Hatuwezi Kupata Tume Huru ya Uchaguzi bila Katiba mpya kwa sababu CCM haitakubali kuwa " Mchimba Kisima kaingia mwenyewe"

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,131
Bunge lina Wabunge wa CCM kwa zaidi ya 98% so hakuna muswada wowote wa kuitia kitanzi CCM utakaopitishwa.

Ni mjinga tu anayeamini CCM itawaondosha Wakurugenzi wa Halmashauri na Walimu kwenye kusimamia Uchaguzi na kuhesabu kura hasa ukizingatia CCM iko Kwenye hatua ya Mwisho ya Product Life Cycle.

Kama vyama Vya upinzani vimeshindwa kupigania Katiba mpya ni heri viungane tu na CCM kwenye Utaratibu wa Nusu Mkate.

Jumaa Mubarak 😄🔥
 
Jumaa Mubarak
Ni Magufuri ndio amekuja kuharibu kila kitu,ila kioindi cha nyuma mbona CCM walikuwa wanashindwa na Wakurugenzi ndio walikiwa wakisimamia uchaguzi.

Ni Magufuri ndio alivuruga
 
Mkapa na JK waliendana na values za democracy na wakurugenzi hawahawa walitumika na haki kutendeka. Ni kauli tu ya Rais Samia ni muhimu sana kuwafanya wakurugenzi watende haki angalao by 60% inatosha si rahisi kuifikia haki kwa asilimia mia kwa sababu ulizozitaja ili hali ya uchaguzi wa 2019/2020 isijirudie.
 
Ni Magufuri ndio alivuruga
Siku mtakayokubali kuwa Mwamba hayupo tena ulimwenguni, ndio siku mtakayo pumzika kuteseka INGAWA kovu haliponi.

Ni hivi, mimi binafsi, kama nisipoingia Jamii forums, nikaona HEADINGS za chawa, huwa sina taarifa yoyote ile ihusuyo serikali na kizimkazi, sisikii popote pale!

Enzi za mwamba, sihitaji simu wala runinga kujua yanayoendelea serikali na kwa mwamba, nikitoka nje ya nyumba tu, wananchi wanazungumza na wako well informed.

Kwa sasa, sio tu hawana taarifa, ila hawana hata interest na taarifa zenyewe; chawa inabidi wapige kampeni ya kuelezea na kueneza habari ambazo hazina hata uhalisi na hivyo kutokuwa na mvuto!

Inabidi zibandikwe na kusambaza picha ili kulazimisha wananchi kuona na kumfahamu kizimkazi, wampende kwa lazima; bahati mbaya sioni huo muitikio huku kijijini kwetu.

Wale mabingwa wa kutangaza DENI LA TAIFA enzi zile, saa hii nasikia wengine wanatangaza KUSTAAFU, maana lililopo enzi hii, ni KUFURU.

Bajeti halisi ya kisiwa haizidi bilioni 500, ambapo walikuwa hawazipati zote mpaka mwaka unaisha, UNAENDA KUCHUKUA MKOPO, unampa bilioni 400 kwa pamoja KISHA unamsifia anafanya maendeleo? Ulitaka afanyie nini hizo pesa ambazo hawajawahi kuzigumia kwa pamoja?

Maisha yapo huku chini, katika population ya watu 62m, ni watu wasiozidi 10m ndio wenye kufanya kazi, biashara, siasa, ufisadi, wizi n.k ambapo 7m wapo Dar; watumishi wakiwa hawafiki 1m.

Watu takribani 50m hawana access na sh 2000 kwa siku, watu wasiozidi 6m wanagawana trilioni 36 kwa mwaka!

Hakuna kinachoendelea chini ya hii FREE BOAT style of governing.

