Bunge la Uingereza vs Bunge la Tanzania

Mbunge

Senior Member
Aug 7, 2008
104
10
Nilikuwa nikitazama bunge la Uingereza juzi na jana kufuatia sakata la Mzee Rupert Murdoch na uvujaji wa siri za serikali na viongozi wa Uingereza.
Nikafananisha bunge hilo na kuona kwamba MKAO wake ndio unaostahili kuwa mkao wa bunge la Tanzania.
Mkao wa hivi sasa wa bunge Dodoma ni mkao uliowafaa wabunge wa chama kimoja lakini sio wabunge wa vyama vingi.
Hawa ni watu wanaopambana kisiasa na kwa hiyo mkao wa kutazamana uso kwa uso, jicho kwa jicho na kila mmoja kuwa na wafuasi wenzake nyuma yake kama ilivyo bungeni Uingereza ndio unaofaa.
Ni kwa sababu hii ndio maana wabunge wa CCM waliochoka kila siku wanakamatwa na Kamera hapa wakiwa sio wanasinzia bali wameishia kabisa usingizini na wanaota ndoto wanazozijua wenyewe.
Bunge hili ndio bunge wanaosema vinginevyo hawana hoja
 
Back
Top Bottom