Bungeni: Milipuko ya mabomu Mbagala yatafuna Tsh. Bilioni 17.4

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
Waziri George Simbachawene amesema Serikali ilitumia kiasi hicho kuwapa pole waliothirika na milipuko iliyotokea Aprili 29, 2009 katika Kambi ya JWTZ KJ 671 na kuua zaidi ya watu 29.

Amesema wananchi 12,647 waliathirika na mlipuko huo uliosababisha huku watu kujeruhiwa na familia nyingi kukosa makazi baada ya nyumba zao kubomoka.

Ameongeza kuwa Serikali iligharamia huduma za mazishi kwa familia 29, na zoezi la kutoa pole lilisitishwa rasmi na Serikali Machi 2020 baada ya waliokusudiwa kujitokeza na kulipwa.

=====================

Jumla ya Sh17.4 bilioni zimetumika kutoa mkono wa pole kwa wananchi 12,647 walioathirika na milipuko ya mabomu yaliyotokea katika kambi ya Jeshi la Wananchi Mbagala jijini Dar es Salaam.

Mabomu hayo yalilipuka Aprili 29, 2009 katika Kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) KJ 671 na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 25, huku mamia ya watu wakijeruhiwa na familia nyingi kukosa makazi baada ya nyumba zao kubomoka kabisa.

Akijibu swali bungeni leo Novemba 2, 2022 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu George Simbachawene ambaye amesema kilichotokea ni mkono wa pole siyo fidia.

Katika swali la msingi Mbunge wa Mbagala (CCM), Abdallah Chaurembo ametaka kujua nini kauli ya Serikali juu ya mapunjo kwa wananchi walioathirika na mlipuko wa mabomu Mbagala ambao ulitokea Aprili 29, 2009.

Waziri Simbachawene amesema katika tukio Serikali iligharamia huduma za mazishi kwa familia 29 zilizopoteza wapendwa wao kutokana na milipuko hiyo ya mabomu.

"Zoezi la kutoa mkono wa pole kwa waathirika lilisitishwa rasmi na Serikali mweziachi 2020 baada ya walengwa wote waliokusudiwa kujitokeza na kulipwa," amesema Simbachawene.

Hata hivyo Waziri ameliambia Bunge kuwa bado kuna watu wanaodai kifuta machozi na wamekuwa wakifiatilia malalamiko yao kuhusu uhalali.

MWANANCHI
 
Naaam Naam hz Bii zipite bila kunyofolewa, thubutu
MAMA.e Watu wanatamani yalipuke mengine wapate kunyofoa tena.
 
Back
Top Bottom