Itoshe kusema, sisi bodaboda, unafuu wetu ulikuwa enzi za MWAMBA, ninyi WAKWAPUAJI, ugumu wenu ulikuwa enzi MWAMBA.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Magufuli ndiye aliyeharibu mfumo mzima wa uchaguzi ni ukweli unaosema kwamba hamna kitachofanyika bungeni maana mazao ya magufuli yamejaa mule, isitoshe kwenye hilo bunge waliopita kwa haki yawezekana wasifike hata watano, wengi wameingia mula kwa kupora kura, kimsingi walijaa mule bungeni wengi ni wezi! Hamna kitachofanyika! Kwa sababu sio kwamba Rais hafahamu anajua nini wananchi wanahitaji lakini kutokana na kuwa na madharau kwa wananchi ndo maana wanachelewesha na kuleta maamuzi yao! Kimsingi mambo haya yanakera sana! Katiba mpya wananchi wanahitaji toka 2014 lakini kila rais akiingia madarakani anasema sio kipaombele chake, lakini pesa wanazozitumia kwa mambo yasio na umhimu ni nyingi tu!! Mm nafikiri wanachokitafuta watakipatq, wasifikiri wananchi ni wajinga, wananchi wa sasa wameelimika sio wale wazamani!!
 
Bunge lina Wabunge wa CCM kwa zaidi ya 98% so hakuna muswada wowote wa kuitia kitanzi CCM utakaopitishwa.

Ni mjinga tu anayeamini CCM itawaondosha Wakurugenzi wa Halmashauri na Walimu kwenye kusimamia Uchaguzi na kuhesabu kura hasa ukizingatia CCM iko Kwenye hatua ya Mwisho ya Product Life Cycle.

Kama vyama Vya upinzani vimeshindwa kupigania Katiba mpya ni heri viungane tu na CCM kwenye Utaratibu wa Nusu Mkate.

Jumaa Mubarak 😄🔥
wewe ni nani unayesema as if unao ufunguo wa kuruhusu nini kifanyike na nini kisifanyike, kama mjinga ndiye anaamini wakurugenzi na walimu wataondolewa kusimamia uchaguzi, basi mpumbavu ni yule anayedhani ccm wataendelea kutawala na kufanya lolote kama wanavyotaka..wewe si ni kipofu, pigia mstari mwisho wa ccm unakuja!
 
Bunge lina Wabunge wa CCM kwa zaidi ya 98% so hakuna muswada wowote wa kuitia kitanzi CCM utakaopitishwa.

Ni mjinga tu anayeamini CCM itawaondosha Wakurugenzi wa Halmashauri na Walimu kwenye kusimamia Uchaguzi na kuhesabu kura hasa ukizingatia CCM iko Kwenye hatua ya Mwisho ya Product Life Cycle.

Kama vyama Vya upinzani vimeshindwa kupigania Katiba mpya ni heri viungane tu na CCM kwenye Utaratibu wa Nusu Mkate.

Jumaa Mubarak 😄🔥
Leo umeamkia wapi?
 
Magufuli, Magufuli..Magufuli was not God, where is he now...yeye peke yake hawezi kuharibu uchaguzi, na wala ccm hawana uwezo kuharibu uchaguzi, wanaoharibu uchaguzi wapo siku zote na kwa sababu za ujinga na ufinyu wa akili wa kutotaka kuwajua ndio maana wanaharibu uchaguzi kila unapotokea na kwa kiwango wanachotaka.
 
Wale Majenerali watusaidie kuondoa ili genge la Wahuni lililo pola chama cha Wakulima na Wafanyakazi na kukigeuza chama cha Wafanyabiashara ya siasa then baadaye ndiyo tuje tuunde katiba mpya itakayo kuwa na muafaka wa kitaifa.
Ila kutegemea CCM ibadirishe mifumo ya kiutawala ambayo inalinda masilahi ya Mabwanyenye,tutasubiri sana!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Magufuli, Magufuli..Magufuli was not God, where is he now...yeye peke yake hawezi kuharibu uchaguzi, na wala ccm hawana uwezo kuharibu uchaguzi, wanaoharibu uchaguzi wapo siku zote na kwa sababu za ujinga na ufinyu wa akili wa kutotaka kuwajua ndio maana wanaharibu uchaguzi kila unapotokea na kwa kiwango wanachotaka.
Kwanini tusitumie technolojia kwenye uchaguzi mtu akipiga kura aione imeenda wapi?
 
