Bunge Maalumu la Katiba laendelea kukusanya maoni!

Nipo tayari kipigania nchi hii bila malipo yoyote. Tuungane jamani tuwatimue hawa manyang'au. Wangine tutawa recruit kama Mungu atakavyojaalia.
 
Kweli ukishangaa ya Musa, utayaona ya Firaoni!

Nami nimemsikia, makamu Mwenyekiti, wa bunge maalum la katiba la magamba, akiwahakikishia waTz kuwa, waendelee kumiminika Dodoma, kwa kuwa maoni yao yanaendelea kupokelewa!

Sasa waTz, tunapaswa kujiuliza , hivi kumbe JK, alipokuwa anateua wajumbe wa Tume ya maoni ya katiba, iliyoongozwa na Jaji Warioba, ili wakusanye maoni nchi nzima, kumbe ilikuwa ni usanii wa hali ya juu!

Kwa kuwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta, naye tumemsikia mara kadhaa akisema kuwa wanaendelea kupokea maoni ya wananchi, kuhusu uundwaji wa katiba mpya, na leo Makamu wake naye ametuhakikishia kuwa wanaendelea kupokea maoni hadi tarehe 27 mwezi huu, watskapofunga pazia la kupokea maoni!

Sasa ndiyo tumethibitisha kuwa kumbe Rasimu ya Tume ya Warioba, ni kweli ishawekwa kapuni!
Nafikiri sasa wameamua kucheza na akili zawatu wanatafuta watu wao wanawapachika majina ya vikundi kisha wanawaita dodoma kupeleka maoni ya ajabuajabu mfano yaliyopelekwa leo eti wanatetea mali zisizo shikika
 
Kweli ukishangaa ya Musa, utayaona ya Firaoni!

Nami nimemsikia, makamu Mwenyekiti, wa bunge maalum la katiba la magamba, akiwahakikishia waTz kuwa, waendelee kumiminika Dodoma, kwa kuwa maoni yao yanaendelea kupokelewa!

Sasa waTz, tunapaswa kujiuliza , hivi kumbe JK, alipokuwa anateua wajumbe wa Tume ya maoni ya katiba, iliyoongozwa na Jaji Warioba, ili wakusanye maoni nchi nzima, kumbe ilikuwa ni usanii wa hali ya juu!

Kwa kuwa Mwenyekiti wa bunge hilo, Samuel Sitta, naye tumemsikia mara kadhaa akisema kuwa wanaendelea kupokea maoni ya wananchi, kuhusu uundwaji wa katiba mpya, na leo Makamu wake naye ametuhakikishia kuwa wanaendelea kupokea maoni hadi tarehe 27 mwezi huu, watskapofunga pazia la kupokea maoni!

Sasa ndiyo tumethibitisha kuwa kumbe Rasimu ya Tume ya Warioba, ni kweli ishawekwa kapuni!
Ni usanii na dharau kubwa kwa umma. Bunge maalum la katiba mpya linajipangia kazi hata ya kukusanya maoni. Na ilishajipangia kudhibiti mihimili mingine ya dola,lakini lenyewe likijafanya ni above board; halitaki kuwekewa ukomo wa vipindi vya mbunge kuchaguliwa, linakataa wananchi ambao ndio waajiri kumwajibisha mbunge asiyetumikia vema wapigakura wake kwa kusitisha ubunge wake. Inakera!!!
 
jamani wametangaza lini? kuwa tupeleke maoni yetu namimi nataka nipeleke!!!!!
 
Maoni??!! Mbona sielewi!! Katika sheria iliyoliweka BMK pia ukusanyaji wa maoni umo?! Nahisi kizunguzungu!
 
Ni usanii na dharau kubwa kwa umma. Bunge maalum la katiba mpya linajipangia kazi hata ya kukusanya maoni. Na ilishajipangia kudhibiti mihimili mingine ya dola,lakini lenyewe likijafanya ni above board; halitaki kuwekewa ukomo wa vipindi vya mbunge kuchaguliwa, linakataa wananchi ambao ndio waajiri kumwajibisha mbunge asiyetumikia vema wapigakura wake kwa kusitisha ubunge wake. Inakera!!!
Taratibu mtafahamu Sitta ni binadamu wa aina gani.
 
