Hennes kolon
JF-Expert Member
- Jan 13, 2023
- 673
- 1,287
wanabodi, si mnakumbuka bunge hilihili lilipitisha ule mkataba wa makubaliano ya awali ya DP world tena kwa kuupa promo kibao na kuusafisha, ili hali mkataba niwa hovyo.
Sasa najiuliza je hawakuona!?au walizidiwa maarifa !mpaka Rais akalalamika juu ya baadhi ya vipengele vya huo mkataba ni vya ajabu.
Je, bunge na spika hawakuviona? au waliamua kujitoa ufahamu? Leo hii mmeskia wenyewe bunge halijaafiki kuhusu ombi la serikali la kufanya marekebisho ya sheria za usimamizi wa raslimali za Tanzania ya mwaka 2017, lengo la ombi la serikali kutaka kufanyike mabadiliko ya sheria za usimamizi wa maliasili ni kutaka kuufanya mkataba ule u fit na sheria maana ulikuwa unakinzana na sheria zetu za usimamizi wa maliasili (bandari) za mwaka 2017.
Swali langu kwa bunge letu, ni nini kimewafanya wabunge wetu wajue ni hatari kubadili/kufanya marekebisho ya hii sheria ya 2017 ya usimamizi wa maliasili!? na wakati huko nyuma tayari walisharidhia ule mkataba mbovu wa Dp world?
Kwa kweli bunge langu linanichanganya, linajichanganya, limetuathiri watanganyika na watanzania kisaikolojia. Nakosa imani kabisa kuanzia Sasa na bunge langu.
NB: Nawashukuru watanganyika wote waliojivika ushujaa kujitoa kuupigia kelele huu mkataba, nadiriki kusema bila makelele yao huenda bunge langu hata hayo maombi ya serikali juu ya kufanya marekebisho ya sheria hizi za 2017 za usimamizi wa raslimali yangepitishwa tena kwa promo nzurinzuri na matarumbeta ya pongezi lukuki.
Mwenyezi Mungu atuwezeshe tufike salama. Aaamen!