Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2023-2024

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
942
MHDANIEL SILLO - TAARIFA YA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI MWAKA WA FEDHA 2023-2024

Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge Mhe. Daniel Barani Sillo ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini akiwasilisha taarifa ya bajeti kuhusu hali ya Uchumi kwa mwaka 2022; Mpango wa maendeleo ya Taifa kwa mwaka 2025 na tathimini ya utekelezaji wa bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2022-2023 na mapendekezo ya mapato na matumizi ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2023-2024

"Hali ya Uchumi wa Dunia kutoka International Monetary Fund (IMF) Aprili 2023 inaonyesha Uchumi wa Dunia ulikuwa kwa wastani wa 3.4% mwaka 2022 ikilinganisha na 6.3 mwaka 2020-2021 ambao ni ukuaji wa chini ya kiwango cha makadirio ya 4.4% ambao ulisababishwa na UVIKO-19, Vita vya Ukraine na Urusi; na mabadiliko ya Tabianchi yaliyosababisha kwa baadhi ya Nchi" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

"Mfumuko wa bei Duniani uliongezeka mwaka 2022 na kufikia wastani wa 3.7% ikilinganisha na 4.7% ya mwaka 2021 na Mfumuko wa bei kwa nchi za Afrika zilizopo Jangwa la Sahara zimefikia wastani wa 14.5% ikilinganisha na wastani wa 11% mwaka 202" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti Kamati ya Bunge ya Bajeti

"Kamati ya Bunge ya Bajeti inashauri Serikali kupitia Benki Kuu ya Tanzania na Wizara ya Fedha na Mipango kuweka mikakati ya Muda Mfupi, Muda wa Kati na Muda Mrefu wa jinsi ya kukabiliana na Mfumuko wa bei unaotokana na uagizwaji wa bidhaa nchini ili kutokuathiri Uchumi wa Taifa" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

"Kamati inashauri Serikali kuwekeza zaidi kwenye Sekta ambayo itawezana na nguvu ya Ushindani ili kuendelea kukuza uchumi kwa kiwango kinachotarajiwa kwa Sekta ya Utalii, Kilimo, Mifugo na Madini" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

"Kwa kuwa Tanzania imefanikiwa kupata masoko ya mazao ya Chakula Katika nchi mbalimbali barani Afrika; kwa kuwa bei ya mazao ya Chakula na nafaka katika Soko la Dunia linatarajiwa kupanda mwaka 2023 kutokana na kupungua kwa bidhaa hizo katika soko la Dunia; Kamati inashauri Serikali kuhamasisha uzalishaji wa Mazao ya Chakula na Biashara nchini pamoja na kuongeza thamani ya Mazao ya Nafaka nchini kwani uchambuzi wa Kamati ulibaini kwamba kati ya Tani Milioni 9.49 za Nafaka zilizozalishwa nchini ni Tani 13,6200 tu ndiyo ziliongezewa thamani" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

"Kwa kuwa soko la bidhaa Tanzania limefanya mauzo mbalimbali kuanzia kipindi cha mwaka 2018-2022 ambapo Tani Milioni 107.06 za bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Shilingi Bilioni 226 zimeuzwa. Kamati inashauri Serikali kuongeza idadi ya Mazao na bidhaa zitakazouzwa katika Soko hilo pamoja na kuongeza idadi ya wanunuzi walioashiria katika kununua bidhaa mbalimbali katika soko; Vilevile kutoa Elimu kwa wakulima juu ya kuuza bidhaa katika soko hilo pamoja na Kuangalia namna ya kuunganisha mfumo wa stakabadhi ghalani katika soko kwani zimekuwa zikiuzwa kwa bei ya juu kuliko stakabadhi ghalan. Hatua hizi zitawaongezea wakulima kipato pamoja na kuliingizia Taifa fedha za kigeni. Kabati inashauri ujenzi wa maghala mapya uendane na ukarabati wa maghala yaliyopo. Serikali iangalie uwezekano wa ujenzi wa vyumba vya baridi kwa ajili ya kuhifadhi Samaki, Mbogamboga, Matunda na Maua kwaajili ya kuuza nje ya nchi pamoja na kuongeza leseni za ujenzi wa maghala ya Mazao ya Kilimo kwa watu binafsi" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

"Mwaka 2023 thamani ya mauzo ya Mbogamboga na Maua ilikuwa ni Dola za Marekani Milioni 286.6 ikilinganisha na Dola za Marekani Milioni 378.6 mwaka 2022 sawa na upungufu wa 25.5%. Kamati inashauri Serikali kukamilisha mchakato wa kufufua Mashamba ya Maua, Mbogamboga na Matunda yaliyopo Wilaya ya Arumeru katika Mkoa wa Arusha. Ufufuaji wa Mashamba utaliingizia Taifa Fedha za kigeni pamoja na kurejesha ajira zaidi ya 2000 zilizopotea" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

"Mwaka 2022 pato la Taifa lilikua kwa 4.7% ikilinganisha na 4.9% katika mwaka 2021. Mwaka 2022 thamani halisi ya pato la Taifa lilifika Shilingi Trilioni 141.87 ikilinganisha na Shilingi Trilioni 135.4 mwaka 2021. Kupungua kwa kasi ya ukuaji wa uchumi katika kipindi husika kulichangiwa na athari za UVIKO-19, Vita vya Ukraine na Urusi pamoja na mabadiliko ya Tabianchi. Changamoto hizi zimepelekea Kupungua kwa uzalishaji wa bidhaa zinazouzwa katika soko la Dunia, kuathirika kwa mnyororo wa ugavi pamoja na kupanda kwa bidhaa za Msingi kama Mafuta na Ngano" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

"BoT inaonyesha kwamba 3/4 ya mwaka wa fedha 2022-2023 uchumi wa Tanzania ulikuwa kwa wastani wa 5.2% ikilinganisha na 4.9% mwaka 2021-2022. Hii inaashiria kuimarika kwa shughuli za kiuchumi katika Sekta mbalimbali pamoja na kuongezeka kwa ajira na mapato ya ndani" - Mhe. Daniel Sillo, Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti

_MG_0047mkoip.jpg
 
Back
Top Bottom