Nimeskia itv. Maswali nilijiuliza ni lini bmk ilipata uharali wa kukusanya maoni? Sheria ya katiba mpya inasemaje? BMK imetoa lini matangazo na kuhimiza wananchi waliokosa fursa hiyo watoe maoni yao? au inatokana na mijadara inayoendelea bmk then wanabaini nani wakuitwa...na kama ndo ivyo kwa nini waweke deadline?

Tunaomba kesi iliyofunguliwa na Kibatali ijumuishe hayo kwa faida yetu.

Kabisa. Huu ni usanii wa mchana kweupe! Hivi kwa nini kama Taifa tumezoea kupindisha mambo? Inatia uchungu sana
 
Sasa nadhani yale makundi yaliyokuwa yanawataka/kushinikiza Ukawa warudi bungeni wameona dhamira ya Ccm iliyokuwa imejificha. Na hayo ni baadhi tu ya mambo mengi ambayo yamekuwa yakifanywa kwa dhamira mbaya huku zikitungwa sheria mbovu na zisizofuatwa kwa maslahi binafsi.
Niwaombe tu watz wote tujitokeze kujiandikisha kupiga kura. Na kwa kuwa wamezoea kuchakachua hapo ndio tutajua hatua stahiki ya kuchukua dhidi ya watawala hawa waovu.
 
Maoni ya nini tena warioba amerudi au

Hiyo tume yenyewe ya warioba august 13 ilipeleka maoni bunge la katiba ikisema yalisahaulika kuwekwa kwenye rasimu inayojadiliwa.Kawaulize walisahauje? Kuna mengi ambayo tume iliacha au ilisahau.
Tume ya warioba wanafiki wakiwa kwenye midahalo wanajifanya ni yao ya kwenye rasimu tu ndio yajadiliwe wakibanwa wanapeleka mengine wanasingizia walisahau.

Nashukuru mwenyekiti wa bunge la katiba alipoulizwa kayapokea ya hiyo tume kivipi wakati haipo akasema kayapokea kama maoni tu ya watanzania wengine.Mbaneni warioba muulizeni umekuwaje kapeleka maoni mapya bunge la katiba? Kuhusu mambo ya ardhi maliasili na mazingira wakati huu?
 
Makamu mwenyekiti wa bunge lakatiba kayasema hayo leo wakati akipokea maoni ya wasanii
yaani hiki ndo kile ambacho mwanajamvi mmoja alikiita wendawazimu. Jamani hivi hakuna mtu wa kuwaambia hawa watu kuwa wanakosea? hivi hawa wanaoleta maoni saa hii walikuwa wapi siku zote za ukusanyaji wa maoni. Yaani hata mwana sheria mkuu halioni hili na kulitolea ufafanuzi wa kina ili isiwachanganye wananchi!
yaani huu ukanjanja sasa umezidi!
 

BUNGE_SITTA.jpg

Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, Samuel Sitta (kushoto) akimsikiliza Rais wa Shirikisho la Wasanii Tanzania (Taff), Simon Mwakifwamba (kulia) wakati wasanii walipokutana na uongozi wa Bunge hilo mjini Dodoma jana na kujadili mambo ya wasanii yanayopaswa kuwamo katika Katiba Mpya. Picha na Emmanuel Herman

Na Neville Meena na Fidelis Butahe, Mwananchi

Jumanne, Agosti 26 2014

Kwa ufupi
Lapokea maoni ya makundi mbalimbali, Katibu atetea, Warioba aponda, Wasomi wasema linakiuka sheria


Dodoma
Kitendo cha Bunge Maalumu la Katiba kukusanya maoni ya makundi na wananchi mbalimbali, kimepokewa kwa hisia tofauti, baadhi ya wasomi wakisema ni kinyume cha sheria na kuonyesha kutapatapa huku Mwenyekiti wa iliyokuwa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba akisema linafanya kazi ambayo tayari tume yake ilishaifanya.

Hata hivyo, Katibu wa Bunge hilo, Yahya Khamis Hamad amesema litaendelea kupokea mapendekezo kutoka kwa watu na makundi mbalimbali hadi hapo litakapohitimisha kazi yake.

Kwa muda sasa, wawakilishi wa taasisi mbalimbali wamekuwa wakifika Dodoma kuwasilisha mapendekezo yao wakitaka yazingatiwe kwenye Katiba Mpya kwa maelezo ya kutoonekana katika rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Suala hilo limezua mjadala hasa katika mitandao ya kijamii ambako watu mbalimbali wamekuwa wakihoji sababu za Bunge hilo kufanya kile kinachotafsiriwa kuwa ni ‘kukusanya maoni', kazi ambayo tayari ilishafanywa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Akitetea hoja hiyo, Hamad alitetea akisema wananchi, watu au taasisi zinazotoa mapendekezo yao zinashirikiana na wabunge katika mchakato wa kile kinachoendelea bungeni hivi sasa.

