kwasababu ya vita ya Urusi na Ukraine haya ndio matokeo yake, tunaumizwa wananchi na mafisadi wajanja kwenye wizara ya nishati.

Watz tumezubaa sana.
 
Back
Top Bottom