Bunge la bajeti kuanza leo; kuna jipya au kupandishwa tena kwa kodi?

dosama

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
912
957
Leo Bunge la Bajeti kwa mwaka 2012/2013 linaanza mjini Dodoma.

Tutarajie nini kipya? Kodi kupanda za Vinywaji kama kawaida yao taifa linaloendeshwa kwa kodi za Pombe na starehe!

Mishahara kupanda kwa sh. 6,500/=! Madini kuendelea kusamehewa kodi!

Wafanyakazi kuendelea kutolipwa malimbikizo ya fedha zao!

Kuongezeka kwa gharama za uendeshaji na kupunguza fedha za maendeleo.

Nini kipya ambacho hakijulikani?
 
ni vituko vya Bi-kiroboto na wabunge wa CCM kuunga kila hoja itakayotolewa asilimia mia kwa mia hata kama haina manufaa kwa wa-Tanzania, kwenye Bajeti hakuna jipya ndugu zangu..
 
Tunasubiri watukomoe wanywaji bia na wavuta sigara,bajeti ya Tanzania mara zote inatoa adhabu kwa wanywaji wa pombe,nadhani ni mikakati ya Ki--OIC,kwani hakuna vyanzo vingine hadi kupandisha kodi ya bia tu kila siku,kama wanafikiria kupunguza bei ya mchele,hata sisi wengine bia ndio mchele wetu,bila kupiga mbili hakuna usingizi unawazia mafisadi wanavyotafuna nchi hadi jogoo linawika.SItashangaa baada ya bajeti tukiambiwa Serengeti itakuwa elfu 3,na pakti ya embassy elfu 3,na soda elfu moja,secta ya madini wamepunguziwa kodi ili wachimbe zaidi na kuvutia wawekezaji wengi kutoka nje wawekeze katika sekta hii na kumalizia dhahabu iliyobaki ardhini etc
 
ok naona james mbatia mbunge wa jimbo la ikulu,mwanaccm wa nccr mageuzi ndo anaapishwa!
 
Ni wakati tena wa kushuhudia Ma-baboon yakisinziasinzia Bungeni na kupiga meza kupitisha na kushadidia maumivu kwa Watanzania.
 
Leo Bunge litapwaya kwani Wazee wakazi watakuwa Msibani CCM wanatamani itokee misiba kwa CDM mfululizo mpaka bunge liishe
 
Ninachojua mimi litakuwa BUNGE LA BAJETI YA KUKUZA DENI LA NCHI.
Matarajio yangu.
Kuongezeka kwa mfumko wa bei
Kushuka kwa thamani ya shilingi
Kuongezaka kwa mabilionea wapya walioteuliwa uwaziri.
Kusikiliza orodha ya mapungufu kibao yakitajwa na waheshimiwa wa CCM na mwisho wakiunga mkono MAPUNGUFU YAPITISHWE
 
Mimi nauliza kama SITTING ALLOWNCE zitafutwa sio tu kwa WABUNGE bali katika mfumo wote wa serikali, ili kupunguza unnecessary matumizi?!.
 
Nnaomba nisaidiwe kuhusu hii bajeti,hivi kila Serikali inapoleta bajeti mpya ni lazima ipandishe kodi/tozo ?Hakuna njia nyingine ya kufanywa kuepuka hili,sababu sisi wananchi wa hali ya chini ndio mara zote huwa tunaumizwa na gharama hizi?Kila siku Serikali unasema inapunguza matumizi mbona hatuoni hatua zinazochukuliwa?Wilaya mpya zinaongezwa bila sababu za msingi/wizi Serikalini/matumizi makubwa ya magari ya kifahari/matumizi makubwa ya Bunge letu kubwa Kama posho nk/fedha zinazoibwa na watendaji wa manispaa(wakurugenzi)hivi hii mianya yote ikizibwa haiwezi kusaidia fedha hizi kutumika ktk miradi ya maendeleo kama shule/barabara/zahanati-mahospitali/kilimo nk.Watanzania ni nani ametupumbaza akili!!!?
 
Mitaa mbalimbali ya mji wa Dodoma magari ya kifaari yamekuwa yakipitapita na mji umeonekana kuchangamka, tunategemea kuona kitimtim tena bungeni hasa ikiwepo tetesi kuwa uwezekano wa bajeti kukataliwa upo.:clap2:
 
Back
Top Bottom