"Tutaendelea kupokea maoni ya wananchi kwa sababu na sisi tunaendelea kujadili, kwa hiyo kadri makundi yatakavyoleta maoni yao, tutayapokea na kuyapitisha kwenye mchakato wa kuyawezesha kuzingatiwa kama yataonekana yanafaa," alisema Hamad.



Warioba na wasomi

Akizungumzia hatua hiyo, Jaji Warioba aliponda kitendo cha kukusanywa upya kwa maoni hayo akisema yalishachukuliwa na Tume yake na kuingizwa katika Rasimu ya Katiba.

"Nyaraka zote za maoni, yakiwamo ya makundi hayo tuliziwasilisha, sasa wanakusanya maoni mapya ili iweje? Wanatakiwa kufuata maoni ya wananchi na si ya makundi na kama wanafanya hivyo basi maoni ya makundi hayo yakusanywe hadharani ili wananchi wayasikie ili nao waweze kuchangia," alisema jana.

Alitolea mfano wa maoni yaliyotolewa na Jumuiya ya Serikali za Mitaa Tanzania (ALAT), kwamba ni makosa kuchukua maoni hayo na kuyaacha yaliyotolewa nawananchi.

"Naona kuhusu ardhi eti wamechukua maoni ya Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, hii si sahihi kabisa. Kama wanajadili suala la serikali za mitaa, ardhi na maliasili wanatakiwa kuyaongeza mambo hayo katika mambo ya muungano kwa sababu hivi sasa mambo hayo si ya muungano na ndiyo maana Tume hatukuyaingiza katika Rasimu ya Katiba," alisema.

Jaji Warioba alilitaka Bunge hilo kutochakachua maoni kuhusu ardhi, maliasili na ardhi ambayo Tume yake iliyawasilisha serikalini ili baadaye yaingizwe katika Katiba ya Tanganyika, "Wakiyaingiza mambo hayo katika Katiba ya Muungano, yatapingana na Katiba ya Zanzibar na kuleta shida."

Mtaalamu wa lugha na falsafa, Faraja Christoms alisema, "Kinachofanyika Dodoma ni dalili ya kutapatapa. Wanatakiwa kukumbushwa kuwa wanachokifanya si sahihi na ni kinyume na sheria, kifupi ni kwamba Bunge la Katiba limepoteza mwelekeo."

Mhadhiri wa Idara ya Sayansi za kwenye Maji na Uvuvi Chuo Kikuu Dar es Salaam (UDSM),Dk Charles Lugomela alisema: "Bunge limekosa mwelekeo kwa sababu Katiba ni suala la maridhiano ya kisiasa na linatakiwa kuendeshwa kwa nguvu ya hoja na si hoja ya nguvu."

Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba Tanzania (Jukata), Deus Kibamba alisema Bunge hilo sasa linakwenda mwendo wa gari bovu, huku akimtuhumu Mwenyekiti wake, Samuel Sitta kuwa analiendesha kwa mtindo wa comedy (vichekesho) na si kufuata kanuni na sheria.

"Ndiyo maana tulimtaka Sitta aliahirishe Bunge kwa sababu anaweza kwa mujibu wa Kifungu cha 28(4) ambacho walikibadili na kujipa mamlaka ya kulifanya Bunge hilo kuendelea mpaka pale itakapoonekana inafaa," alisema Kibamba.

Mtaalamu wa lugha ya Kiswahili, Dk Aldin Mutembei alisema: "Kinachofanyika Dodoma ni makosa na wajumbe wanafanya mambo ambayo hayakutakiwa kufanyika, kifupi ni kwamba wanakwenda kinyume na utaratibu."

Mutembei alisema kitendo hicho kinastaajabisha na ni matokeo ya kutofuatwa kwa sheria zilizozalisha Bunge hilo na mchakato wote wa kuandika Katiba Mpya.



Maoni ya Takukuru

Miongoni mwa makundi yaliyowasilisha maoni ni Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) ambayo imependekeza kuanzishwa kwa divisheni katika Mahakama Kuu ya Tanzania itakayokuwa na wajibu wa kusikiliza kesi zote zinazopelelezwa na kufikishwa mahakamani na taasisi hiyo.