Bunge lina Wabunge wa CCM kwa zaidi ya 98% so hakuna muswada wowote wa kuitia kitanzi CCM utakaopitishwa.

Ni mjinga tu anayeamini CCM itawaondosha Wakurugenzi wa Halmashauri na Walimu kwenye kusimamia Uchaguzi na kuhesabu kura hasa ukizingatia CCM iko Kwenye hatua ya Mwisho ya Product Life Cycle.

Kama vyama Vya upinzani vimeshindwa kupigania Katiba mpya ni heri viungane tu na CCM kwenye Utaratibu wa Nusu Mkate.

Jumaa Mubarak 😄🔥

Tanzania tulikuwa tunaenda vizuri, na ila Kuna mjinga mmoja kaja kuharibu kila kitu. Sasa nchi imekuwa ya machawa.
 
Siku mtakayokubali kuwa Mwamba hayupo tena ulimwenguni, ndio siku mtakayo pumzika kuteseka INGAWA kovu haliponi.

Ni hivi, mimi binafsi, kama nisipoingia Jamii forums, nikaona HEADINGS za chawa, huwa sina taarifa yoyote ile ihusuyo serikali na kizimkazi, sisikii popote pale!

Enzi za mwamba, sihitaji simu wala runinga kujua yanayoendelea serikali na kwa mwamba, nikitoka nje ya nyumba tu, wananchi wanazungumza na wako well informed.

Kwa sasa, sio tu hawana taarifa, ila hawana hata interest na taarifa zenyewe; chawa inabidi wapige kampeni ya kuelezea na kueneza habari ambazo hazina hata uhalisi na hivyo kutokuwa na mvuto!

Inabidi zibandikwe na kusambaza picha ili kulazimisha wananchi kuona na kumfahamu kizimkazi, wampende kwa lazima; bahati mbaya sioni huo muitikio huku kijijini kwetu.

Wale mabingwa wa kutangaza DENI LA TAIFA enzi zile, saa hii nasikia wengine wanatangaza KUSTAAFU, maana lililopo enzi hii, ni KUFURU.

Bajeti halisi ya kisiwa haizidi bilioni 500, ambapo walikuwa hawazipati zote mpaka mwaka unaisha, UNAENDA KUCHUKUA MKOPO, unampa bilioni 400 kwa pamoja KISHA unamsifia anafanya maendeleo? Ulitaka afanyie nini hizo pesa ambazo hawajawahi kuzigumia kwa pamoja?

Maisha yapo huku chini, katika population ya watu 62m, ni watu wasiozidi 10m ndio wenye kufanya kazi, biashara, siasa, ufisadi, wizi n.k ambapo 7m wapo Dar; watumishi wakiwa hawafiki 1m.

Watu takribani 50m hawana access na sh 2000 kwa siku, watu wasiozidi 6m wanagawana trilioni 36 kwa mwaka!

Hakuna kinachoendelea chini ya hii FREE BOAT style of governing.

Itoshe kusema, sisi bodaboda, unafuu wetu ulikuwa enzi za MWAMBA, ninyi WAKWAPUAJI, ugumu wenu ulikuwa enzi MWAMBA.

Tukubali Magufuli kwenye siasa aliboronga. Huwezi ukasifia uchaguzi wa 2019/2020. Utakuwa ni unafiki.
 
Hii nchi ni ya wote sio ya CCM pekee. Kama CCM wanadhani wao ndio wamuliki wa hii nchi waendeleze ujinga wa 2019/2020
 
Covid 19 ilifanya kazi kubwa na nzuri March 9 ,2021 na umma kufahamishwa March 17 , 2021

Kazi imebaki kwa watanzania kukamilisha na kufuta mpango ule haramu uliokuwa umesukwa October 28, 2020.
 
Watanganyika wamekusikia
 
Back
Top Bottom