Kitila Mkumbo
JF-Expert Member
- Feb 25, 2006
- 3,354
- 1,944
Nchi yetu ipo katika hali ya dharura kutokana na kutaabika kwa wagonjwa mahospitalini bila msaada kufuatia mgomo unaoendelea wa madaktari.
Itakuwa ni aibu kwa Bunge kuanza kikao chake leo kama vile mambo ni kama kawaida. Hata wabunge wenye hoja binafsi wangeziweka pembeni kwanza ili mojawao aombe kuwasilisha hoja ya dharura kuhusu hili la mgomo kama alivyofanya Wenje kuhusu umeme Mwanza katika kikao kilichopita. Tayari tunaonekana kituko, hili la mgomo wa madaktari litafanya baadhi ya binadamu wenzetu katika nchi zingine waanze kushuku ubinadamu wetu! Na huu utamaduni wa kuamini kwamba ubabe wa fukuzafukuza ni suluhisho la migogoro linazidi kutudhoofisha kifikra na kutufanya tuonekane ndondocha.
Na wabunge wanapojadili hili la mgomo, kama kweli watajadili, watambue kwamba kitendo chao cha kushinikiza na hatimaye kuidhinishiwa posho zisizo na tija, kimehalalisha na kuimarisha zaidi madai ya madaktari. Ujumbe wa posho za wabunge ni mmoja tu, nao ni kwamba kumbe serikali yetu ina uwezo wa kutekeleza madai yote ya madaktari. Kumbe basi tatizo sio uwezo, bali nia na mgomo ni njia mwafaka zaidi katika kushinikiza watawala kubadili nia.
Lakini je kuna mtu anasikiliza, na wakisikia wanajali?