Pia, inashauri kuanzishwa kwa ‘Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa na Uhujumu Uchumi' ambayo itakuwa moja ya taasisi za uwajibikaji zinazotajwa katika sura ya 13 ya Rasimu ya Katiba.

Katika Rasimu iliyotolewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Takukuru haikutajwa kwani ilipaswa kuwa kwenye Katiba ya Tanganyika.

Mapendekezo ya Takukuru ni miongoni mwa mengine saba ambayo uongozi wa Bunge Maalumu umeyapeleka katika kamati zote 12 ili kubaini iwapo yanafaa kuingizwa kwenye Rasimu ya Katiba kabla ya kamati hizo kuwasilisha taarifa zake za uchambuzi bungeni kuanzia wiki ijayo.

"Si kwamba yote ni sura mpya, mengine ni nyongeza katika ibara sura zilizopo kwenye Rasimu ya Katiba, kwa hiyo kwa sababu wajumbe walishafanya uchambuzi wa sura zote, itakuwa rahisi kwao kujua wapi waingize kipi," alisema Hamad.



Mapendekezo mengine

Mapendekezo mengine yaliyofanyiwa uchambuzi ni yale yanayohusu muundo wa serikali ambayo yamewasilishwa na mwanasheria na mwalimu, Onesmo Kyauke ambaye katika mapendekezo yake, ametaka muundo wa muungano usizingatie idadi ya Serikali, bali mgawanyo wa madaraka wa nguzo tatu za dola ambazo ni Mahakama, Bunge na Serikali.

Pia yapo mapendekezo yanayohusu masuala ya ardhi, mazingira na rasilimali za Taifa, kutoka Tume ya Mabadiliko ya Katiba ambayo ni mapya kwani hayamo kwenye rasimu ya sasa.

Taasisi nyingine zilizowasilisha mapendekezo ya sura inayohusu masuala ya ardhi, mazingira na rasilimali za Taifa ni Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na wajumbe wa Bunge Maalumu wanaotetea wakulima, wafugaji na wavuvi.

Pendekezo jingine ni lile la sura mpya ya Serikali za Mitaa na ugatuaji wa madaraka kwa wananchi yaliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba pamoja na Alat.

Pia yapo mapendekezo kuhusu haki za wakulima kutoka Chama cha Wakulima wa Pamba Tanzania (TACOGA), ambayo uongozi wa Bunge umeelekeza yajadiliwe pamoja na yale yanayohusu ardhi bila kusahau mapendekezo ya Shirikisho la Wasanii (Taff).

CHANZO: Mwananchi
 
Nimesikia bunge maalum la katiba bado linakusanya maoni.

Nimesikia kuna kundi la wakulima liliwasilisha maoni yake kwa Sitta,

Nikasikia tena juzi kundi la wasanii limewasilisha maoni yake na Mwenyekiti akalisifu sana,

sasa najiuliza...

1. Mbona muda wa kutoa maoni umeongezwa kimya kimya, si umma ungetangaziwa ukajua ili ujiandae vizuri.

2. Hata hivyo mimi nina maoni yangu, Sitta utaniwezeshaje ili kufika Dodoma kuleta maoni maana si wote wenye uwezo wa kufika huko.

3. Nasikia mwisho wa kutoa maoni ni kesho tarehe 27/8, ombi langu kwako naomba uongeze muda ili makundi mengi

yaweze kuwasilisha vinginevyo katiba yako itakuwa ya upendeleo na ya wachache.
 
  • Thanks
Reactions: Gor
Wamepanga kuchakachua maoni yetu,yote ni geresha tu,lengo kuuu ni kuingiza mambo yao
 
Naona mmekutana makanjanja wenyewe, haya tunawapisha

Makanjanja ni wewe ambaye kichwani hauna kitu,unapelekwapelekwa tu mi ccm,hata hilo hulioni,kila jambo unashabikia,liwe baya kwako zuri,liwe halikadhalika,kweli Tanzania kuna mijitu yenye IQ ndogo!
 
Knowledge is power,if you think education is expensive try ignorance.Niwatakie afya njema wananchi wenzangu na kumshukuru Mungu kwa kutuwezesha kuendelea kupumua ikiwa ni pamoja na kushuhudia fursa hii adhimu ya maajabu yanayo endelea ndani Tanzania.

