Bunge kuvunjwa kwa Kutumia Katiba ya 1977 !?(Theory/nadharia)

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200
Tunaona jinsi serikali ya CCM mara baada ya uchaguzi wa Oktoba 2010 inavyobanwa kila upande kutokana na vyama vya upinzani kujiongezea viti bungeni na huku chama tawala CCM kujikuta viti vimepungua na ruzuku pia toka serikalini.

Si hilo tu bali tunaona jinsi CCM inavyotumia kila mbinu kujitwalia nafasi za Umeya, Udiwani na kadhalika baada ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 2010. Na serikali kuandamwa kwa kutowajibika ktk kashfa za ufisadi, umasikini kuongezeka n.k

Je, mambo yakiwa magumu CCM ikitumia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 yenye marekebisho madogo ya mwaka 1992 na 2005 na kumshindikiza Rais J.K Kikwete kuvunja Bunge kutokana na kubanwa mbavu ni halali? Ikizingatiwa kuwa wabunge wa vyama vya upinzani wamechaguliwa na wananchi na sio Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maana chama tawala kinajua wapi waelekeze nguvu kama uchaguzi mpya ukiitishwa kabla 2015. Pia tunaona katika kikao cha Bunge kilichoanza february 2011 mjini Dodoma CCM inavyotumia wingi wake wa wabunge na spika kukandamiza hoja za wabunge ambao si wa CCM, ingawa wabunge hao ni wawakilishi wa wananchi.
 
Hawawezi kutumia Katiba ya zamani,; ni sheria mpya tu ndizo ziko effective.
 
Back
Top Bottom