Wakati nilipokuwa mdogo niliamini na kuheshimu dhana nzima ya usomi nikiamini mtu aliyesoma hustaarabika na kufungua muuno mkubwa wa fikra zake kwa faida yake na taifa kwa ujumla.Lakini niliamini elimu ndiyo ufunguo wa maisha ikiwa itatumika katika misingi mizuri inayo kubalika japo sikuwa na mawazo kuwa elimu inaweza kuwa kigezo cha kuzika na kufifisha fikra na mawazo mbadala hususani kwa wasio na elimu.


Leo hii ni mkubwa,mawazo na fikira zangu zinashangazwa na jinsi maarifa waliyoyapata wenzetu wameyageuza kuwa silaha ya kuwakandamiza wanyonge kwa kupuuza mawazo yao.Huwezi kuamini aliye na elimu na asiye na elimu wote sawa kwenye nchi yetu kwa kuwa hata hao maprofesa tuliokuwa tunawaheshimu kama think tank yetu nao wamekubali kurudia ujinga kama wale wasio kuwa na elimu.


Taifa linaangamia kwa kukosa maarifa ndiyo maana kigezo cha knowledge is power kinakosa mashiko katika zama hizi za sayansi na teknolojia.Wale wabunge wa bunge maalum la katiba(BMK) walioko Dodoma wengi wao ni wasomi walioweza kuaminiwa na taasisi mbalimbali kutokana na uwakilishi wao pale bungeni,ni watu wazima ambao kwa kigezo cha elimu naamini wamestaarabika na wanaweza kutumia elimu yao kwa faida ya wote.


Pamoja na weredi wao katika mambo ya sheria kama wengi waliobobea wameshindwa kusoma sheria vizuri ya mabadiliko ya katiba na kuacha kilicho wapeleka pale Dodoma,siamini kuna bahati mbaya katika kufasiri sheria bali kinacho tumia ni mwenye nguvu apite.

Msomi mmoja nayeitwa Vere Nazarian ana sema Whenever you read a good book,somewhere in the world a door opens to allow more light.Nami najiuliza elimu yenu ndugu wajumbe imewafungulia nuru ipi ikiwa mnacho kifanya hakina kichwa wala miguu.


Mwenyekiti wa bunge maalum ni msomi wa sheria,mwanasheria mkuu ni msomi wa sheria na miongoni mwa wajumbe wake ni wasomi wa sheria,hayo makengeza ya kutoweza kuisoma sheria vizuri wameyapata wapi ndani ya bunge hili ikiwa wana kubaliana na mzaha unaoendelea ndani ya bunge hili ili kubariki tu utafunaji wa pesa za wavuja jasho wa nchi hii.


Sheria ya mabadiliko ya katiba imeweka wazi kazi maalumu ya bunge hili kinachofnyika ndani ya bunge hili kinasababishwa na jeuri ya nani!Kazi ya kukusanya maoni ilikwisha fanywa na tume ya jaji Warioba,hii tume ya mwanasheria Sitta imeundwa kwa mujibu wa sheria ipi!


Twende mbele turudi nyuma,taifa kweli linaangamia kwa kukosa wasomi wenye weredi kwa kuwa tulio nao wameamua kuidhalilisha taaluma yao na kuruhusu akili ndogo kutawala akili kubwa.Kwetu sisi waislamu kinacho fanyika ndani ya bunge hili tunasema Inna ilah wainna lilah raajun.


Rais haoni kinachotendeka au ndiyo maazimio ya CC ya chama chake kuvurunda zaidi,nimeamini kuwa kweli la kuvunda halina ubani lakini tukiacha hali hii iendelee kwa kuwa tu watu wanataka kujaza matumbo yao matokeo yake nini!

Tusijivunie ujinga wa Watanzania na uoga wao kwa kuwaamulie sivyo ndivyo,huenda majuto ana weza kuja kuwa mjukuu katika kipindi ambacho hakuna pakushikilia.


Katiba ni maridhiano lakini ikiwa maridhiano hayo yana lenga upande mmoja kwa kuwa wao wana POWER sisi hatuna POWER wajue wanajidangaya ila wanapaswa kujua ballot is strong tha bullet.


Tunaomba vyombo vyote viliangalie hili kwa umakini kabla peoples power haijafanya maamuzi kwani sauti ya wengi ni sauti ya Mungu. Ni vizuri busara ikachukua mkondo wake kuliko ubabe kutawala
 
Back
Top Bottom